How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday 16 May 2013

CCM kukacha midaharo: Ukihiyo na ukame wa mawazo?



Wengi wanakumbuka jinsi utawala wa sasa ulivyoingia madarakani kinamna.Hapa hatumaanishi kule kuchafuana na wizi wa fedha za umma Benki kuu (EPA) wala uchakachuaji. Watakumbuka kuwa rais Jakaya Kikwete, tofauti na mtangulizi wake, hakuna kitu anachokiogopa kama midahalo. Kwa vipindi vyote viwili alivyogombea, Kikwete alikuwa tayari kufanya loolote lakini siyo kushiriki midahalo. Ingawa hajawahi kueleza kwanini hakupenda kushiriki midahalo,hii imejenga dhana kuwa aliiogopa kutokana na kuwa na welewa mdogo wa mambo. Maana, wanaoamini hivyo wanasema kuwa kama angeshiriki angevuliwa nguo na ubovu wake kuonekana. Hivyo, kuepuka hilo, wanaongeza: Aliamua kuingia mitini kila alipoalikwa kwenye mdahalo.
Ushahidi mwingine ni kwamba tangu Kikwete aingie madarakani, hajawahi kwenda chuo kikuu kubadilisha mawazo na wanafunzi kama wenzake waliomtangulia walivyokuwa wakifanya. Hii kwa wachambuzi inaweza kutafsiriwa kama ukihiyo. Wapo wanaoshangaa jinsi Kikwete huyu huyu asiyependa mambo ya kisomi, alivyoridhika na kupenda kutumia udaktari wa heshima. Maskini ameonyesha ugumu wa kuelewa wanasema. Watangulizi wake wote walipewa shahada nyingi za heshima tena kuliko yeye. Lakini huwezi kusikia Dk Nyerere,Dk Mwinyi wala Dk Chinga. Ni Dk Kikwete pekee anayeweza kujisanifu bila kustuka.
Wakosoaji wake wanasema wazi: Kama kuna kitu Kikwete anapenda basi si kingine zaidi ya kuhudhuria maziko na kusafiri nje.
Hivi karibuni dhana hii ya kuogopa usomi ulipata mashiko pale iliposemekana Katibu mkuu wa CCM Abdulrahaman Kinana aliukacha mnyukano baina yake na Katibu mkuu wa CHADEMA Dk Wilibrod Slaa. Je Kinana alifuata mkumbo wa Kikwete au kuogopa kuvuliwa nguo hasa wakati huu anapokabiliwa na shutuma za kusafirisha pembe za ndovu na kuingiza na kuajiri wahamiaji  haramu nchini? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa. Je watanzania wanawachukuliaje viongozi kama hawa wasiokuwa na mawazo bali dili? Tutafakari pamoja.
Wapo wanaosema kuwa kweli midahalo inawapiga chenga CCM. Hata hivyo,  wanawasukumiza kwenye kashfa na kuhujumu taifa na kusema kuwa CCM kwa hili hawana mpinzani.

7 comments:

Jaribu said...

Si kitu cha kushangaza, CCM imejaa madakta vihiyo. Wote hao wakina Kinana na mkuu wake wana vipaji vya kulaghai na kusuka dili, lakini siyo kujimwaga kwenye midahalo. Kama unakumbuka Kikwete alivyokuwa anaboronga Davos mpaka Gordon Brown akamkatisha.

Kikwete akitaka kuonyesha ujanja wake anawahutubia wazee wa Dar ambao wanamuona kuwa yeye ni genius.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Napenda siku moja kusikia kuwa na bi mkubwa almaarufu Mwalimu Sally Kihiyo kapewe udaktari kama wa akina Nchimbi kama siyo wa Kikwete.

Jaribu said...

Lah! Huo utakuwa mtafaruku! To be fair, wakiwa Madakta Kikwete wawili sidhani kama tutaona tofauti yoyote, itakuwa ni kipofu mmoja kumuongoza kipofu mwingine.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu acha utani eti kipofu kumuuongoza mwingine siyo! Je itakuwaje kama taahira atamuongoza taahira mwenzake? Kwa jamaa walivyo hamnazo watapata matapeli wa kuwavisha hiyo aibu. Juzi Kibaki alipewa PhD ya heshima akasema hajui kama ana la kuifanyia. Laiti angemualika Kikwete kwenye kutunukiwa angemshauri ajiite Dk Mwai Kibaki jambo ambalo kama siyo kumfanya Kibaki azimie basi angesema neno lake maarufu. " Wewe hovyo na bure kabisa. Mafi ya kuku." Sijui Njaa Kaya anegjibuje.

Jaribu said...

Ha Ha! Sikujua Mwai Kibaki ana maneno. Njaa Kaya angetabasamu tu kujifanya hakusikia

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kumbe humjui baba Dave siyo? Moi Kibaka si mtu wa kudandia umaarufu wa shilingi mbili. Ule ni mtambo wa maneno tena mbofu mbofu. Amesoma Enzi zile akadaka shahada zake mbili na kuonyesha uwezo wa hali ya juu tofauti na Mr Zilch wetu ambaye hata hiyo shahada nadhani aliipata kwa vile alikuwa mkereketwa wa CCM. Haiingii akilini zama zile mtu anamaliza chuo na Bcom eti anakwenda kuhenyeka kwenye ukatibu wa CCM wilayani ambao sasa ni kimbilio la matapeli walioshindwa katika fani zao kama vile waandishi habari makanjanja na vibaka wengine wasio na elimu. Lazima kuna namna. UDSM wangekuwa siyo wanazi chini ya mjikombaji mwingine Mkandala tungeomba tupate lau Research Papers zake tuone pumba alizoandika jamaa huyu ambaye hawezi hata kujiandikia hotuba fupi ya maneno 250.

Jaribu said...

Hata mimi nilishangaa nilivyosikia historia hiyo, nikafikiri kuwa labda kwa sababu katoka Msoga, Nachingwea haitakuwa sehemu mbaya. Sikujali sana enzi ile kwa sababu nilifikiria anaweza akabadilika, mpaka nilivyosikia anashabikia udakta wa heshima nikaona kumbe jamaa hamnazo. Kama alivyosema Obama, "Hata ukimpaka nguruwe lipstick atabakia kuwa nguruwe tu."