How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday, 30 April 2016

Mlevi kutaja walioficha njuluku nje


            Baada ya kufichuliwa ukwepaji mkubwa wa njulu kule Panama, nafanya mipango kwenda kule kuibua wafichaji wa Kibongo ambao wameponea chupuchupu kutotajwa japo wengi wengine bado wamo kwenye documents ambazo hazijashughulikiwa. Kwa sasa nawasiliana wanasheria wenzangu tuliokutana kwenye chuo kikuu cha Yaleyale Jürgen Mossack na Ramón Fonseca wa Mossack Fonseca company kutaka wamwage mtama mwingine hasa wenye majina ya wabongo. Mnadhani utani? Hawa jamaa ni washirika zangu wa siku nyingi; na lazima tuwatumbue watu hapa. Tunataka tupate majina ya majambawazi ya kibongo na kumpa Dk Kanywaji Makufuli tuone kama atafanya kile kilichowashinda watangulizi wake ambao nao tuna wasi wasi wana njuluku ughaibuni hata kama si Panama.
             Najua sasa vibaka wetu wanene wanajisifu kuwa wao ni safi kwa vile majina yao hayamo kwenye orodha hii wasijue kuwa mambo bado ukiachia mbali kuwa bado ya Cayman Bahamas, Dubai, Switzerland, Hong Kong, Mautius Island of Man na kwingineko hayajamwagwa hadharani ili waumbuke vizuri. Nawashauri wangoje kwanza. Kwani, mpango wangu ukifanikiwa, wengi watabaki bila nguo. Na hii ni kweli wala sitishii.
            Hata yule Jaji gabacholi wa Kenya Kalinipa Rawalu Absii Kalu alitajwa na waziri mmoja wa Ka-Game hawakutajaria wangetajwa tena kavukavu bila kuficha wala kufunika majina yao mwingine aliyetajwa bila kutegemea ni ni Riz wa Ghana na Congo na sister yake Kabila ambaye alikuwa mwanafunzi wangu pale Kinondoni seco kabla sijarejea vyuoni kunyaka shahada kama sina akili nzuri baada ya wabongo kunitilia mtima nyongo. Mwingine aliyevuliwa nguo huku mjomba wake akiwa tayari uchi si mwingine bali anko Bonge Khubuluse Xuma wa Sauzi anayesemekana kuwa na njuluku kama Bill Gate.
            Baada ya kupata inshu toka kwa washikaji zangu wa pale Panama City kwenye mtaa wa 54th East. Naona yule anatikisa kichwa asijue nimetia timu sana kwenye jiji hili la kisasa ambao umaridadi na utajiri wake umetokana na chumo la wizi ambalo mabwege wengi huibia kaya zao na kwenda kuficha kule.
            Baada ya kukamilisha kila kitu, nitamshauri Dk Kanywaji awasiliane na mamlaka za Uswisi mara moja ili kuleta ule mshiko ambaye Njaa Kaya alijifanya hamnazo na kuzuia uzirejeshwe kayani ili kusaidia mambo mengine kama vile elimu na afya. Kwa vile Olivier Chave ni mshikaji wangu ambaye tulikuwa tukinywa pamoja alipokuwa balozi hapo Dar, lazima atakuwa tayari kumpa tafu rais Kanywaji tena bila masharti wala kusitasita. Pia nitamshauri afufue makabrasha ya Daudi Balalii ili kujua kama kweli alidedi au anakula mikuku mitaa ya Washington kama siyo Hawaii. Kama alirejesha namba, washirika zake lazima wajulikane na kutumbuliwa tena haraka sana wakiwa uchi.
            Katika nusa nusa yangu nshapewa inshu kuwa wabongo walioficha njuluku Panama ambapo wako kwenye rada yangu ni pamoja na Njaa Kaya aliyekalia orodha ya majina aliyopewa.
            Mwingine anayepaswa kuchunguzwa vilivyo hata kufikishwa kwa pilato ni munene wa Takokuru ambaye alipewa inshu nyingi za ufisadi na ufichaji njuluku nje lakini akayatumia kujipatia nshiko kiasi cha kutokea kuwa bonge ya bilionea. Hata mjengo wake wa kule Beach siyo noma. Lazima naye afanyiwe kweli aeleze alivyochuma hiyo njuluku ya kuweza kuwa na mjengo wa kukata na shoka kama huu.
            Mwingine ambaye nilishapewa inshu yake ni jizi Kagoda ambaye ameficha mabilioni ya madafu Dubai na Panama na kwingineko ambako bado navuatilia.
Pia yume mzee wa Vijisenti ambaye naye alikatiwa sana njuluku kibao tokana na kuwawezesha wachukuaji waitwao wawekezaji kuingia mikataba ya kijambazi ambayo licha ya kufilisi kaya yetu, imesababisha kaya yetu kuonekana kama shamba la bibi aka kichwa cha mwendawazimu kwa kila jizi kujifunzia kuiba.
            Majizi ya Escrew nayo yanasemekana kuficha njuluku nyingi kule Panama, Singapore na kwingineko ambako bado nafuatilia kwa karibu ili baadaye niyavue nguo ingawa yako uchi tayari kiasi cha kufanya umma ushangae namna Dk Kanywaji anavyoyagwaya na kujifanya hajui chafu yake.
             Mwingine ninayepanga kumfuatilia ni Mzito Kabwela aliyeficha majina aliyowahi kudai alikuwa nayo lakini akagwaya kuyaweka wazi. Kuna mlevi amenitonya kuwa naye si safi. Kwani alitumia mwanya ule ima kujipatia umaarufu au kuwatoa njuluku watuhumiwa.  Ndiyo maana napendekeza rais Kanywaji ambane mbavu aeleze anachojua na kwanini alificha majina ya wezi wakati anajua jinsi wanavyoua walevi wengi kwa umaskini ukiachia mbali huduma mbovu za kijamii zilizohujumiwa kiasi cha kutisha.
            Loooh! Niliataka kusahau wengine ambao nitawashughulikia. Wote wanaoficha njuluku kwenye mijumba na migari ya bei mbaya hapa hapa downtown lazima nao nitawashukia bila kuwasahau wale viongozi wa kiroho wenye uroho wakwasi. Lazima waeleze walivyochuma huo ukwasi kama hakuna namna. Maficho ya njuluku si Panama wala Isle of Man au Jersey bali hata Masaki na kwingineko kwa wanene.
Pfyaaa, pfyaaa. Hii chafya nayo jipu!
Chanzo: Nipashe.

Tuesday, 26 April 2016

Kijiwe chadurusu daraja la Kigamboni


















Baada ya rahis Joni Kanywaji Wine Makufuli kufungua daraja jipya la Kigamboni alilopendekeza liitwe mzee Mchonga, Kijiwe kilikaa na kudurusu baadhi ya mambo kuhusiana na daraja hili adhimu na la kwanza la aina yake “Duniani.”
Mgosi Machungi anaingia akiwa amevaa picha ya daraja la Kigamboni kifuani. Anaamkua na kuchonga, “Wae waiokuwa wakisema kwao ni kama Ulaya sasa wajiandae kuja si kushangaa fei tu bai hata daaja jipya la Kigamboni aka mzee Nchonga.”
Mpemba anadakia, “Hayawi hayawi sasa huwa; ngalau sasa kaya yetu yaweza kuwa kama Ulaya yakhe. Nataka sasa lijengwe jingine kutoka hapa Bongo hadi Pemba wallahi ili tuachane na kuzama baharini na kuliwa na samaki.”
Kapende hakubaliani na mawazo ya wenzake. Anakwanyua mic, “Kipya kinyemi japo kidonda muangalie. Tokana na kaya yetu kuwa ya kifisadi na roho mbaya, sina cha kufurahia. Maana, sina uhakika kama daraja husika limekidhi viwango vya usalama vya kimataifa,” anapiga chafya na kuendelea, Je mradi walingana na thamani ya mabilioni yaliyounguzwa pale au wajanja weshapata chao?”
Kabla ya kujibiwa, Mipawa anakula mic, “Nami nina shaka kweli kweli. Hata hivyo, nashangaa hii tabia ya kutaka kugeuza kitu kuwa mtu.Kwanini liitwe Nyerere na si mashujaa wengine kama vile mzee Mpayukaji, Mkwawa au Milambo kama si Nyungu ya Mawe hata Eddie Sokoine?”
Kutaja tu jina langu naangua kicheko ila sisemi chochote. Nikiwa natabasamu kwa kuitwa shujaa hata kama wa kijiweni, Mbwamwitu anadaka mic, “Nyang’au sasa watatukoma. Humkusikia rais Joni Kanywaji akiwatupia kimondo kuwa wote waliozoea kusema kila kitu kiko kwao sasa wanaisoma namba na kuchukua tahadhari? Ngoja Flyovers za kumwaga uone Bongo itakavyopiku majiji yote ukanda huu.”
Mipawa anamchomekea Mbwamwitu, “Hapo kaka umeua.  Sijui kama hawa jamaa wapenda sifa na dezo ukiachia mbali majivuno wataanza kusema kuwa na daraja la Mchonga liko kwao. Usishangae kusikia likiitwa Kinyata badala ya Mchonga. Walipojenga flyover na barabara kubwa miaka iliyopita walijivuna sana wasijue nasi tulikuwa nyikani tukisuka mipango namna ya kujiondoa na kadhia ya kuonekana kichwa cha mwendawazimu ingawa hatujatoka huko bado.”
Mijjinga aliyekuwa akimtext mshikaji wake anaamua kutia guu, “Kama wasemaji walioonyesha shaka, nami nina mashaka na maswali kadhaa kuhusiana na daraja hili na Maflyover pendekezwa. Je yanadumu na ni salama? Nikiangalia mijengo iliyojengwa kigabachori na kifisadi, sina imani na mradi huu. Nitakachofanya ni kupunguza safari za kwenda Kigamboni ili kuepuka maafa.”
Msomi Mkatatamaa anaamua kuingia fosi, “Kaka wala huna haja ya kuacha kwenda Kigamboni kwa kuogopa kuliwa na samaki. Mbona kaya zima ni bomu! Angalia utitiri wa vituo vya kuuzia mafuta jijini na kwenye miji mingine. Unadhani hata hapa tuko salama? siku vitakapolipuka–kama utanusurika–utayakumbuka maneno haya. Si hilo tu. Hii mijengo iliyorundikana kama uyoga nayo mtaiweka upande gani?”
Sofia Lion aka Kanungaembe anaamua kutia timu, “Kama waliosimamia kazi ya ujenzi wa daraja hili walikuwa wakweli, hakuna haja ya kuogopa ingawa hili nalo laweza kuwa gumu hasa ikizingatiwa kuwa hii ni kaya inayotawaliwa na Chukua Chako Mapema bila kuwajali wenzako hata wewe mwenyewe baadaye. Kuna haya ya sirikali kufanya uchunguzi wa mradi mzima ili kujiridhisha kuwa hakuna ufisadi uliofanyika hapa ili tuweze kuwa na imani na mradi uliogharimu mabilioni ya fedha yetu ya kodi.”
Kanji anamchomekea Sofi, “Da Sofi iko kuna mimi veve hapa. Kama sirikali nafanya chunguzi takuwa juri sana. Kama taacha vatu iliwe na samak basi laumu yeye.”
“Nakuna veve vapi Kanji acha uhuni,” anachomekea Mchunguliaji aliyekuwa akisoma gazeti.
Mheshimiwa Bwege anaamua kutia buti, “Kanji mbona unafikiri kama jana! Unadhani watawala wetu wanaogopa lawama? Ukiwalaumu sana sana watakuchukia kama jamaa waliokosoa utumbuaji majipu wa bwana nkubwa wakaishia kutishiwa na kuitwa majipu. Mie naungana na wale wanatakaoamua kupunguza safari za Kigamboni basi.” Anampa kikombe muuuza kahawa amtilie kahawa na kuendelea, “ Hivi mliona yule nyampala wa mkoa alivyowachoma wenzake wakaishia kusimamishwa ulaji? Ama kweli nyampala ameonyesha kujitahidi ingawa sikubaliani na ukurupukaji unaosikiliza upande mmoja. Rahis hakupaswa kuamua pale pale kana kwamba ajira za wanene ni mnada. Alipaswa kuwaita wahusika na kuwapa nafasi ya kujitetea ili wasitumie kisingizio hicho mbele ya pilato.”
Msomi anarejea, “Usemacho ni kweli. Japo rahis ana nia nzuri tu, anapaswa kufuata sheria ili kuwa na utawala bora na wa sheria. Pia asichukie wala kuogopa kukosolewa. Itakuwa zahama kama atapenda kusikiliza vibwagizo vya wanyampala wake wanaofanya usanii na kutetea kitumbua chao. Lazima akubali kuwa hawezi kujua yote wala kuwa sahihi wakati wote. Isitoshe hii kaya ni yetu sote naye yuko pale kututumia na si kutuburuza au vipi?”
Kijiwe kikiwa kinanoga si lakipita shumbwengu la Willy Kabwea, wacha tulitoe mkuku!
Chanzo: Tanzania Daima.

Sunday, 24 April 2016

Letter to Janet Magufuli

   Dear First lady, Janet Mugful,
            Congrats on becoming the fifth-first lady of the republic of Bongo.
Allow me to humbly and sincerely touch base with you. To be open and frank, I adore you like I do to Maria Julius Nyerere the first-First Lady of this hunk who served diligently and trustworthily so as to be missed even after over thirty years of her noble service.
Janet Magufuli, Tanzania's new First Lady            You, too, contrary to your greedy and venal predecessors minus Maria, seem to have understood how irky boozers feel about the biz of using Ikulu to print and mint dosh illegally.  For, since your hubby took the reins of power, I’ve never caught wind of any speculations about your new First Non-Governmental Organization (NGO) aka the First Lady’s money-making company disguised as an NGO.
            Boozers asked me to write this letter as their appreciation for your patriotic and trustworthy resolve especially refusing to ride on your hubby’s back and make a killing quickly by duping our sisters, mothers and daughters that you fight for them as if the ministry responsible isn’t there. Your knockback to forming an NGO makes boozers happy so to speak. They’ve always suspected such NGOs that they call private companies for thievish and hooked on First Ladies. Why use your hubby’s office as if you’re brainless? Why forming an NGO after your hubby becomes president? Keep this up dear lady to see to it that the devil doesn’t cheat and hoodwink you just like others we love to hate for their ravenousness and nearsightedness.
If you keep in on with that, your ideal example will save much dosh especially at this time power’s used as a spoon to scoop ill-gotten wealth. Indeed, power, especially in corrupt hunks like ours lulls and corrupts absolutely. Keep on defeating the devil and greed. Stay put as you only advise; and care for your hubby at this time he’s ruling the hunk instead of wasting time and face chasing dirty and quick bucks that’ll, in the end, make you look bad if not being called a bandit. So, too, make sure that your kids and relatives are not getting near to the biz of the hunk. If your friends or relatives come asking you to talk to the big man about offering positions, tell them to go to hell. Beware. Many’ll befriend you so as to get away with murder. Never allow them to use you as if you’re naïve just like those we know to have been used by their shogas to get some ulaji they are now losing like crazy.
            I’m not writing this to make myself look good or get close to the seat of power like those I know who say even unthinkable things that birds can’t believe in. I’m sincerely and happily writing this as a testament that boozers don’t like First NGOs or nepotism and cronyism as we used to evidence them in the past. I don’t expect to hear that your son or daughter’s a millionaire or chasing small positions in the party of your hubby like it used to be sometimes back. Like Maria Mchonga, you’ve proved that first lady sans NGO is possible and honourable. Please maintain this sanity to see to it you make a good precedent to top up Maria’s. Boozers like the way you’ve kept a low profile especially after your hubby became head. Boozers are happy about this. I think even Joni is happy. You can see it in his face. For, he doesn’t have a wife who wants him to bend some rules in order to enable her do simian biz. Keep in on making him happy by avoiding temptations of making dosh even if it means to endanger his admin especially after exiting power. Who wants his sweet to become a disgrace especially after vacating the seat of power? Who wants to be accused of doing biz in Ikulu or inviting her relatives and other bêtes noirs to rob the boozers? Who wants to be jeered and mocked by boozers, birds and goats after exiting power? Go ask Ana Tamaa Makapi or Sal Jake. Do you think they are as happy and respected as Maria is? Their myopia and greed are not torturing them. Kula na kulipa. The other day I evidenced birds jeering and mocking them simply because they misled their gullible and myopic hubbies so as to do business in the holy of the holy. Theirs was what boozers call bedroom politics whereby unwise people sharing the bedroom with the big men use them as tools for exploiting paupers already pauperized by visionless and thievish rules of their hubbies which Joni seems to avoid like leprosy.
            Dear Mom, allow me to wind up this epistle here wishing you well as I strongly commend and advise you to stay put to see to it that shetani wa utajiri doesn’t get you. Amen.
Break a leg mom.
Source: Guardian.

Chini ya Kikwete tulikuwa taifa la walevi


            Sina nia ya kumkandia rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye huwa sipendi kumuita dokta kwa vile hajasomea shahada ya uzamifu. Ila naweza kueleza kuwa chini ya utawala wake–kama ulivyoumbuliwa na aliyemrithi–ulikuwa wa kilevi kwa namna fulani. Hapa ninaposema ulevi lazima nieleweke. Simaanishi ulevi wa pombe bali kujisahau na kuwasahau wanyonge. Leo nitajaribu kudurusu namna sekta muhimu ya elimu ilivyokuwa imetelekezwa na tukashikilia–au kutoa vipaumbele kwa mambo ya kilevi tu–huku wanafunzi wakizidi kuumia. Leo nitajaribu kulinganisha baadhi ya huduma na watendaji na elimu na walimu.
            Hakuna tatizo linaloihangaisha serikali ya rais John Pombe Magufuli–kati ya mengi–kama la ukosefu wa madawati mashuleni hasa shule za msingi. Unashangaa kwa mfano kukuta hata short time guest houses zilizotamalaki nchini zina viti wakati mashule hayana viti. Hii maana yake ni kwamba biashara ya ngono wakati mwingine inaonekana kuwa na thamani kuliko elimu.
             Ukienda kwenye mabaa unakuta viti vimejaa hata vingine havina wa kuvikalia wakati watoto wa hao hao wanaokunywa wanakaa chini. Hata ukilinganisha wauza baa na walimu utagundua kuwa baadhi ya wauza baa wanaotesha vitambi wakati walimu wakikonda. Ukiangalia hata polisi ambao kazi yao inapaswa kuwasulubu na kuwakausha kama si kuwakondesha, wana vitambi ikilinganishwa na walimu waliokondeana.
            Ukitoka hapo waangalie wanasiasa ambao kimsingi ndiyo wanaotunga sheria. Wengi wanalipwa mabilioni wakati wataalamu wakikimbia nchi tokana na mishahara haba wakati wao si wataalamu wa chochote zaidi ya siasa.
            Kituko kingine japo kinasikitisha ni ukweli kuwa pombe inapatikana kila mahali nchini. Vitabu viko wapi? Hakuna. Tuna viwanda vya bia vingi wakati watunzi na wachapishaji wa vitabu wakizidi kudodeana kutokana na kutokuwa na mkakati wa serikali wa kutumia kazi zao kama ilivyokuwa awali.
            Sambamba na kupatikana pombe, hata kondomu zinapatikana lakini vitabu hakuna na kama vikipatikana vingine havikidhi viwango tokana na ubadhirifu bado vinatumika wakati vinavyokidhi viwango vikidoda kutokana na watunzi kutokuwa na mjomba kuwatetea. Watu wanaandika au kutunga vitabu vya ajabu na kuviweka kwenye mitaala wakati wakikataa vitabu vya maana.
            Wakati wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji walikuwa wakikwepa au kusamehewa kulipa kodi, watoto wetu waliongezewa ujinga badala ya maarifa tena kwa kutozwa kodi ya kulanguliwa. Tuna vyuo vingi vya hovyo kama St. Joseph ambacho hivi karibuni kilibainika kuwa bomu. Kama haitoshi, tuna academia za kitapeli ambazo zinakazania watoto waongee kiingereza lakini bila maarifa. Je kiingereza ndiyo elimu na maarifa au ni zaidi ya lugha?  Je Academia hizi zinakaguliwa vya kutosha kuona kama zinatoa maarifa yanayohitajika badala ya kusikiliza matakwa ya wazazi ambao wengi si wataalamu wanaoamini kuwa kujua kuongea kiingereza ndiyo kuelemika ili kuwatoa fedha?  Kiingereza ni muhimu hasa wakati huu wa utandawazi na tukizingatia kuwa kiingereza ni lugha kubwa kuliko yoyote duniani;na inatumika karibu duniani kote. Hata hivyo, tunapaswa kuwapa na ujuzi na maarifa watoto wetu. Mwandishi wa makala hii–pamoja na kusoma shule za “Kiswahili”–ameandika vitabu vingi vikiwemo vya kiada ambavyo vinafundishwa kwenye nchi zinazoongea kiingereza kama Afrika ya Kusini na Zimbabwe ambazo kiingereza ni kama  lugha yao ya kwanza–kuonyesha kuwa elimu si lugha bali maarifa.
            Chini ya Kikwete tulilewa na biashara hasa uchuuzi kiasi cha kuufanya kama jibu la kila tatizo. Hadi sasa walimu hawafundishi kwenye madarasa yao waliyoajiriwa kufundisha; badala yake wanafundisha kwenye madarasa ya tuisheni na hakuna anayestuka. Sisi tuliosoma miaka ya themanini hatukusoma tuisheni; lakini bado tuliweza kufanya vizuri tokana na kuwa na mfumo mzuri wa elimu. Chini ya ulevi wa kimfumo, leo tuna kila aina ya upuuzi unaiotwa elimu wakati ni upuuzi na ujinga. Nidhamu na motisha kwa wanafunzi imetoweka baada ya kushuhudia watu ima wakiimbia umma au kuuza mihadarati na kutajirika hata kama hawajui kusoma na kuandika. Watu wanafikiria kutunga mistari ili waukate wakisahau kuwa ni wachache wanaoweza kuukata ikilinganishwa na wengi wanaoukata kutokana na elimu zao.
            Uoza chini ya Kikwete ulikuwa mwingi tu hadi kukawa na dhana kuwa nchi ilikuwa ikijiendea tu bila mwelekeo wala kiongozi.
            Tumalizie kwa kumtaka rais Magufuli lazima aondoe hii kadhia kwa kuufumua na kuusuka mpya mfumo wetu wa utawala; kwani ni wa kilevi zaidi ya uchapakazi wala kutumia akili. Kituko, hata ikija kwenye siasa, tuna vyama hadi vya mfukoni vikijiita wa siasa wakati ni vya mission to town. Hapa hujagusia hata imani zetu ambapo tuna hata dini za ajabu ajabu zinazofanya miujiza ya kuwaibia wananachi wetu huku serikali ikiangalia tu.Tuna kila aina ya upuuzi kuanzia wa kufikiri hata kutenda. Kwa kuangalia haya yote kati ya mengi, unaweza kujenga hitimisho kuwa chini ya utawala wa Kikwete nchi ilikuwa imegeuzwa ya kilevi kiasi cha kufanya kila kitu kilevi wakati wale waliopaswa kutustua nao walikuwa wana ulevi wao kama kusafiri nje, kuombaomba, kushabikia upuuzi, kutegea, kutofanya kazi, kutofikiri bila kusahau kufuja na kuiba kana kwamba hakuna kesho. Nadhani hili ni somo kubwa kwa Magufuli.
Chanzo: Tanzania Daima.

Friday, 22 April 2016

Makonda asimhadae rais na dunia


            Akitoa salamu za mkoa wa Dar Es Salaam hapo Aprili 19, Mkuu wa mkoa, Paul Makonda, aliwaacha wengi hoi alipojitahidi kujifagilia na kulinda kitumbua chake. Alisema kuwa tangu ateuliwe kuwa mkuu wa mkoa, vijana wengi wamejenga imani na matumaini makubwa kwa rais John Pombe Magufuli. Yeye ni mkuu wa mkoa wa Dar. Je amezunguka lini nchi nzima kuongea na kupata mawazo ya vijana wengi na wengi kiasi na wa wapi kama si uongo (uingi ni dhana tegemezi). Huwezi kujenga hitimisho la jumla kama hili ukaheshimika au kuaminika kisomi. Je Makonda aliongelea vijana wapi kati ya wale wanaofaidi matunda ya taifa na wale wasio na wa kuwakingia kifua kama alivyofanyiwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete baada ya kutuhumiwa kumdhalilisha mzee Joseph Warioba? Je anaongelea vijana wapi kati ya wale wa CCM na wa upinzani au wa vijijini na mijini?
            Kuna haja ya maafisa wa umma kujiamini na kuacha kujikomba na kujidhalilisha ili wasitimliwe kwenye ulaji wao. Makonda aliwaacha wengi–hasa wale waliomwangalia usoni na kusikiliza na kuchambua alichosema–wakati akitoa madai haya ya ajabu kidogo. Alisema eti vijana wamekuwa wakimuuliza kama rais Magufuli huwa anacheka. Ajabu kwenye mstari huo huo Makonda alisema kuwa Magufuli hutumbua majipu akiwa anacheka! Sasa kama anafanya kazi ya kuumiza kama vile akicheka, vijina hao (wa kubuni bila shaka) walitaka kicheko gani wakati ni rahisi kwa Magufuli kucheka hata kama anafanya kazi ya kuhuzunisha? Nadhani alichofanya bila kujua ni kumjenga Magufuli kama mtu mkatili anayeweza kucheka mahali anapopaswa kununua hata kulia. Hadithi za Makonda zinanikumbusha nilipokuwa kidato cha pili. Wengi wa marafiki zangu nami tulizoea kujitambulisha kwa vijana wa form one kama form fours wakati tulikuwa form two tu.
            Tunachojifunza hapa si sababu ya kuongopa bali ile hali ya baadhi ya watu kujidhalilisha kwa kila njia hata za uongo bila kujua kuwa kuna watu wenye akili (tena wasomi na wachambuzi) wanaowasikiliza ukiachia mbali wanaowalenga nao kuwa na akili. Hii maana yake ni kwamba watu wa namna hii (wasiojiamini) wana kila uwezekano wa kuwachusha hata kuwakera wale waliowaamini madaraka wasijue udhaifu wao. Watu wa namna hii ni rahisi kufanya makosa tena ya kijinga tu. Japo suala la kama rais anacheka au ananuna au vinginevyo si muhimu, kwa mlengwa mwenye kuwa makini linaonyesha ni namna gani mteule wake anavyomuona au kutaka wa kuweza kudanganywa na maneno matamu hata kama ni ya uongo. Sidhani kama Magufuli alifurahia sifa kama hii isiyo na msingi. Sijui kucheka au kununa kwa rais ni tatizo ambalo linawakabili hao vijana waliomtuma Makonda. Nadhani–kama kweli–wangekuwapo vijana wa kumtuma Makonda kwa rais, basi wangemtuma aulize ni kwanini anawapa vyeo wazee na walioshindwa kwenye uchaguzi wakati vijana wapo na hawana ajira na mahitaji mengine ya msingi.
            Si mara ya kwanza kwa safu hii kuandika juu ya Makonda. Tunajitahidi kumfuatilia ili kuona mwisho wake utakuwa vipi hasa ikizingatiwa kuwa uibukaji wake una wingu zito ambalo–hata kama wenye mamlaka ya kuteua hawakuliona au kulipuuzia–kuna siku litajidhihiri na ukweli kudhihirika bila uficho wala kuwa na dirisha na kuuzuia au kuubadili,
            Sioni kama kuna sababu ya kudanganya au kugeuzana mabwege wakati lengo (kama kweli ni hilo) la kuwa kwenye ofisi za umma ni kuutumikia na si kuutumia umma. Sidhani kama rais anahitaji vibwagizo hata visivyoingia akilini kama ilivyokuwa kwa Naibu waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani hapo tarehe 29 Machi akiwa Chato tena mbele ya rais akisema kuwa atatundika umeme hata kwenye matoroli na juu ya miti. Hii haingii akilini; na wala haimfurahishi unayemlenga. Ukitaka kujua inasikika na kutafsirika vipi, vaa viatu vya unayemlenga. Hizi ni siasa za kujikomba na za kibabaishaji. Nani anataka sifa za kipuuzi?
Hii inanikumbusha mwanasiasa mmoja wa Kenya ambaye hakujua Kiswahili vizuri. Katika kumfurahisha rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi, alistukia (tena kwa bahati mbaya ya kutojua Kiswahili) akisema, “Piga makofi Daniel arap Moi” badala ya mpigie makofi.
            Kisa hiki cha Moi hakina tofauti na hiki cha Makonda cha kujumlisha (generalization) vijana wote kuwa wamefurahia kuteuliwa kwake. Sijui kama vijana kama watoto wa akina Mzee Joseph Warioba aliyemnyanyasa wamefurahia uteuzi huu ambao kimsingi umetokana na kadhia hii. Ni bahati mbaya kuwa Makonda na wale waliomuumba na kumteua hawataki kugusia kashfa ya kumdhalilisha Mzee Warioba. Sidhani kama vijana wasio na tabia ya kujikomba wanafurahia uteuzi wa Makonda. Kimsingi, Makonda, sawa na wateule wengine, wanapaswa kuwa wakweli kuwa uteuzi wao umewafurahisha wana familia na marafiki zao lakini si vijana wote wa Tanzania au Dar Es Salaam. Sijui kama vijana wa Ubungo ambao mbunge wao aliwekwa ndani kwa kuwatetea walipokuwa wakihujumiwa na waajiri wao wana furaha anayosema Makonda. Ni bahati mbaya kuwa waliomuumba na kumteua Makonda hawakutaka kuliona hili kama lilivyo. Badala yake wameingiza ushabiki wa kisiasa na kuweka historia mbaya kwa vizazi vijavyo. Wakati mwingine najiuliza mtu wa kuteuliwa na mtu mmoja kupewa madaraka na jeuri ya kumweka ndani mwakilishi wa umma wakati anawakilisha tumbo lake na yule aliyemteua tofauti na mbunge anayewakilisha wananchi kwa malaki. Tunamkomoa na kumdanganya nani na kwanini na kwa faida gani na ya nani wakati cheo ni dhamana tena ya muda tu?
Chanzo: Mwanahalisi. 

Uliwahi kufurahi kutangaza kifo?


Naona yule anatikisa kichwa akidhani mibangi na ulabu vimeanza kunitia kichaa. Si kichaa wala roho mbaya au kuwanga vinavyonisumbua kufurahia kutangaza kifo au vifo vya gendaeka. Nina sababu tena zenye siha na mashiko. Hivi uliwahi kujiuliza kama hawa gendaeka wanaoibia kaya yetu kana kwamba ndiyo mwisho wa dunia  waliwahi kufikiri kuwa kuna bwana death? Nauliza hivi kutokana na ninavyowaza na kuyaangalia maisha hasa uhai kama msomi, fyatu na mja mwenye adabu.
Baada ya kugundua kuwa kaya yetu–kwa miongo zaidi ya mitatu–ilitawaliwa na kuliwa na gendaeka tuliofanya kosa kuwaamini madaraka tukidhani ni wenzetu, niliamua kujiuliza kama ingekuwa ni mimi ningefanyaje. Jibu nililopata ni kwamba nisingefisidi wala kuibia kaya kwa vile kuna siku nitarejesha namba tena niondoke mtupu kama nilivyokuja. Hivyo, wanaodhani niandikacho ni mibangi na uchizi nadhani hapa tutaelewana.
Siku rais Braack Obamiza alipotangaza kifo cha Osami bin Laden, hakuwa na chembe ya huzuni hasa ikizingatiwa; huyu jamaa alikuwa ameishasababisha vifo vya jamaa wengi wasio na hatia tokana na wendawazimu wake. Hivyo nami ninaposikia fisadi mmoja amerejesha namba huwa nafurahi kama sina akili nzuri. Kwanini? Simple; ufisadi umeishaua walevi wangapi tokana na kusikinishwa na wanahizaya hawa? Mie wakirejesha namba nafanya sherehe kama ilivyotokea niliposikia kuwa jambazi moja lililokwapua mabilioni kwenye Belly of Tembo (BoT) liitwalo Matusi Liyumbayumba lilirejesha namba. Hakuna siku nilikogeka kama siku Dadi Balaliii, yule jambazi, aliyewezesha ujambazi wa EPA aliporejesha namba kama kweli amerejesha namba.
Hivyo, leo ninapoandika waraka huu ili kuwafikirisha wanaofikiri kwa masaburi wasijue kuna kesho, nina furaha. Hata hivyo, nina huzuni hasa mafisi na mafisadi yaliyotumiwa na wanene zaidi yanaporejesha namba; kwani huwa furaha kwa mabwana zao ambao mara nyingi–ima huwadedisha ili kuficha chafu yao–au kuomba wafe ili siri zao ziwe salama. Unadhani baada ya fisadi hili jambazi kufa juzi wale waliolitumia lilipokamatwa na simu lupango likitaka kuwasiliana na munene hawajafurahi?  Najua wengi wananiona kama mwanga kufurahia msiba wa gendaeka. Nifanye nini iwapo nayo yanafurahia mateso na vifo vya walevi yanayosababisha tokana na kutoidurusu kesho na maisha ya waja? Hata liliporejesha namba lile jambazi la kigabacholi lililokuwa likimwita first lady wa mzee Ruxa shem, nilisherehekea kwa kuvuta mibangi na kunywa kama sina akili nzuri.
Siku mijambazi ya Kagoda, EPA, Escrow na mingine ikirejesha namba lazima nisherehekee; kwani namba ya wauaji itakuwa imepungua kinamna. Guess what. Nimefikia hatua hii–ambayo wasionijua vizuri wanaweza kusema ni kuwanga au kukata tamaa–baada ya kugundua kuwa sheria zetu za hovyo na za kikale huyasaidia majambazi kama haya hata kutoozea lupango. Kwa vile wenye madaraka tena ya kuazima ya hapa duniani wanakula na majambazi na kuyakingia vifua kama alivyofanya Njaa Kaya kwa jamaa wa mihadarati, ufisadi, ufichaji njuluku ughaibuni, mafisadi na majambazi, bwana God ameamua kutulipia wanyonge tunaonyongwa kwa umaskini wa kutengenezwa na hawa wajalaana audhubillahi mina sheitwaan rajiim.
Hebu tuwe serious kidogo. Hivi ukisikia mijambazi kama vile Jimmy Rugemalayer, Singasinga, Roast Tamu na mingine imenyotoka roho utafurahi kiasi gani? Hebu nieleze; ukisikia mijambazi kama hii iliyoibuliwa juzi kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani imenyotoka roho utafanyaje zaidi ya kumshukuru Subhana? Adui yako muombee kifo siyo njaa maana anaweza kuwa na uchache akala na kunenepeana wakati wahanga wake wakiteketea.
Je ni walevi wangapi wanajazwa ujinga na umaskini kutokana na ufisadi ulioua mifumo yetu? Je ni wangapi wanapoteza maisha kutokana na kutopata huduma wakati wakubwa wanaopaswa kusimamia haki wanakwenda kutibiwa hata mafua Ulaya na India? Hebu fikiria. Kama fyatu kama mimi naudhiwa na ujambazi unaoendelea kayani hivi, hao wenye akili timamu tena waathirika wasio na bangi na ulabu wa kuwatuliza wana hasira kiasi gani? Uzuri ni kwamba kul nafsi zalikatu maut yaani kila nafsi itaonja mauti. Naongea kishehe kidogo kuonyesha kuwa mimi si Maimuna ati.
Mlevi nina uga madhubuti adhimu na adimu wa kutolea hasira zangu ambao kwa kitaalamu huitwa venting. Je ni wahanga wangapi hawana pa kutolea hasira zaidi ya wanyonge zao kama vile bi wakubwa zao mambo yanapoharibika? Je hawa mafwisadi wameishavunja ndoa ngapi ukiachia mbali kusababisha vibaka kuchomwa moto baada ya kusikinishwa? Laiti wachovu wa kaya hii wangekuwa na akili na usongo kama vyangu, wasingehangaika kuwachoma moto vibaka–ambao hata hivyo siwatetei–badala ya kuchoma mibaka? Au wanangoja mkono wa Bwana God tu utende haki?
Leo sichongi sana. Nina furaha ajuaye Bwana God. Anapokufa fisadi mimi kwangu sherehe. Ngoja nikitoe nikapate misokoto na ulabu kusherehekea maamuzi ya haki na sahihi ya Bwana God kwa wachovu na walevi. Nina furaha kutangaza kifo cha fisadi nonihino kilichotokea kule kwa wazito na habari ziwafikie wahanga wote ili washerehekee.
Chanzo: Nipashe.

Wednesday, 20 April 2016

Kijiwe chatongoa Nkapa Foundation


            Hivi karibuni bwana nkubwa bingwa wa kuzodoa wenzie Ben Tunituni Makapi alikuwa na harambee ya kuchangia kampuni yake iitwayo Makapi Foundation. Kwa vile huyu bwana aliwahi kuwika kuliko hata jogoo kiasi cha kuogopewa akiwa kwenye ulaji–kabla ya kugeuka zilipendwa hasa alipobainika kufanyia biashara patakatifu pa patakatifu–wanakijiwe walipenda kwenda kumdeku alivyo mpole na tegemezi sasa.
            Kapende ndiye anayeanzisha mada, “Nadhani wote mnajua kuwa kesho ni siku ya harambee ya kunchangia Mr Ben na kampuni yake ya Makapi Foundation.”
            Kabla ya kuendelea, Mijjinga anauliza, “Sisi ulaji na biashara ya wanene tena waliotuchuuza kwa wachukuaji waliowapa jina zuri la wawekaji vinatuhusu nini?”
            Kabla ya kuendelea Mipawa anakatua mic, “Mie inanihusu sana hasa nikikumbuka nyodo za jamaa. Mie nitakwenda–licha ya kutoa mchango wa kahawa–kuona jamaa alivyolainika kiasi cha kutegemea magacholi na wengeni wenye kutia shaka kumchangia kile ambacho hakupaswa kuomba kwa vile alikuwa akikimilki. Ama kweli cheo ni dhamana,” anamalizia huku akiangua kicheko.
            Mgosi Machungi anakamua mic, “Hawa anaochangia njuuku huyu jamaa mwenye nazo wamekosa pa kuziweka. Huenda kuna kitu wananunua. Kama anataka njuuku si angeenda kwenye benki na kuchukua kwenye akaunti ya Kiwia Coaa mine na kuchota atakavyo?”
            Mheshimiwa Bwege anaramba mic, “Usinikumbushe Kiwila na uwekezaji wa kijambazi ndugu yangu. Nadhani jamaa anatukoga. Ana shida gani ya njuluku wakati akienda pale MM bank anachota njuluku toka kwenye akaunti ya Fursa Sawa kwa Yote? Ama kweli waroho hawatosheki. Pamoja na kufanya biashara akiwa kukuu yeye na nkewe, vigegemezi na vivyele bado anaendelea na biashara hata ya kubomu! Ajabu, wakati Makondakonda akiwafukuza ombaomba wa mitaani, anawagwaya hawa wanene wa maofisini. Hivi harambee siyo uombaomba hata kama unafanywa na wanene?”
            Kabla ya mheshimiwa Bwege kuendelea, Mbwamwitu anamchomeka, “Mmesahau kuwa jamaa alitubinafsisha na akajibinafsisha mwenyewe? Huoni anavyochangiwa na wale aliotubinafsisha kwao asijue naye amajibinafsisha?”
            Msomi Mkatatamaa anaamua kutia guu, “Najua wengi wanashangaa ni kwanini kuhudhuria changishafedha ya mjivuni. Mie naliangalia hili tofauti. Lazima twende kujenga urafiki na kujua jinsi mambo yanavyokwenda halafu tumripoti kwa Dokta Kanywaji atumbuliwe jipu. Bila kwenda pale kuona nani ametoa nini na kiasi gani kujua kama analipa au kukwepa kodi au kushiriki kwenye kashfa na ufisadi mwingine, hatuwezi kuwajua na kuwashughulikia. Lazima twenda pale na kujua ni wafanyabiashara wangapi wanamfadhili ili tujue kama wana udhu au la.”
            Kabla ya kuendelea, Mpemba anakula mic, “Yakhe hapa wanstua kweli. Lazima nienda jua kama hii kampuni yajamaa yafanyiwa ukaguzi wa mahesabu. Pia nitataka kujua kama ile ya nkewe ya Fursa sawa kwa wote kama nayo yakaguliwa ati. Hapa lazima twende jifunza yale tusojua ili tuyajuapo tuyafanzie kazi ya kutumbua majiipu.”
            Kanji aliyekuwa akiangalia tu anakula mic, “Mimi ona wile hii kitu juri sana. Kama kuba nastaafu nanza biasara na nasaidia sikini iko jambo juri sana. Pia napata fursa juana na fanyabiashara ile nasaidia vakati iko darakani nayo isaidie yeye na yeye isaidie vananchi.”
            Sofia Lion aka Kanungaembe hakubaliani na mshikaji wake Kanji. Anakula mic, “Nadhani mnene yeyote akitaka kuwasaidia wananchi aanzishe sera nzuri na si za kuwachuuza halafu anakuja kuunda kampuni ya ulaji binafsi kwa kisingizio cha kuwasaidia. Kama alishindwa kuwasaidia alipokuwa anaongoza lisirikali ataweza kwa vijisenti hivi vya kusimangiwa anavyopewa na wanaomsanifu au uvuvi wa kufikiri?”
            Maneno ya Sofi yanamkuna Msomi kiasi cha kumuangalia kwa mshangao huku akimpoka mic, “Da Sofi siku hizi umegeuka mwanamapinduzi wa kupigiwa mfano. Kwa mtu aliyekusikiliza miaka iliyopita akaondoka, akishiriki vikao leo anaweza kushangaa kuwa huyu anayeongea huenda ni pacha wako. Usemayo ni kweli. Kama gendaeka alishindwa kuwasaidia hao anaodai anataka kuwasaidia leo amepata wapi huo upendo kama siyo kuwatumia kutafutia ulaji kama alivyokuwa akifanya bi mkubwa wake na yule wa mrithi wake? Nadhani tungefanya kila iwezekanavyo tumfikishie taarifa Dokta Kanywaji ili aamuru makampuni uchwara kama haya yakaguriwe na kutumbuliwa. Hamkuona alivyomkataza bi mkubwa kufanya biashara hii ya NGO?”
Mijjinga naye anaamua kurejea, “Nadhani tukubaliane. Jamaa baada ya kuachia ulaji, ameamua kujifunza toka kwa wenzake wa kaya zilizoendelea ambao huanzisha Foundations ili kuendelea kuwatumika umma. Hata hivyo, alishahau kitu kimoja muhimu kuwa wenzake hufanya hivyo kuendeleza mazuri waliyofanya tofauti na hawa wetu wanaotafuta sehemu ya kuendelea kulia na kupatia umaarufu. Kusema ukweli sioni cha mno wala cha maana Dungong Ben anacho kwa walevi ambao–kama wengi walivyokwishasema–aliwachuuza tokana na ujinga na uvivu wake wa kufikiria hadi kumpa ujiko Dokta Kanywaji. Hivi mzee Ruxa, Ben na Jake wangefanya vizuri unadhani Dokta Kanywaji angekuwa big deal kama alivyo sasa? Naona tukubaliane. Twende kule kumzomea hakuna cha nini wala nini na kumwambia dogo Makondakonda naye amtimue au vipi? Lazima tukate mzizi wa fitina. Umeona ambavyo Dokta Kanywaji wala hakuhangaika kwenda kule?
            Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shumbwengu la Ben. Acha tulikimbize ili kulimwagia kahawa ya moto!
Chanzo: Tanzania Daima.

Tuesday, 19 April 2016

Tanzania haipaswi kuwa ombaomba


            Akiongea kwenye ibada ya pasaka, rais John Pombe Magufuli aliwataka watanzania kuchapa kazi ili Tanzania iweze kuondokana na uombaomba na utegemezi wa makombo ya misaada toka ughaibuni. Na kweli, siku chache baada ya rais Magufuli kuyasema  haya Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ilitangaza kusitisha msaada wa dola za kimarekeni milioni 700 tokana na kutoridhishwa na uchakachuaji uliotokea Visiwani kwenye uchaguzi uliobatilishwa mwishoni mwa mwaka jana bila sababu. Hata hivyo, ni bahati mbaya kuwa taifa letu–ukiondoa serikali ya awamu ya kwanza–limekuwa ikitawaliwa na viongozi wenye mawazo tegemezi na mafisadi kiasi cha kutegemea kuombaomba bila hata kuona aibu. Wazo la kujitegemea ni la kimapinduzi kama litafanyiwa kazi na pia kujitegemea huku kutalenga kutenda haki na si kufanya madudu kama ya Visiwani. Inatia aibu kuona kiongozi wa nchi kwenda kwa viongozi  wenzake wa nchi nyingine kujidhalilisha kana kwamba hana ubongo na anaongoza watu wasio na ubongo wala mikono. Ni aibu hasa kiongozi anayefanya hivyo anapokwenda kule akidai anaongoza taifa huru lakini lisiloweza kujitegemea hata baada ya kuwa huru kwa miongo zaidi ya mitano. Taifa ombaomba si huru. Taifa tegemezi si huru. Kwani wanaolifadhili ndiyo wanaoliwatawala kwa mlango wa nyuma kama ilivyo kwa mataifa mengi ya kiafrika ambayo yamekalia raslimali lukuki lakini watawala wake wakazivuja na kwenda kuomba bila hata chembe ya aibu. Tunampongeza na kumshajihisha Magufuli alifanyie kazi hili kwa vitendo na haraka sana ili taifa letu liweze angalau kuwa huru.

            Haiwezekani nchi iliyojaliwa raslimali kama vile ardhi nzuri yenye rutuba na madini kila aina, bahari, mito maziwa, mbuga za wanyama wa aina mbali mbali na watu kuendelea kuishi kwa kujidhalilisha ikiombaomba. Kuendelea kuomba –hata kama hili laweza kuonekana kuwa tusi –ni ushahidi kuwa ima tuna matatizo ya kiakili, na kama siyo sisi bali wale wanaotutawala wawe ni wafadhili au wafadhiliwa.  Ili kuweza kujitegemea, tunahitaji kufanya yafuatayo:

            Mosi, tuwe na uongozi na usimamizi bora wa raslimali zetu. Hapa lazima tupambane na maadui kama vile ukwepaji kodi, uvivu, misamaha ya kodi, uwekezaji wa kijinga na kifisadi na pia matumizi mabaya ya raslimali zetu.

            Pili, lazima tujenge utamaduni wa uwajibikaji unaoandamana na uchapakazi wa kweli na si kwa viongozi tu bali watanzania wote kwa ujumla wao. Mfano, watanzania wanapaswa kujua kuwa wana mchango mkubwa katika ubomoaji wa taifa letu. Kadhalika, wana mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa letu. Wapo wenzetu wanaowasaidia wageni kuibia taifa letu kwa kupewa vijisenti kidogo wakati wageni hawa wezi wakiondoka na mabilioni ya shilingi. Rejea utoroshaji wa wanyama, madini na raslimali nyingine. Hawa wanapaswa kukamatwa na kunyongwa ili kuwa onyo kwa wote wanaodhani Tanzania ni shamba la bibi.

            Tatu, lazima kuwepo na mfumo unaosimamia na kutekeleza nidhamu ya matumizi ya mapato na fedha ya umma tena wenye uwazi na ukweli.

Nne, lazima tuwe na mfumo wa sheria zenye kusimamia uwekezaji ambao utasaidia kupambana na kuwashughulikia wale watakaokwenda kinyume na dhana nzima ya uwajibikaji na matumizi bora ya mali za umma. Mfano, sheria itamke wazi wazi kuwa atakayeshindwa kuelezea namna alivyochuma mali zake, atafikishwa mahakamani na mali husika zitatwaliwa na serikali. Pia sheria hii itasaidia kurejea mikataba ya kijambazi na kipumbavu tawala zilizopita zilizoingia kwa sababu ya maslahi ya watu wapumbavu, vipofu na waroho wachache. Ni bahati mbaya kuwa tangu aingie madarakani na kuanza mapambano dhidi ya ufisadi, rais Magufuli hajagusia namna atakavyofumua mikataba hii ambayo imegeuka mashimo makubwa ya kuzamisha fedha za taifa. Wengi wangependa kusikia mikakati yake juu ya kupambana na kadhia hii ambayo watangulizi wake waliogopa kutokana na kufaidika nayo.

Tano, bila kuwa Katiba mpya yenye kuanisha wajibu na haki za watanzania, tutakuwa tunatwanaga maji kwenye kinu. Mfano, unapokuwa na rais ambaye yuko juu ya sheria, ataweza kuitumia nafasi hii kujitajirisha na kufanya atakavyo kwa vile hakuna anachochelea. Tawala zilizopita zimetupa somo kuwa rais anapokuwa juu ya sheria inakuwa rahisi kwa waliomzunguka kuyatumia madaraka yake vibaya kuwaibia wananchi huku wakijitajirisha na wananchi wakiendelea kuwa maskini bila sababu. Uzoefu wa kashfa kama Kiwira na EPA unapaswa utupe somo kubwa juu ya namna madaraka ya rais yanavyoweza kufujwa na wahalifu waliofanya hivyo wakaepa mkono wa sheria kutokana na rais kuwa juu ya sheria. Hata hii kadhia ya ukwepaji kodi, ufisadi na misamaha ya kodi imechangiwa kikubwa na hali ya rais kuwa juu ya sheria.

 Sita, ili kufanikisha yote hapo juu, lazima–kama taifa na jamii ya watu wanaojua wanachofanya–turejeshe maadili ya utumishi wa umma na ikiwezekana kwa watanzania wote kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya kwanza. Kila mtanzania ajaze ripoti ya mwaka ya mapato na matumizi yake, kutangaza mali zake na kutoa maelezo ya namna alivyozichuma ili kubaini kama ni kwa kufuata sheria au kifisadi.

Tumalizie kwa kumsisitizia rais na serikali yake wajenge mfumo wa kitaasisi utakaoliwezesha taifa kujiondoa kwenye aibu na kadhia ya uombaomba usio na ulazima. Watanzania lazima tujisute na kuonea aibu kadhia ya kuishi kwa makombo kama mbwa.
Chanzo: Mwanahalisi.

Monday, 18 April 2016

Hii ni kwa watani wangu wahehe tu


Akina Kilango wasipangiwe kazi nyingine


            Hivi karibuni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, John Pombe Magufuli, aliwaacha wengi hoi pale alipomtumbua jipu aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anna Kilango Malecela baada ya kumpelekea taarifa zisizo za kweli. Bila kusita wala kuficha, rais aliamua kutengua uteuzi wake jambo ambalo limewafurahisha wengi licha ya kuwa onyo kwa wengine. Wengi walishangaa; hasa ikizingatiwa kuwa Malecela alikuwa ana siku 30 tu kwenye nafasi hiyo. Kitendo hiki–licha ya kumstua mhanga–kitakuwa kiliwastua wengi na kuwa kama onyo kuwa hapa hakuna mchezo unapovurunda. Nashauri rais akaze Kamba na kumulika si kuhusu wafanyakazi hewa bali masuala mengine kama vile usafi, uchapakazi, ufuataji sheria (maana tangu aanze kung’ata, mawaziri wake wamekuwa wakifanya kazi ya zimamoto ili kumfurahisha badala ya kufuata sheria) uadilifu, ufanisi na mengine mengi yanayoendana na uongozi. Namshauri rais ajenge uongozi badala ya utawala. Maana wakuu wengi wa mikoa na wilaya walikuwa wanajiona kuwa watawala zaidi ya viongozi wakati jukumu lao ni kuongoza na si kutawala. Wapo waliofikia kujiona ni marais kwa vile wameteuliwa na rais. Ukale huu unapaswa kukomeshwa. Hapa ndipo mtihani kwa rais Magufuli uliopo. Kwani mara nyingi, amekuwa akisisitiza umuhimu na ulazima wa kuwatumikia wananchi na siyo kuwatumia kama ilivyokuwa imezoeleka wakati wa utawala wa kiza uliofikia hata kufuta magazeti yaliyouambia ukweli.
            Hata hivyo, tuseme wazi; pamoja na rais kufanya maamuzi mazuri na haraka na kwa wakati, ametuacha hoi kiasi cha kuhisi kama anajipinga kama siyo kuanza kutuchanganya na kujichanganya. Kwani, akitengua uteuzi wake, alikaririwa akisema kuwa Malecela atapangiwa kazi nyingine! Kazi gani nyingine na ipi wakati ameishavuruga wazi tena ndani ya muda mfupi? Anampangia kazi nyingine ili aende huko nako kuvurunda akitaraji kupangiwa kazi nyingine? Kuendelea kuwapangia kazi nyingine wavurundaji baada ya kuvurunda nyingine ni kuotesha majipu mapya tena sugu ambayo yatalisumbua taifa. Mbona wezi wa bandarini hawakupangiwa kazi nyingine zaidi ya kufikisha mahakamani. Hata kumpelekea taarifa za uongo rais ni kosa la jinai. Kwani, kufanya hivyo, kunaweza kuvuruga mipango ya taifa na kusababisha hasara na usumbufu kwa wananchi. Kosa jingine walilotenda akina Kilango ni kutaka kubariki wizi wa fedha za umma kwa kuficha wafanyakazi hewa. Ina maana rais asingestuka na kutuma wachunguzi wake, wafanyakazi misukule waliokuwa wamefichwa na akina Kilango wangeendelea kulipwa mishahara kinyume cha sheria jambo ambalo ni wizi tu wa kawaida.
             Hoja nyingine ni kwamba kama rais alikuwa na haja ya kuendelea kumwajiri au kumteua mhusika basi angempa onyo kuliko kumfukuza kwa mkono wa kulia na kumrejesha kwa mkono wa kushoto. Huku ni kujipiga mtama kiutawala. Tanzania si maskini wa nguvu kazi. Wapo wenge walio tayari na wanaoweza kuchukua nafasi hiyo na hiyo nyingine anayotaka kupewa mtu aliyefeli wazi. Kwani, lazima yeye? Kupangiana kazi nyingine kunatokana na tabia chafu za kikale ya kuhamisha watu wanapovuruga sehemu itamgharimu rais; na itamwonyesha kama mwenye hangover ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo kimsingi, ndilo chimbuko la uoza na ufisadi vinavyomsumbua rais. Tanzania ina watu wengi wasio na kazi tena wenye taaluma na uzoefu tu ambao hawatokani na familia za kikubwa au vigogo wa chama. Hivyo, tungeshauri akina Malecela waachwe nje wakaonje joto ya jiwe ili liwe somo kwa wengine. Kwanini mtu ahangaike wakati akijua kuwa akivuruga atapangiwa kazi nyingine?  Mbona baadhi ya wabovu waliotimliwa Ikulu hata kabla ya rais kuingia hawakupangiwa kazi au kuna watu na viatu?
            Tumhamasishe rais abadili kila kitu hasa mfumo na utaratibu wa kizamani. Mambo ya kupangiana kazi nyingine ni ya kizamani. Kufanya hivyo ni kujichanganya na kujidanganya. Unaweza kuwaonea huruma baadhi ya watu chini ya mashikamano ya chama au ukaribu.  Mwisho wa siku, watakuangusha na kukuacha ukisononeka kwa aibu. Tanzania ni kubwa. Pia ina watu wengi tena wenye sifa kedekede. Kama msumemo kata mbele na nyuma bila kujali nani ataumia kama astahili.  Haki ni haki daima; huvunja hata milima. Lazima tufike mahali tukubali kubadilika kabla hatujabadilishwa na mahitajio ya wakati. Kwa wanaojua maana ya demokrasia na uongozi unaotegemea utashi wa watawaliwa, Malecela hakupaswa kufikiriwa kuteuliwa; achilia mbali kuteuliwa. Je wako wangapi kwenye wateule wa Magufuli walioshindwa kwenye kura za maoni lakini wakazawadiwa vyeo kama sehemu ya kupeana ulaji? Je hili si jipu tena sugu na linalonuka? Tafadhali rais Magufuli, usigeuke nyuma ukageuka jiwe–tena jiwe lenyewe la chumvi–kama mke wa Luti. Tufikie mahali tuweke uzalendo mbele tukijua na kuamini kuwa Tanzania ni zaidi ya kundi dogo la watu wanaojuana, kulindana na kufadhiliana.
              Hata kwa Malecela kuteuliwa ilikuwa ni makosa ingawa hatulengi kukosoa mamlaka ya rais kufanya hivyo. Kwanini kuteua watu walioshindwa kwenye kura za maoni jambo ambalo linaonyesha ni namna gani umma–tena wa watu wa kwao–uliwakataa baada ya kushindwa kuhudumia vilivyo kwenye vipindi vyao vya ubunge?
            Tufunge hoja kwa kumtaka rais asiposimbuke na kondoo mmoja aliyejipoteza wakati kuna kondoo wengi wasio na hatia.
Chanzo:Mwanahalisi

Wageni wanaokwepa kodi wafukuzwe nchini


Unaweza kusema Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Pamoja na kugeuzwa–hata kuitwa shamba la bibi–bado inaendelea kuvumilia uhujumu uchumi wa ajabu huku watu wake wakiendelea kuwa maskini. Taarifa za wageni kukwepa kodi hata kutorosha fedha na nyara za taifa zinaanza kuzoeleka. Ndani ya mwaka mmoja, yameripotiwa matukio ya wafanyabiashara wa kichina ima kutorosha fedha, kukwepa kodi au kutoa Ankara zenye kuonyesha fedha pungufu tofauti na waliyopokea. Inashangaza sana jinsi watuhumiwa wanavyoendekezwa. Kosa la kukwepa kodi ni kubwa hata katika mataifa tunayoona yameendelea ambayo ustawi wake umetokana na kukusanya mapato na kuadhibu vikali wanaokwepa kodi.
Nchi za magharibi zina makosa makubwa ambayo mtu akiyatenda anapoteza haki ya kugombea uongozi. Mojawapo ya makosa haya ni kukwepa kulipa kodi, kuficha mapato, kushindwa kutangaza mapato, ushiriki ugaidi na mengine mengi. Haya ni makosa yasiyo na mjadala wala msamaha anapoyatenda mtu. Kinachoshangaza, inakuwaje Tanzania haiigi mfano toka nchi hizi ambazo nyingi huifadhili. Haiwezekani taifa likaruhusu wamachinga toka nje kuja kufanya biashara na shughuli ambazo watu wetu wanaweza kuzifanya. Kuendelea na mchezo huu–licha ya kuwa motisha kwa wageni wahalifu kujazana nchini–ni ushahidi kuwa hatuko makini. Hata hawa wanufaika wa upungufu huu licha ya kutuibia, wanatudharau na kutuona kama hamnazo. Mswahili akikwepa kulipa kodi, kutorosha fedha au nyara huko uchina, atafia gerezani kama siyo kunyongwa. Kama taifa–tufikie mahali–tufanye vitu kama watu wenye akili na si mataahira na wapumbavu wasio na akili wala wasioweza kujifunza toka kwa wengine. Hivi inahitaji shahada ya sheria au biashara kujua kuwa wageni hawapaswi kufanya shughuli au biashara zinazopaswa kufanywa na wazawa? Je hili nalo linangoja wafadhili walisemee ndipo tustuke na kuchukua hatua? Si uzushi. Ongezeko la wamachinga toka nje hasa Uchina, Uturuki na India ni ushahidi kuwa mfumo wetu ni wa hovyo na wa kijinga unaopaswa kubadilishwa haraka. Tunatoa changamoto kwa rais John Magufuli kuliangalia hii kwa upana na makini sana ili kuepuka kuendelea kuwa maskini kwa kujitakia kutokana na mfumo na sheria mbovu. Pia kuna haja ya kuwalaumu wananchi wetu wanaoshirikiana na wageni kuibia taifa lao halafu hili likishatokea hao hao wanaanza kulalamika wakati nao ni sehemu ya jinai hata kama si wote.
Kwa vile wageni si watu wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi, adhabu inayowatosha na kuwafaa ni kuwatoza faini kubwa, kutaifisha mali zao na kuwafunga kisha kuwafukuza nchini. Pia serikali isimamie sheria zinazotamka wazi uwekezaji ni nini badala ya kuwaacha wageni kuja kuchukua kazi zetu huku watu wetu–hasa vijana–wakiendelea kusota kwa kukosa kazi na kipato. Sijui kama machinga wetu wanaweza kwenda Uchina na kufanya shughuli za kimachinga na mamlaka za kule zikawanyamazia tu.
Wakati wa Tanzania kugeuzwa shamba la bibi au kichwa cha mwendawazimu umekwisha. Watanzania lazima tustuke na kuamka na kuacha kushirikiana na wageni eti kwa vile wanatuhonga mabaki ya chumo la wizi wanalotuibia. Unashangaa namna wageni wanavyokuja nchini–wengine hata kinyume cha sheria–na kupangishwa nyumba, kupewa leseni za kufanya biashara ya kimachinga. Unashangaa zaidi kuona wizara ya Mambo ya Ndani ikiendelea kuwatumia polisi wake kuwasumbua wananchi wakati wageni na wakimbizi haramu wa kiuchumi wakizagaa nchini. Lazima tuwe makini kwa kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na kitambulisho cha uraia, anwani ya kudumu na kuhakikisha mfumo wetu unakuwa wa kompyuta ambapo kila mtu atakuwa na namba maalumu ya utambulisho yaani Social Insurance Number (SIN) au namba yoyote itakayoamriwa na mamlaka ili kuwatambua na kuwahudumia watu wake. Nikitolea mfano hapa Kanada, huwa serikali haitumii fedha nyingi kulinda mipaka yake. Badala yake, serikali ya hapa imetoa namba kwa raia na wakazi wa hapa na kuziweka kwenye mtandao wa kompyuta. Kila unapokuwa nchini Kanada, ukitaka kupata huduma kama ya kupanga nyumba, kupata leseni ya udereva, kujiandikisha au kuandikisha mwanao shuleni, kupewa huduma hospitali, huwa unaulizwa namba yako na hadhi yako ya kuwa Kanada. Bila kuwa na namba ya utambulisho–licha ya kutoweza kupata taarifa–utalipotiwa polisi na kuchukuliwa hatua mara moja. Sisi tunashindwa nini kuiga hili. Ajabu, badala yake watu wetu wanaigizi mambo ya kipuuzi kama kutoga masikio, kuvaa milegezo na upuuzi mwingine. Wakanada hawamwamini yoyote hasa mgeni; na huwezi kuishi hapa au kufanya biashara au shughuli yoyote chini ya meza. Mfumo huu–licha ya kuhakikisha usalama wa nchi–unasaidia kupunguza kutumia fedha nyingi mipakani ukiachia mbali kukatisha tamaa wageni kuingia nchini.
Bila kubadili sheria na mfumo wetu, tutaibiwa sana hasa wakati huu wa utandawazi na kukua kwa teknolojia ambayo wahalifu huitumia kufanya uhalifu.
Tumalizie kwa kuitaka serikali ibadili na kutunga sheria zenye mashiko na meno ili kupambana na wakimbizi wa kiuchumi wanaoibia taifa letu huku watu wetu wakiendelea kuwa maskini bila sababu za msingi.
Chanzo: Tanzania Daima, Aprili 17, 2016.