How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Tuesday, 1 July 2014
Makongoro Mahanga akubali kughushi PhD
Makongoro Mahanga, Naibu Waziri Kazi na Ajira kwa mara nyingine amekubali kuwa alighushi sifa zake za kitaaluma. Hii ni baada ya Makongoro kudaiwa na mwanaharakati wa haki za binadamu Keinerugaba Msemakweli kumtuhumu yeye na wenzake kuwa walighushi shahada zao.
Baada ya kutolewa tuhuma hizi, Makongoro alifunga kesi ya madai ya kukashifiwa akidai mabilioni ya shilingi hapo mwaka 2002. Ajabu ya maajabu Mahanga wala hakuwahi kufika mahakamani kuhudhuria kesi yake kiasi cha kumlazimisha hakimu kuifuta. Mahanga anatuhumiwa sambamba na Deodorus Kamala ambaye ni balozi wa Tanzania Ubelgiji, Emanuel Nchimbi, Mary Nagu,Victor Mwambalasa William Lukuvi na wengine.
Kitendo cha Mahanga kushindwa kuhudhuria na kuthibitisha madai yake ni ushahidi tosha kuwa bado ni kihiyo tu atake asitake, Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Polisi mpo wapi, mhalifu amejitokeza!?
Anon unauliza jibu wakati kuna swali: Je polisi wao si wahalifu ima wanaowalinda au kushirikiana na wahalifu?
Anon, nadhani inatokana taarifa za kitelijinsia ili Wakuda waingie!
Post a Comment