Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Sunday 12 May 2013

Leo acha tuwatanie viongozi wetu



Wote majina yao yanaanza na J,
Wana watoto waliowaruhusu kutumia madaraka yao vibaya kutajirika ingawa majina ya watoto wao.
Wote wanavaa miwani.
Wote wanasifika kwa kuvutia wafuasi wao bila sababu wala sifa za msingi zaidi ya  kile wazungu huita cheap popularity. Mmoja anapenda sana kuchekacheka wakati mwingine kuimba na kuchezacheza.
Wote wameficha ukatili wa kutisha kwenye matendo yao ya kuvutia umma.
Wote wanakumbwa na kashfa ambazo zimefunikwa. Mmoja anakabiliwa na kashfa ya wizi wa pesa Benki Kuu nchini mwake wakati mwingine akikabiliwa na kashfa za ufisadi na ubakaji
Wote wanapenda sana kusafari nje ya nchi zao kiasi cha kukatisha tamaa
Wote wameishaanza kususwa na wakongwe na waanzilishi wa vyama vyao. Mmoja alisuswa na JK Nyerere na mwingine amesuswa na Desmond Tutu BOFYA HAPA.
Wote wameonyesha kukatisha tamaa wale waliowaamini na kuwachagua.Ni viongozi wa hovyo.
Wote wana wasemaji wao wenye kutia kila aina ya shaka ukiachia mbali kupwaya.
Wote wanasifika kwa kupenda matumizi na matanuzi na familia zao.
Wote wana utitiri wa watoto wa kuzaa ndani na nje ya ndoa.
Mwisho, Inasemakana wote wanapenda totoz sema mmoja kwa kificho na mwingine wazi wazi.
Unaweza kuongeza au kuendeleza.....

4 comments:

Mtwangio said...

Kama hali hii itaendelea Afrika ya kutokuwepo kuhisi majukumu na kuwajibika na kuwajibishwa kwa viongozi kama zilivyokuwa nchi za wezentu ambazo uongozi upo mikononi mwa umma kamwe ujambazi,ufisadi,dhuluma na kudhalilishwa kwa wananchi hakutokwisha.Tuangalie mifano mbalimbali ya viongozi wasiowajibika,kutuma madaraka yao vibaya au hata wanapokutwa na kashfa ya aina moja au nyingine utukuta kwamba wanawajibishwa kwa kusimamishwa mahakamani,na mahkama inakuwa sio ya ngojera na hukumu inatolewa kutokana na kosa lilivyo,aidha kifungo,kifo au kuuzulishwa madaraka.Lakini katika nchi zetu ambazo viongozi wameunda tabaka la ambao kwamba (elites)kiasi ambacho huwezi kuwagusa kwa chochote kile na kama ikitokea baadhi yao wenyewe kwa wenyewe kujikwaa kwa njia moja au nyingine ndio utakuta wanaondoleana fadhila na wepesi si ama ni aina ya adhabu ya wenyewe kwa wenyewe na wala si kwa masilahi ya nchi na wananchi.

Tukumbuke kwa mafano kashfa ya rais wa marekani Bill Clinton na Monica Lewinsky ambayo ilikuwa chupuchupu Clinton atoke madarakani au tukumbuke hivi karibuni kashfa ya mmoja wa mawaziri wa ngazi za juu Ujerumani baada ya kujulikana alighushi shahada yake ya juu ya Phd mara moja na bila ya kusita alijiuzulu na kuomba radhi kwa kosa alilolifanya.kwa serikali ya china waote tunajua kwamba ufisadi na wizi wa aina yoyote ule kwa kiongozi unaishia kaburini.

Kwetu sisi hakuna miiko ya uongozi na hata kama ipo ipo tu katika makaratasi kufikia hadi hii leo kwa afrika ukitaka utajiri wa haraka harak uingie katika siasa na ukifanikiwa kuuramba ubunge au uwaziri ndio tena wewe na familia yako imeshatoka.

Najua bado tuna safari ndefu ya kufika walipofika wenzetu kwamba madaraka ni kuhudumia watu na nchi na ni kuwajibika na kuwajibishwa na wala si mali ya mtu binfsi na familia yake.Tusikate tamaa ni maswala ya wakati japo njia ya kufikia huko ina miiba na mbigili nyingi.

Jaribu said...

Zuma na Kikwete, pwagu na pwaguzi, dumb and dumber.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtwangio usemayo ni kweli tunahitaji mabadiliko ama kwa watawala wetu kujibadilisha au kubadilishwa katika namna yoyote. Natamani yaliyotokea Libya yangetokea nchini mwetu au hata kwa majirani zetu ili kuwaamsha wengi wanaodhulumiwa na majambazi waliowaamini.
Jaribu you mean these guys are yin and yang? So be it. Umeniacha hoi pale kwa Pwagu na Pwaguzi maana zama zao ilikuwa ni vituko vitupu.

Jaribu said...

Indeed, Mhango, yin and yang. Wote wawili ni janga la Taifa!