How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday, 9 April 2016

Mlevi: Itungwe sheria ya kunyonga mafisadi

             Baada ya wale ambao hukuwatarajia kutumbuliwa tena uchi na wengine kulala lupango, Mlevi nina mpango wa ima kwenda mjengoni au kwa Dokta Joni Kanywaji Makufuli kuwachomea utambi ili itunge sheria kali dhdi ya wanaoiba mabilioni. Nitapendekeza wanyotolewe roho hadi kudedi kabisa kabisa.
            Hapa sitasikia stori za haki za binadamu. Kwani washenzi hawa  wameua wangapi kwa ukapa wa kutengenezwa? Hivi kweli hawa nao wanahitaji kufaidi haki za bindamu wakati matendo yao si ya kibinadamu?
            Leo mnawapeleka lupango wakiwa nan doo zilizojaa kila kitu ili iweje? Hawa hawastahili kufungwa bali kunyotolewa roho kabisa. Tunawafunga kwa faida ipi huku wakilala white house na kula bure baada ya kutembeza nchiko? Kwani hatujui kuwa wanene wakifungwa wanaishi kama vile wako uraiani? Muulize yule jambazi wa benki
            Nilipokuwa uchina kwa rafikiyangu Kil ua Them nilishuhudia vigogo wengi wakitwangwa shaba bila huruma na hakuna aliyesikiliza upuuzi unaoitwa haki za binadamu. Anayefanya unyama kama uhujumu anakoma kuwa binadamu. Hivyo, hasatahiki haki za binadamu. Ingekuwa inawezekana ningependekeza wote waliokwisha kufikishwa kwa pilato achukue maji anawe mikono yake na kuwaambia,”Damu yenu sidaiwe ila msulubiwe na iwe hivyo.”
            Majizi yote yaliyohujumu kaya kutokana na kuwa wake, wakwe, watoto, marafiki au mashemeji wa wakubwa lazima yanyongwe. Kama siyo kulindana na kuogopana chini ya dhana ya kuanza upya, hata haya MaWAMA, ma-Fursa Sawa kwa Walaji yalipaswa kufumuliwa na majambazi yaliyoko nyuma yake yakanyongwa au kufungwa maisha bila kumuangalia nyani usoni. Kwani hatuyajui wala kuyaona majambazi ya kiume na kike yaliyofilisi kaya yetu kutokana na kuwa na uhusiano na wanene? Nani hajui kuwa bi wakubwa wawili waliotangulia walikwapua kwa kutumia vishirika uchwara na vya kiwizi? Bring them to book Dr Mugful please before I commit suicide.
            Ni vitegemezi vingapi vya wanene vimepewa vyeo si kwa sababu vina sifa za ziada zaidi ya majina ya madingi yake? Ni vitegemezi vingapi vya wanene sasa ni vihishimiwa hata vimilionea wizi kwa vile ni vitegemezi vya wanene? Kwani hatuvijui wala havijijui? Nilipokuwa Uchina nilimshuhudia mnyongaji aitwaye Fire nyong Yote akiwanyotoa roho mafisadi wanene wanene wa kichinaizi bila kujali vyeo au majina yao au ya madingi wao. Mna habari kuwa hata bi mkubwa wa Mkiti Mao Zedong aliwahi kuhukumiwa kifo baada ya kugundulika kuwa alitumia madaraka ya mwenyekiti Mao vibaya? Sasa kama bi Mao mzima anahukumiwa kunyotolewa roho, hawa wetu vinuka mavi ni nani?
            Leo hii mijizi kama Has Kitne, Haoi Msumari au Chose Sunare yangekuwa yameishaoza kama ingekuwa uchainizi. Kule wasingejali kuwa mengine ni makwe ya wanene au mashoga wa wake wa wanene au mashemeji wa wanene. Hata yale majambazi manene ya EPA, Kagoda, Kiwira na mikashfa mingine bila kusahau Escrew yangekwisha nyongwa na kuzikwa kwenye makaburi yasiyo na alama kama Gaddafi. Unacheza na wachainizi nini? Hata hawa wahalifu wa kichainizi wanaotorosha vipusa vyetu ingekuwa kwao wasingefungwa zaidi ya kunyongwa ili kutoa somo kwa wanaodhani Uchaina ni shamba la bibi au kichwa cha chizi kujifunzia kunyoa. Wala Uchainizi siyo the land of Vasco da Gama au No-Man’s land ya akina Ben Tunituni Dugong Makapi na wezi wenzake walioleta wachukuaji wakawapa jina zuri la wawekaji wakati walikuwa wanaweka wanachukua waa.
            Tuache utani. Naandika waraka huu kwa wahishimiwa kuwa watunge sheria ya kunyonga mafisadi hata kama mafisadi hao ni wenzao wanaodai uchache kwa makampuni ili kupitisha mazabe na madudu yao. Akina Rich Ndassi wananipata bila shaka hapa.
Kama waishiwa watakaidi agizo langu basi nitawahamasisha walevi wavamie mjengo na michupa yao na ulabu watembeze–wewe! Shika adabu yako! Hayo tuyaache. Nitawahamasisha walevi wavamie mjengo wakiwa uchi ili kuwamwagia radhi watakaokataa kupitisha sheria ya kuwanyonga wabaya wao.
Najua wapo waishiwa watakaoogopa kupitisha sheria hii kwa kuogopa wenzao au wao kunyotolewa roho. Hivi miishiwa inayoomba mshiko kwenye sirikali za wilaya si ya kunyotolewa roho hii? Lione lile linasoma na kunisonya wakati limenenepeshwa na njuluku za rushwa. Kwani hatuyajui maishiwa yanayokwenda mjengoni kuwakilisha mitumbo ya kwa kisingizio cha kuwakilisha walevi?
            Tokana maishiwa yanayokula rushwa kama yalivyokwisha kuanza kutumbuliwa, Mlevi ana mpango wa kutangaza walificha njuluku nje. Hii ni baada ya wezi wetu na ndugu zao kutoonekana kwenye karatasi zilizovujishwa hivi karibuni kuhusiana na maficho ya njuluku kule Panama. Panama wamenusurika; Bahamas, Dubai, Switzerland, Isle of Man, Cayman na kwingineko hatapona. Hivyo, asije fisadi akakudanganya kuwa yu safi kwa vile jina lake, mkewe, kitegemezi au mramba makalio wake hajatajwa. Wanazo njuluku nje hata hapa hapa Afrika. Ukienda pale Mauritius utagundua utajiri wa kijambazi wa ajabu uliofichwa kule na mafwisadi wetu wanaojifanya kujionyesha kama watu wema wakati wengi wao ni mijambazi ya kutupwa.  I know them; and one day I’ll name and shame them. Believe ye me.
            Leo sichongi sana. Ngoja niwahi kwenda kuandaa orodha ya majambazi tena wakubwa wakubwa ambayo ukiisoma hutaamini macho yako.
Chanzo: Nipashe, Aprili 9, 2016.

No comments: