The Chant of Savant

Tuesday 27 September 2011

Mwanamke ahukumiwa kwa kuendesha gari!

Je mwanamke akivaa hijab anaruhusiwa kuacha mikono yake wazi hadi tuone bangili na saa? Je hijab ni ushungi au kile kinachomstiri kiwiliwili chote?
Je huyu naye kavaa hijab au ninja, mbona kabla ya mapinduzi ya Iran hatukuwahi kuona maninja kama hawa?

Je hao wawili hapo wamevaa hijab au mavazi ya makabila fulani?


Mahakama moja nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanamke mmoja kuchapwa bakora kumi kwa kosa la kuendesha gari.Kituko hiki cha aina yake kilitokea wakati nchini Tanzania kuna fukuto la baadhi ya viongozi wa kiislamu kujiingiza kwenye kumtetea mkuu wa wilaya ya Igunga kwa kuvuliwa mtandio ambao wao wameutafsiri kama hijab! Viongozi hawa wa kujipachika wamesikika wakikitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwaomba msamaha utadhani wao ndiyo waliovuliwa hiyo hijab! Je hii inasababishwa na kukosa kazi, elimu ya kutosha au ajenda ya siri? Kwanini hawa "mashehe" wasivue majoho na kuvaa magwanda ya kisiasa kwa kuanzisha chama chao badala ya kujificha nyuma ya uislam? Je hawa hawautukanishi uislam kama wenzao wa Saudia?

Wakati huku kwetu uislam ukitumika kumtetea mwanasiasa ambaye hata dini yake haswa haijulikani kutokana na aina ya maisha anayoishi, waislam wenyewe wanamdhalilisha mwanamke kwa kumwadhibu kwa kufanya kitu ambacho ni halali na haki yake!
Kweli dunia ina vituko. Je hapa tatizo ni uislam,wahusika kutoujua uislam, siasa au unafiki? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Shughuli ipo na hili jambo sasa naona linaenea hata kuna habari niliisikia nadhani ilikuwa Ufaransa nako ni marfuku kuvaa hivyo kazini pia shuleni pia hata hapa Sweden inakuja ...