How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 16 January 2018

Je ndugu Reginald Mengi anajua dhuluma inayofanyika kwenye magazeti yake?

            Image result for photos of reginald mengi     Image result for photos of gaudensia mngumi   Nimeamua kutundika makala hii lau kwa sababu kuu kadhaa. Mosi, ni baada ya kudai malipo yangu kwa ndugu Reginald Mengi kwa kufanya kazi katika magazeti yake kwa miaka mitatu bila malipo. Pili, kuzungushwa kiasi cha kuhisi huenda kuna kamchezo ambako wengi wasio na ujasiri wala uwezo wa kupambana nako wanakwazwa nako. Tatu, uwezekano wa hujuma hata kutokuwa na mawasiliano mazuri katika makampuni ya Mengi. Nne, kutaka wahusika wajue kuwa huu ujipu wao hauvumilki na wanachofanya ni dhuluma. Tano, kutaka wahusika wawajibike tokana na umma kujua mambo ambayo kimsingi ni kinyume cha wanavyojionyesha au kujitangaza.
                     Sijui kama  mzee Mengi anajua kuwa kwa sasa wachangiaji wengi kwenye magazeti yake wamekuwa wakidhulumiwa kwa madai mbali mbali na hasa wengine kutumia mbinu ya kukwepa kuwasiliana na wahusika au kusimamisha huduma yao bila kujali hata madhara kwa pande mbili. Maana anayelaumiwa kwa sasa si mwingine isipokuwa Mengi mwenye makampuni yake.  Mfano, mimi nilipewa safu mbili na nikachangia kwenye magazeti ya the Guardian on Sunday na Nipashe Jumamosi kwa miaka mitatu mfululizo bila malipo. Kila nikiulizia malipo yangu nilikuwa nikiambiwa kampuni haina fedha kwa sasa. Je hii ni kweli? Sikuamini mtu kama ndugu Mengi anayesifika wka ukwasi wake kuishiwa kiasi hiki. Hivyo, nachukulia kilichofanyika kama visingizio vya kufanyiwa dhuluma kitendo ambacho si haki na ni ushenzi. Ushenzi huu niliofanyiwa na magazeti ya Mengi ulisimamiwa na watu wawili mmoja mhariri wangu Gaudensia Mngumi ambaye sijui kama ni mzima kiakili ukiachia mbali kuonekana wazi kuwa kihiyo wa kutupwa. Wa pili ni Edmund Msangi  bosi wa Gaudensia ambao wote ni kabila moja. Sijawahi kufanya kazi na watu wapuuzi na wenye ujinga kama huu. Mpaka sasa nashangaa Mengi alivyowaajiri majipu kama haya.
                         Kwa ufupi, msomaji, haya ndiyo yaliyonikuta ambayo nimeamua kuyaweka wazi hapa lau wahusika wajue kuwa hakuna anayevumilia dhuluma na ufisadi wao. Nashauri wote walioathrika kama mimi wajitokeze lau dunia ijue aina ya watu tulio nao nchini.
Kwa ufupi, kwa wasomaji wangu waliozoea kusoma makala zangu toka kwenye magazeti tajwa, siko tena na nimedhulumiwa. Habari ndiyo hiyo.

2 comments:

Anonymous said...

Inaonekana tangu uhamie ughaibuni umesahau mauzauza ya matajir wetu uchwara. Nimjuavyo Mengi si tajir wa haki . Laiti siri na ufisadi wa awamu ya mzee ruksa vingemfumliwa, Mengi angebaki bila nguo. Si kama alivyo. Tangu Magufuli aingie madarakani mafisadi na wapigaji wengi wanabangaiza na kuungaunga huku wakiwaibia msiowajua kama nyinyi. Pia kuna uwezekano hao wahariri wako wakawa ndiyo wezi wako. Pole sana kaka yangu. Hiyo ndiyo bongo yetu iliyobakia.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Ndugu Anon.
Shukrani kwa uliyonijuza. Nitayafanyia kazi.