- BAADA ya tapeli a kisiasa Mwigulu Nchemba kufanikiwa kuwarubuni vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ni mkereketwa wakati ni mganga njaa aliyeshindwa kitaaluma, ametengeneza utambuliko wake maalum akitaka aendelee kujiandalia maisha ya kupewa ulaji zaidi hata ikiwezekana urais kama ilivyotokea kwa Jakaya Kikwete. Kikwete alipomaliza chuo kikuu na kujikuta hana sifa za kuajiriwa kwenye kazi za maana aliamua kujirejesha chamani ambako alipanda taratibu hadi kuwa rais. Huenda kwa kuangalia trajectory ya Kikwete, mropokaji Nchemba naye ameamua kujijengea mazingira. Hata hivyo si kwamba nataribi. Naamini atapotezwa kabla ya kufika popote na kama siyo kuzikwa kisiasa baada ya Kikwete kuondoka madarakani. Hakika ivumayo haidumu. Angalia anavyojivisha magwanda ya ajabu ajabu ili aweze kujitofautisha na wababaishaji na mafisadi na mafisi wenzake ambao bila shaka hawatapenda hii. Haya magwanda yenye kufanana na jeshi hata kama siyo la wananchi yangevaliwa na upinzani bila shaka jeshi lingetoa karipio kwa vile limo kitandani na CCM. Pamoja na malengo binafsi, licha ya huu kuwa upogo na upendeleo ni uhuni wa kawaida unaopaswa kulaaniwa na kuzuiwa na wananchi mara moja.Inakuwaje mhuni mmoja na msasi wa ngawira aruhusiwe kuvaa bendera ya taifa kienyeji hivi hivi?
How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Friday, 28 February 2014
Ijue sare ya Jeshi la Mafisadi Tanzania(JMT)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Kweli inatisha
Je tufanyeje kupambana na manyang'au hawa?
Post a Comment