Hakuna ubishi kuwa rais Jakaya Kikwete ataingia kwenye vitabu vya historia kama rais aliyehudhuria misiba na maziko mengi kuliko waliomtangulia. Kwa juu juu hili linaweza kuchukuliwa kuwa ni mapenzi na kuwajali watanzania. Kwa undani, rais anapaswa kutupiwa lawama za kuwa legelege kwenye kupambana na ujambazi, ufisadi, mihadarati na jinai nyingine zinaua watanzania wengi. Blog hii pamoja na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Sengondo Mvungi, inamtaka rais Kikwete aache kushabikia misiba. Badala yake awahakikishie watanzania ulinzi.
6 comments:
Akienda Atalaumiwa Asipoenda Atalaumiwa,wacheni kulalamika kama mabahalula,au wanawake wa mama ntilie
Mbona Nyerere hakwenda na hakuna anayemlaumu acha ushamba hata kama umepewa uhuru wa kujieleza, angalia kinachoongelewa badala ya kudandia hoja.
Mhango, nafikiri huyo jamaa wa juu ndiyo yule juha aliyempigia magoti Kikwete mchangani kwenye hizo picha ulizoweka nyuma.
Jaribu hujakosea. Kuna mijitu bila kujikomba na kutupiwa makombo haiishi. Wengine hata hayo makombo hawapati zaidi ya kuwa na ugonjwa wa kujipendekeza. Ogopa njaa hasa ya upstairs kaka.
Otherwise vipi makazi mapya?
Kila la heri
Poa, ingawa Louisina vitu vingi vya Kiswahili sivipati, kama nazi na dagaa kwa sababu ni watu wachache. Lakini katika kusaka ugali inabidi ukose mambo mengine, kwa hiyo silalamiki sana.
Mie navipata sana kuanzia Nazi, ugali wa ulezi hata nyanya chungu kwa ajili ya bi mkubwa.
Kila la heri ndugu yangu.
Post a Comment