Kwa wanaojua kilichompata akina
Augustine Lyatonga Mrema, kuna uwezekano kuwa kinachoendelea ndani ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni mwanzo wa mwisho wa mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA.
Kama Mrema, Zitto alilelewa na
CHADEMA sawa na Mrema na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kama Mrema, Zitto ameponzwa na tamaa kutaka
madaraka, sifa na kuonekana ni bora kuliko wengine. Kama Mrema, Zitto
ameonyesha papara na uchu mkubwa wa ukubwa. Kama Mrema, Zitto ataondoka CHADEMA
na CHADEMA haitakufa sawa na Mrema na CCM.
Tofauti ya Mrema na Zitto ni
kwamba Mrema aliondoshwa CCM si kwa kutumiwa na chama kingine zaidi ya mipango
yake ya kuusaka ukubwa. Hapa unaweza kuwaunganisha watu kama Seif Sharrif Hamad
ambaye kuondoka kwake CCM hakukuiyumbisha sawa na alivyoondoka Mrema sawa na
itakavyokuwa kwa Zitto na CHADEMA.
Tofauti na Mrema, Zitto
ameondolewa mapema mno. Hakufaidi ulaji ndani ya serikali kama ilivyokuwa kwa
Mrema aliyejijengea sifa ya utendaji hata kama ulikuwa wa kiimla na kihuni.
Zitto anaingia kwenye vitabu vya
historia kama kijana aliyeanzia kwenye mavumbi ingawa anawez akurudi kwenye
mavumbi kama hatarejea CCM ambao wanadai kumtumia. Ushahidi ni ile hali ya
mkutano wake na waandishi wa habari kuandaliwa na kusimamiwa na UVCCM jambo
ambalo Zitto na wenzake hawajakanusha. Huenda watafanya hivyo ingawa it is a
bit too late too little.
Hakuna nyundo itakayommaliza
Zitto kama kukiri kwa “mtu wake”, Dk. Kitila Mkumbo kuwa kweli waliandaa waraka
uliowatia kitanzini pamoja na juhudi za bila mafanikio za kumtenga Zitto na
waraka huu.
Maswali makuu,: Kama kweli Zitto
hakuhusika na waraka husika wa uhaini na usaliti chamani, kwanini hakuukana
alipokutana na waandishi wa habari? Kwanini Zitto alikuwa too apologetic and
diversive kwenye press conference yake? Kwanini Zitto aliruhusu waasi
waliokwisha aangukiwa na panga la CHADEMA kuupamba mkutano wake kama hakuna
namna?
Je mwanzo wa mwisho wa Zitto
ndiyo unaanza? Je ni mapema kuanza kuandika tanzia yake kisiasa au kutegemea
kumuona akifufukia CCM?Je kweli Zitto hakutumiwa na CCM iwe kwa bahati mbaya au
makusudi? Rejea uhusiano wake na marehemu Amina Chifupa.
No comments:
Post a Comment