The Chant of Savant

Sunday 19 May 2013

Udini: Kikwete anamdanganya nani?


Magazeti ya leo yamemkariri rais shehe Jakaya Kikwete akisema, “Wanaohamasisha vurugu hizo ni watu wenye uhusiano ya karibu na watu wa nje ambao mambo yakiharibika nchini watakuwa wa kwanza kupanda ndege, ilhali wakiendelea kutoa matamko ya uchochezi wakiwa nje ya nchi wakati wengine wakiendelea kuumia.”
Kwanza,inaonyesha kuwa ima rais anawafahamu wahalifu hawa ila hataki au anaogopa kuwashughulikia. 
Pili, inaweza kuonyesha kuwa rais hajui anachosema na kama anajua basi anaongopa kwa makusudi. 
Tatu, inaonyesha kuwa rais anaishi kwenye dunia isiyokuwepo. Maana kwa cheo chake hakuwa na haja ya kulalamika bali kuchukua hatua na vitendo vikaongea badala ya kulalamika.
Nne, kwa wanaojua chanzo halisi cha mitafaruko ya kidini nchini, wanajua kuwa shehe Kikwete anatafuta wa kuwatwisha mzigo wake. 
Tano, kauli ya ustaadh Kikwete inajenga hisia kuwa kuna watu anataka kuwalinda kwa sababu ajuazo.  Sita, CCM na Kikwete ndio chanzo kizuri cha udini tunaoona kwa sasa kutokana siasa zao mufilis.
Blog hii imewahi kutoa vyanzo vikuu vya unaoitwa udini kuwa:
Kwanza, ni maisha magumu yaliyosababishwa na ufisadi na uongozi mbovu ambao umehujumu uchumi badala ya kuukuza.
Pili, ujinga ambapo watu wasioandaliwa vizuri kielimu na kimaadili wanadhani kuwa adui wao ni watu wa dini tofauti zao wakati ni watawala wanaowahadaa ima kwa vijizawadi na pesa kidogo au uhuru bandia wa kuhubiri maovu. Nani hajui kuwa mihadhara ya matusi na uongo ni chanzo kizuri cha migogoro ya kidini? Nani hajui kuwa wahubiri au wahadhiri kama wanavyopenda kuitwa ingawa siyo ni vihiyo wasio na elimu hata ya dini yao? Nani hajui kuwa wahubiri wengi hawahubiri kwa ajili ya Mungu bali kupata pesa ya kusukumia maisha? Wengi hawana elimu wala ajira wala biashara zaidi ya kuhubiri fujo zinazoshabikiwa na baadhi ya matajiri uchwara ambao wanafaidika kutokana na vurugu hizi kwa kuwataarifu mabwana zao kuwa kazi inakwenda vizuri. Tuliwahi kumtaja kiongozi wao aitwaye ustaadh Ilunga ambaye anahubiri maafa tena kwenye mitandao bila Kikwete na genge lake la Usalama wa Taifa kumchukulia hatua. Mara hii shehe Kikwete kasahau alivyopandikiza udini kwenye kampeni za mwaka 2005 kwa kudai CUF ni chama cha kiislam kabla ya kuishiwa na kuja na CHADEMA kama chama cha Wakristo kwenye kampeni zilizofuata? 
Mwisho, chanzo kikubwa na migogoro ya kidini ni Kikwete mwenyewe ambaye amekuwa akifumbia macho majibu halisi ya tatizo. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

7 comments:

Mtwangio said...

Mhango,sababu zote sita ulizozitaja kuhusu ustadhi Kikwete zina ukweli kwa upande mmoja au mwingine.Na kama wanasiasa wetu walivyo kwa kupuuzia jambo ambalo wanaliona kabisa baada ya miaka kadhaa litaleta msukosuko mkubwa nchini na wanadhani kwamba kwa vile wao ni watawala na kwa kutegemea serikali zao na vyombo vya dola vya usalama wanaweza kuyakabili hayo yakitokotea.

Lakini inapotokea kwamba swala linapokuwa la udini na ukabila inabidi serikali kutolivumilia na kulivalia njuga kuhakikisha kwamba waazilishi wa uchochozi,fitina na mtafaruko wa aidha dini au ukabila wanastahiki kuonywa na kama wanaendelea basi wanastahiki kuchukuliwa hatua za kisheria za kuhatarisha usalama wa nchi au hata kuitwa mahaini na kuhukumiwa hukumu ya maahini.

Mhango,mimi nilitka kidogo nirudi nyuma wakati wa utawala wa Baba wa taifa ambaye aliipenda nchi yake na wananchi wake na nadhani utakubaliana nami kwamba alijitahihidi kwa kuhakikisha anaweka mihimili na misingi imara ya taifa letu kwamba kusiwepo na udini amabao utahatarisha usalama wa taifa letu wala kusiwepo na ukabila ambao pia utahatarisha uiano na usalama wa taifa letu.

Mtwangio said...

Naam.Mwalimu alianza na upande wa lugha kutukusanya watanzania kuongea lugha ya kiswahili na kuwa ndio lugha ya elimmu na lugha ya taifa(wapo wengi wanamlaumu kwa hili na kusema kwamba ni moja ya mapungufu yake na kulinyima taifa elimu na kuwa leo Tanzania ipo nyuma kielimu)naweza kusema kwamba hawakumwelewa wenye kuona hivyo ingawa mjadala huu si mahala pake hapa.

Aliona hatari ya udini katika taifa endapo tu udini utachukua nafasi na kwa vile yeye ni msomi "intelectual" aliisoma historia ya kidini vizuri kuanzia ulaya mwanzo mwa karne ya 15 hadi 18 na aliona matatizo ya udini mpaka historia yetu ya leo kwa kupatikana kwa uhuru kwa India kisha kugawanyika nchi hiyo kwa sababu ya kidini leo tuna India ya majority ya udini wa kihindu na Pakistani yenye majority ya udini wa kiisilamu na hadi leo nchi mbili hizi bado zinaishi katika chuki za kidini hii ukiachilia mbali kuuana wana dini wa dini mojo kwa hoja ya madhehebu kama tunavyoona leo hii nchini Pakistani,Irani,Iraq.Lebanon hadi leo hii tumeshawapata Boko Haramu ambao wanahatarishia amani na usalama wa nchi ya Nigeria eti wanataka kutwala kwa sheria ya kiisilamu kama wanavyotaka wanaojiita Uhamsho wa Zanzibar kudai kutawala kwa sheria ya kiisilamu ni kuleta uhasama ndani yanci na kuirudisha nyuma nchi kimaendeleo kwani hakuna utawala wa kidini au sheria kama wanavyoiita bali ni unafiki tu wa makuhani wa kidini na watawala kama ilivyo Saudi Arabia na Iran.Hata kuna mzee mkereketwa wa kiisilamu alimuuliza mwalimu kwamba je waisilamu nafasi yao ipo wapi katika kupigania uhuru wa tanganyika?Mwalimu alimjibu jibu jepesi sana kwamba siiwezi kuigawa Tanganyika kama ilivyotokea India na Pakistani.Lakini hata hivyo mwalimu hakuelewekwa wakamtuhumu kwamba ni mdini na amewapendelea wakristo katika utawala wake!!!!Na madai haya naweza kusema ndio chanzo cha vurugu za kidini nchini kwetu baada ya kufa kwa Baba wa taifa.

Mtwangio said...

Kuhusu ukabila alihakikisha kwamba kusiwe na kupotezwa kwa haki ya matanzani kwa sababu ya ukabila na leo taifa letu ni katika mataifa machache sana Afrika kwamba mtu anaweza kutafuta mshirika wa maisha katika kabila lolote lile muda wa kudumu tu washirika hao wameridhiana na ukabila na udini unawekwa kando,tulikua hatuulizani kabila wala dini kama tunavyoulizana leo,ujirani wetu ulikuwa ujirani mwema na majirani waliishi kwa kusheherekea sherehe zao za dini kwa pamoja lakini leo hii kuna fatwa kwamba muisilamu haruhusiwi kusheherekea krismasi wala kuwapa wakristo hongera ya sherehe zao,na tulikuwa wakati ule jirani kama ni mkristo anataka kuchinja kuku upewa kijana wa kiisilamu ili wachinje majirani washirikiane kula kuku huyo wakati ule ujirani wa kuliana ulikuwepo.Hi leo hakuna ujirani wa aino hiyo wala mapenzi ni chuki'kudharauriana na unafiki wa kijamii na hasa toka upande wa waisilamu kutokana na kutoandaliwa vyema kielimu kama ulivyosema na kutokana kuingiliwa na taathira za nje hasa dhehebu anaojiita Wahabi,hawa wamekua ni fitina kubwa katika nchi nyingi duniani na kwa vile kama ulivyosema wataalamu wetu wa kidini aidha kwa nja,umasikini na kutoandaliwa vyema kielimu wapo tayari kubeba bango la dhehebu hilo na kuleta mtafaruko ndani ya nchi.kwa hiyo PETRODOLLAR inafanya kazi yake kirahiiiiiisi!!!Nadhani utakumbuka vyema Mhango kwamba Mihadhara ya kidini ilianza na kushamiri katika awamu ya pili,kuvunjwa kwa maduka ya kuuza nyama ya nguruwe ilitokea awamu ya pili, je waisilamu walipata wapi hari hiyo au ukereketwa huo kama si kuvimba vichwa kama watoto wadogo kwamba baba yao aliyopo madarakani ni mwisilamu kwa hiyo wanaweza kuanza utundu wowote ule au uhuni wowote ule na baba akawa kimya!

Mtwangio said...


Kuondoka kwa mwalimu Nyerere, Mhango,ndio chanzo cha tatizo la udini ususa upande wa waisilamu wameibuka na madai mabali mabali hata kudai ni wao na sio nyerere ndio waliofanikisha kuleta uhuru Tanganyika na nyerere amewazidi akili!!Kana kwamba Nyerere alikuwa mchaawi wa kukubalika kila nalowaambia waisilamu hao.Ilipokja awamu ya pili kama wanasiasa walivyo Rais mwinyi akachukua advantaje ya malalamiko ya waisilamu kwamba nyerere aliwapendelea wakristo nae akaja na ajenda ya kidini iliyokuwa wazi na kwa vile alikuwa Balozi wetu nchini Egypt katika kipindi cha kufa kwa Rais Abdel Nasser na kuja Rais Anwar Sadat na sadati kuyageiza maadili yote ya uongozi wa Abdel Nasser na kutumia karata ya udini mapaka kufikia kuitwa Rais mwenye imani(ya kidini)na akawa anaswali ijumaa kila wiki katika misikiti mbali mbali na katika hutuba zake alikua akianza na kwa "BISMILLAHI" Mwinyi akulaza damu kama mwanasiasa na kwa vile ni muiislamu na wakati umefika akatafuta cheap popurality ya kisiasa kwa kumuiga sadati au kufuata nyao za sadati akafunja maadili yote ya uongozi ya mwalimu mpaka kufikia kuwa muhandisi wa azimio la Zanzbar.na kswali misikitini,kuhudhuria hitima na maulidi na kutoa hutuba nae kwa kuanza na "BISMILAHI"Na kuwa karibu sana na waisilamu na waarabu na wahindi mapaka Ikulu kugeuka nyumba ya walanguzi kama ilivyoiita Mwalimu Nyerere.Na waisilamu walipiga shangwe kwa kuwepo raisi mwenye imani-ya

Mtwangio said...

Naam,ilipokuja awamu ya tatu hali haikuwa nafuu serikali ya ccm haikuzinduka au hata kuchukua hadhari kwa hatari ambayo ilishanza kujitokeza ambyo mbegu zake zilipandwa na Rais Mwinyi hadi hii leo waisilamu wanamuheshimu sana na kumtukuza kwa mjina ya mzee rukhsa na raisi mwisialmu wa kwanza katika jamuhuri ya muungano wa Tanzania.Kwa hiyo mihadhara iliendelea kwa kasi sana na hadi hii leo katika jamii yetu ya kitanzania neno KAFIRI au MAKAFIRI limekuwa la kawaida sana aidha kafiri huyo awe wa nyumbani au wa nje au makafiri hao wawe wa nje na hutuba za misikitini zimekua za uchochozi na kutia fitina hadi hii leo tumefika kuchomeana misahafu na mabibilia na kuinajisi pia kwa mikojo na mavi,kuchomeana misikiti na maknisa na hatimaye kulipuana mabomu!sasa kama wasemavyo kwamba kila kitendo kinachotekea huwa na jibu lake na lazima litokee na haya ndiyo majibu yake katika jamii yetu na kama serikali ya CCM hakuangalia kutazalika Boko Haramu ya Tanzania!

Mtwangio said...

Cha kushangaza zaidi katika awamu tatu ni kuongezeka makanisa uchwara,makanisa ya wachungaji na wahubiri wezi makanisa kila kichochoro wachungaji wake wanajitajirisha kwa kupitia ujinga wa waumini utadhani waumini hao wamerogwa kwa wafuasi wa yesu au kanisa tunajua wazi na kwa yakini Yesu na wanafunzi wake walikuwa ni masikini na umasikini ulikua ni moja ya sharti ya kuwahudumia kondoo lakini wachunganji wa leo si wachungaji bali wamevaa ngozi ya kondoo na kuwararua vipande vipande kondoo zao na kujitajirisha wao hali Mhango inabashiri nini?wachungaji wa kiisilamu wa kiafrika ni masikini hawana ujanja kama wa wachumgaji wa kikristo wa maknisa uchwara tofauti na wachungaji wa kiislamu katika nchi za kiarabu nao hawatofautiani kabisa na achungaji wa makanisa uchwara ya kiafrika kwani wao ni matajiri kupindukia wakati wafuasi wao ni masikini na wanaendelea tu kuwanyonyo kwa jina la Mungu.Leo dini imekua ni biashara,njia ya kujipatia jina la ugaidi kama Usama na wanafunzi wake hadi hii leo uisilamu ambao unajulikana kama ni dini ya amani imekua ndio dini ya kuhatarisha amani duniani.Mhango, namalizia kw akusema tusimlaumu sana ustadhi kikwete bali tumuonee huruma kwa kurithi tatizo la vurugu za kidni ambazo zilizipandikizwa na awamu ya pili na ya tatu na tatizo hili kama sisi ni wananchi wa Tanganyika nasema Tanganyika ni tufanye majuhudi ya pamoja ya kulipigia makelele kwa serikali yoyote ile aidha hii iliyokuwepo madarakani au zijazo la hasha tutauana wenyewe kwa wenyewe kwa ukereketwa wa kidini ambao unajawzwa na viongozi wetu wa kidini wajinga na wahuni na serikali kukifumbia macho wakidhani kwamba tatizo hilo kwao wao ni sehemu tu ya kubaki CCM madarakani hata kutumia mbinu chafu za kulipua kanisa la Arusha na nimeshaanza kusikia uvumi eti ni wakristo wenyewe kwa wenyewe ndio waliorushiana bomu hilo kwa tofouti zao za madhehebu na masilahi ya kibiashara ya kidini!!!!!!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtwangio, kwanza nakushukuru kwa mawazo yako pevu pamoja na mchango wa mara kwa mara. Hakika Mwalimu aliona mbali ingawa sasa wajinga na waroho wachache wanaharibu legacy na nchi yake. Sina shaka watakuja kujichanganya kiasi cha ndoa yao hii ya mashaka kubackfire kama ilivyotokea baina ya Marekani na Osama. Watajihadaa na kufanya kufuru zao kwa muda lakini watakuja kulipia siku si nyingi. Udini, ukabila, ujimbo na upuuzi mwingine hauwezi kufanikiwa. Ulisikia upuuzi wa Kikwete kumpigia debe rafiki na mshirika wake Lowassa akisema kuwa ni jembe. Kama Lowassa ni jembe basi Kikwete ni kijiko au tuseme upawa. Hawa watu wameishiwa hata na common sense kuweza kuelewa discourse ya sasa ambapo umma umewachoka na unawachukia ukijua fika wao ndiyo chanzo cha mabalaa yake. Kikwete anahaha kama Mkapa kutafuta kibaraka atakayelinda madhambi yake kama alivyomfanyia Mkapa baada ya kuasisi na kushiriki ujambazi wa EPA uliomwinginza Kikwete madarakani. Je watanzania watajirahisi kuendelea kutumiwa kama nepi kipindi hiki? Siamini kabisa kuwa watu wetu wataendelea na mawazo mgando huku wakichezewa mahepe na matapeli wachache. Tuzidi kuomba Mungu waumbuane na kugeukana.