Kwa waliiosoma zile enzi za gold watakuwa wanakumbuka waticha walivyotufyatua hadi tukafyatua masomo kama hatukuwa na akili nzuri. Nikiwa nakumbuka enzi hizi, si juzi nilipigwa na butwaa nusu kanywaji kanifyatue. Ni pale kitegemezi chetu Fyatu Junior kilirejea toka skuli.na kutua home kwa madaha, madoido, na ngebe. Bila ajizi, nilifyatuka na kukiuliza kitegemezi kama kilikuwa kimeshinda mtihani. Tofauti na siku zote, kilikuwa kina bashasha na furaha hadi nikafyatuka na kustuka kunani? Baada ya kutoka airport na kutua home, Fyatu Jr. alichonoa gazeti akunipa nisome. Lahaula Walakuata Illabillah! Sikuamini macho yangu. Ilibidi niazime miwani ya Bi Mkubwa lau nisome kitegemezi kilichotaka nisome.
Baada ya kuwafyatua mafyatu wakanipa unene si nilipeleka kitegemezi chetu intaneshno skuli kifyatue elimu nisijue watakifyatua kifyatuke hadi kinifyatue!. Kwanza, nilidhani kilikuwa kimeshinda mtihani. Kabla ya kukipongeza, niliuliza kilikuwa kimeshika nafasi ya ngapi. Bila ajizi, si kikanifyatua na habari iliyoinifyatua nusu nipate kichaa. Hata kabla ya kuniruhusu nifyatuke na kujua kunani, si kilifyatuka kilifyatuka kuwa tangu siku hiyo, maticha walikuwa wamepigwa marufuku kufyatua fimbo wanagezi! Hivyo, kitakuwa kikienda shuleni wakati ambao kingeamua na kuchagua masomo ambayo kingetaka.

Kwa vile mie ni bonge la mwanafalasafa, niliamua kufyatuka na kukifyatua. Nilikipasha kuwa kuanzia siku hiyo, kitakuwa kikichangia gharama za maisha zilizopaanda pale kayani. Kabla hata hakijajibu, nilikifyatua tena kuwa kitakuwa kikijilipia karo na tozo za ufyatuaji na upigaji zisizo na kichwa wala miguu zisizokoma huko skulini kwake. Furaha na ngebe kilivyokuja navyo, ghafla, vilifyatuka kikaufyata na kuelewa kuwa ufyatu wangu si wa kufyatuliwa tena na kitegemezi nilichokifyatua mwenyewe. Bila aibu, kilifungua friji kutaka kuchukua soda. Nilikifyatua kuwa kuanzia siku hiyo, kitabidi kinunue friji yake na soda zake vingenevyo viboka na mengine home ruksa.
Baada ya muda, fulifanya kikao na Bi Mkubwa kutathmini namna ya kufyatua kitegemezio fyatu kilichofyatuka kikataka kutufyatua kisijue tungekikifyatua kwanza. Hivi, hawa waliokuja na huu utopolo na uzwazwa wanazo au wanajifyatua na kuiga mambo ya kitasha. Kama kaya inataka kutenda haki kuzuia huu ukatili wa viboko, basi tuliamua kuja na mkakati wa kuwashauri mafyatu wanene mazwazwa wanaofyatuliwa kizwazwa na kutaka kujifyatua na kuufyatua uzwazwa huu.
Mosi, sasa nafyatua rasmi. Kuanzia sasa, wale wote tulioramba bakora za maticha tulipwe fidia. Hatutaki dhuluma. Eti kitegemezi kifyatuke na kukosea nikiache! Haya maisha au masihara? Eti kitegemezi kikifyatuka na kulia ukipe simu au badala ya kukifyatua konde au bakora, ukiombe msamaha! Kutokana na kadhia hii, napanga kupeleka mswada kigwenani utanaotaka mamlaka zifyatuke na kufanya kweli. Mfano, kama viboko ni unyanyasaji, basi vitegemezi vikitenda kosa lolote vipelekwe kwenye kituo cha ndata na kufunguliwa kesi. Pia, watoi waruhusiwe kufyatua mambo yote ya kiutu uzima tunayofyatua. Wakitaka kuoa au kuolewa, kunywa, kuvuta, kuchelewa kurudi kaya, hata kuacha skuli, ruksa.
Pili, napendekeza vitegemezi vipangiwe zamu ya kununua matumizi yote ya nyumbani. Kufanikiwa, lazima viwe ana ajira au namna ya kujipatia kipato. Vikitaka na ajira, madingi wote wanaofanya kazi au kuwa viongozi waachie ngazi ili kaya iendeshwe na vitegemezi kitoto muone ngoma itakavyo noga japo ngoma ya kitoto huwa haikeshi. Kadhalika, vitegemezi viruhusiwe kuopoa au kuopolewa na mishaangazi na mibabu mikware navyo vifaidi tunayoyafaidi kama kweli kuna kufaidi kama siyo kufyatuliwa kizwazwa. Mambo yakienda ndiyo siyo, tusilaumiane.
Tatu, baada ya vitegemezi kukabidhiwa majukumu ya kiutu uzima, itungwe sheria kuwa yeyote atakayemkoa, kumfyatua bakora kitetgemezi hata kumfinya apelekwe kwa pilato. Kitegemezi kikichelewa kurudi hata kulala nje, kisiulizwe ili kifaidi huu uhuru usiona mipaka japo una udhuru kwa pande zote. Kwa vile vitegemezi visivyopenda kuamka mapema, visiamshwe kwa vile vikichelewa skuli, hakuna adhabu. Badala yake vipewe biskuti, pipi, na simu vikajiejoi. Kama kweli nia ni kutenda haki, basi vitegemezi viruhusiwe kwenda baa na kupata kanywaji halafu muone ngoma itakavyonoga. Vipewe leseni za kuendesha magari na hata kugombea urahisi, uishiwa, na ulaji mwingine.
Japo mashabiki wa ufyatu zwazwa huu wanaweza kujifyatua na kuona balaa hili kama usasa, tuweni makini na wakweli. Hivi watoi wakianza kuwageuzia kibao, mtamlaumu nani au nanyi mmejifyatua na kugeuka watasha msijue nyuma pazia mnafyatuliwa? Je, tunashabikia uzwazwa huu utokanao na wengi kujihisi watasha wakati hawajawahi kutia mguu majuu? Hivi, mnajua wenzenu walivyofyatuka wakajifyatua na kuacha vitegemezi viwafyatue hadi wanakufa bila msaada kama vile hawakuzaa, kulea, kusomesha wala kufanya lolote? Haya, jifyatueni kipofupofu na kizwazwa ila msilaumu kuwa profesa sikuwaasa tena bure.
Huyu dogo kachelwa. Ngoja nitafuta bakora yangu nimfundishe nilichomfunza mgoshi Machungi. Ama kweli wamejifyatua na kujichanganya na kujua kututenda.
Chanzo: Mwananchi Jtano juzi.

No comments:
Post a Comment