How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday 30 May 2013

Maskini Profesa Anna Tibaijuka!


Ingawa kibonzo hiki kinaweza kutafsiriwa kama utani, kina ukweli zaidi ya utani. Kwa ufupi ni kwamba Msaoud Kipanya anajaribu kuonyesha jinsi waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi profesa Anna Tibaijuka yumo kitanzini baada ya Yuda Iskariot yaani bosi wake kumuacha asulubishwe. Pia ni suto kwa wana taaluma wanaoacha taaluma zao na kujiingiza kwenye siasa za kifisi na kibabaishaji. Na kama kuna vipande thelathini vitakavyomsulubisha profesa Tibaijuka si vingine bali vile vilivyotolewa na mwenye nyumba ya Indira Gandhi na ile ya  Getrude Rwakatare ambayo ilijengwa kwenye eneo lisiloruhusiwa kisheria. Je Tibaijuka ataufyata na kuendelea kuramba matapishi yake au ataamua kulinda heshima yake na kuachia ngazi? Time will accurately and punctually tell.

2 comments:

Jaribu said...

Tofauti kati ya Idd Amin na Dr Mkono-wa-Nchi-za-Nje ni kwamba Idd Amin alikuwa anawaua wasomi wakati huyu kihiyo anawachezea; lakini wote ni anti-intellectual. Vile vile Idd Amin alikuwa anajilimbikizia vyeo vya jeshi na medali wakati huyu ni mpenda shahada za heshima.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Wow! Uchambuzi wako nimeukubali hata kama ni sentensi chache,inasikitisha kuona wasomi wetu wamegeuka kama vile vyangudoa wanaoweza kutumiwa na kila mpuuzi!