How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 8 July 2014

Kwa dada wa Kitanzania



Baada ya kusoma gazetini BOFYA HAPA  kuwa dada wa kitanzania wanapelekwa China kuuza miili yao nilishawishika kuandika comment ifuatayo:Tamaa, ujinga, kutaka kuukata, umaskini na roho mbaya vinaponza watu wetu. Nashukuru mwandishi ameandika hili ingawa hata wakaposoma hawataamini hadi yawakute. Siku hizi kila mtu anataka kwenda ng'ambo hata bila mipango na taarifa sahihi. Wataumia wengi kama serikali yenyewe inaendeshwa na wasanii. Kimsingi, haya magenge ya kusafirisha binadamu yanashirikiana na viongozi wakubwa serikalini. Hii ni jinai sawa na madawa ya kulevya ambayo inalindwa na rais aliyekiri kuwa na majina ya vigogo wake asiwashughulikie. Dada zetu wanapaswa kutulia na kuanza kubuni mbinu halali za kuishi badala ya kujidanganya na kudanganywa kuwa ughaibuni ndiyo kuna maisha. Kwenda ughaibuni si kosa iwapo utafanya hivyo kwa njia halali na zinazowezekana na kueleweka badala ya kukubali kila ahadi za kipuuzi. Hilo moja. Kuna waganga wa kienyeji na wachungaji uchwara wanaotajirika na kuharibu maisha ya wanawake wengi kwa kuwahadaa kuwa wanaweza kuwafanikishia wanachotaka. Mtadhalilishwa, kunyonywa, kudhulumiwa hata kuuawa kwa tamaa na ujinga wenu. Tieni akilini. Kama mambo yamekushindwa kwenu utayaweza ugenini?

2 comments:

Anonymous said...

Haya ni matokeo walia tumboni, hawa kabla kujiingiza kwenye haya majanga kuna cores drivers na ndiyo hizo zinarudisha nyuma maendeleo Afrika.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umesema vyema. Ila sijui kama watasikia na kukoma. Mie ningeona ingekuwa vyema kama wangejinyamazia wakaendelea na utumwa wao wa tumbo.