How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Thursday, 31 July 2014
Kwani tuzo za Kikwete zina nini na wanigeria?
Habari iliyosambazwa kwa vyombo vya habari ni kwamba rais Jakaya Kikwete amepewa tuzo nyingine ya The Icon of Democracy. Ajabu pamoja na wahusika kujisifu, ukichunguza sana unagundua kuwa nyuma ya tuzo hii kuna wanigeria. Kulikoni? Je kuna matapeli wanaomzunguka Kikwete na kusuka apewe upuuzi huu ili baadaye wahusika waje kumtoa upepo au kutafuta fursa na kuchukua kwa njia za uwekezaji uchwara kama ilivyokuwa kwenye tuzo nyingine ya kutia shaka ya The Most Impactful Leader of Africa iliyotolewa na Jarida lenye uhusiano na wanigeria? Maana tunaambiwa yupo Mwandishi wa habari ambaye pia ni pastor Elvis Ndubuisi Iruh kwenye tuzo ya sasa sawa na African Leadership Magazine ambalo makao yake makuu ni 13 Mambilla street,Off Aso Drive, Asokoro.P. O. Box 9824 Garki – Abuja, Nigeria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
16 comments:
Hivi Ulimboka mwakilishi wa wanyonge yupo wapi hivi sasa, hawa watoa zawadi wanatumia utaratibu upi. Natambua kwamba sisi waafrika tunadahraulika kirahisi kwa sababu viongozi wetu wa Afrika na matendo yetu. Na sasa mpaka taasisi pia zinafuata hadithi hizo hizo
Anon hata nami najiuliza wamewezaje kumpa hiyo "tuzo" wakati ana madudu kibao kuanzia Ulimboka, Kibanda, mauaji ya Arusha, mauaji ya polisi mara kwa mara, ufisadi, uchakachuaji kura, wizi wa EPA, uzururaji, wizi wa mali za umma, uzembe, ubabaishaji orodha ni kubwa tu.
Kweli wanigeria wamempata kibonde wao na tutasikia mengi.
Nadhani tulie kuwa tuna rais bomu na washauri wasio na akili timamu.
Toba Toba hizo tunzo hutolewa na mafidasi kwa mafisadi
Tujiulize kafanya nini duniani Kila kukicha kapewa tunzo?
Tumechoka na tunzo za ufisadi
Anon 10:10 na 06:48 mmenena. Ni kweli hatupaswi kushangilia bali kuomboleza kwa jinsi rais wetu anavyochezewa na matapeli wa kinigeria. Alichofanya hadi kupewa tuzo cha mno ni kuwa bogus president who can be duped and fooled easily by con men. Cheap popularity is the calamity behind Kikwete's uselessness.
Nigeria kutoa tunzo Toba ni ya Tatu duniani kuzalisha mafuta lakini masikini hadi Leo
Lakini sishangai kumpa tunzo kwani wana Lao wanalolitafuta
Kwani humjui hata mkewe na Obasanjo ni Shangingi la Kigogo Dar jina lake Salma
Tunzo kwa shemeji hiyo
Wampe na PHD basi tujue moja sijawahi kuona duniani mtu mwenye PHD Kama jakaya
Mungu ibariki Tanzania na Watanzania
Wampe U professor
Kwani ni vasco dagama
Kwa kuzurura ughaibuni kusiikokuwa na tija wala fadhila kwa Tanzania
Mkapa alisema msichague rais kwa uzuri wa sura
Mambo yote London
Kuna mtu kanunuliwa appt
Upps semeni yote jamani
Tunataka rais safi 2015
Na hapa ni mali pake uwazi na ukweli hakuna ulimboka
Anon hapo juu mmenena. Nadhani wahusika wamepata salamu. Kazi kwao kufanyia kazi mawazo yenu.
Katika marais JK umeundoa Hadhi ya urais
Umeweka wasaidizi vilaza ikulu imekuwa Kama chooni
Umekuwa mswahili ,kigeugeu
Kama makarani Mangesani mtaa wa maminyi. Bagamoyo
Unatukera
Ushauri wa bure
Washauri wako wengi bomu bomb
Shule zenyewe za kuunga kuunga
Unategemea watakupa ushauri gani zaid ya ushirikina na umbeya
Na hizo risala unazosoma unazipitia kabla au unasoma tu
Toba yarabi zisome kabla nyingi ni mabomu
Tuombe Mungu balaa hili limalize muda wake na kutokomea hata kuangamia, Pia tuombe na kuwa makini tusichague balaa jingine kama hili., Yana mwisho haya japo tumeishaumia.
Post a Comment