How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday, 30 November 2013

Who is fooling who hither?


We recently heard them bickering over many things. One of those many things was  or Coalition of Willing (COW) that's made of Kenya Rwanda and Uganda as opposed to Burundi DRC and Tanzania. After  many theatrics and ho-haa now we are told that East African Countries are together as one. Is this possible or some are just buying time? We recently evidenced Kenya, Rwanda, South Sudanese and Uganda's president inaugurating Railway project that will unite their respective countries. Burundi and Tanzania stated categorically that what the COW plus South Sudan were doing were against EAC Protocol. Before long we are now witnessing the signing of East Africa Monetary Union Protocol. Again, who is taking who for a ride? We are used to such ballyhoos by our politicos trying to severally serve individual interests such as one of them becoming the first EAC president after being in power in his country for decade. Another dictator who has lorded it over his people would like to avoid being toppled by  the tribe he kicked out and the other one is trying to dump his landless people while his family and he sits on the land as bigger as Nyanza Province in Kenya.

Kikwete anapopewa uchifu na fisadi Chenge


Picha kwa hisani ya Ippmedia
Kitendo cha mkoa wa Simiyu kumpa uchifu rais Jakaya Kikwete ni cha ajabu kidogo. Hivi walikosa mtu wa kkufanya hivyo hadi wamchague fisadi Andrew Chenge kumpa "heshima" ambayo licha ya kuanza kugeuka aibu imekosa maana kabisa. Je namna hii Kikwete anaweza kumfungulia mashtaka fisadi huyu au wote lao ni moja? Washauri wa Kikwete wana kazi ya ziada.

Mlevi kumilki bunduki aue kila anayemuudhi

Baada ya kushuhudia walevi wanavyodedishana kwa shaba, mlevi kwa vile nina usongo na maadui zangu wengi, lazima nimiliki bunduki.
Ukiwa na bunduki hata kama ni ‘apeche alolo’ utaonekana unazo, wasijue wengine wanamilki bunduki ili kutengeneza njuluku hata kama ni kwa njia ya jinai. Siku hizi kaya yetu haina tofauti na Sauzi au kwa Joji Kichaka ambako chuma ni sehemu muhimu ya maisha. 
Bunduki zinanikumbusha usemi maarufu wa Sarah Palin aliyesema, “we say keep your change, we'll keep our God, our guns, our constitution.”
 Tofauti ni kwamba, sisi lazima tuseme, “with our guns we’ll take your coin and destroy your doctored constitution. Our guns have become our source of liberation however in an illegal way and sense.”
Nitawaandama wabaya wangu kuanzia ndata hadi wale wanaommendea bi mkubwa au kutaka kuninyanyasa au kunibambikizia kesi uchwara.
Nani anataka kuona anatembezewa undava ndava wakati ana cha moto? Rafiki zangu ndata mkae mkao wa kudedi kwa shaba kwa vile mnajidai sana na vya moto vyenu, msijue nami nitakuwa nacho cha moto ili iwe jino kwa jino.
Na sitaki kusikia mkilalamika kuwa nimetangaza vita ya kudedisha ndata wakati mkiwaacha wenye vya moto mnaokula nao wadedishe watu na wanyama wetu kila uchao bila kuchukua hatua.
Kama hamtachukua hatua mimi nitawachukulia hatua nyinyi bila kujali nini wala nini.Mafisadi wakae mkao wa kuliwa. Hamuwezi kuiba njuluku zetu na kuficha ulaya mkataka sisi tufe njaa.
Kwa vile mnaogopa cha moto, lazima niwe nacho ili siku nikijisikia kuchacha, nije tugawane kabla sijawamiminia risasi. Mie siwaogopi kama hawa wanaowaogopa na kuwafunga. Lazima mrejeshe changu nami niende kupata raha kama nyinyi.

Pia nitahakikisha na bi mkubwa anakuwa na cha moto chake ili kuwaandama wale mamanzi wanaotaka kuniibia na kunigeuza buzi. Kwa hiyo vyangu kaeni mkao wa kudedi kwa shaba za bi mkubwa ambaye anajulikana kwa kutopenda masihara.

Kwa vile nshawatonya, kazi kwenu. Mkiniona mnatimka kama vile mmeona chizi. Mkiendekeza njaa zenu na ujinga wa si mbaya inzi kufia kidondani, shauri yenu. Ili kuongeza njuluku za kupatia kilaji na kujidai, nitakuwa nikikodisha gun yangu kwa majangili ili wakiua tembo na faru tugawane.

Pia nitahakikisha nakodisha gun yangu kwa majambazi ili wakipata kitu kidogo na kikubwa tugawane.
Kwa vile ujambazi, ufisadi na jinai nyingine kwenye kaya vinakubalika na kuruhusiwa, why should I worry? Money by all means. To me the end justifies the means. I have nothing to lose except my uchovu au vipi? Mambo ni kwa gun!
Nitaitumia bunduki yangu kutishia wale wanaojishaua kwenye mabaa. Ukipingana nami nakutolea gun.
Kwa vile mimi hamnazo najua itakuwa shughuli kupata gun. Hata hivyo, kukwepa kikwazo hiki naandaa njuluku zipatazo madafu laki tano kuwahonga wale wanaotoa gun.
Siku hizi murume ni kuwa na gun. Ukipenda mtu halafu mtu mwingine akaingia kwenye anga zako, unamdedisha kwa shaba.
Wale dada zangu kutoka karibu na mlima Nonihino wanaopenda kugonganisha magari, wakae mkao wa kuuawa.
Sitajali ni uncle au broo. nikigundua unatulisha sahani moja, natwanga shaba tu.  Mie siyo kama Kapuyanga anayeepua vitoto vya shule halafu anavitishia kwa SMS.  Ukiniudhi nakushindilia chuma bila kujinyotoa roho. Nikiona vipi najidedisha ili kuepuka kile Wakameruni huita to have a date with the judge au kumuona pilato ili akubabuseya.
Kwa vile mimi sina miwaya si kama Kapuyanga anayeambukiza miwaya na vitisho, wale Njaa Kaya aliosema wanapata vimimba kutokana na kiherehere, waje kwangu. Sana sana licha ya kuwaambukiza kitambi nitawaambukiza ulevi.
Makonda wanaopenda kunyanyasa abiria wakae mkao wa kuliwa. Nikipanda dala dala lako ukaanza kuleta za kuleta nakufyatua. Nisivyopenda nyodo na mitusi yenu ya nguoni lazima nitadedisha wengi.
Manesi na wakunga wanaopenda kuwatukana wagonjwa hasa akina mama wanaokwenda kujifungua pale Ailala, Mwanyamanyala na Meteke mkae kwa kurambwa shaba.
Kama bi mkubwa atakuja pale kujifungua mkamtukana au kumtakisha chochote kitu, mjue sitawapa njuluku bali shaba.
Wauza baa wenye tabia ya kusachi mifuko ya walevi, kaa mkao wa kuliwa shaba. Nikiingia kwenye baa yako kunywa halafu ukanigeuza buzi lazima nikuchune kwa shaba kabla hujanichuna.
 Hata wale waajiri wanaodhulumu wafanyakazi wao wakae mkao wa kuliwa shaba. Ukiniajiri halafu ukaanza kuniletea za kuleta ninapodai ujira wangu, jua sitakwenda kwenye vyama vya wafanyakazi zaidi ya kukurambisha shaba mchana kweupe.
Wenye mbavu za mbwa wajiitao wenye nyumba wenye tabia ya kunyonya na kunyanyasa wapangaji kaeni mkao wa kufa.  Maana nikipanga kwenye ubavu wa mbwa wako ukaanza kutaka kunigeuza buzi, jua umekufa wakati si wako.
Maana kuna mijitu kuwa na nyumba inaona kama ni kuwa na kila kitu. Ukiwa mpangaji unaonekana kama huna future.
Haijui kuwa wengi wenye nyumba ni wapangaji wa jana na wapangaji wa leo ni wenye nyumba wa kesho. Mijitu mingine mijinga na mipumbavu ikiwa na nyumba inasahau kuwa ni biashara kama nyingine.
Lazima uheshimu mpangaji kwa vile mteja ni mfalme. Wenye nyumba na makonda ni watu wa ovyo wanaopaswa kudedishwa kwa shaba.
Naona yule anatikisa kichwa. Simaanishi kila mwenye nyumba lazima apigwe shaba. Namaanisha wale wenye nyumba wanaodhani kuwa na nyumba ni waranti ya kunyonya na kunyanyasa wengine.
Nikiwa na bunduki yangu kila kitu ni shaba. Akikatiza mbwa nafyatua. Akikatiza inzi nafyatua. Hata akikatiza munen… shaabaa tu.
Leo natuma salama na rambirambi kwa rafiki yangu Saleh Saggaf kwa kuondokewa na mama yake. Inshallah Allah atawaimarisha na kuwawezesha kuvuka kwenye kipindi hiki kigumu.

Chanzo: Nipashe Jumamosi Nov., 30, 2013.

Friday, 29 November 2013

Did Zitto author his own obituary-cum-dirge?


Though it's still early to write a dirge or obituary for former Deputy General Secretary of Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Zitto Kabwe (MP), it's close to call. Looking at the heavy, stinky, messy and hot soup Kabwe's in; my crystal ball tells me I’d do. Though I’m not writin' the obituary even the dirge. Others can do.
Today I’m addressin' the whole fracas CHADEMA is in. Refer to the hype-touted, “the Kitilya-Zitto-Mwigamba dossier. I don’t want to lawyer anybody or judge anyone. Looking at the look of the things I must say, Zitto's history as far as membership in CHADEMA is concerned. I've a number of reasons to believe so.
Firstly, Mkumbo’s self-inculpatory confession, if anything, put the last nail in Zitto’s political coffin. By admitting they wrote the dossier that aimed at placing Zitto in power illegally and covertly, the trio committed what Indians call suttee. Kitila said he saw nothing wrong with his dossier then he confessed to have authored the dossier. He went a mile ahead apologizing. If you see nothing wrong with your dossier, what are you apologizing for in the first place?
Again, why did Mkumbo and Zitto want to resign from their position if they felt and understood that they committed no sin? When the politburo sensed their ploy and attempt to resign honourably, it axed them so that they’d go down dishonourably. I know Zitto’s fans and sympathizers are asking: Will our hero survive? Zilch, by all means and possibilities.
The other day when I read some headings saying that Kitila-Zitto axis would spill beans I waited anxiously to find that instead of spilling beans, the duo were too apologetic and beaten. If anything, such an expected U-turn forced speculators to say that the guys were now done. It means. They’d no beans to spill after theirs were spilled by CHADEMA bigwigs who caught the trio with their “pants down.” What else can you expect out of such desperate situation whereby the suspects are as good as cadavers? Done deal uh!
Two weeks before the moment of truth surfaced for the duo, I penned a piece asking Zitto to live up to his words. It's as if I knew what’s coming. I’m not a con astrologer to say that I saw it in my books. It's coincidental that I said what would happen before long. I take no credit save that I’m happy that I can see the future however accidentally and vague as it may seem.
Let me delve into the dossier that showed Zitto and Kitila the door. When cornered, the vulture cries eagle. So too, when Mkumbo was cornered he said that Zitto wasn’t aware of the dossier! Does it cross the mind even that of the dove? If he didn't know the said dossier why didn't he distance himself from it when he met the media? What does this mean really? Does it mean that Mkumbo-Mwigamba gang wanted to use Zitto or vice versa? So what?
Why people think that it’s easy to jump a smoking gun? How can you conceal your courtship to the girl you're intending to marry? Who wants to fool who hither? Let me say it clearly and loudly. Zitto knew everything. This is why he didn't and he can't recant the dossier. Moreover, CHADEMA’s been so tolerant and patient pointlessly for long. Time to act's now and now's the time to act decisively for once and for all. Dude set a precedent that political opportunism and prostitution don't pay.If they do, he who banks on them commits political suttee as it is in this saga-cum-case.
Anyway, when Zitto faced the media, he avoided eleven charges placed against him. Instead, he gerrymandered about ho-haa and other bull-cock tales. Why? Was there anything sinister Zitto didn’t want us to know? Again, this is not my question. It's the question that CHADEMA lawyer, Tundu Lissu asked when he faced the media to reciprocate to Zitto-Mkumbo face-the-media opportunity that took place a day before.
 Although much has been said, one might still ask,: If Mkumbo Dossier aimed at enabling CHADEMA to win why did the author turned it into a top secret involving only a select few? How can you help a party by concealing the strategy from it?
In my piece on asking Zitto to live up to his words I advised him to quit active politics and do the job he loves, teaching. It's time I give him more wisdom nuggets that if he still wants to be in the game, he’d follow Warrid Kaboro. Return back home to CCM that's said to be using  him. Again, does it make sense to cry for the milk one spilled thanks to his myopia, greed and rush?
In sum, Zitto deservedly got what he asked for. Mwana mkaidi. Though insanity will dictate that Zitto’s facing his Waterloo due to religionism, regionism and whatnot, the truth's the he authored his obituary-cum-dirge. Will he evolve from the ash? Perhaps. It amounts to miracles, miracles, miracles ad infintum.
Source: Business Times Nov., 29, 2013.

Zuma aonyesha tamaa na kufuru zake

 Jacob Zuma's Nkandla residence
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini huwa hakaukiwi vituko. Ukiachia kashfa yake ya kujipatia mamilioni ya dola kwa kumtumia mhindi rafiki yake na kashfa ya ubakaji, Zuma anakabiliwa na kashfa nyingine ya kutumia pesa ya umma kujenga makazi ya kifahari kijini kwake Nkandla, (kama yanavyooneka hapo juu). Hata hivyo, mahakama ilimsafisha kwenye kilichoonekana kama mizengwe. Japo si wote, watawala wetu ni wezi, waroho, wenye roho mbaya na majizi ya mali ya umma. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

Wednesday, 27 November 2013

Mali yaamua kumshughulikia Sanogo

 Malian coup leader Capt Amadou Sanogo address troops on 3 April 2012
Kiongozi wa mapinduzi yaliyoiingiza Mali kwenye mtafaruko wa kidini na kisiasa, Amadou Sanogo yuko korokoroni akikabiliwa na mashtaka ya mauaji. Sanogo afisa wa cheo cha kati jeshini asiyejulikana, aliishangaza dunia pale alipomwangusha rais wa zamani wa Mali Amadou Touman Toure. Sasa kibao kimemgeukia kama kilivyomgeukia mwenzie wa Guinea  Moussa Dadis Camara. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

Je huu ni mwanzo wa mwisho wa Zitto Kabwe?



Kwa wanaojua kilichompata akina Augustine Lyatonga Mrema, kuna uwezekano kuwa kinachoendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni mwanzo wa mwisho wa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA.
Kama Mrema, Zitto alilelewa na CHADEMA sawa na Mrema na Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Kama Mrema, Zitto ameponzwa na tamaa kutaka madaraka, sifa na kuonekana ni bora kuliko wengine. Kama Mrema, Zitto ameonyesha papara na uchu mkubwa wa ukubwa. Kama Mrema, Zitto ataondoka CHADEMA na CHADEMA haitakufa sawa na Mrema na CCM.
Tofauti ya Mrema na Zitto ni kwamba Mrema aliondoshwa CCM si kwa kutumiwa na chama kingine zaidi ya mipango yake ya kuusaka ukubwa. Hapa unaweza kuwaunganisha watu kama Seif Sharrif Hamad ambaye kuondoka kwake CCM hakukuiyumbisha sawa na alivyoondoka Mrema sawa na itakavyokuwa kwa Zitto na CHADEMA.
Tofauti na Mrema, Zitto ameondolewa mapema mno. Hakufaidi ulaji ndani ya serikali kama ilivyokuwa kwa Mrema aliyejijengea sifa ya utendaji hata kama ulikuwa wa kiimla na kihuni.
Zitto anaingia kwenye vitabu vya historia kama kijana aliyeanzia kwenye mavumbi ingawa anawez akurudi kwenye mavumbi kama hatarejea CCM ambao wanadai kumtumia. Ushahidi ni ile hali ya mkutano wake na waandishi wa habari kuandaliwa na kusimamiwa na UVCCM jambo ambalo Zitto na wenzake hawajakanusha. Huenda watafanya hivyo ingawa it is a bit too late too little.
Hakuna nyundo itakayommaliza Zitto kama kukiri kwa “mtu wake”, Dk. Kitila Mkumbo kuwa kweli waliandaa waraka uliowatia kitanzini pamoja na juhudi za bila mafanikio za kumtenga Zitto na waraka huu.
Maswali makuu,: Kama kweli Zitto hakuhusika na waraka husika wa uhaini na usaliti chamani, kwanini hakuukana alipokutana na waandishi wa habari? Kwanini Zitto alikuwa too apologetic and diversive kwenye press conference yake? Kwanini Zitto aliruhusu waasi waliokwisha aangukiwa na panga la CHADEMA kuupamba mkutano wake kama hakuna namna?
Je mwanzo wa mwisho wa Zitto ndiyo unaanza? Je ni mapema kuanza kuandika tanzia yake kisiasa au kutegemea kumuona akifufukia CCM?Je kweli Zitto hakutumiwa na CCM iwe kwa bahati mbaya au makusudi? Rejea uhusiano wake na marehemu Amina Chifupa.

Tuesday, 26 November 2013

Liberia’s State House and Drugs

Although there’s no good news, news that the head of Liberian presidential motorcade, Perry Dolo was caught red handed ferrying drugs is good news. Dolo’s alleged to have used presidential escort vehicle famously known as Escort 1 to smuggle 297 kilograms cannabis from neighbouring Sierra Leone.         
          AFP quoted Anthony Souh, Director of Liberia’s Drug Enforcement Agent (DEA) as saying, “He took the car during his day off to go do this thing. He was not on duty, but he used the official car.” Again, whether Dolo had a day off or not is another issue. Many still wonder.  How such a sensitive device could be taken as easy as that. Does it mean that the state house has no supervision to know as to when Escort 1 is at work or not? Does it make sense to say that Escort 1 was taken without authorities being aware if at all its function is to lead presidential motorcade? Whose motorcade did it lead when it went to a neighbouring country to smuggle cannabis? How many times has Dolo been doing this? How many Dolos does Africa have?
Being President Ellen Johnson-Sirleaf confidante, many are still looking for the connection so that they can connect the dots. Again, how could Dolo confidently involve in such crime without backing or the knowledge of those above him?
When it comes to scandals, Sirleaf is not new to scandals and controversy. Before Dolo’s scandal, there was the scandal involving her family. It came to light that her two sons are holding high position in her government something that many interpret as nepotism.
Sirleaf’s son Charles is deputy governor of the Central Bank of Liberia. Another son, Fumba is head of the National Security Agency. The third, Robert, is a senior adviser and chairman of the state-owned National Oil Company of Liberia. What makes things worse is the fact that those two sons of the president were appointed by the president herself. Such a move, apart from being construed as nepotism, it is seen as pointlessly turning Liberia into Sirleaf’s kingdom if not a family estate. All this defeats the expectations Liberians had when they voted in Sirleaf as a first female president. The world was used to hear such things happening in kingdoms such as Saudi Arabia, Kuwait and other venal states such as former Zaire, Congo, Guinea Equator, Togo and Gabon where rulers turned those countries into private ventures they’d share with the members of their clans and families.
When Sirleaf’s scandal involving her sons surfaced, Sirleaf’s noble prize co-recipient, Leymah Gbowee registered her dissatisfaction with the way the country was being manned by Sirleaf, Gbowee was quoted as saying, “I've been through a process of really thinking and reflecting and saying to myself 'you're as bad as being an accomplice for things that are happening in the country if you don't speak up.”  So she decided to speak up.
When Gbowee was asked for her comment on Sirleaf’s son’s allegations of corruption she minced no words, "He's a senior economic adviser and that's well and good - but to chair the oil company board - I think it's time he stepped aside."
Although Sirleaf has been making Liberians to believe she will thwart corruption, it came to light that she is a pillar of corruption. The 2012 U.S. State Department has report had this to say about Liberia, “Officials engaged in corrupt practices with impunity.” So too, the report talked about weakness in the country’s judicial system and a lack of political will to fight corruption.
Mid last year, the Head of Liberia Anti-Corruption Commission (LACC), Cllr. Frances Johnson-Allison said that friendship and family pressures were seriously hampering President Johnson-Sirleaf's stance against corruption and other negative vices in the country. Interestingly, neither president herself nor her spokesperson denied or disputed such allegations.
Looking at the above mentioned scandals involving president Sirleaf, it is going to be difficult for her to distance herself with Escort 1 scandal. Now that it is an open secret that presidential vehicle has been smuggling drugs into Liberia, how many such greedy and myopic persons Africa has in many state houses? Is this the reason why some African countries have become a good hub-cum-corridor of drugs?  Is it why some African rulers have nary even wasted any time to launch war against drug trafficking? Again, was Dolo acting solo or in conjunction with others?  There are many more questions than answers.
Source: The African Executive Magazine Nov. 27, 2013.

CHADEMA: Kwenye msafara wa mamba kenge wamo


KWA wenye kufuatilia siasa zetu za ulaji, urushi, unafiki na ubangaizaji, hawakushangaa kilichotokea kwenye chama kikuu cha upinzani Chadema. Baada ya Chadema kuwachukulia hatua za kinidhamu “waasi” ndani ya chama, mitandao ya kijamii ilifurika maoni. Yalikuwamo maoni ya aina mbili, yale ya wanaoipongeza Chadema kuondoa kansa na wale wanaoiponda kwa kuizushia kila aina ya uchafu hata usioingia kwenye akili hata ya njiwa.
Wahenga walisema; Kwenye msafara wa Mamba na Kenge wamo. Ama kweli hawakukosea wahenga kwa vile tumekuwa tukishuhudia wanasiasa uchwara na nyemelezi wakihama vyama lakini bado wakibaki wakimtumikia baba yao ambaye kila mmoja anamfahamu.
Tuliwaona akina Shibu—da, Mre—ma, Mba—tia, Che—yo na wengine wengi wakijiacha uchi kutokana na kutumikia mabwana wawili. Hata hivyo, wahusika walisahau kitu kimoja cha msingi, za mwizi siku zote ni arobaini.
Ukiangalia walichokuwa wakijaribu kufanya waasi wa Chadema, unagundua utoto na ukosefu wa mikakati hasa ikizingatiwa wakati walipokuja na mkakati wao. Huwezi kuanzisha mabadiliko ya uongozi ndani ya chama kwa njia ya mlango wa nyuma ukafanikiwa.
Hata kama una hoja na sababu ya kufanya hivyo utakwama kutokana na uharamu wa njia uliyotumia. Waingereza husema, the end justifies the means lakini huwezi ukahalalisha mbinu iliyogunduliwa na bazazi na nyemelezi Macchiavelli alipokuwa akitumikia usomi na utawala wa Kirumi ili kuishi.
Leo hii tutasikia mengi kuhusiana na Chadema. Hata hivyo, haya yanayotumiwa na wachovu na wabaya wa Chadema kuipaka matope si mapya. Usishangae kusikia uchaga, udini, ukanda na hata u-dot.com kwenye uchafu huu wa rejareja.
Huwezi kuwashutumu wenzako udini, ukabila na ukanda wewe usiwe nao. Unatumia vigezo gani kufikia hitimisho hili kama si kuwa muathirika mkubwa wa mabalaa?  Kwa wanaojua maana ya kukinzana na siasa huru, wana ushauri mmoja wa muhimu, ukiona wenzio hawakutaki si unakitoa na kwenda kule unakopendwa? Kwani chama ni baba au mama yako? Kwani lazima wewe na wenzako tu?
Ingawa ni mapema kusema, kinachoendelea ndani ya Chadema, ni matokeo ya kazi chafu ya ibilisi mwenyewe aliyewatuma wajumbe wake kwenda kuvurugu upinzani. Hamna kingine. Haiwezekani kuanze vurugu na miparurano wakati wa kujiandaa kuelekea uchaguzi. Hili si jipya. Tumewaona watoto wa yule mwovu wakivihama vyama wakati kama huu. Akina Steve Wassi—ra wanajua ninachosema hapa. Akina  Nsanzu—gwanko pia wanafahamu hili. Je watashinda?
 Wakati umefika kuwaambia wapinzani wa kweli kuwa muwe makini kwenye msafara wenu. Hamna tofauti na msafara wa Mamba ambao hujazana Kenge. Hivyo, kila mnapomgundua Kenge muonyeshe njia arejee huko kwa wenzake.
Situmii mfano wa Kenge kutaka kutukana au kudhalilishana. La hasha. Hii ni hekima ya wahenga ambayo tuliirithi wote. Kwanini Kenge aandamwe hivi? Nani hajui kuwa Kenge akiona mvua inaanza kunyesha hukimbilia majini? Akili au matope? Anyway, Kenge ni hayawani. Ila ni kujinyang’anya tunu ya ubinadamu kwa binadamu kutenda kama Kenge.
Kwa waliofuatilia sekeseke na mshike mshike kwenye Chama cha Chadema, walishangaa uvumilivu uliokuwa umechaguliwa na chama kama njia ya kujijenga. Huwezi kujijenga kwa kukumbatia Kenge ndani ya msafara wa Mamba.
Hakuna sehemu tulibaki kinywa wazi kama kwenye uchaguzi uliopita ambapo chama kilimsimamisha mwanachama wake kiliyeona amekidhi viwango vyake lakini mmoja wa viongozi tena wa juu wa chama akaamua kukisaliti na kumuunga mkono mgombea wa chama kingine. Hata kama chama kingekuwa kilikosea, kuna taratibu lakini siyo kukomoana na kusalitiana.
Wakati mwingine ni pale chama kilipotoa msimamo kama chama lakini baadhi ya viongozi wake wakakataa kusimamia msimamo wa chama. Kwa hili hata angekuwa mwalimu Nyerere asingevumilia kama walivyofanya Chadema.
Kwa vile siku zote huwa tunajifunza kutokana na makosa, wakati wa Chadema kutowaangalia nyani usoni umefika. Siasa za vyama ni kile wanachoita Waingereza to toe the line. If you can’t toe the line your political carrier in the party is on the line. Huwezi kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
Haiwezekani na kama ikiwezekana ni kwa muda tu. Ukigundulika unaadhibiwa bila kujali kuwa unajulikana au kukubalika. Kuwa na mawazo mbadala hata mkinzano si dhambi katika siasa za vyama. Kinachotakiwa ni kufuata utaratibu uliowekwa hata kama kinachodhamiriwa ni kubadili baadhi ya mambo chamani. Lazima kufuata utaratibu uliopo kichama na kisheria.
Kwa vile Chadema wameamua kuweka chama kwenye mstari, mengi yatasemwa. Wanapaswa kujiandaa kuyasikia haya na kukabiliana nayo vilivyo kama taasisi. Wabaya wao watawapakazia kila baya.
Watawakaribisha waasi kwenda kufanya nao biashara waliyokuwa wakiifanyia nyuma ya pazia kama njia ya kulipiza kisasa na kufanikisha kile walichokuwa wamekula njama kukifanya, kuwazuia kuingia madarakani.  Je watafanikiwa?
Itategemea na Chadema itakavyocheza karata zake hasa kuwaeleza wapiga kura nini kilikuwa kikiendelea ili waamue wenyewe. Je kupakaziana mabaya kutaondoa yale mabaya yanayojulikana kutendwa na wapinzani wa Chadema?
Je Watanzania ni majuha na wasahaulifu kiasi cha kuambiwa kuona tofauti ya ukweli wanaouona? Je nani huyu anayeweza kuwa mkubwa kuliko chama bado akaendelea kuwa kwenye chama hicho akitaka kitende atakavyo badala ya inavyotakiwa? Kuna haja ya kutafakari.
Wabaya wa Chadema wameishaandaa mabaya tena mengi tu. Lazima Chadema wajiandae kulisikia na kuliona hili kila siku hadi uchaguzi. Wabaya wa Chadema pamoja na mawakala na makuwadi wao waliojazana kwenye upinzani wataanza kutangaza injili ya udini na ukabila. Je wataweza kuzificha na kuzifunika zile za ubakaji, ufisadi, ujambazi, utoroshaji pesa na nyingine nyingi kama zinavyowaandama wapinzani na wabaya wao?
Tuhitimishe kwa kuwashauri Chadema kusimama kidete, kutenda haki na kuhakikisha demokrasia, kanuni na taratibu vinafuatwa ili kuepuka kutoa silaha kwa maadui ili wawamalize kirahisi. Ama kweli, kwenye msafara wa Mamba na Kenge wamo. 

Chanzo: Dira Novemba 26, 2013.

Mkapa: Usemayo kweli japo nyani haoni ...?



HAKUNA  sehemu mstaafu Benjamin Mkapa aliniacha hoi kama pale aliponukuliwa hivi karibuni akisema, “Kutegemea Serikali peke yake kulete maendeleo kutafanya maendeleo kuvia kwani nchi yetu ni kubwa na watu ni wengi na matarajio ni makubwa na gharama zake ni kubwa na mapato ya Serikali hayawezi kukidhi mahitaji yote.”
Ni kweli kuwa hakuna anayeweza kutegemea Serikali akapata maendeleo. Je kuna anayeweza kujiletea maendeleo chini ya Serikali isiyotengeneza mazingira ya kufanya hivyo?
 Ni bahati mbaya kuwa kinachoisumbua Tanzania ni matokeo ya sera za akina Mkapa ambao badala ya kujenga uchumi imara wenye kujitegemea kwa kulinda rasilimali zetu walizigawa kiasi cha kuwaacha Watanzania wakihangaika kana kwamba nchi yao haikujaliwa neema.
Hebu jiulize. Chini ya utawala wa Mkapa na chama chake unaoendelea kuwapo madarakani Tanzania inapoteza mabilioni mangapi kwenye ukwepaji kodi, ufisadi, rushwa, uzururaji na wizi unaofanywa na wakubwa?
Mkapa mwenyewe aliondoka akiwa amejitwalia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira na hajataka kuongelea hili. Je Mkapa anadhani kuwa Watanzania hawajui jinsi alivyolitia hasara Taifa kutokana na kujitwalia Kiwira ambapo Serikali ililazimika kutumia pesa nyingi ya walipa kodi kuununua toka kwake wakati yeye aliupata kwa  bei ya chee sawa na asilimia moja ya thamani ya mradi?
Kwani Watanzania hawajui kuwa Mkapa , familia yake na wakwe zake waliununua mradi kwa Kiwira kwa shilingi  milioni 70 wakati thamani yake wakati ule ilikuwa shilingi trilioni nne?
Je pesa iliyopotea hapa ingeweza kutengeneza ajira ngapi au kuwawezesha Watanzania kujiletea maendeleo?
Je kwanini Mkapa aliamua kujitwalia Kiwira chini ya kampuni yake ya kifamilia ya ANBEN yaani Anna and Benjamin?
Jibu hili hapa, “Watu wanaogopa maisha baada ya kustaafu urais, uwaziri, ukurugenzi ukuu kwenye shirika la umma, ndiyo maana vinapokuja vishawishi hawawezi kuhimili.”
Hakuna ubishi kuwa Taifa letu limo msambweni hasa tukizingatia malengo tuliyokuwa tumejiwekea wakati wa kudai uhuru. Ni bahati mbaya kuwa miaka Zaidi ya hamsini tangu kupata uhuru, watu wetu bado wanasumbuliwa na mambo yale yale tuliyodai tungetekeleza baada ya kupata uhuru.
Wakati na baada ya kudai uhuru, Tanzania ilisema wazi kuwa ilikuwa na maadui wakubwa wanne yaani malazi, umaskini, ujinga na dhuluma.
Baada ya kupata uhuru hapo mwaka 1961 Serikali ya awamu ya kwanza chini ya mwanzilishi wake Mwalimu Julius Nyerere ilianza kuhangaika kupambana na maadui tajwa. Kwa kiasi fulani Serikali ya awamu ya kwanza ilifanikiwa sana hasa kutokomeza ujinga, magonjwa, dhuluma ingawa umaskini hakuguswa.
Baada ya kuondoka madarakani kwa mwalimu akiwa anajivunia kuwa na Watanzania wengi wenye kujua kusoma na kuandika, wenye kupata huduma za afya hata kama hazikuwa za kisasa na wenye kuchukia rushwa na dhuluma, waliofuatia waliamua ima kwa upogo au makusudi kuturejesha miaka mia nyuma. Ghafla tulianza kusikia sera za ajabu ajabu kama vile ruksa , baadaye utandawazi na mwisho maisha bora ambavyo vyote havina tija kwa watu wetu.
Je nini chanzo cha haya yote? Chanzo kikuu kinaweza kuwa wanasiasa wenye sura mbili au Zaidi. Tutafafanua.
 Leo ukimsikia rais mstaafu Benjamin Mkapa akitoa nasaha unashangaa alikuwa wapi.
Hivi karibuni alikaririwa akiwa na viongozi wastaafu wengine wa Afrika akilaani rushwa wakati yeye ndiye alikuwa muhimili wake.
 Rejea waziri wake wa fedha Basil Mramba aliyewahi kudai kukwa alito msamaha kwa kampuni ya Alex Stewart kutokana na amri ya Mkapa.
Je kama siyo  kupewa rushwa, Mkapa aliingiliaje shughuli za wizara ya fedha bila kulishwa kitu? Ni bahati mbaya kuwa Mkapa hajawahi kukanusha wala kuzungumzia hili kwa kuhofia kuzuka mengine mengi.
Ukiacha hilo, juzi juzi Mkapa alisikika  akiwahimiza Watanzania walinde rasilimali za Taifa wakati ni Mkapa yule yule aliyezitoa zawadi kwa wawekezaji chini ya dhana yake uchwara ya uwekezaji ambao uligeuka uchukuaji.
Tuliwekeza kwa wingi lakini  tukaibiwa kwa wingi zaidi. Tutatoa mifano.
Wakati Mkapa akijisifu kuvutia wawekezaji, Taifa letu liliingia mikataba mingi ya kijambazi kiasi cha uwekezaji kuwa chanzo cha maafa yetu badala ya nyenzo ya ukombozi.
Ni bahati mbaya sana kuwa Mkapa amesahau yote kiasi cha kudhani wengine nao wamesahau.
Nani hakumbuki Mkapa alivyofikia hata  hatua ya kumnyang’anya uraia Jenerali Ulimwengu kutokana na magazeti yake wakati ule kuanika rushwa na ufisadi wa Serikali ya Mkapa? Nani hakumbuki msemo wake maarufu wa masimango kwa waliompinga au kumwambia ukweli wa “ wana wivu wa kike na ni wasomi uchwara”?
Leo ukimsikia Mkapa unaweza kudhani ni  mzalendo wa kweli wakati siyo. Sura mbili za Mkapa zinanikumbusha sura nyingi za aliyewahi kuwa kiongozi wa juu Edward Lowassa ambaye amejitokeza kuwa mtetezi mkubwa wa wananchi,  wakati ni Lowassa yule yule aliyewadhulumu hao hao wananchi kwa kuingiza kampuni la kijambazi la Richmond lililoiba pesa ya walipa kodi na kulifiilisi shirika lao la umeme la TANESCO kiasi cha mgao na ulanguzi wa umeme kuwa the order of the day. Je huu si undumila kuwili?
Tuhitimishe kwa kumshauri Mkapa kuwa anafikiri na kukumbuka kabla ya kusema. Vinginevyo anazidi kutusimanga kwa kutomchukulia hatua kwa madhambi aliyotutendea yeye na wenzake.
Ushauri wa bure kwa Mkapa na wengine wenye mawazo kama yeye. Hakuna anayependa kutegemea Serikali kumletea maendeleo.
 Pia hakuna anayetaka kuongozwa na Serikali zigo inayomuibia maendeleo kutokana na wakubwa zake kuiba, kutumbua na kutapanya mali na fedha za umma kama alivyofanya kwa kujitwalia mgodi wa umma.

Chanzo: Dira Novemba 25, 2013.

Monday, 25 November 2013

Angola yaharamisha Uislam akili au matope?

Angola Bans Islam
Taarifa zilizotufikia ni kwamba taifa la Angola limekuwa la kwanza duniani kuharamisha Uislam kwenye ardhi yake. Hatua hii imekuja kutokana na juhudi za Angola kupiga marufuku dini na madhehebu ambayo hayamo nchini humo kisheria.Taarifa nyingine zinasema kuwa serikali imeanza kuangusha misikiti huku iliyonusurika kuendelea kufungwa hadi hapo baadaye. Je hatua hii italisaidia au kuliumiza taifa hili lililokwishaharibiwa na vita? Je marufuku hii ni ya kudumu au ya muda. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

Sunday, 24 November 2013

Are we blessed or cursed?

 
The adage has it, "blessed is the hand that giveth than the one that taketh"
Forgive me. When I remember this maxim and look at how African presidents go shamelessly cup in hand begging, I feel infatuated and reduced to a gawk.
When I survey all riches and wealth our continent is endowed with, truly I feel bad and nauseated. That is when the urge to share my feelings with my readership, twanging like hell, pop in.
I am not writing this to satirize anybody. It is a self-reflection aiming at knocking sense into heads so that we can re-correct ourselves as we kick start the whole process of getting out of this mess-cum infamy.
I still remember seeing one former regional commissioner of Dar es Salaam expelling the matonyas from his Heaven of Peace. They’re degraded and shoveled into trucks like sand ready to be dumped in rural areas where everything sinister is sent. Had he known that he’s acting like a croc laughing the gator!
When this was going on, I just asked myself. "What if one day donor nations do the same to their Matonyas in suits?"
Yes, these guys can do. They've third world countries to dump their cargo.
I went on self-quizzing. "Was it the scenario of nyani that does not see its butt?
I didn't get the answer. For I still see no difference between a beggar in expensive vehicles and suits and the one in rags. A beggar is beggar so to speak.
Does the beggar feel comfortable about begging? Who knows? If I were one, I think, I’d not even walk around in the streets thump up and chest beating for begging.
 Even when I come back from begging missions I’d insinuatingly report my mission not with pomp and confidence as I always see some other punks do in some quarters.
I remember the guys in Brazil. After finding that begging is degrading, they turned to organizing and sensibly using their resources and now they’re picking up some speed to Canaan!
Yes one person’s trash is another’s treasure. The sage has it. The minerals we’re abusing like trash are but treasures for others. Some like China are even watering their lips wishing they’d a tenth of what we’re abusing!
Is it the tale of giving a coin to a dog or playing music to the goat? Nay, I don’t think so. Let us stomach it. How many arms do those we beg have?
Do you remember the biblical Zacchaeus? When he went to Jesus seeking salvation he found that he’d what it take but he’s his own obstacle!
Looking at minerals in Kahama, Buzwagi, Geita, Mwadui, Makongorosi, animals, rivers, oceans, rivers, lakes and what have you, like Zacchaeus, I find myself muffled! This reminds me of Mwalimu Nyerere who once said "You have all wealth. But you’re sitting on it" He’s pretty rights in couple of things the chief of which is not to misuse the minerals. His was to reasonably and diligently make use of them in future. Sadly though, this future’s no more. If it is, it is nothing but a letdown!
Nyerere wanted to jump start the process by laying foundation. He educated and inoculated his people to prepare them for the future he foresaw. Sadly again, he didn't know that sometimes the lion can sire a hyena!
He didn't foresee the fact that contagious diseases like selfishness, hopelessness, uselessness, greed, corruption, myopia, wealth worshiping and other hitches would strike!  
Nyerere’s failed by his disciples. Has this vice been stamped out of the society? To know this well, remember the factories, schools, hospitals, dispensaries and shambas he established without languishing in begging. Where are they now? We’ve pointlessly and senselessly thrown them to investors. Have we ever evaluated how much we get as a hunk or are we satisfied with what a few individuals from this art of destruction?
As a nation, I am sure it’s sad. But as for a few individual success can be seen. We've secret millionaires even billionaires.  There’s a downfall though. What does it help to have a drop of millionaires amidst the ocean of paupers who live on less than a dollar a day? Shame on you!
You know what. I command much respect for being a factory of words. I put smile on faces. But do you know the secret behind all this success? Let me whisper it into your ears. "I went to free schools during Mwalimu’s era" Warning though. Don’t try or dream about this presently. People will laugh at you.
Note of reminder. By then there were no hundreds of mines even tourism was boycotted because the old man’s a staunch socialist who refused to self-degrade and being cheated by money printers and minters in the name of economic adjustments and other blah-blah. He did all above mentioned as a free leader not ruler. He didn't have his hands and legs tied on conditions and orders from abroad.
Mchonga used to rant even rave at the so-called donors now we revere. They indeed feared and respected him. His was not like what we’re facing today whereby donors are yet other gods!
I know many people don’t like them. But this is vindicating them. They’re not forcing anyone to go beg from them. Theirs is business as usual. Theirs is to make profit not humanity. Sometimes we blame these guys for no reason. We want them to be fair. Perfect. Are we fair to our hoi polloi? We complain they’re exploiting us. Well. Aren't we exploiting ours? Some are exploiting even their wives and kids by rooting family treasurers! Donors have aids to show. What do we have? Donors even discipline themselves when it comes to spending their tax payer’s money. What of us?
Please understand me. I've visited many rich countries. I've never seen the leaders of these countries wasting a lot of time and resources on merrymaking things like us. Let’s face it and fear each other not. One day I’ll survey how the leaders of developed countries do their business. I’ll go as far as visiting the lives of their spouses who are always in oblivion not in lime light like ours. While the leaders of developed countries are building their societies; we’re fond of building castles whereby our country is a pauper? Why aren't we ashamed of this hopelessness-cum uselessness?
Our counterparts are using medium size vehicles for the business of their governments. Contrary though, we’re fond of oil guzzlers and long and large motorcades almost for every who’s who in the government. Sadly, even our spouses, vitegemezi, who never see a ballot box, are enjoying the same king size motorcades.
Source: Thisday Nov., 25, 2013.

Saturday, 23 November 2013

Mlevi amuomboleza Dk. Mvungi



Kwa majonzi na moyo uliopondeka, mlevi leo kwa namna ya pekee anaomboleza kifo cha gwiji wa sheria Dk. Sengondo Mvungi aliyenyotolewa roho na walioitwa majambawazi.

Je! kweli aliuawa na majambazi au maadui zake wa kisiasa? Napata shaka hasa pale ndata wanaposema eti wamekamata bastola yake lakini si kompyuta mpakato au laptop kwa kimakonde. Je! kunani? Kwanini wapate bastola lakini washindwe kupata mpakato wake?

Sambamba na kuomboleza kifo cha Mvungi, naomboleza kifo cha kaya. Maana kaya si salama tena hasa wakati huu ambapo wanaopaswa kupambana na ujambazi wanaupamba. Imefikia mahali hata nikipata kanywaji na kuvuta mibangi yangu sijihisi raha kutokana na woga wa majambazi.

Sambamba na haya, naomboleza kifo cha njuluku zangu zinazoibwa kila siku na kutengeza mabilionea kwenye kaya ombaomba na kapuku ya kutupwa.

Kesho sitashangaa kusikia hata wauza dini wenye roho mtakachafu wanayemuita mtakatifu kuwa kwenye orodha ya mabilionea wetu wa kutia shaka ingawa si wote.

Hapa mzee Mengi na Bakhressa inabidi mnielewe. Sina ugomvi na ukwasi wenu. Waliobaki niwie radhi, sina imani nanyi. Nina sababu. Huwezi kuwa mtuhumiwa wa EPA, Richmonduli na Kagoda ukawa bilionea wa kweli zaidi ya kibaka na jambazi anayeitwa bilionea kwa makosa.

Huwezi kuwa mbunge anayelinda maslahi ya biashara uchwara za baba yako inayoitwa yako ukawa bilionea wa kweli. Hivi ubilionea mnaujua au mnausikia tu?

Huwezi kuwa bilionea kutokana na kukwepa kodi, kutorosha pesa yetu, kuwauzia walevi bidhaa mbovu na upuuzi mwingine. Kwangu wewe ni kibaka au niseme mbaka mkubwa tu hata kama kuna wanaokudanganya na kukuita mheshimiwa.

Wewe ni mheshimiwa anayepaswa kunyea debe Segerea na Ukonga. Bahati yenu mnao wezi wenzenu wanaowadekeza na kuwakingia kifua. Siku nikichaguliwa kuwa munene, nitawanyonga kama kuku kama si kuwapiga mpini kama mbwa mwizi. Nina hasira kutokana na jinsi ujambazi wenu ulivyomuua rafiki yangu Dk. Mvungi.

Turejee kwa Dk. Mvungi. Hakika alikuwa mlevi wa midahalo na muumini wa dini tofauti nami ambaye dini yangu ni kanywaji na tubangi na kubwabwaja.

Tulikutana kwa mara ya mwisho pale South Law Chembers aliyoianzisha na Dk. Harrison Mwakyembe mwaka 2002 pale Mnazi Mmoja mtaa wa Lumumba zilipokuwa ofisi zao.

Tulibishana sana juu ya uhalali na ukweli wa dini. Katika mabishano yetu alionyesha utaalamu wa kujenga hoja na kuhimili maswali yangu chokonozi na ya kilevi na kibangibangi.

Dk. Mvungi alikuwa mwalimu sawa na mlevi tofauti ni kwamba yeye hakuanzia ualimu kama mimi. Alifundisha chuo, nikafundisha sekondari ingawa kama majadiliano ninayofanya yataenda vizuri, niko mbioni kufundisha chuo lau niitwe lecturer au profesa. Hayo tumuachie mwenyewe bwana mkubwa aliyeko juu.

Dk. Mvungi alibobea katika sheria sawa nami niliyebobea katika ulevi na usuluhishi wa migogoro. Cha kujivunia ni kwamba alikuwa msomi wa kweli na siyo wale wa kughushi tuliowazoea kayani.

Historia yake inasema kuwa alianzia uandishi wa habari bila kuusomea wakati mimi nilianza uandishi kabla ya kuusomea na baadaye kuusomea.

Alipata shahada yake ya mwisho nje kama mimi ingawa hakufanya kazi majuu kama mlevi mwenyewe.

Nakumbuka, Dk. Mvungi alikuwa mwalimu wakati nikisomea sharia pale chuo kikuu cha Manzese ingawa hakunifundisha. Alikuwa mtu mchangamfu na mwenye kuchanganyikana na watu bila kujali makando kando ya vyeo na usomi kama viherehere, wanywanywa na malimbukeni wanaodhani kuwa kusoma ni kujitenga na watu wakati ni kuwatumikia na si kuwatumia kama ilivyo kwa wengi kwa sasa.

Alikuwa mpare ambaye hakuujua ubahiri. Alikuwa mtu wa watu tofauti na wengi wa hadhi yake waliojiona wametoka anga za juu.

Kitu kingine cha kukumbukwa ni kwamba alipenda haki sawa nami ambaye niko tayari kuifia kama alivyofanya.

Ukipenda na kutenda haki, ujue you are on the line those thinking you’re in their way will nary let you live longer. Again, is there any person who won’t return the number? Shame on Mvungi’s killers whoever they are! Looooh!

Naona mibangi na gongo vimechanganyikana na kupandana kiasi cha kunilazimisha kuongea kimombo na kisambaa, oh tate nane tate nane.

Thijui ninyamaze niache kuthema haya ninayothema au? Vudee mpo? Hi five basi!

Nalaani waliomuua, wawe majambazi au wanasiasa.
Katika kuomboleza kifo cha rafiki na msomi mwenzangu Dk. Mvungi, acha niushukie ujambawazi mbuzi. Ujambazi umekuwa tatizo linalolelewa na kuengwa engwa na wenye pawa kwenye kaya. Nasema ukweli hata kama ni kilevi.

Nilijisikia vibaya kiasi cha kutaka kugeuka gaidi nilipoona wale waliotuaminisha kuwa wanaweza kupambana na ujambazi wakati wakiupamba nao kwenda kuwahani wafiwa na kupewa nafasi za juu wakati kazi yao ndiyo matokeo ya kifo cha marehemu.

Wako wapi waliotwambia wana orodha za majambazi wakaishia kula na kulala nao? Niliumia kusikia kuwa majambazi wa Kagoda walitangazwa mabilionea kayani wakati wa msiba wa Dk. Mvungi.

Kutokana na hujuma aliyofanyiwa Dk Mvungi, mlevi napanga kuhamia uhindini Kariakoo na Posta ili kuishi mahali salama. Nikipanga kuhamia Oyesterbay na kwingineko kwa wenye nazo sitaweza wakati sina fweza ya ufisadi wala bwimbwi?

Acha nihamie kule tubanane huko hata kama sina sifa ya kuishi kwenye nyumba za dezo za Asajile Mwaijumba. Nitalazimisha hivyo hivyo hata kama sina magendo na dili za kuficha. Heri kuwa mtasha mweusi wa Kariyakoo au Postale kuliko kuwa marehemu nikiwa bado wamo. Kama wakubwa wameamua kututosa unategemea nifanye nini?
Kwa vile nina majonzi ya kuondokewa na mlevi mwenzangu, acha niende kupata kanywaji huenda nitaganga hasira na mavune yangu. Rest In Eternal Peace (RIEP) Sengondo Mvungi my friend. 

Chanzo: Nipashe Jumamosi Nov., 23, 2013.