How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 1 July 2014

Makongoro Mahanga akubali kughushi PhD

Dk. Makongoro Mahanga
Makongoro  Mahanga, Naibu Waziri Kazi na Ajira kwa mara nyingine amekubali kuwa alighushi sifa zake za kitaaluma. Hii ni baada ya Makongoro kudaiwa na mwanaharakati wa haki za binadamu Keinerugaba Msemakweli kumtuhumu yeye na wenzake kuwa walighushi shahada zao.
Baada ya kutolewa tuhuma hizi, Makongoro alifunga kesi ya madai ya kukashifiwa akidai mabilioni ya shilingi hapo mwaka 2002. Ajabu ya maajabu Mahanga wala hakuwahi kufika mahakamani kuhudhuria kesi yake kiasi cha kumlazimisha hakimu kuifuta. Mahanga anatuhumiwa sambamba na Deodorus Kamala ambaye ni balozi wa Tanzania Ubelgiji, Emanuel Nchimbi, Mary Nagu,Victor Mwambalasa William Lukuvi na wengine.
Kitendo cha Mahanga kushindwa kuhudhuria na kuthibitisha madai yake ni ushahidi tosha kuwa bado ni kihiyo tu atake asitake, Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

3 comments:

Anonymous said...

Polisi mpo wapi, mhalifu amejitokeza!?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon unauliza jibu wakati kuna swali: Je polisi wao si wahalifu ima wanaowalinda au kushirikiana na wahalifu?

Anonymous said...

Anon, nadhani inatokana taarifa za kitelijinsia ili Wakuda waingie!