The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Tuesday, 11 June 2013

Jeshi linaendelea kuiteka na kuitawala Tanzania

Habari kuwa aliyekuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  Ret. Leut. Gen Abdulrahaman Shimbo (anayekula kiapo kulia pichani) ameteuliwa balozi wa Tanzania nchini China ni matusi ya nguoni. Kumbe Shimbo alipokuwa akiitishia CHADEMA alikuwa akitumikia chama chake! Ni utapeli kiasi gani wakuu wa majeshi kuwa makada wa CCM? Hii si mara ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi za juu wa jeshi kuonyesha kuwa kada wa CCM. Alianza mkuu wa majeshi mstaafu aliyekuwa na kashfa nyingi za ufisadi Gen. Robert Mboma alipotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM wananchi wakambwaga. Alifuatia IGP mstaafu Omar Mahita ambaye kashfa ya kuzaa na mtumishi wa ndani ilimwacho hoi kisiasa. Sasa kuteliwa kwa Shimbo ni ushahidi kuwa Tanzania inatawaliwa kijeshi kichinichini. Ushahidi zaidi ni kujazana kwa wanajeshi kwenye nyadhifa tata za wakuu wa wilaya na mikoa na sasa kwenye balozi zetu. Hakika huu licha ya kuwa uzembe na uhovyo wa Kikwete ni ufisadi wa kimfumo. Ama kweli akutukanaye hakuchagulii tusi. Tunalaani mchezo huu mchafu wa kujuana kulindana na kufadhiliana kwa kodi za wananchi.

Monday, 10 June 2013

Rwanda wamefikia hapa?

photo
Tanzania inaanza kuonja joto ya jiwe kwa kimbelembele chake. Hivi karibuni rais Jakaya Kikwete alipayuka kuwa imla wa Rwanda Paul Kagame ajadiliane na waasi wa FDLR walioko kwenye misitu ya DRC. Rwanda kwa kutumia vyombo vyake vya habari hasa gazeti la New Times wameamua kumvua nguo Kikwete. Hiyo katuni ni ushahidi mmojawapo. Kwa wanaojua jinsi Tanzania ilivyochangia kuwaingiza akina Yoweri Museveni na Kagame madarakani wanashangaa kutenzwa hivi. Laiti Tanzania chini ya Ali Hassan Mwinyi wasingedanganywa na Museveni na kuruhusu ndege ya rais wa zamani wa Rwanda kutunguliwa tusingefikia hapa! Je Tanzania itajifunza au itaamua kuzifunza adabu tawala zilizotokana na kazi ya mikono yake? Tumefilisi nchi yetu tukimwonea Idd Amin  ili kumuingiza Museveni na baadaye kushiriki kwenye jinai ya Rwanda kwa kuruhusu mkutano wa Arusha wa 'Amani' ufanyike huku tukijua fika yatakayojiri na sasa tunalipwa hivi!
Ajabu wachovu kama hawa ndio wanaotushawishi eti tuungane nao kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki wakati wana matatizo mia kidogo! Hawana ardhi, hawana demokrasia wala subira wa nini hawa? Siku zote tunasema heri tuungane na Zambia kuliko vijiinchi visivyo na kichwa wala miguu.

Sunday, 9 June 2013

Kumbukumbu ya Vuyo Mokoena

Tuimbe pamoja
Vulek’a amazulu,
Iyez’i Ngonyama
Kwancibilik’izintaba
Kwasha nemimfula
Avulek’a amazulu,
Iyez’i Ngonyama
Kwancibilik’izintaba
Kwasha nemimfula
Lungis’indlela zakho,
Lungis’ukuhamba kwakho
Iyeza iyez’i
Ngonyama yamazulu
Lungis’indlela zakho,
Lungis’ukuhamba kwakho
Iyeza iyez’iNgonyama yamazulu
Avulek’a amazulu
Iyez’i Ngonyama
Kwancibilik’izintaba
Kwasha nemimfula
Avulek’a amazulu,
Iyez’i Ngonyama
Kwancibilik’izintaba
Kwasha nemimfula
Lungis’indlela zakho,
Lungis’ukuhamba kwakho
Iyeza iyez’iNgonyama yamazulu
Tafsiri.
Funguka enyi mbingu 
Yua aja Mfalme wa mbingu
Milima na mporomoke
Nanyi mito mkauke
Yuaja Yuaja 
Mfalme wa mbingu.
Yanyoshe mapito yako
Zinyoshe njia zako
Yu aja yu aja
Mfalme wa mbinguni


Kwa wiki mbili binafsi nimekuwa nikimkumbuka marehemu Vuyo Mokoena nguli wa muziki wa injili wa Afrika Kusini  aliyefariki Mei 28, 2008 baada ya kuugua leukemia. Leo tarehe nawakaribisha wapenzi na marafiki zake kumpa nafasi kwenye mioyo na maombi yenu.

Zimbabwe: Mugabe Gives a Shining Legacy

When Kenya fell in mayhem in 2007/2008 doomsayers said it’s the end. We still vividly remember how former president Mwai Kibaki, who, in a sense, is the cause of all this megalomania, was demonized as a power-hungry monster. Again, after realizing his faults, Kibaki turned things around by ushering in the New Constitution whose fruits are calmness and democracy in the country. What transpired in Kenya is history. However, Kenya’s tribulations ended up in the rebirth of a nation. 
Something similar to what transpired in Kenya did happen in Zimbabwe recently. Zimbabwe’s president Robert Mugabe, maybe, was more demonized than any current president in Africa. His unforgivable 'sin' was, and still is, the rectification of the economic imbalance in Zimbabwe. Bold as he always has been, Mugabe took on contentious issue of land. Since her independence in 1980 till up to when Mugabe decided to redistribute the land, many Zimbabweans lived like squatters in their own land. Knowing the price many Zimbabweans paid during Liberation Struggles, Mugabe stood firm to see to it that land issues are addressed once and for all. However, there were many shortfalls and outbursts towards this process that, for the first time in history, saw a president taking the burden of his people.
When Mugabe decided to take land from white settlers who got it illegally, and gave it to the Africans, he was branded a stinking racist. Again, was he? Mugabe’s bold step, just like Liberation struggles, had a price tag on it. Zimbabwe was subjected to economic sanctions which nearly brought the country to the status of a failure state. The aim was to instigate Zimbabweans to turn against Mugabe just like in Libya. Against all odds, it did not work. Again, Mugabe stood his ground to see to it that the interests of Zimbabweans were protected.
Things went from bad to worse. Once again, Mugabe shrugged everything off and went ahead to redistribute the land. His detractors backed by Zimbabwe’s former colonial master, Britain, took on Mugabe. They branded his land policy disastrous. Was it? Time will tell.
The recent re-writing and the signing of the New Constitution of Zimbabwe into law do comfortably empower me to give accolades to Mugabe. Indeed, those who painted Mugabe with the same brush branding him a stinking racist and dictator have nothing more to offer. Currently, Zimbabwe is back on the right track. The economy is tanking and chances are that soon Zimbabwe will regain her lost glory.  Looking at the look of things, I feel comfortable to congratulate and encourage Mugabe to do even more.  How the economy is doing can be reflected in the words of Finance Minister Tendai Biti who was quoted last year by the Voice of America as saying, “By the end of the year we would have reduced our primary balance to zero, in other words our books will balance and we are not going to carry a deficit in 2013.” Biti comes from the opposition. Thus, what he said should not be misconstrued as being political yada yada.
Another thing that proves Mugabe is going to leave a shining legacy is the fact that for the whole time he led a Government of National Unity, he tolerated and withstood all challenges resulting from it. Now that Zimbabwe has a New Constitution decided upon by Zimbabweans and signed into law, once again, Mugabe’s scored higher than anybody could bet. The other day I told a Canada-based Zimbabwean friend, professor  Eliachim Sibanda, that I was intending to write this piece. He encouraged me to write it.  We put our heads together. Our take is that Zimbabwe can benefit from the new constitution. We found that with a new constitution Zimbabwe assures the international community and Zimbabweans that soon she will conduct a free and fair election as it transpired in Kenya which by coincidence used to have the GNU like Zimbabwe.
Also, the new constitution entrenches liberties and rights to the people of Zimbabwe. If anything, nothing attracted me in the new constitution like chapter three which, under article 33: Duty to respect fundamental human rights, among other things stipulates as thus, “All persons, including juristic persons and all- organs and agencies of the State and Government, including local government, must respect, protect, promote and fulfill the rights and freedoms set out in this Chapter.”  What else do we want Mugabe to do? This means. Zimbabweans will have their voices been heard in every aspect and matter of their nation. It also will enable calm and peace to return so as to attract foreign investment back to Zimbabwe.
Interestingly, Mugabe’s bold take aims at empowering Zimbabweans by enabling them to enjoy and benefit from their resources. This is different from many African countries where incumbent leaders are throwing everything away to foreign investors for the fear of being demonized. The sage has it that the man is the one who stands alone. Mugabe has proved this to be very true to letters.

Like Kenya that recently evolved from ashes, Zimbabwe’ll soon be born again. This indicates that, like Kibaki, Mugabe will leave a very shinning legacy so to speak. He will go down history as the father of two constitutions in Zimbabwe. Let us encourage Mugabe to do more instead of frustrating and demonizing him. Well done Jongwe Bob!
Source:The African Executive Magazine June 5, 2013.

Hili bonge la pointi ingawa ni mkanganyiko!

Serikali mia marais elfu je hiyo pesa ya kuwalisha na kuwaendesha itatoka wapi?

Saturday, 8 June 2013

Sasa mlevi atangaza kugombea urais

Hii si fununu si umbea na udaku. Kwa vile katiba mpya imetangaza rasmi kutambua mgombea binafsi, mlevi sasa natimiza azma ya kugombea urais kuwakomboa walevi. Japo niliwahi kugusia kuwa nina mpango wa kugombea urais, sasa natangaza rasmi; kwenye uchaguzi ujao nitakuwamo kwenye sanduku la kura.
Juzi nililewa na kuvuta kama sina akili nzuri. Nilikesha nikisherehekea hatua hii adhimu ya kuwakomboa walevi toka kwenye mikono michafu ya mafwisadi na majambaziii.  Naona yule anasonya.  Mwingine anacheka utadhani utani. Kwa taarifa yenu, nitagombea urais tena wa muunganiko na si wa Danganyika. Nataka niwe top boss wa kaya hii ya walevi ili niwaonyesha wavivu wa kufikiri jinsi ya kuongoza na si kutawala.
Huna haja ya kucheka wala kushangaa mlevi kugombea. Kama inawezekana kwa mafisi na mafwisadi kugombea, nini tatizo mlevi kugombea huu ulaji wa dezo? Kwa taarifa yenu, nina sifa zote za kuwa rais. Kwanza, nina elimu ya kutosha. Nina shahada gunia za PhD tena si za heshima wala za kughushi kama akina Emmy Nchimvi, Bill Lukuvi, Marry Nagu, Makorongo Mahanga,Didass Makalio na wengine wengi walioogopa umande ima wakaishia kughushi.
Pia nina sura nzuri ya kuvutia wapika kura ya kula. Afya yangu ni fiti. Hata nikinywa, kubwia na kuvuta sianguki kwa vile niko gado kishenzi. Hivyo, kwa sifa za haraka haraka mie ndiye kidume pekee anayefaa kuwa rais wa kaya hii inayohitaji mkombozi ambaye imemngojea kwa miaka mingi. Mie ni yule aliyetabiriwa na manabii kama Mchonga huku nikapigwa vita na mashetani kama yule habithi Shehe Yaya.
Pia nina mitandao ya kutosha ambayo lazima iingie viwanjani na kunisakia kura kwa udi na uvumba. Sina haja kuiibia Banki Kubwa wala kujiingiza kwenye biashara ya Kikagoda wala kuwatoa kafara walevi kwa wachukuaji waitwao wawekezaji. Mie ni mzalendo wa kupigiwa mfano.
Ili kuwashawishi walevi wanipe kula, nina mpango wa kufanya yafuatayo.
Mosi, nitatangaza mali zangu za bi mkubwa na vitegemezi na marafiki zetu.
Pili, nitaarifu walevi kuwa nikiingia madarakani, nitapunguza baraza la mawaziri. Nina mpango wa kuwa na mawaziri 20 tu ambapo watapatikana kwa njia ya kuomba kuajiriwa na si kuteuana wala kulipana fadhila.
Tatu, nikiishaingia madarakani, nitafuta cheo cha First Lady. Hili nalo juzi lilitaka kuvunja ndoa yangu na bi Mkubwa. Nilimwambia fika kuwa nikiwa rais sitaki nisikie habari za NGO za uongo na ukweli wala yeye kwenda kushindania vyeo vya kichovu kwenye chama changu na Pilau Mahanjumati Ulabu na Pilau (MUP).
Juzi kulikuwa hakukariki nyumbani kwangu. Maana baada ya kumwambia bi mkubwa kuwa sina mpango wa kumruhusu aitumie ikulu kufanya biashara alitangaza mgomo wa kila kitu kuanzia jikoni hadi kwenye bedroom. Nilipomtaarifu yaliyowapata marais kama Lora Gbagbo ambaye ananyea debe na mkewe, alinielewa. Bila kumuelimisha nadhani angeanza kuhujumu harakati zangu ya kuwania ukuu. Maana, baada ya kusema wazi kuwa utawala wangu hautakuwa biashara ya familia kama wale, bi mkubwa na vitegemezi vyetu walianzisha kigwena kuhakikisha sipati ukuu. Baadaye niliwahakikishia kuwa serikali yangu haitakuwa family business wala ya ubia kwa vile ni hatari ikitokea ukaondoka madarakani.
Baada ya waambia vitegemezi vyangu yanayomkuta yule jamaa wa Masri Mubaraak Kibaraak na wanae walinielewa wakakubali kuwa lazima kila mtu ale jasho lake. Ili kumridhisha bi mkubwa, nilimwambia kuwa kama katiba mpya isingefuta ubunge msukule bin underwear aka viti maalumu,ningempachika pale.
Nne, ili kuhakikisha nashinda, nitaanza kutangaza sifa zangu kaya nzima. Nina mpango wa kupeleka picha zangu wa wataalamu wa picha ili wafanya photoshopping niweze kuonekana kijana kuliko nilivyo. Kuanzia juzi napaka  piko kuficha mvi. Pia naitwa mzee kijana. 
Tano, nitahamasisha walevi wote kaya nzima wanipigie kampeni ya baa kwa baa. Sitaruhusu upuuzi wa kitanda kwa kitanda ili wasiambukizane miwaya kama wale wachovu waliokuwa wakitumia kampeni hii ya kimalaya. Wala sitaruhusu mambo ya mafiga matatu maana asili yake nayo ni uchangu.
Kwa waliofuatilia mikakati yangu siku zilizopita wanakumbuka nilivyotangaza neema kwa waandishi wa habari. Nawashauri kuanzia sasa wanipigie kampeni nishinde kitsunami na kuondosha kadhia ya kutekwa na kunyofolewa kucha na kutobolewa macho. Nawashauri wanoe kalamu ila wasitegemee kuteuliwa ukuu wa wilaya na mkoa. Wanipigie kampeni wakijua kuwa nia yangu si kulipana fadhila bali kukomboa kaya toka kwenye mikono michafu. This time around the kaya won’t go to the dogs anymore. Believe ye me everybody.
Kwa wasiojua chama changu kitukufu ni kwamba sera yangu kuu ni kuhakikisha kila mtu anapata uwezo wa kuweka mahanjumati na pilau mezani huku akishushia na ulabu. Nani asiyependa ulabu iwapo tunaambiwa hata peponi utakuwapo? Kwanini tusianza kuuramba ulabu kabla ya hata ya kufariki na kuingia huko peponi? Kwa maana nyingine ni kwamba sera yangu ni kuwaingiza walevi peponi kabla ya kurejesha namba. Mnaonaje sera hii walengwa?
Tano, ili kupata kura ya kula, nina mkakati wa kufanya kile wazungu huita miracles. Nitawambia baadaye hiyo miujiza.
Sita, nitafutilia mbali mikoa na wilaya vilivyoanzishwa kisiasa na kutengenezeana ulaji kichovu na kifisadi.
Saba, nitahakikisha naweka sera ya kuzuia watumishi wa serikali kuwa na nyumba ndogo; zinamaliza pesa ya kaya bila sababu. Pia ni mwiko kwa mtu kuiba wala kuficha pesa nje ya kaya.
 Saba, ili kuepusha mzigo kwa walevi, sitakuwa nikifanya ziara ughaibuni mara kwa mara.
Nane, nitasafiri ughaibuni mara nne kwa mwaka.
Tisa, nitakuwa nikiandamana na watu wachache ambao majina yao hayatafanywa siri kama ilivyo.
Kumi, tumekubaliana na bi mkubwa kuwa hataruhusiwa kudandia safari zangu unless otherwise.
Kumi na moja nimemshauri bi mkubwa atumie muda wake mwingi kujitafutia elimu badala ya kufikiri juu ya NGO za kufanyia biashara ikulu. Maana elimu yake ni ya UPE na alikuwa mwalimu wa chekechea.
Kumi na mbili nawataarifu wapiga kura na mashabiki wangu kuwa sitajiingiza kwenye biashara yoyote. Sitanyakuwa kiwanda wala mgodi wala sihitaji kuwekewa kinga kwenye katiba.
Kumi na tatu, nitabadili katiba na kutamka wazi kuwa rais akiiba,kufanya biashara ikulu au kushiriki ufisadi anyongwe.
Kumi na nne, natangaza kuwa hata nitakapokuwa nikisafiri kwenda uwanja wa ndege au matembezini sitahitaji misiruru ya magari na wala body guards. Vya nini iwapo sina mpango wa kumuibia mtu wala kuridhi tabia za kikoloni kama wengine?
Kumi na tano, nina mipango gunia. Mengine nitawaeleza siku za baadaye.
Kumi na sita, nawashauri wote mniamini na kunipa kula ili mpate kula. Hata nikiwaingiza mkenge mvumilie na wala msilalamike.

Kumi na saba, kula la heri.
Chanzo: Nipashe Jumamosi Juni 8, 2013.

Tunamuombea Mandela aka Madiba (Diba) apone haraka

Nelson Mandela in June 2010
Taarifa za kulazwa tena kwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Nelson Mandela Madiba zimetustua hasa ikizingatiwa kuwa ni mwezi jana tu alipokuwa amelazwa kwa ugonjwa wa mapafu. Kwa umri wake lolote laweza kutokea. Hivyo blog hii inachukua fursa ya pekee kumuombea na kuwataka wengine wamuombee kipenzi chetu Mandela.
Mungu mponye Madiba wetu.
Amandla!

Tuesday, 4 June 2013


Kurejea kwa mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)  Absalom Kibanda ni faraja na furaha na habari njema kwa waandishi wa habari. Kibanda ambaye alitekwa na kuumizwa vibaya hadi kunyofolewa kucha na kutobolewa jicho alikuwa nchini Afrika Kusini akitibiwa tangu alipofanyiwa unyama Machi 5. Kwa wanaojua roho mbaya na unyama vilivyolikumba taifa letu wanahoji kama kurudi kwa Kibanda ni jambo la busara au kujitoa kafara ili amalizwe vizuri kama kweli chanzo cha masahibu yake ni kazi yake na si mengineyo. Je nani amemshauri Kibanda kurejea nchini hata kabla ya uchunguzi wa masahibu yake haujakamilika? Je 'wabaya' wa Kibanda watakubali yaishe au watataka kummaliza ili siri yao isifichuke kama kweli chanzo cha masahibu yake ni kazi yake? Je kesi ya Kibanda itaishia kuwa kiini macho kama ya Dk Ulimboka ambaye ameacha maswali mengi kuliko majibu? Je ni kitu gani kimemmotisha Kibanda kujirejesha kwenye mikono ya mauti kirahisi hivi?
Ni mapema kuelezea. Wapo wasiomtakia mema wanamlaumu wakisema kuwa likimpata tena asilielie. Wanaompenda tunasema:  Alluta Contiunua. Tunachukua fursa hii kumtakia afya njema Kibanda na familia yake huku tukimpa pole kwa yote yaliyomsibu.

Sunday, 2 June 2013

This is special for al Ustaadh Kikwete

Dear your Excellency sheikh Jake Kikwete,
Assalaam Alaykum Wallahmatullillahi Wabarakatuhu.
 Take note that it took me hours to decide how I'd communicate with you. Being your biggest fan, it’s not easy to decide to differ from you. You know what. Since those time of promising maisha bora kwa wote that turned out to be maisha balaa, I've always trusted you religiously. I've concurred with you almost in all issues you raised and the words you said even if they caused me suffering. The other day my wife narrowly survived a divorce after saying that your wife whom they taught together at a certain primary school’s aloft and forgot the way they suffered together.
Jokes aside, a few years ago one shenanigan cheated death by the skin of his teeth after I attacked him with kung fu and judo for saying that your promises of Maisha bora was a big lie any politician in this hunk’s ever told.  To show my love to you, I spent many months without going to swallow kanywaji at our pub after such bad words were uttered against you.
Given that you know I’m the guy who can shed his precious, and ‘expensive’ blood for you, I’m sure you’ll take my advice seriously especially on this sensitive issue of religious bigotry-cum- hooliganism.
True, this time after you said that those sowing the  seeds of hatred among our people are foreigners I decided to disagree with you for the first time. Sorry about that. So too, sorry about not calling your doctor like those who don’t know how one becomes a doctor do. I've a number of reasons why I decided to part ways with you.
I divorced you after you’re quoted as saying that those causing religious mayhem to our hunk are foreigners. Sir, I beg to differ. They’re but home-grown terrorists waiting to attack. I’ll humbly give you a few of them and how they’re created by Satan himself or herself. Who knows his or her sex?
Home-grown terrorists were created when some sick and skin politicians started preaching religious hatred especially when they branded Chama Cha Wananchi (CUF) an Islamic-cumPemba’s party. Being megalomaniac and stupid, the same politicians are now saying that Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) is a Christian-cum-Chagga’s party.  Wameishiwa hao. Sadly though, such goons are not saying that Chama Cha Mapinduzi is Fisadi-cum-Fisi’s party.
Now let me tell you how to go about this mess in your house. Firstly, ban these damn mihadhara conducted by illiterates or semi illiterates who've got neither job nor means of sustaining themselves but only through enticing their masters wherever they're.
Secondly, fight graft that’s causes destitution that forces people to apply any tricks of survival even if it means to exterminate our hunk. Hawa jamaa ni njaa na ujinga vinavyowahangaisha. Arrest and jail them. Even in Saudi Arabia where Islam’s born such megalomania isn't allowed.
Thirdly, instead of fighting religious bigotry verbally just do it practically. Swahili’s it that empty words can’t break the bone. You've already said a lot if not too much.  You know what. Actions speak louder than words.
One boozer said that saying that the terrorists preaching hatred in our hunk are foreigners is but hogwash and a lie of the year.   He taxed you to mention their names. He even cautioned about saying you know them just like you did when you said you know those selling drugs in the hunk without apprehending even a single person. He added that your government’s made by a bunch of thieves and con men and con women who’re after self-serving. This fyatu’s talking like a barrel of gun. He added that by consisting of such bête noires, it is but a damn seating-lame duck or a do-nothing cabal of wicked creatures headed by you.  He’d to run for his life before completing his insults. For, I removed my knife from its sheath to slit his neck and feed his tongue to dogs.
After the fyatu escaped I told listeners that it’s a storm in the cup of tea and you won’t be moved by anybody. Uh-oh! Though I differ with you, I can’t say such nonsensical things. Again, please sir, fight this cancer scientifically instead of fighting verbally. It is but an advice.
Who are we to tell the naked truth next week? Top secret! Again, who knows? Maybe, just maybe it’ll be Prof Anna Tiba-Ijuka shall our ever smart building go on crucify her. Maybe, J4 Kawa-dog who inflated the results or Fake Doctor Emmy Nchimbi whose docket needs to be erased if not being given to a sane man or woman.
By the way, Vasco da Gama was seen in Tokyo recently enjoying with his Queen Imelda Sally.
As for Mihadhara full of madhara, please Ustaadh, Sheikh Jake, keep a distance from those goons. They may be the causal agents for you to be invited to the ICC after some souls are neutralized in this megalomania. As for Ntwara’s stuff, try to sit down with the Chingas instead of dispatching Jeshi la Walevi wa Tanzia. It won't work.
Ya Ustaadh Wabillahi Tawfiq.
Source: Thisday Jan. 3, 2013. 

Saturday, 1 June 2013

Gesi Mtwara, nilisema mtumie 'GESHI' si jeshi


Juzi niliposikia kuwa wananchi wasio na hatia kule Ntwara `walibondwa’ na hata wengine kunyotolewa roho, niliumia sana. Hadi ninapoandika pombe na bangi vimenitoka kiasi cha kuwa normal na kuandika kitu serious seriously.
Usishangae kuona naandika kwa kuchanganya lugha. Ni sababu ya huzuni na usongo. Kama wao wanachanganya mambo, kwanini mlevi nisichanganye japo sijachanganyikiwa na kuishiwa kama wao. Sijui haya matumizi mabaya ya jeshi yanalifundisha nini?
Katika nasaha zangu kwa watawala wetu wanaoanza kuonekana vichwa ngumu, nilishauri mgogoro wa gesiasili watumie nguvu ya ‘GESHI’ yaani Gawaneni, Elimishaneni, Shirikianeni, Heshimianeni na Ishini (kwa haki na amani).
Pia nikaasa kuhusu ‘POLISH’ yaani Pataneni, Ongeeni, Laumianeni Ila Siyo Hujuma. Mie wala sikumaanisha mtumie jeshi na polisi. Kwani kazi ya polisi ni kulinda usalama au kuuvuruga kama ilivyotokea Ntwara?
 Mbona kazi ya jeshi ni kulinda mipaka yetu na si kupiga watu.  Kumbe jamaa hawakunielewa! Laiti wangenielewa wasingeaibika na kuhatarisha mstakabali wa kaya bila sababu yoyote ya maana, zaidi ya roho mbaya na uroho.
Au hawakunisoma. Je, walinisoma wakanielewa ila wakaamua kujifanya hamnazo na kufanya vitu vya ajabu ambavyo mwisho wake, unaweza kujikuta  wana poop kwenye debe kule The Hague kama akina Chaz Taylor na Laurent Badboy na nkewe?
Chonde chonde ndugu zanguni. Hii kaya ni yetu sote kwa pamoja na kwa usawa, japo kuna wanaoiibia huku wengine wakifa makapuku.  Japo kuna ngurumbili wanajiona wao ni wenye na wala kaya na wanakaya ni mabwege, kuna siku kibao kitawageukia wajute kuzaliwa.
Siamini kama tuna haja ya kufika huko mapema hivi. Je, haya ndiyo maisha bora mliyotuahidi ambapo mnatupa maisha balaa ya vipigo na udhalilishaji? Sioni sababu ya kugombea neema ya gesiasili kiasi cha kuigeuza kuwa laanaasilia.
Sioni mantiki ya jeshi linaloitwa la walevi kuwatwanga hata ‘kuwadedisha’ na kuwapora walevi ambao kimsingi ndiyo wanaotoa uchache wa kulisha na kuliendesha.
Jamani, tusikubali aibu na jinai hii. Naaamini mheshimiwa Mkubwa ananisikia. Kama hanisikii watu wake wananisikia na kunielewa. Siku hizi Jeshi la Walevi wa Tanzia, usichanganye na lile la Wananchi, please. Sitaki kichapo japo kwa making- fu yangu hakuna wa kuniweza.
Jeshi la walevi imegeuka Jeuri ya Walaji Teketeza Walevi. Sisi walevi huwa tunalipa jeshi ulabu na maisha bure. Linakula na kunywa bure. Je hii ndiyo shukrani au ni shukrani ya punda?
Tunafanyiwa hivyo kwa sababu ni walevi au what? Kama wana maguvu kwanini wasiende kupambana na mafisadi na majambazi yanayoibia kaya yetu na kutuacha walevi apeche alolo?
Tahadhali. Leo sijapiga ulabu wala kuvuta sigara kubwa. Nina akili timamu na uchungu ambavyo vimenisukuma kuandika waraka huu kwa watulao wetu wote, ambao walevi huwaita watawala.
Sioni mantiki ya wachukuaji waitwao wawekezaji wasiowekeza kitu zaidi ya ghilba na milungula kututesa kiasi hiki. Basi badilini jina la kaya kutoka Tanzia kwenye Tanzawekezaji au Tanzachukuaji tujue ili tusiendelee kuwaghasi bure.
Walevi, kwa mfano, wanataka wajue ni kwanini zabuni ya kujenga m-bomba wa hiyo gesi inayoaanza kutuchoma kabla ya kutumulikia, ilitangazwa lini na nani na kwa vigezo gani na vipi?
Nauliza kutaka kujua na si kuwachokonoa wakubwa wenye maulaji yao ya siri na hovyo kwenye mradi wa gesiasili.
Hao Wachina wanaojenga hilo bomba walishindana na nani kupata hiyo tenda? Je haya ndiyo mantiki ya ziara ya bwana elephant Amdaraman Kinamna kule China hapo mwezi Machi mwaka huu?
Naomba mnielimisheni hata kama elimu yenu imeishageuka mitumba ambapo watoto wanafelishwa tena baada ya kulanguliwa kununua ujinga na wakubwa, eti wanafuta matokeo utadhani wao ndiyo Baraza la Mitihani.
Si mkubali na kusema kuwa mmeshindwa tena vibaya? Kila siku `rongo rongo’ maisha bora maendeleo wakati ni urongo mtupu. Mnadhani maisha bora na maendeleo yenu yana- reflect walevi wote? Acheni uhuni jamani tukae tujenga kaya na kuishi kwa neema badala ya nakama.
Katika majibu nitakayopewa ili nielimike halafu niende kwetu Ntwara, niwaelimishe akina Njomba na Somoe sitaki kusikia upuuzi wa J4 Kawa-dog, ambaye nimeishamwamuru aachie ngazi lakini anang'ang'ania eti kwa vile anatoka sehemu moja na Njaa Kaya mkuu.
Wazungu huhoji, what do you expect when "The blind leads the blind?" yaani kipofu akiwaongoza vipofu wote wataangamia kwenye mashimo. Juzi eti yule tapeli bingwa wa kughushi aitwaye Emmy Nchimvi, alikwenda Ntwara kusuluhisha.
Asuluhishe nini wakati naye anahitaji kusuluhishwa na kusulubiwa kwa kashfa yake ya kughushi? Nilitaka kupasuka niliposikia eti na Saydu Mwemae alikuwapo.
Aende kule kusaidia nini iwapo ndata wake wanaoongoza kwa kuwanyotoa roho walevi kwa risasi zilizonunuliwa kwa njuluku zao? Wajomba zangu kule Bush-angle husema ‘Kachenjere’ wale wa kule Ithekahuno husema ‘Thie ngui iwe.’
Kwa ushenzi sitatoa tafsiri ila wenye akili wamenideku. Mnaaendekeza uroho halafu mnajifanya wazalendo wa kaya wakati ni wasaliti maafriti watupu. Shame on you once again!
Nina `mihasira’ kiasi cha kutamani niende niyanase vibao na kuyafunga pingu na kuyatupa Segerea na Ukonga kama Saddam alivyofanyiwa, kwa kutupwa kwenye gereza la Abu Ghraib alikokuwa akifungia na kunyongea walevi wa kayani mwake.
Asijue naye siku moja ataingia  na kunyongewa pale Kadhimiya ambako nilihudhuria majilini kumsanifu kama alivyokuwa akisanifu wale aliokuwa akionea na kunyonga.
Nilidhani kashfa ya uuzaji wa vipusa na mibwimbwi ingewafungua macho jamaa lakini wapi.
Hebu tujiulize swali moja dogo. Inakuwaje jeshi linalopaswa kulinda mipaka yetu inayochezewa na wageni kama ilivyoripotiwa hivi karibuni, kuwa wasomali kadhaa wanaingiza watu kayani watakavyo hailindwi.
Badala yake linatumika kubonda na kudedisha walevi wa Ntwara ambao dhambi yao ni kudai haki yao? Hili ni jeshi tena au geresha?
Tumalizie kwa kutoa ushauri mpya ingawa magamba yameishaanza usanii wa eti kutaka wakubwa wa Ntwara wafukuzwe wakati wa kufukuzwa ni mkubwa wao wote.
Don’t throw innocent officials under the bus to spere his boss who always has proved to sleep on the wheel.  Kuna kipindi inabidi watawaliwa waongoze njia watawale na watawala wafuate waone raha ya kufanya hivyo hasa pale wanapothibitisha kuwa wameshindwa kulhali.

Chanzo: Nipashe Juni 1, 2013.

Thursday, 30 May 2013

Maskini Profesa Anna Tibaijuka!


Ingawa kibonzo hiki kinaweza kutafsiriwa kama utani, kina ukweli zaidi ya utani. Kwa ufupi ni kwamba Msaoud Kipanya anajaribu kuonyesha jinsi waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi profesa Anna Tibaijuka yumo kitanzini baada ya Yuda Iskariot yaani bosi wake kumuacha asulubishwe. Pia ni suto kwa wana taaluma wanaoacha taaluma zao na kujiingiza kwenye siasa za kifisi na kibabaishaji. Na kama kuna vipande thelathini vitakavyomsulubisha profesa Tibaijuka si vingine bali vile vilivyotolewa na mwenye nyumba ya Indira Gandhi na ile ya  Getrude Rwakatare ambayo ilijengwa kwenye eneo lisiloruhusiwa kisheria. Je Tibaijuka ataufyata na kuendelea kuramba matapishi yake au ataamua kulinda heshima yake na kuachia ngazi? Time will accurately and punctually tell.

Tuesday, 28 May 2013

Tufanye mpango Kikwete aende kutalii mwezini

Picha kwa hisani ya Michuzi blog


Wapo waliomheshimu na kumwita Vasco da Gama wakimaanisha yule jambazi wa kireno aliyezunguka dunia akitafuta pa kupora. Wasio na muda wa kufichaficha walimwita mzururaji huku wale wanaomheshimu walimwita mtalii. Wengine wanamwita msanii kutokana na tabia yake ya kufanya mambo kisanii. Yote amefanya hili la kuizunguka dunia limemkaa. Rais anazurura utadhani waziri wa mambo ya nchi za nje! Kwa vile Kikwete na mkewe walishaizunguka dunia nzima, napendekeza afanyiwe mpango aende kutalii anga za juu kupitia mradi wa sasa wa kupeleka watalii kule unaofanywa na vyombo vya anga binafsi.

Uombaomba wetu ni wa kujitakia


TAARIFA na ripoti za kufichuliwa wizi wa mabilioni ya shilingi unaotokea kila mwaka zinasikitisha sana.
Hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alifichua kuwa makampuni ya uchimbaji madini kwa mwaka wa fedha uliopita yalikwepa kulipa kodi kiasi cha dola za Marekani bilioni moja.
Hii ni pesa nyingi hasa kwa taifa maskini na ombaomba kama Tanzania. Hizi dola bilioni moja ni makampuni ya madini tu. Je, hayo makampuni ya simu, wahamiaji haramu wanaofanya kila aina ya biashara halali na haramu, mabenki, waagizaji na wauzaji bidhaa nje, makampuni ya utalii, maduka ya kubadili fedha za kigeni, wafanya magendo na wengine wanatuibia mabilioni mangapi?
Inatia kinyaa kuona mamlaka zinazembea kukusanya kodi na badala yake zinaendekeza kukopakopa na kuombaomba bila sababu ya msingi.
Ukiangalia mianya ya misamaha ya kodi na ukwepaji kodi nchini, unagundua kuwa taifa letu ni tajiri sana. Laiti ungepatikana uongozi unaoweza kukusanya kodi hata kwa kiwango cha robo, taifa letu linaweza kujitosheleza kwa bajeti yake na kuwa na kiasi cha kuweka benki.
Ni aibu na ajabu kuona kuwa pesa tunayodhalilishwa kwayo kwa njia ya kuombaomba na kukopa ni tone katika bahari ikilinganishwa na ile tunayozembea kukusanya na kufuja.
Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa njia ya kuzembea kukusanya kodi na badala yake ikawekeza kwenye kuombaomba na kukopa hovyo tena mikopo yenyewe yenye riba kubwa.
Kama kuna jinsi ya kuelezea hivi, ni kwamba tuna umaskini na uombaomba wa kujitakia. Ni kwanini hatuoni hata aibu kuona rais wetu anavyodhalilika kila uchao kwenda nje kuomba wakati pesa inapotea hivi hivi kutokana na watu wachache mafisadi na waroho kuruhusu wengine waibe pesa yetu na kusamehe kodi ukiachia mbali kuachia mianya ya kukwepa kodi? Tunamkomoa nani?
Je, kwanini wakubwa wetu wanafanya hivi? Jibu ni rahisi kuwa wameridhika na mabaki ya ‘ten percent’ wanayopewa kiasi cha kushindwa kuelewa kuwa wangeamua kukusanya kodi na kusimamia rasilimali zetu vizuri wana uwezo wa kujilipa hata mara tatu ya mabaki wanayohongwa.
Kama siyo hivi ni nini? Kwanini wanafanya hivyo wakati wana elimu ya kutosha? Lazima kuna sababu tena zaidi ya hiyo tajwa hapo juu. Hata hivyo, tunaweza kufupisha matatizo yote kwenye neno moja tu- UFISADI.
Hivi karibuni Mbunge Zitto Kabwe Kigoma Mashariki (CHADEMA) alikaririwa akishangaa kuhusu hujuma hii tunayotendewa kama taifa.
Alisema kuwa Rwanda ambayo wateja wake wa simu ni wa kampuni moja ya Vodacom, iliweza kukusanya kodi ya dola milioni 14 wakati Tanzania yenye makampuni mengi ya simu ilikusanya kiasi cha dola milioni 1.4. Kabwe alisema: “Sasa serikali ikusanye kodi iache bla bla, TCRA ipewe mamlaka kama TMAA, sasa imetosha.”
Kinachoshangaza ni kwamba Kabwe alipofichua hujuma hii kwa taifa, mamkala husika zilikuja na vitisho kuwa ni kinyume cha sheria kufuatilia shughuli zake.
Je hawa jamaa wa TCRA wanadhani hayo maofisi wanayotumia kuhujumia taifa ni mali ya mama zao?
Inahitajika roho ya mwendawazimu kukubali kuwa taifa lenye kila aina ya rasilimali hasa madini linaweza kuzidiwa na viinchi jirani kama Kenya na Rwanda ambavyo havina rasilimali hata nusu yetu.
Sijui kwanini hatujisuti na kuona aibu tunavyoonekana mataahira waliokalia utajiri mkubwa huku tukiombaomba kuanzia misaada hadi rushwa?
Tumejigeuza majuha na hayawani kama samaki aliyekufa kwa kiu kutokana na kushindwa kutumia maji aishimo!
Tusiwe kama tembo ambaye huwa ana nguvu nyingi ya kuangusha miti lakini akaishi bila hata kibanda huku akishindwa na nyuni ajijengeaye kiota pamoja na udhalili na utepetevu wake.
Ajabu ya maajabu yetu ni pale tunaposhabikia kuwa na serikali kubwa bila sababu.
Kila awamu ukiachia mbili za mwanzo inasifika kwa kuanzisha wilaya na mikoa mipya ili kukidhi haja binafsi za baadhi ya wanasiasa wakubwa au marafiki zao. Pigo ni pale tunaposhabikia hata kununua migari ya bei mbaya karibu kwa kila mkubwa hata wa ngazi ya chini.
Kama wendawazimu unaoendelea hautakomeshwa, tutaendelea kuonekana kama jamii ya mazuzu na wehu.
Tutashindwaje kuonekana mataahira iwapo tunao ubingwa wa kurudia makosa na madudu mengi hivi?
Ni ajabu kuwa hata watawala wetu hawalioni hili. Kwanini, kwa mfano, kuendelea kushuhudia rais wetu akiombaomba kana kwamba nchi yetu haikujaliwa raslimali na akili?
Sijui kama rais anajisikia vizuri kwenda kuwapigia magoti marais wenzake kuomba hata pesa ya bajeti. Tumsaidie rais wetu aachane na udhalili huu.
Ni bahati mbaya kuwa mfumo wetu umekuwa wa kihasara hasara. Hebu angalia kwa mfano tulivyo na serikali kubwa bila hata sababu ya kufanya hivyo.
Ni bahati mbaya kuwa tangu kuondoka mzee Mwinyi karibu kila rais aliyeingia baadaye alianzisha au ameanzisha wilaya na mikoa bila sababu za msingi zaidi ya masilahi binafsi ya baadhi ya wanasiasa.
Mkapa alianzisha Mkoa wa Manyara nyumbani kwa waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye huku Kikwete akianzisha Katavi nyumbani kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Geita, Njombe na Simiu. Tunaongeza mikoa kwa utajiri gani?
Hebu kwa mfano angalia majirani zetu wa Kenya. Serikali mpya pamoja na kuruhusiwa kuunda baraza la mawaziri wasiozidi 22, kwa kuzingatia mzigo kwa uchumi, iliunda wizara 18. Sie tunao 50 na ushei! Hii ni akili au matope?
Kwa ufupi ni kwamba kinachoisumbua nchi yetu si ukosefu wa rasilimali kuanzia watu hadi madini na vitu vingine bali ombwe la utawala.
Utawala wa namna hii hauwezi kuivusha nchi yetu zaidi ya kuizamisha kama inavyoanza kujidhihirisha ambapo rasilimali zetu zimegeuka laana badala ya Baraka.
Kuna haja ya watawala wetu kujua kuwa kila jambo lina wakati wake. Wajifunze kutoka kwenye tawala zilizowahi kuamini kuwa haziwezi kuguswa na walalaho. Mfano wa karibu ni anguko la aibu na ajabu la Muamar Gaddafi kule Libya hivi karibuni.
Chanzo: Tanzania Daima Mei 28, 2013.