The Curse of Salvation

The Curse of Salvation

Tuesday, 11 April 2017

Mpayukaji anapogeuka mwimbaji rap

makondaa

I vividly see it coming
Yes, it is truly coming
I can hear people fervidly yelling
Yes, I see them surreptitiously infuriated
The time is coming
When everything
Is going to be alarming
I see it coming
Yes, it is indeed coming
Bashite is packing
Yes, he will be soon going
 Mr Biggie must be thinking
To justice being done.
            Kwa wasiojua kitasha tusameheana. Kimsingi, kinachoongelewa ni kwamba ngome zitaanguka au kwa kinyasa ndoga ziyawa zawelale. Maana ngoma hii ilivyochefua na kutega wengi, nani alijua kuna ambao wangeramba matapishi yao na kuisifia na kudai wanaipenda wakati waliiponda?
Tokana na wengi kujiingiza kwenye mambo ya rap, nami kama Mpayukaji mtakatifu na mkuu nimeamua kutia timu lau nisikike hadi wahusika waipate kama siyo kunipata. Siogopi kufungwa hata kuzodolewa. Hapa lazima niangushe mistari lau ujumbe uwafikie wahusika. Guess what. Baada ya Nay wa Kutega kuwatega wakategeka, nami ameninasa kiasi cha kuvamia kunga kama si fani. Hapa lazima nifunge nyama ili farasi wafungiane nyama na nyangwa. Naweza kuonekana kijana wa zamani, ila bado ninayo mapya tena mapya kweli yanayowakonga roho wanene.
Japo si mpenzi wa ma-rap na marapu rapu tokana na kelele zake ukiachia mbali wanaoyatoa kuonekana kama hamnazo japo wanazo, huwa sipendi miziki hii. Lakini tokana na wimbo wa Wapo, nami nimejikuta nipo. Hivyo kuja na vimbwanga hivi uvisomavyo.
Ngoja nirejee wimbo ulionikuna kiasi cha kunisukuma kuvamia fani isiyo na wenyewe.
Naanza kushuka hivi:
A free hunk that’s never enjoyed freedom
Yes, it’s the hunk of doom
Vroom
 Acha niimbe kwa kimakonde
Nasema wapo
Wapo yes wapo
Tena wapo wapo
Wapo hapo hapo
Nasema wapo na kweli wapo
Wapo wanaoburuzwa
Sema wapo
Wapo wanaoburuza
Sema wapo
Wapo wanaojishebedua
Sema wapo
Wapo wanaoogopa kukosolewa
Sema wapo
Wapo wanaojua jua hata kama hawajui
Sema wapo
Wapo wanaobangaiza
Sema wapo
Tena wapo wateule
Sema wapo tu
Wapo wanaojigonga
Sema wapo
Wapo tena wengi
Wapo akina Bashiiit
Wapo tena sitawashit
            Kwa wasioinyaka, huu ni usawa wa kupenda rap. Mimi ni nani iwapo hata mzee M7 siku hizi ni rapper? Mimi ni nani nisiwape rap. Do you need more rap? Tell me. Do you need more rap?
            Naona yule anatikisa kichwa akidhani nafanya yote haya tokana na kanywaji au bangi.  Ushindwe. Kama hujaelewa somo basi umekwisha. Hujui kuwa baada ya jamaa wenye mabavu kutaka kila mchovu anyamaze, tumegundua namna ya kuwapa vipande vyao? Kama si rap, nani angewashikisha adabu akina Bashiit hadi wakajipiga mtama na kuramba matapishi yao? Ukisikia wapo wanaoramba matapishi na kujipiga ntama jua wapo? Nikisema wapo nawe jibu wapo.
Wapo walioanza kuharibikiwa, jibu wapo.
Wapo wanaochezea nafasi zao kwa kulinda makapi, sema wapo.
Wapo wanaojifanya miungu watu, sema wapo, wapo wanaojifanya wanajiamini wakati ni woga wa kawaida, sema wapo.
Wapo wanaofikiri kinyume, sema wapo.
Wapo walioghushi vyeti, sema wapo.
Wapo wakiulizwa  wanasingizia mihadarati, sema wapo.
Wapo akina Dav Bashite, sema wapo.
Wapo  waliojisahau, sema wapo.
Wapo wanaopinga kila kitu, sema wapo.
Wapo wanaochuuzana, sema wapo.
            Hebu tuache utani. Kwanini tusiwashauri wapingaji kugeukia rap ili hoja zao zisikike na kuheshimiwa. Maana baada ya kuona akina Rema wakipotezewa muda lupango, kuna haja ya kutafuta mbinu nyingine ya kupeleka ujumbe. Najaribu kupiga picha mzee Freeperson Mbhowe akiwa kwenye gwanda lake akila mic na mzee Sugu huku Joni wa Nyika na Tunda Lisssu wakimwaga vibwagizo kabla ya mzee Eddie Ewassa na Freddie Sumuye wakimwaga mistari ya kiutuuzima. Ngoma itanoga pale mzee wa Madevu kutoka mitaa ya Uondwe akimwaga vina kwa chati kabla ya mzee Ibra Pumba kumtungia mipasho ya kumpinga.
            Hebu jaribu kupiga picha dokta wa Majibu akimwaga vina kuwapasha mashakunaku kuwa wanapenda udaku na kujadili watu badala ya masuala akaishia kufanya hilo hilo analowashitakia wenzake. Kabla ya ngoma kutua piga picha bi nkubwa Sammie akisuluhisha kwa kumwaga vina vya kutaka kila mmoja aheshimiane na mwenzake huku brother Katelephone Aliyejaliwa akija na mistari ya Faru Joni kabla ya dokta wa Kusheini kuja na mistari dhidi ya jamaa mwenye madevu. Mwisho wa yote ni pale walevi wakatapoingia na mistari yao kusema wamechoshwa kuburuzwa na kutishwatishwa wakati kaya hii ni yetu sote bila kujali ukubwa wa cheo cha mlevi.
            Napiga picha walevi wakiimba
“Tunataka kaya yetu, tunataka.
Tunataka uhuru wetu, tunataka
Tunataka tuheshimiwe, tunataka.
Tunataka Bashite awajibishe, tunataka.
Tunataka haki na usawa, tunataka.
Tunataka walioghushi watumbuliwe, tunataka.
Tunataka makaburi yafukuliwe, tunataka
Tunataka tuyafunike wenyewe, tunataka.
Tunataka tunataka tunataka demokrasia na heshima, tunataka.
            Naona sauti imekauka hadi kuhitaji kanywaji. Lo! Hata kumbe sijapata majani lau nitulize kichwa na kuondoa mawazo yatokanayo na kadhia ya akina Bashite!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.

I like Sepedi music


Sunday, 9 April 2017

Kikwete anapogeuka mali adimu!

Image result for photos of kikwete in parliament
            Hivi karibuni jambo moja lenye kuzua utata lilitokea bungeni ambapo rais Mstaafu Kanali mstaafu Jakaya Kikwete alishangiliwa na wabunge kuliko ilivyowahi kutokea bungeni. Wapo wabunge waliosema wazi kuwa wanammiss. Je kwanini walifanya hivyo? Hii nadhani inatokana na kutopenda au kufurahia namna mambo yanavyokwenda ndani ya serikali, Chama tawa na nchi nzima. Kwa namna hiyo basi, namuonea huruma Magufuli kutokana na kuchukiwa kwa sababu ambazo nyingine ni za kujitakia na nyingine ni matokeo ya hao hao wanaokuwa missed. Je mapenzi haya mapya ni matokeo ya ukosefu wa kumbukumbu au usanii?
              Wakati mwingine unaweza usimuonee huruma Magufuli hasa kutokana na kushindwa kufukua makaburi na kushindwa kuyafukia kiasi cha sasa kuanza kuandamwa na makaburi hayo hayo. Sijui kama na Kikwete alidhihakiwa na kujiridhisha kuwa shangwe hiyo ilitokana na mapenzi ya kweli au ngoa na visasi ukiachia mbali kujiridhisha angalau. Rafiki yangu mmoja alinipigia sifa kutaka mawazo yangu. Nilijibu kwa mkato kuwa njaa au tumbo vinapopindua kichwa, lolote laweza kutokea.  Kwani, waliomshangilia Kikwete ni hao hao waliomrushia kila dongo baada ya kudhihirisha kuwa alikuwa rais wa hovyo aliyepoteza muda kuzunguka dunia na kuacha taifa lijiendeshe lenyewe huku kila mtu akijifanyia atakavyo. Hii ndiyo maana haya mapenzi mapya yanatia kila shaka.
            Leo tutagusia baadhi ya sababu zinazofanya Magufuli achukiwe. Na ataendelea kuchikiwa sana tu kama ifuatavyo:
            Mosi, ni kutokana na hatua ya Magufuli ya kubadili mfumo na utaratibu wa kiulaji kwenye chama chake kwa kupunguza nafasi za wajumbe wa baadhi ya vikao vya chama kiasi cha kuwanyima wengi ulaji wa dezo waliouzoea bila stahiki. Hii hatua ni nzuri kwa wanachama waliokuwa wakibebeshwa mzigo; au kushuhudia ruzuku ya chama chao kuishia kuliwa na kundi dogo la wachache. Hata hivyo, kwa walionyang’anywa ulaji, watamchukia sana hasa ikizingatiwa kuwa watu wengi huwa hawapendi mageuzi au mabadiliko.
            Pili,  sababu nyingin ni kuzuia wabunge na maafisa wa serikali kuibia umma kwa njia ya vikao, makongamano na warsha na kusafiri hovyo hovyo ughaibuni kama ilivyokuwa huku wakijilipa au kulipwa marupurupu kibao kwa uzururaji huu ambao, kimsingi, haukuwa na tija kwa taifa. Hatua hii ni nzuri kwa wananchi wa kawaida waliotwishwa mzigo kiasi cha kodi yao kuishia kuliwa na genge chache la wamangimeza huku wao wakiteseka.
            Tatu, kupiga vita ufisadi na mihadarati nalo ni jambo litakalofanya Magufuli achukiwe sana hasa ikizingatiwa kuwa utawala uliopita ulikuwa ni kama umehalalisha jinai hizi. Wauza unga hawataacha njia yao ya kutajirika haraka izibwe kirahisi, huku washirika zao ambao ni maafisa wa serikali waliowezesha biashara hii kwa kupewa chao nao wakimchukia Magufuli.
            Nne, kitu kingine kitakachofanya Magufuli achukiwe sana ni ile hali  ya kuonyesha upendeleo na kukumbatia hata kukingia kifua baadhi ya wasaidizi wake wanaoonekana kuwa kama hawaguswi. Mfano mdogo ni kitendo chake cha kupuuzia kubatilisha uteuzi wa mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ambaye anakabidhiwa na tuhuma za kughushi, kuvamia kitu cha Clouds na mengine mengi kama vile ubabe hata ubabaishaji. Hili halina faida yoyote kwa Magufuli. Kwani, hata wananchi wa kawaida waliokuwa wakiunga mkono juhudi za Makonda, wameanza kuhoji kunani haguswi. Unaweza kuona utitiri wa miziki iliyotungwa kumshambulia yeye.  Wananchi watazidi kumtupa mkono Magufuli katika hili kutokana na tabia yake kutumia muda na nguvu nyingi kumlinda mtu mmoja ambaye akiondoka hakuna kitakachoharibika.
            Kinachogomba zaidi, hata Makonda mwenyewe amegundua udhaifu wa Magufuli kiasi cha kufanya kila liwezekanalo kumsifu, kufanya anachodhani kitamfurahisha rais ili aendelee kumuona mwenye manufaa kwake. Hata hivyo, mbinu hii inaanza kupata pigo hasa baada ya rais kuruhusu wimbo wa Wapo unaoongelea walioghushi vyeti ukitaja wazi wazi jina la Bashite au Daudi Bashite linadaiwa kuwa jina hali la Makonda. Pia kumteua profesa Kitila Mkumbo aliyewahi kusema kuwa Makonda hastahili kuendelea kuwa mkuu wa mkoa hata kwa wiki moja ni dalili kuwa Magufuli ameanza kuona ubaya wa kumtetea mtu mmoja dhidi ya umma wa watanzania. Kimsingi, kama Magufuli ataendelea na msimamo wake wa kumkingia kifua mtu aliyekwishachafuka, itamgharimu kisiasa bila sababu yoyote ya dhahiri wala ya msingi.
            Tano, ni ile hali ya Magufuli kujenga chuki bila sababu na vikundi vingi kama vile wapinzani na vyombo vya habari kwa kuminya uhuru wao kiasi cha kumuona kama rais mbabe.
            Sita, ni ile hali ya kujichanganya au kujipinga. Kwani alipokuwa Zanzibar kwenye kilele cha maadhimisho ya Mapinduzi alikaririwa akimshangaa rais wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar (BMZ) Dk Ali Mohamed Shein kuwapa nafasi wapinzani kwenye serikali yake jambo aliloapa kuwa lisingetokea chini ya utawala wake. Je amefanya nini baada ya kumteua Profesa Kitila Mkumbo kwenye serikali yake hata kama ni jambo jema kwa nchi?
            Tumalizie kwa kumtaka Magufuli aendelee na mageuzi huku akiachana mengine yasiyo na maana wala faida kwa taifa kama kumkingia kifua mtu binafsi mwenye matatizo yake binafsi.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili leo.

Saturday, 8 April 2017

In the Commemoration of Nomthandazo''THANDI" Mnyiphika

Although Thandi is long gone, her memory and celebrated works are still in our memories and prayers. She entertained the world. I still listen to her tunes not to mention always supporting her group Makgarebe Amacha a Bachobela. In brief I always say Ntate Theula Moya orr Almighty Father Deliver the Holy Spirit.

Thursday, 6 April 2017

South Africans’ short memories sad


 xenophobic attacks in South Africa
Thousands march against the recent wave of xenophobic attacks in South Africa through the streets of Johannesburg on April 23, 2015. Unemployment it is certainly not caused by foreigners. PHOTO | GIANLUIGI GUERCIA | AFP  
           The xenophobic attacks in South Africa targeting immigrants from neighbouring countries are the continuation of a scourge that has been going on for many years now. The motive, even motif, behind this psychosis revolves around the rampant poverty and unemployment many black South Africans face. Although it is true that this is an endemic problem, it is certainly not caused by foreigners. Therefore, attacking and sending the African immigrants packing won’t solve the problem.
CORRUPTION
            For the enemy is within and not without. Instead of addressing the real problem, which is the enduring legacy of apartheid, some South Africans wrongly believe that people from neighbouring countries are to blame for their suffering. The true sources of poverty are landlessness, ignorance and mega corruption. What the majority of the mobsters think are the causes of their miseries are not. Immigrants don’t own land or run the government that’s supposed to address this fubar situation.
               Some 75 per cent of South Africa’s arable land is in the hands of the minority whites, while the government is managed by a few blacks who enrich themselves, leaving the majority in abject poverty.
END INEQUALITY
               Interestingly, even the government seems to be at home with xenophobia because it helps distract the attention of many poor South Africans. Nevertheless, this is a temporal reprieve for the ruling class and the haves. Anybody who wants to solve the problems of South Africa must address the real causes of misery caused by inequality and corruption. This is the only way poor South Africans can solve their problems. For, once they’re done with the foreigners who happen to be fellow Africans, they’ll turn against one another. This pointlessly puts South Africa in harm’s way.
REPEATING HISTORY
               Just recently, the Economic Freedom Fighters, South Africa’s new and radical political party, tabled a Motion in the parliament seeking to have the government start expropriating land for the landless. The Motion was defeated. Land issues have always been thorny for the post-apartheid governments. No leader since Nelson Mandela has ever wanted to touch such a hot potato that is likely to trigger unrest and wreak economic havoc. Again, for how long will the authorities avoid this issue? What alarms is that the South Africans that many other African countries helped to fight apartheid seem to have so easily forgotten that they replicate the same vices they fought just a few years ago.
            In economic and realistic terms, is it true that African immigrants are the ones causing the miseries of the majority black South Africans? If you compare the wealth South African Indians own to the peanuts African refugees make in South Africa, you’ll find the allegations to be baseless and preposterous.
OMINOUS FUTURE
           It is easy to foretell what’ll happen once the South African xenophobes are done with the immigrants. They’ll turn against the rich blacks, Indians and whites before turning against one another based on ethnicity. Once they’re done with the immigrants, which, of course, is stinking discrimination, only to find that their problems are even bigger, they’ll turn against their compatriots. This is the rule. Founding Tanzanian President Mwalimu Julius Nyerere used to say that once a human tastes human flesh, he will never stop. The same perpetrators of the xenophobic atrocities could end up becoming refugees in the countries of those they’re now attacking.
AVOID DISCRIMINATION
               It will be for the second time. This time around, they won’t get the warm welcome they were accorded when they were fighting apartheid. Recently, some Nigerians took to the streets, asking their government to reciprocate by expelling South Africans. Suppose all the African countries heed the call and sever ties with South Africa, will its ailing economy survive really? Essentially, no discrimination is good whether it is committed by whites against blacks or blacks against blacks or others. It is a crime all need to abhor and fight. What’s going on in South Africa is but an antithesis to the rainbow nation that doesn’t look like the rainbow itself.
FIGHT HATRED
           Is it because the rainbow does not have the black in its colours? Is it because desperation and ignorance have been allowed to become the modus operandi for destitute South Africans? Indeed, South Africans need to be helped out of this malady. It is important to note that hate begets hate. Why’ve South Africans forgotten so quickly and easily?
Source: Daily Nation Kenya, April 7, 2017.

Wednesday, 5 April 2017

Laiti wakuu wa mikoa na wilaya wangeiga mfano wa Mjema

  Image result for photos of sophia mjema
 
            Hatua ya mkuu wa wilaya Ilala,  mheshimiwa Sophia Mjema, ya kuuzindua umma kwa kuukataa mwiko wa kuwa shuhuda wa uhujumu wa taifa letu ni ya kupigiwa mfano. Tokana na ushupavu wake,  uzalendo na ujasiri aliweza kuvamia kiwanda feki na cha kitapeli cha toys za kuchezea watoto huko Mabibo jijini Dar Es Salaam. Kiwanda hiki kinachomilkiwa na matapeli wa kihindi, licha ya kutolipa kodi tangu kianzishwe mwaka 2006, kinawalisha wateja bidhaa bandia na zisizo na viwango. Kwani, ilibainika kuwa kinatengeneza toys kwenye mazingira hatarishi  na kuweka lebo za China wakati bidhaa husika hazitoki huko. Je mamlaka za viwango zilikuwa wapi wakati upuuzi huu ukifanyika kama kweli wanafanya kazi zao vizuri na kitaalamu? Je kiwanda hiki kimeishambaza bidhaa hizi haramu kiasi gani nchini? Je kuna viwanda bubu kama hivi vingapi nchini? Je wakubwa wetu wanaohusika hawajui au kuna namna wanavyonufaika na hujuma hii kwa taifa?
            Tokana na hatua hii ya kipekee na kizalendo, tungeshauri serikali kuwakamata wahusika na kuvifungia viwanda hivi ili liwe somo kwa wengine wanaodhani Tanzania ni shamba la bibi ambapo matapeli toka nje wanaweza kuja na kuchuma utajiri kwa njia haramu na kuhujumu taifa. Hawa wanapaswa kukamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi, kudanganya na kulisha watu wetu bidhaa feki na zisizo na viwango. Itakuwa ni ajabu kama wahusika watatozwa faini huku wazawa waliobainika kuingiza magari kwa kuyaficha kwenye mitumba wakionzea ndani chini ya kosa la kuhujumu uchumi. Tungeshauri viwanda kama hivi vitaifishwe huku wahalifu husika wakibanwa na kulipa kodi ambayo wamekwepa kwa muda wote waliofanya biashara kabla ya kuwatupa gerezani. Pia kiwanda husika kichunguzwe kuhusiana na kadhia ya kuajiri wafanyakazi wa kigeni bila kufuata utaratibu. Mbali na hilo, mamlaka zinazohusika na kusajili biashara na viwanda ziwajibishwe kwa ima uzembe au kushirikiana na wahusika kuhujumu taifa. Maana haiwezekani kiwanda kama hiki kifanye kazi zake kwa miaka yote hii kikiwa bubu na bila kulipa kodi. Je ilikuwaje mamlaka za maji na umeme zikakipa huduma kiwanda hiki bila kujiridhisha kuwa kimefuata taratibu zote za kufanya biashara nchini? Je kuna uwezekano kuwa kiwanda hiki kinaweza kuwa kimekwepa kulipia umeme na maji?
            Pia tungeshauri wakuu wa mikoa na wilaya kuiga mfano huu na kuhakikisha shughuli zote haramu zinamulikwa na wahusika kuchukuliwa hatua. Kwani, ukiachia mbali kutolipa kodi ya mapato, kuuuza bidhaa feki na jinai nyingine, kiwanda husika kilibainika kuwanyonya wafanyakazi wake ambao wengi ni wazawa. Kama haitoshi, kiwanda husika kiliwalazimisha wafanyakazi kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi na magumu huku wakilipwa malipo kidogo kulingana na kazi wanazofanya.
            Hakuna ubishi; wakuu wengi wa mikoa na wilaya wanapoteza muda mwingi kuwadhibiti wapinzani wakati wakiachia jinai hii ya kuhujumu uchumi ikiendelea kuudhoofisha uchumi wetu na hali za maisha ya watu wetu. Je taifa limeishapoteza fedha kiasi gani ukiachia kunyonywa na kudhalilishwa kwa raia wake? Je kweli Tanzania inahitaji uwekezaji huu wa kijambazi? Japo kweli tuna shida ya uwekezaji nchini, uwekezaji wa namna hii ni hatari kuliko kutokuwa na uwekezaji kabisa.
            Katika kukagua nyaraka za kiwanda husika, Mjema aligundua kuwa kina namba za kodi (TIN) wakati hakilipi kodi. Je hapa hakuna jinai nyingine ya kughushi nyaraka za umma au kuzipata kwa mlango wa nyuma kinyume cha sheria? Je hawa wamilki wa kiwanda husika wanaishi nchini kihalali na wana vibali vya kufanya na kuishi nchini kama wanavyopaswa? Je ni wafanyakazi wangapi wa mamlaka zinazohusika wanaowasaidia wahalifu hawa kiasi cha kula nao? Hapa lazima kuwa na mkono wa watu wenye mamlaka si bure.
            Tumalizie kwa kumpongeza Mjema kwa kuwataka wakuu wengine wa mikoa na wilaya kuiga mfano wake katika kupambana na wahalifu wanaohujumu nchi na uchumi wetu. Waache kukaa maofisini na kutoa maagizo wakati mambo yakiharibika. Wakati wa Tanzania kuondokana na ujinga na uhayawani wa kutumiwa na wahalifu wachache wa ndani na nje ni sasa. Tunashauri wahusika wazisake bidhaa zote ambazo ziko kwenye soko na kuzikamata na kuziteketeza ili liwe somo kwa wahalifu wengine. Pia huu uwe mwanzo wa kubaini viwanda vingine kama hivi nchi ambavyo bila shaka viko vingi tu. Hii maana yake ni kwamba taasisi husika na watendaji wanapaswa kuacha mazoea ya kukaa maofisini wakisubiri kuletewa kila kitu. Mambo ya kuwaamini wafanyabiashara yalishapitwa na wakati. Biashara haina kuaminiana tokana na ukweli kuwa lengo kubwa la wafanyabiashara karibu wote ni kupata faida hata kama ni kwa njia ya kuvunja sheria au kuwanyonya watanzania kama ilivyobainika kwenye kiwanda hiki feki.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatan leo.

Kijiwe chanasa kwenye mitego ya Nay wa Kutega

Huwa wanakijiwe hawapendi mipasho wala muziki wa rapurapu uliojaa marapurapu kimawazo na kifalsafa. Mara hii, Nay wa Kutega katutega hadi tunajikuta tukiizunguka radio tukirudi ngoma ya Wapo akina Bashite kiasi cha kutegwa kama wale waliotegwa wakapiga marufuku mkuu akategua baada ya kunaswa. Unacheza na ngoma iliyowachengua na kuwachanganya wenyewe. Hakuna aliyechenguliwa  kama Kijiwe na dokta Mwakiwembe na Kanywaji hadi wakachangia mistari. Unafanya nchezo nini?
            Mbwamwitu kajilawa leo. Ajabu ameingia na radio. Kabla ya kuamkua, Mkurupukaji anamkurupusha “mzee vipi mbona umekuja na radio utadhani Mipawa kijijini kwao Kolomije Usukumani au una cha mno cha kutujuza. Mwaga pweti basi?”
            Mbwamwitu anajibu “wewe unaishi dunia gani usiyejua kinachoendelea Danganyika bin Bongolalaland usawa! Ama! Hujui kuwa ninatesa na mitego ya Nay wa Kutega aliyowatega wasiotegwa wakategeka na kunasa kiaibuaibu hadi wakamkubali? Hebu kula ngoma hii.” Anafungulia radio na muziki wa Wapo unahanikiza. Wapo wanaoburuzana, wapo, wapo wanaosagana, wapo , wapo wanaolindana, wapo, wapo wanaodanganyana kwa kulindana , wapo, wapo wanaodai wanajiamini wakati ni woga, wapo, wapo, wapo akina Bashit, wapo, wapo akina Bashite, wapo…. Wapo wapo wapo wapo tu.”
            Baada ya kutengua kitendawili kwa kusikiliza muziki wa Bashite Wapo, Kapende ananena “alaa! Unaongelea hili zali lililowaacha watukufu uchi huku wakijifanya kukubali na kusifia kilichowatia ukakasi wasijue tunajua mchezo mzima? Ama kweli, ukisikia sanaa ndiyo hizi. Yako wapi; walituzodoa kuwa tunapenda udaku wakaishia kuupwakia tokana na kujifanya hawashauriki?”
            “Mwenzenu niiposikia nikajua mtego umenasa tena kirahisi. Kwanini  hawakutaka kujua kuwa huwezi kujua yote na azima Basheti atumbuiwe tu? Why didn’t they undershtands a simple thing aik this?” Mgoshi Machungi anaamua kujikumbusha darasa lake la nane na nkoloni.
            Mijjinga anakula mic “sasa kama kujichanganya nakunasa kwenye mitego huku, Nipe Mapepe wamefukuza wanini wakati jipu lenyewe linazidi kuiva kiasi cha kuanza kujitumbua lenyewe ukiachia mbali uoza wake kuzidi kumchefua hata daktari mwenyewe? Au anataka mtumbuaji atoke Koromije au hadi akina Ney wakorome na kukoromija zaidi kuwaamsha wachovu? Je wengine waliofungiwa miziki yao watafunguliwa lini au hadi wawaguse wanene na kuwaaibisha baada ya kuwashika na umma kuwaijia juu? Beng’we ni makoye gambiti lulu.” Kabla ya kuendelea Mzee Maneno anachomekea “hiyo lugha gani ndugu yangu au unaongea kwa lugha kama matapeli wa neno? Si utafsiri lau kiduchu lau tuelewe na kuhoji mantwiki ya kunachotaka kueleza au vipi?”
            “Hiyo ni lugha ya kiKolomije ambayo maana yake ni  jamani haya matatizo kweli kweli sasa hasa usawa huu ambapo mtoto wa Kolomije anakoromewa na kuromijiwa hadi munene anaanza kujipiga mtama kwa kuruhusi vigongo vinavyomnanga au ndiyo mwanzo wa kuvunja ndoa yao ya mashaka? Who knows  what doctor Booze is contemplating ?” anajibu Mijjinga.
            “Wapo wapo wanene waliofoji vyeti; wapo waniolindana; wapo wakoromije:.” Radio ilihanikiza baada ya Mbwamwitu kuifungulia ghalfa. Acha nasi tuanze kuitikia “wapo tena wapo wapo wapo wakingoja kutumbuliwa hata kama ni wa Koromije.”
            “Yakhe sasa hii nvurugu. Sie tusojue rapu mwatuweka wapi au nami nirapu kipemba?” Mpemba analalamika.
            Msomi Mkatatamaa ankula mic “Hapa lazima tuseme ukweli. Hakuna cha kupenda wimbo wa Nay wa Kutega bali kuficha uso ili kuepuka aibu. Amewachonganisha na umma kiasi cha kusoma alama za nyakati na kuramba matapishi yao. Kama waliupenda wimbo huu, kwanini waliupiga marufuku na kumkamata wa Kutega? Wameumbuka; hata wafanye vipi kutuweka sawa, tunajua wameumbuka kweli kweli tokana na ubangaizaji na ukandamizaji wao. Eti wasivyo na aibu wanasema nasi tukaao vijiweni tuingizwe kwenye wimbo."
            Kabla ya kuendelea Kanji anakula mic “hii Kokomije naleta tabu sana kwa kaya. Sasa kama vote nasema toka nangoja nini? Mimi iko kwenda Koromije kukoromije yeye na ile nalinda yeye.”
            Sofia Lion aka Kanungaembe anamchomekea Kanji “thubutu yako urejeshwe Bombei bila nguo. Huyu haguswi. Ni kipenzi cha mwenyewe kwa sababu wajuazo. Ama kweli walisema wahenga. Ukishangaa ya Kanywaji utaona ya Koromije! Hivi kunani katika kulindana huku na kwanini? Inaonekana dokta kazimia kwa mgonjwa halo halo!”
            Mheshimiwa Bwege anakula mic “Mie muziki huu umenikuna. Sijawahi kuona wanene wakipashwa na kupashika hadi wananasa kwenye mitego kama ilivyotokea. Tokana na kujikomba, kila kigogo sasa anataka apige picha na Ney wa Mitego wakati ni unafiki mtupu. Kama muziki huu unawakuna, kwanini waliupiga marufuku? Sijui hapa wanamdanganya nani kushindwa kukiri kuwa wameurejeshwa kwa kuogopa hasira za umma? Mie nashauri waliupiga marufuku muziki huu na kumweka lupango wa Mitego washughulikiwe lau tujue walifanya makosa badala ya kutufunga kamba kuwa wanauzimia huu muziki wakati rohoni wanaugulia wakitafuta namna ya kumkomesha aliyewatega. Asipochunga ataishia kutegwa badala ya kuwatega wao.”
Kijiwe kikiwa kinanoga si akapita dokta Mwakiwembe na Nay wa Kutega! Acha tumpe kampani wa Kutega huku tukimzomea doc kwa kuramba matapishi yake. Kufumba na kufumbua si yakapita mashankupe ya ndata na BASUTA? Acha tuwasute na kuwazomea kwa kujikomba!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
           
           
          

Sunday, 2 April 2017

BASATA na Polisi acheni kujikomba

            Baada ya rais John Pombe Magufuli kutengua marufuku ya wimbo wa Wapo waEmanuel Elibariki aka Ney wa Mitego na kukamatwa kwake, tokana na katazo la Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na kukamatwa na jeshi la Polisi, tunaweza kusema kuwa sasa wanaojikomba na kujifanya wanajua hisia za rais wamekwama. Yaani mnakamata mtu bila kumpa onyo au haki ya kujitetea bado mnaona mnatenda haki kweli?
             Kwanza, ni aibu kwa taasisi zinazoendeshwa kwa fedha za umma kama Basata na Polisi kujikomba. Huu ni ushahidi kuwa taasisi hizi ima hazijui kazi zake zaidi ya kujigeuza vikaragosi vya kueneza woga na ujinga nchini au zinafanya kazi kwa woga usio na msingi ukiachia mbali kutaka kuwafurahisha wakubwa hata kama ni kwa kuwaumiza watu wasio na hatia.
            Pili, wapo waliopongeza hatua ya rais na kulaani hatua za Basata na Polisi. Kimsingi, hapa hakuna cha kupongeza hasa ikizingatiwa kuwa rais ndiye aliyeachia mambo haya kiasi cha kuyajengea mazingira hadi kujenga dhana nyingine kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa woga na kupinda sheria hasa wanapoguswa wasiopaswa kuguswa au watu walio karibu na rais au hata kumgusa rais mwenyewe tokana  na mambo wanayotenda dhahiri.
            Tatu, sioni sababu ya kumpongeza rais kwa alichofanya hasa ikizingatiwa kuwa amejitahidi kukwepa aibu kwake na serikali yake ukiachia mbali kushtakiwa. Kama atajifunza tokana na kadhia hii litakuwa jambo la maana kwake na kwa taifa kwa ujumla. Haipendezi rais kuwa anaingilia kila jambo.  Kwanini rais hakuwaamuru Basata na jeshi la polisi au waziri anayehusika kutenguamarufuku ya wimbo wa Mitego na kushikiliwa kwake kinyume cha sheria? Sitaki rais wetu ageuzwe rahisi na wale wanasukumwa na woga na kujikomba kiasi cha kushindwa kusimamia sheria na haki. Nadhani baada ya rais kutengua uwaziri wa Nape Nnauye baada ya kuunda tume ya kuchunguza kashfa ya kuvamiwa kwa vituo vya Clouds, wanywanywa na woga walidhani hii ndiyo sera yake, kulindana, kutishana na kuumizana bila sababu.
            Nne, hata hivyo rais alitumia busura kuepuka serikali yake kuadhiriwa mahakamani. Hivyo, basi tokana na alichofanya rais,  Mitego ashitaki serikali kutaka afidiwe kwa mateso na athari alizozipata yeye binafsi na kazi yake ili liwe somo kwa wote wanaotumia madaraka vibaya kwa sababu za kulindana na masuala binafsi.
            Baada ya kusema haya, acha nimshauri rais Magufuli kuwa na subira linapotokea jambo japo si yote yanayotaka subira. Mfano, anapogundua kuna madudu yanayosababisha hasara kwa taifa, lazima achukue hatua za tahadhali mapema. Inapokuja kwenye masuala kama ukosoaji, rais anapaswa kuacha vyombo husika vitimize wajibu wake au kuingilia kwa kuwatumia wasaidizi wake badala ya kujiingiza kwenye mambo yasiyo ya hadhi yake kama kwenye kadhia hii ya Mitego ambaye bila shaka sasa anachekelea kuwa rais amemsaidia kuwa maarufu na kuonekana shujaa bila ulazima kama rais angekuwa anaacha walio chini yake waache kufanya kazi na maamuzi kwa woga.
            Sita, tunashauri wakuu wa vyombo husika waliotoa amri hizi za kijinga watajwe hadharani na kuwajibishwa mara moja ili liwe somo kwa wengine wenye kuendeshwa na woga na kujikomba kufanya maamuzi yao.
            Saba, kwa kuamuru wimbo wa Mitego uendelee kuchezwa, ni dalili kuwa sasa rais anaanza kuona madhara ya Bashite kwa utawala wake. Haiwezekani mtu mmoja tena asiyependa kujitetea wala kutoa ufafanuzi kuhusiana na tuhuma dhidi yake aliweke taifa rehani. Bashite ni nani katika Tanzania? Kwanini watendaji wetu wanakuwa wepesi kuwaadhibu watu wema wakati wakiwakingia kifua waovu? Hili halikubaliki tanzania. Kama ambavyo rais amekuwa akionya watanzania kuepuka kujenga mazingira yanayovunja amani nchini kwa kutolea mfano wa kilichotokea Rwanda mwaka 1994, vivyo hivyo, naye aepuke kupalilia hayo mazingira kwa kuwatendea watanzania kibaguzi na kiupendeleo kama ilivyo kwenye sakati la Bashite.
            Nane, uzoefu unaonyesha kuwa rais Magufuli hana mtu wa kudumu. Rejea alivyombadilisha Katibu Mkuu kiongozi, Ombeni Sefue hata baada ya kuwa amemhakikishia kuendelea kuchapa kazi lakini akamuondoa. Hata Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam ambaye yuko katikati ya kadhia hii anapaswa kuchukua tahadhali kuwa hakuna aliyeshindana na umma akaushinda. Angekuwa mkomavu kisiasa, angeachia ngazi kwa hiari yake ili lau umma umsamehe kama kweli alighushi hivyo vyeti na kuvamia Clouds.
            Tumalizie kwa kuwapongeza wote waliosimama kidete na kulaani ujinga uliokuwa umetendeka ambao ulionyesha wazi kuminywa kwa haki za kikatiba za watanzania za kutoa mawazo bila pingamizi wala kutishwa ilmradi wasivunje sheria. Hongera Ney wa Mitego kwa kutengua kitendawili cha Bashite ambacho kilianza kuwa donda ndugu na jipu kubwa tu lenye kumngoja rais alitumbue mara moja. Turudie, tanzania ni zaidi ya rais, Bashite na yeyote yule anayedhani ana haki ya kuwa juu ya wengine. Ni nchi ya kidemokrasia inayopaswa kuongozwa na sheria, kanuni na katiba chini ya matakwa na shuruti zote za utawala bora na wa sheria.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili leo.

Saturday, 1 April 2017

Dingi anapowachanganya walevi na kuchanganyikiwa

       Juzi nikiwa zangu kwenye misele si nikajikuta kwenye ufunguzi wa barabara za ghorafa kwenye kaya ambayo si baraba kiuongozi ukiachia mbali kuwa fiti kiuongo. Tokana na kutaka kujua nini majaliwa si yule dingi msaidizi namba mbili, ya walevi na kaya yao, si nikajikuta nikisikiliza mipasho ya dingi kwa mashakunaku na mashambenga wanaotaka amtoe mwanae wa pekee ili wamsulubu. Hawajui kuwa baba yuko ndani ya mwana na mwana yuko ndani ya baba na afanyacho mwana amefanya baba. Hamkuona juzi munene wa umbea alivyofurushwa kwa kutaka kumchunguza mwana?
            Dingi akiwa amepania si akaanza mipasho kama ya wale waimba twaarabu japo si waarabu! Kwanza, aliotongoa kuwa kuhusu maendeleo ya barabara ghorofa na ushamba wa walevi. Nilidhani hii ndiyo inshu iliyokuwa imemleta pale. Sikujua nilikuwa nimenoa kama yeye! Si akaanza kurusha mipasho na michemsho kwa wana mitandao na mitindio bila kuwasaza wale wabaya wanaomsakama mwanae kipenzi mwenye jina kama la mtume Po! Huku walevi waliokuwa wakisema mara amsulubu au kumtumbua si wakaisha kutumbikia nyongo kwa kukosa utumbuzi! Dingi bila kujali kuwa yuko pale kwa kura za kula za walevi akila na kusaza si aliwazodoa kuwa yeye hababaishwi wala kuingiliwa! Aliendelea kuchonga ‘ukiniingilia ujue umekwama.’ Sitakusikiliza. ‘mimi ni dingi anayejiamini hata pasipohitaji kujiamini kama kukingia kifua ufisadi na utapeli kama ule alioshitakiwa nao mwana wa Bashit, washit sorry Bashite. Badala ya dingi kuzima moto si aliukoleza mafuta huku akiwakwaza wateule wake wanaoshughulikia na umbea waliokuwa wameunda tume ya kuchunguza maovu ya mwana wa pekee.
            kama haitoshi, dingi aligoma kutumbua kile akipendacho. Badala yake alifoka na kuahidi kuwapuuza wale wanaomzonga mwanae kipenzi. Tokana na imani yangu ya uongo kuwa kaya yetu ni ya haki na usawa, si niliishia kuchefuka kiasi cha kutapika! Kipindi kile tulipofungwa kamba na kuwekwa sawa kuwa mambo ya kulindana na kubebana yalikuwa historia, si niliishia kujishangaa kwanini nilipoteza kura yangu. Nikiwa nimechanganyikiwa nisiamini niliyokuwa nikishuhudia si bongo akatunanga walevi kuwa tunapenda udaku. Hasira zilinipanda kiasi cha kumkumbuka bunga na kidhabi mmoja limbukeni aliyetunanga kuwa sisi tulikuwa wavivu wa kufikiri asijue alikuwa kiongozi wetu katika jinai hii aliyotuzushia. Jiulize; hata muulize. Aliishia wapi pale alipoweka na Dalila kishawishini akatuuza na kutuchuuza bila kujisaza. Ama kweli wakati mwingine ulevi wa maulaji ni hatari kuliko wa kanywaji. Nani alijua kuwa kinda lingejisahau wakati mabaya yake yanajulikana?
             Baada ya dingi kurusha makombora yake nilianza kumuonea huruma yule kidhabi na tapeli mwingine aliyekuwa akimhubiri mwana wa pekee asijue lao moja. Yule jamaa mwenye jina sawa na la paka Jimmy nadhani atakuwa ameumia na kuumbuka kama wale mashambenga. Maana, jamaa badala ya kuhubiri injili ya ufufuko na uzima, alihubiri ile ya visa, visasi na maangamizi asijue dingi atamstukia na kumtupia makombora ambayo bila shaka yamemmaliza. Je jamaa naye anaogopa nini kama hauzi bwimbwi? Au ni ile mimali isiyo na maelezo aliyowapora kondoo wajinga wa kaya ya walevi. Naona akae mkao wa kuliwa kama si kutumbuliwa.
            Hakuna kilichonitia aibu kama dingi kujiingiza kwenye siasa za chumbani mbele ya dingi wa kimataifa tena wa mshiko na njuluku. Sijui  kama ana washauri. Na kama anao sijui kama wanamshauri au anawapuuzia. Kama anawapuuzia si waachie ngazi badala ya kujidhalilisha kama wale viranja wake aliowaaibishia kwa kupinga amri zao. Ama kweli, heri kulewa kanywaji kuliko ulaji. Sijui hapa aliyelewa kati ya mashambenga na mashankupe wanaomkamia mwana wa pekee wa dingi kipenzi, dingi mwenyewe na mwana mwenyewe. Katika ulevi na ujinga wangu nilichanganyikiwa baada ya dingi kunichanganya, kujichanganya na kuchanganya kaya nikadhani ndoa ya baba na mwana ingevunjiliwa mbali nisijue kuwa si hivyo. Sasa tazama mwana tena chizi kapewa rungu. Je wanyonge tutapona? Waulize wale wa runinga na radio ya mawingu aliowavamia na kutia kashkash hadi wakahama mawimbini kwa siku mbili. Hapa sijui anayetawala na kutawaliwa ni nani kati ya baba na mwana. Sijui anayemtumia mwenzake kati ya wawili hawa ambao uwili wao unatisha ukiachia mbali kuwa zaidi ya utatu mtakatifu. Sijui huu niuite uwili mtakachafu au uwili mchanganyikiwa.
            Du, bangi, gongo na usingizi vitu vibaya. Kumbe naota! Kama si hivyo, nani alijua kuwa mhalifu tena aliyechapia na kukimbia umande angekingiwa kifua hiki ambapo akina Keinerugaba wanawagalagaza akina Makorongo Muhanga waliojiita madaktari wakati ni waganganjaa na matapeli. Ama kweli mwenye mapenzi haoni! Inakuwaje vitu simpo na vya wazi vinawapiga chenga madaktari? Inakuwaje kihiyo na kishite anamtapeli hadi kumlazimisha msomi kutia heshima na ulaji wake kitanzini? Ama kweli, ukishangaa ya Njaa Kaya utaona ya Kanywaji! Nani alijua kuwa kaya yetu ingeendelea kuwa gamba na chaka la matapeli na mafisadi wa elimu ukiachia mbali walevi wa madaraka? Ama kweli hii ni kaya ya walevi au Bongolalaland aka Danganyika. Vinginevyo ningewaona walevi na michupa yao wakienda kusafisha ofisi zao kwa kuwaponda wachafu waliojazana huku wakiwaburuza na kuwatukana kuwa ni wadaku mchana kutwa.
Kumbe naota!
Chanzo: Nipashe Jumamosi leo. 

Wednesday, 29 March 2017

Kumbe Tanzania imefika hapa!

            Wengi wa wapenda demokrasia, haki na usawa nchini watakuwa wameshangazwa na hata kuchukizwa na yaliyojiri hivi karibuni. Ni kuhusiana na sakata la kughushi; mbali na la uvamizi wa vituo ya Clouds.  Hii ni baada ya kuachishwa kazi kwa aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye. Hata hivyo, kosa lake halikuwekwa wazi ukiachia mbali kujengeka hisia kuwa kadhia hii ilitokana na Nape kuunda tume ya kuchunguza uvamizi wa vituo tajwa hapo juu. Japo rais hapaswi kuingiliwa kwenye mamlaka yake ya uteuzi au utenguzi, kuna haja umma kujulishwa hasa, ikizingatiwa mhusika alikuwa ameshikilia madaraka ya umma. Je kweli kosa la Nape ni kuunda tume kuwachunguza wateule wasioguswa?
Japo ni haki na mamlaka ya rais kuteua na kutengua, kuna haja, wadau yaani wananchi, kujulishwa kinachoendelea jikoni; kuepuka kujengeka dhana ya udikteta, upendeleo na upatilizaji kwa wenye mawazo tofauti. Umma unapaswa kujulishwa nani wanapaswa kuguswa na nani hawapaswi kuguswa hata watende makosa makubwa kiasi gani. Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayopaswa kuendeshwa kwa haki, kanuni, sheria na usawa bila kusahau katiba inayotamka wazi kuwa watanzania wote ni sawa na wana haki sawa.
Mengine yaliyoibuka kwenye kadhia tajwa ni matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Inakuwaje mtu mmoja, tena asiye na stahiki kisheria kutumia vyombo hivi kwa maslahi binafsi na katika mambo binafsi kama ilivyokariri taarifa ya uvamizi wa Clouds? Mbali na hili, inakuwaje, kama taifa, tunaanza kuminya na kutishia vyombo vya habari ambavyo viko kikatiba na si kwa mapenzi ya mtu hata awe na mamlaka kiasi gani? Inakuwaje; wahusika wanashindwa kujua vyombo vya habari ni sauti ya wasio na sauti au voice of voiceless dhana nyepesi kabisa kujua? Rejea namna rais alivyokaripia na kutishia vyombo vya habari kuwa kama vinadhani vina uhuru, it is not to that extent au si kwa kiwango hicho. Haya si maneno ya rais anayefuata na kulinda katiba wala kuheshimu uhuru wa kiraia.
Katika kutishia na kuonya vyombo vya habari, rais alisikika akijigamba kuwa yeye ni rais anayejiamini na ambaye utawala wake hautokani na ushauri, usaidizi wala ushirika wa mtu yeyote. Kwani alipokwenda kuchukua fomu za kugombea urais, licha ya kutoshauriwa na yeyote, alikwenda peke yake. Hii ni kweli; japo sijui kama alijipigia kura na kushinda. Isitoshe, rais wa nchi anapaswa kuwa rais wa wananchi wote bila kujali tofauti zao. Hili, hakika, ndilo ambalo rais amekuwa akilihubiri; japo anaonekana kutolitenda.  Kwa maneno ya rais, ni kwamba utawala wake ni wake binafsi. Je inawezekana taasisi kubwa na muhimu katika taifa ikadhibitiwa na mtu mmoja hata awe mjuaji kiasi gani? Urais kama, taasisi ni mkusanyiko wa vyombo vingi. Hivyo, unahitaji maelfu ya wananchi ili uweze kufanikisha malengo uliyokabidhiwa na wananchi. Hata wafalme huwa hawatawali peke yao pamoja na ufalme kuwa sawa na mali ya familia.
Japo simuonei huruma Nape kwa yaliyompata hasa ikizingatiwa alichangia kikubwa kuyaunda, nampongeza kwa kufia ukweli. Socrates (469 B.C. to 399 B.C), mwanafalsafa wa zamani wa Kigiriki aliyesifika kwa kupenda ukweli aliwahi kunena “do not be angry with me if I tell you the truth” yaani usinichukie ninapokwambia ukweli. Yesu naye alisema ‘tuitafute kweli; kwani itatuweka huru.’ Hii maana yake ni kwamba mtu anayechukia na asiyependa kweli si huru. Anahitaji uhuru hata kama ana uhuru wa kisiasa. Je hatuhitaji uhuru utokanao na kweli hata kama unawaudhi wenzetu tena wenye madaraka? Je kadhia inayomkabila mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ya kughushi vyeti vya kitaaluma na kuvamia Clouds si ukweli tunaoutaka kama jamii ili, licha ya kutendeana haki kwa usawa, utuweke huru? Nani huyu mtumwa asiyependa kujua kweli imuweke huru? Je tunaweza kushindana na kweli na kuishinda tukawa salama kama jamii na taifa? Leo tutakwenda na falsafa ya Socrates tokana na mfano bora alioacha wa kuitafuta kweli hata kwa gharama ya maisha yake kama ilivyomtokea pale aliposhitakiwa kuwa alikuwa akiwaharibu vijana kwa mafunzo yake. Baada ya kuhukumiwa kunywa sumu aina ya Hemlock au Conium maculatum, Socrate alisema “yapo maarifa ya kweli na katika kujua hili hujui kitu.”
Tukirejea kadhia zetu hapo juu, nani hajui kuwa mengi yaliyojitokeza ni ya kweli? Nani hajui kuwa tumeanza kujenga taifa la watakatifu wasiokosea, wanaojua kila kitu na taifa la wasio na haki wala maarifa ukiachia mbali stahiki na haki ya kueleza mawazo yao? Nani huyu fedhuli anaweza kufunga mawazo? Je inawezekana? Ukijua hili jua hujui na kama hujui kuwa hujui basi hujui na utajua,
Tumalizie kwa mfano wa Socrates kuwa tusiogope kusema ukweli kwa kuhofia kufukuzwa, kunyamazishwa au kutishwa. Ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa mambo yanavyokwenda, licha ya kuwa tofauti na mategemeo yetu, sivyo ndivyo. Uhuru wetu kama wana jamii una thamani na gharama ambavyo hakuna anayeweza kuvipoka huku nasi tukiangalia. Ama! Tanzania imefikia hapa!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.
 

Mgoshi Apendekeza Kijiwe Kihamie Koromije