How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday 13 May 2013

Filamu ya wasaudia 'waliolipua' kanisa yachukua sura nyingine




Ingawa serikali ya Tanzania imefanya siri kuachiwa kwa raia wa kiarabu iliyosema walikamatwa kuhusiana na kulipua kanisa kule Arusha, kitendo chake cha kuwaachia kinyemela kinazidi kufichua usanii na ushenzi wa nmana yake. Kwanini kuwakamata watu wasio na hatia ili kuwatumia kuuhadaa umma kuwa vyombo vya usalama vinafanya kazi vizuri? Mbwembwe zote za mara Interpol mara FBI mara vyambo vyetu vya usalama zimeishia wapi zaidi ya kuonyesha ubabaishaji wa kutupwa? Kwanini kuwadanganya watanzania ukiachia mbali aibu itokanayo na upuuzi huu maisha ya watanzania yanapochezewa na wanasiasa wachovu. 
Kwa kiasi fulani conspiracy theories zinaanza kupata mashiko kuwa matukio ya kigaidi yanayolikumba taifa yanatekelezwa na usalama wa taifa ili kuwaondoa watanzania kwenye mijadala muhimu yenye kutishia uhai na uhalali wa serikali zigo inayoongozwa kwa sifa moja ya kuwa fisadi. Wakati wa mjadala wa gesiasili Mtwara, tuliletewa filamu ya Kibanda. Tuliposhupalia hili la Usalama wa Taifa (TISS) kuwa nyuma ya filamu hizi, tuliletewa filamu ya Rwakatare kabla ya hii wasaudia kulipua Kanisa huko Arusha. Wapo wanaoamini kuwa mauaji na hujuma hizi ni kazi ya Usalama wa Taifa kutokana na kutumiwa na watawala wetu wasio na huruma na watu wala kujali na kuheshimu uhai wa raia. Kama wanaweza kuuza mamilioni ya watanzania kwa wawekezaji watashindwa kuruhusu tukio la kuua watu watatu wanne na kujeruhi makumi kadha ili kulinda uoza na jinai vyao?
Kama wanaweza kuweka rehani vizazi vijavyo watashindwa kutoa roho mbili tatu hapa na pale ili kuhamisha mawazo ya umma wasijue kinachoendelea nyuma ya pazia? Natamani kitabu changu cha NYUMA YA PAZIA kingechapishwa watu wakaona yaliko nyuma ya pazia.
Ni aibu kwa nchi kuendesha kijambazi na kihuni huku vyombo vya usalama vilipwa mabilioni ya shilingi chini ya bajeti fichi lakini visifanye chochote zaidi ya kulinda ufisadi na ubabaishaji. Hakika maneno ya Katibu mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa kuwa rais Jakaya Kikwete na chama chake ndiyo walioanzisha  vurugu za kidini yameanza kupata mashiko. Kanisa lilipolipuliwa huko Arusha tulipewa haraka haraka taarifa kuwa wahusika walikuwa ni waarabu sawa na mkenya wa Ulimboka. Sijui na huyo mkenya maskini kaishia wapi? Ngoja tusikie akina Salva Rweyemamu Rweyependekeza Abunwasi watasema nini. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

No comments: