How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 24 July 2014

Futari au aina mpya ya hongo na ufisadi?


Kumezuka utamaduni wa kutumia vibaya fedha za umma kwa maslahi binafsi. Siku hizi ni fasheni kwa viongozi hasa marais, mabalozi, makampuni hata mashirika kufuturisha. Je hii ni futari au hongo na matumizi mabaya ya fedha za umma? Kwa mfano rais anapata wapi fuko la kufuturisha mikoa karibu yote huku mabalozi nao wakifanya hivyo? Ajabu hata makampuni yanayosifika kwa kukwepa kodi na kutoa huduma mbovu kama vile ya simu nayo yanafuturisha! Inatia kinyaa kuona makampuni kama vile ya kuuza ulevi na upuuzi mwingine eti nayo yanafuturisha. Je tatizo hapa ni njaa au ujinga wa watu wetu? Yaani tumegeuzwa taifa la njaa lenye kuweza kufakamia kila upuuzi hata bila kuuliza kama ni halali au haramu?

15 comments:

Anonymous said...

Ufisadi ni uhalifu tuu!!, sawa na uhalifu mwingine wowote hule au kuvunja miiko ya dini.

Hivyo tusichangue dhambi au mazingira ya dhambi. Vyote ni uvunjaji wa taratibu na amri za Mungu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umesema vyema. Heri wahusika wangekusikia wakatia maanani na kuondokana na dhambi hii ya majivuno na kugeuza wenzao mabunga.

Anonymous said...

Turarisha watu kwa pesa za umma ziko kwenye Bajeti ya serikali bongo Watu wanapenda sana shughuli ili waonekane umekuwa fashion now days makampuni yote ya ufisadi na mashirika hutumia mwezi wa ramadhani kuficha madhambi Yao
Nasikia kutapika now days Kila glob za bongo Watu wanafuturusha Kama kweli wanampenda mungu ingekuwa bora waja fanya ya maana kwa Watanzania wakati wa Ramadhan
Kwani futari it's only few hours it's gone

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umeweka pointi nzuri japo wahusika wanajifanya kutosikia tupo tunaokerwa na ujambazi huu wa mchana wa kujificha kwenye dini. Mwezi mtukufu umegeuzwa mwezi mtukutu.

Anonymous said...

Tatizo la Watanzania hawawezi kuishi bila party hasa mafisadi tulipokuwa watoto mwezi wa Ramadhan Kila kitu kilikuwa ok hata wenye mabaa walitumia mwezi huo kukarabati baa au restaurant zao
Lakini Leo si Ramadhan , shabani, hata miraji
Kila kukicha party party
Zinageuzwa fashion
Toba mungu wangu Tanzania it's the among the poorest
Country in the world but when it's comes party we the the first , where do we get money for that

Anonymous said...

Asante anon hapo juu
CCM wanalijuwa hili na ndo maana Kila kukicha misaada kwa Watanzania mpk lini
Tujuulize Kenya wametushinda nini hata pesa ikawa na thamani kuliko yetu,
Watanzania amkeni hakuna msaada usio Kuwa na maslahi kwa mtoaji
Hizo futari and it's only one month zitawatokeeni puani
Kama kweli wanajali maisha ya Watu why wasitoe Kila siku Kama ilivyo ulaya Watu wanapewa chakula bure na salvation amry

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu mmezidi kushindilia. Ni kweli. Wengi wa watu wetu wanapenda ubwete na dezo wasijue ndicho chanzo cha maafa yetu. Mmeona jinsi magabacholi wanavyotupa viungo vyetu kama mbwa huku nao wakituandalia futari baada ya kutuibia? Ukiangalia hata hao walaji hapo juu walivyofurahi huku mtoto wa fisadi mkuu akiwasanifu unatamani mbingu ipasuke uingie ili usiwe sehemu ya aibu hii. Watu wanapwakia kila upuuzi in the name of ramadan. Ni laana wala si neema.

Anonymous said...

Watanzania tunapenda sana ufahari
Tangu mitandao imezuka imekuwa nongwa
Ukitaka kuwajuwa watanzania angalia glob ya mashughuli na ni mashughuli party heziendani na hali halisi wanapata wapi fedha tenacha kushangaza hata marais ,wake zao na vogogo utawaona nao wamealikwa huko
Kweli tembo wetu watapona , sembe itachwa kuuzika
Wameifanya pasipoti ya tanzania inanuka duniani
Poleni wabongo lakini 2015 ndo uwamuzi sahihi mfifanye makosa, wapeni fundisho walipo madarakani waende shule

Anonymous said...

Afutulishe Na ofisi za ubalozi za Tanzania duniani basi tujeu moja
Wabunge ulizeni bungeni hii futari inakota kasma gani kwenye Bajeti
Tumechoka na futari za kifisadi mungu atawalaani kwani mwezi mtukufu kutumia fedha za haramu ni makosa
Hospital hazina dawa, wanafunzi Hawana madawati tena dar es salaam mji mkuu aibu aibu aibu
Isiyo na kifani

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu mmenena bila woga. Tuendelea kupaaza sauti yetu huenda hawa wanaotugeuza mabunga na mataahira wakabadilika na kufahamu kuwa janja yao imegundulika.
Kila la heri na asante sana.

Anonymous said...

Watizame wana haha kuchagua vyakula
Only few hours wanakwenda chooni it's over
Na CCM wanajuwa njaa itatuuwa
Pilau,chips, kuku , biriani unauza utu wako myGod

Anonymous said...

Pinda naye kaanda futari angalia hizo picha mjengwablog
Mpk na jk yupo
Toba kweli chukuwa chako mapema
Tumekwisha
Bado Lowassa nawe fururisha basi

Anonymous said...

Na sumaye pia, January , migiro,na zee usingizi bungeni
Wasira na Samuel Sita na Anna makinda japo tangu ulipokuwa Spika unasema jina lako Anne mbona tangu awamu ya kwanza ulikuwa Anna

Anonymous said...

Anon
Mmesahau tena na sala imefanyika na jk yupo Toba
Hapo kitimoto kililiwa in few month ago
Jamani kiama ki karibu
Mufti naye yupo kibaraka wa CCM
Tunamjua sana alikuwa eti mganga kabla mufrit
Alioa shangingi , Malaya Ashura Toba japo kwamwacha
Lakini you can't change history

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon hapo juu msemayo yana hoja kwani tutaona wengi wanaotaka wawe rais siyo watutumikie bali kututumia kama alivyofanya huyu tapeli msanii anayemaliza muda wake aliyetuingiza mjini kwa Ari mpya na Nguvu mpya na Kasi mpya (ANGUKA).