Baada ya kuzinyaka kuwa
watuhumiwa wakuu na wengine mizigo kusafishwa na wenzao, nilipatwa na shambulio
la moyo kiasi cha kukikimbizwa hospitalini ambako niliishia kumuona daktari na
kuwekewa drip za maji na kuamriwa kurejea home.
Kama si
kurejea home na kupata kanywaji na bangi huenda sasa ningekuwa past tense. Maana
nilivyostuka sina mfano. Hivi nani hapa anamdanganya nani? Ajabu na walevi nao
wamepokea sanaa hizi kwa upole na vicheko utadhani hawatalizwa zaidi kwa
kutengenezewa mi-escrow mingine tena
mikubwa kuliko huu wa akina Rugemalayer, Singasinga na Njaa Kaya. Hapa lazima
tuseme ukweli kuwa wahusika waliowasafisha wenzao huenda wameogopa kumwagiwa
mtama wao na kuishia kuumbuka. Hata hivyo, wajue. Kuna siku tutachenchiana
kiasi cha kuchimbika bila jembe. Kuna siku patakuwa hapatoshi hasa baada ya
kugeuza kaya shamba la bibi. Heri kufa kuliko kuendelea na upuuzi ambapo mipapa
inaibia kaya na kusafishana huku walevi wakizidi kunukishwa na kuchafuliwa na
ukapa na umaskini. To be open and frank, I
don’t subscribe to these sanaaz za kusafishana. Kama jamaa hawa ni safi na si mizigo basi ni
uongo wa aina yake sawa na kusema kuwa mamba hana meno. Kama wezi ni safi,
kwanini wasafishwe na wenzao badala ya pilato? Wapelekeni kwa pilato walale
lupango ushahidi utolewe uone kama hawatanyea debe.
Kwa lugha
rahisi, escrow si wizi bali
ujasiriamali ambapo walio nyuma yake ni mashujaa wa kustahiki kupewa nishani za
kuendeleza kaya. Mnamgeuza nani bwege hapa? Tubuni kabla ya kiama chenu kufika
hasa pale nitakapowahamasisha walevi kuwavamia popote mlipo na kuwapondaponda
na michupa ya gongo kabla ya kuwachoma kwa misokoto ya bangi. Huu nao eti
unaitwa utawala wa sheria wakati ni wizi wa mchana.
Kaya yetu
imegeuka ya vibaka, mibaka na majambazi. Mchovu akiiba kuku anafungwa maisha
wakati mibaka ikibaka mabilioni ya escrow inasafishwa! Kibaka akibakua kidani
anachomwa moto wakati mipapa ikichoma mafuta kwenda Ulaya kujaza akaunti zao
ughaibuni.
Kinachokera ni
pale mibaka hii mijambazi kuita mabilioni vijisenti au hela ya ugolo wakati
tunanyotolewa roho na ukapa wa kutentenezwa na wana hizaya hawa waja laana
wakubwa. Mshindwe na kunyong’onyea.
Wajua?
Nilipopatwa na shambulio na moyo bi mkubwa alinicheka baada ya kupata nafuu
baada ya kupata msokoto na mchupa wa gongo. Guess
what. Alinishangaa kwa kutegemea nguruwe aone uchafu wa ngiri au ngamia
amcheke nundu ng’ombe. Kusema nilijiona
bwege kama wachovu na walevi waliogeuzwa mabwege wakabwegeka kweli kweli
wasikengeuke wala kujivuvumua hasa wakati huu wanapoliwa mchana kweupe bila
kuona hata aibu ukiachia mbali kuhisi uchungu.
Hakuna waliponiacha
hoi wahalifu hawa kama kudharau mjengo uliowa tia hatiani wahusika kiasi cha
kuamuru watimliwe. Ina maana waheshimiwa
waishiwa ni waongo na wambea wakubwa wanaowanea wenzao wivu tena wivu wenyewe
wa kiume? Tell me please. Je mama
kipaza sauti binti Microphone wa kucheza makidamakida anageuka mamba awararue
hawa ngiri na nguruwe au naye atanywea baada ya kupozwa na chochote kitu? Je waishiwa
wanaokabiliwa na kibarua cha kurejea kwa wapika kula ya kura nao watajinasua na
kashfa hii ya kuwadhalilisha na kuwaonyesha waongo vipi? I am still waiting to see. Ama kweli ukishangaa ya escrow utaona ya
Sefui! Yaani baba zima linaamka na kusimama na kutangaza bila aibu kuwa nguruwe
ni kiumbe msafi kuliko sungura na njiwa!
Go tell it to the bird Sifui hata
kama unawafua wachafu wenzio. Hapa hakuna
cha usafi bali usafishanaji ambapo mmesafishana kwa vile wote ni wachafu na
mmenufaika na wizi huu. Hata ndege hawezi kuamini "ukweli" huu kuwa
wahusika ni watu safi. Je kama ni safi kwanini mliwafukuza kama hakuna kitu
kimefichwa au kufanyiwa uchakachuaji ili kulindana na kuepuka kuumbuana? Sijui kama
waziri tena Muongo aliyedaiwa kubeba mabunda ya fedha kwenye magaunia kweli ni
safi. Hapa nadhani tunachopaswa kujiuliza ni: Je alipopakia mabulungutu ya
njuluku kwenye mabox na magunia alikwenda kugawana na nani au alitumwa na nani
kama si wanene wote? Je huyo Ngurumisha wa ikuu naye ni safi wakati ushahidi uko
wazi kuwa alikatiwa akalegea?
Je inakuwaje
ikuu ijifanye mahakama wakati kuna mahakama tena tunazoambiwa ni huru wakati
kilichofanyika ni kuziingilia na kuzinajisi kiasi cha usafi, integrity and
impartiality vyake kuwa kwenye shaka? Haiwezekani hata kama nafikiri kilevi
mtuhumiwa huyo huyo awe mshitakiwa, mwendesha mashitaka na hakimu haki
ikatendeka. Wahusika ni sehemu ya utawala. Kwanini utawala huo huo uwe ndiyo
umechunguza na kutoa hukumu kama si kulindana? Wangejua nina PhD katika sheria,
criminology and penology, investigation,
constitution, na madude mengine mwengi wasingefanya waliyofanya.
Ukiachia mbali
Muongo, hakuna waliponiacha hoi kama kumsafisha hata A Liar Kim Maswiswi. Nadhani
wafanye haraka wawasafishe na akina Rugemalayer na Singasinga hata Annae
Kajuamlo Tiba-Ijuka haraka sana.
Hebu tuwe
wakweli kidogo japo kwa nukta moja. Hivi kweli akina Emmy Nchimvi aliyegushi
shahada ya uzamivu si mizigo kweli? Mbona madai ya umizigo wao yalitolewa na
wazee wa chata akina Andaraman Kinamna na Nipe Mapepe Ninaye? Ina maana hawa
vigogo wa chata na chata lao ni waongo wa kutupwa? Je hapa mkweli ni nani kati
ya watuhumiwa wanaowasafisha watuhumiwa wenzao na wabwabwajaji wa chata? Hapa kweli
ni kasheshe tena kasheshe kweli kweli! Yaani tumejirahisi na kuamua kugeuza
kaya chaka la majambazi kirahisi hivi! Ama kweli alijisemea mzee Mchonga kuwa
ikuu imegeuzwa kuwa genge la wezi. Msinichukie wala kunichukulia mihatua. Haya si
maneno yangu. Ni maneno ya Mchonga mwenyewe. Nani kama Mchonga ajitokeze
tumuone na kumzodoa.
Ama kweli
kama wahusika wamesafishwa basi wamesafishwa kwa majitaka. They are still stinkingly dirty and guilty.
Tuonane wiki
ijayo wapendwani.
Chanzo; Nipashe Mei 16, 2015.
3 comments:
nani mchafu anamsafisha mchafu nani wanamahesabu hasi ukijulimsha hasi Jawabu ni....! Au tuite Hiyo ndiyo hadithi hadithi yenyewe, utaumu.......!
Sefue anayewakilisha serikali chafu inayotaka kuwasafisha wachafu wenzake ndiyo walengwa. Kimsingi, hili dili ni la Kikwete mwenyewe anayepaswa kusafishwa kwenye tanuri kule Segerea. Kisheria, anayepaswa kumsafisha mtuhumiwa ni mahakama na si ikulu. Iweje wachafu wanaohitaji utakaso wawatakase wachafu wenzo wakati wote wanahitaji utakaso
Salaam Mwalimu Mhango,
Ningesoma habari hii ya neno kusafishwa kwa maana ya kumtoa mtu mchafu sehemu ambayo alipofanya machafu yake ingekuwa ni furaha kubwa kuona kwamba serikali tunayo ambayo inaamka wakati wa karibu na uchaguzi kwa kutuziba macho na midomo.Lakini kusafishwa kwa watu hao na ikulu yetu ambayo imegeuka si takatifu tena ili hali bado wanaendelea kunuka hata ukiziba pua na mdomo bado utasikia uvundo tu, hizi sio habari njema kabisa.Swali linalojiuliza lenyewe hapa ni kwamba je nani anamsafisha nani,ikiwa wote wapo katika pipa linalonuka?kuna hali ambayo kila siku inazidi kuijjenga katika akili yangu kwamba hawa tunaowaita viongozi wetu wanaijua sana saikolojia ya wananchi wao kwamba ni watu wa kuwaburuza tu kwa njia zote ambazo zinazostahiki kuwaburuza wananchi hao ni wananchi mabwege ambao wanakubali kudanganyika mchana kweupe.Iweje leo nchi iwe ina sheria na kanununi ambazo zinabaki katika makaratasi tu?Viongozi hawa wanajua kwa uhakika kabisa kwamba nchi ni miliki yao,sheria zipo mikononi mwao na madaraka ni mali yao binafsi.
Mwalimu Mhango,hali halisi kwa jinsi inavyoendelea tangu kuingia kwa awamu ya pili inanifanya kuwa na mshaka hata kwa hivi vyama vya upinzani tulivyokuwa navyo nimefikia kuamini kwamba na wao wanayanyemelea madaraka wakiyapata tu hali hii itaendelea kubaki pale pale sina uhakika kabisa kwamba upinzani utapofika madrakani watakuwa na uwezo wa kumuwajibisha kiongozi yoyote yule wa CCM aliefuja madaraka kwa kutumia ofisi vibaya, na kutumia vibaya mali na rasilimali za nchi.Je Mwalimu muhango,unadhan itakuja siku wasimamishwe mahakamani viongozi wa awamu ya pili mpka ya nne kwamba wameizamisha nchi na kujitajirisha wao wenyewe na familia zao?Je unadhani itafika siku kwamba mikataba yote mibovu iliyosainiwa na CCM itarudiwa upya na hata kubatilishwa?Je unadhani kuna siku pesa zetu mabilioni ya mashilingi ambazo leo hii zinaitwa ni za ugoro na vijisenti tu tutarudishiwa wenyewe?
Mwalimu Mhango,si kwamba mimi nimekata tamaa lakini naona viongozi wetu waliopo madarakani na wa upinzani wote ni sawa na sarafu moja tu japo ina nembo tafouti katika sura ya sarafu hiyo lakini itabakia ni sarafu ile ile tu hakuna mabadiliko.Mabadiliko ni lazima yasimamiwe na wananchi wenyewe kwa kusuka au kunyoa lakini je viongozi wetu wana hofu na wananchi hao kwamba itafika siku moja watawageukia tu?Nina mashaka na hilo kwani viongozi hao wanalala usingizi mnono na ndoto kubwa za kuzidi kujitajirisha na bila ya kuwa na hofu yoyote na wananchi wao.
Natamani kama neno kusafisha lingetumika katika maana ya kuwaondoa wachafu wote wa kaya kuliko kutumika kuwarudishia heshima yao ya uongozi na kisiasa ili wazidi kulindana wenyewe kwa wenyewe na kuendelea kupeana vyeo wenyewe kwa wenyewe siku za usoni na watoto wao na kuzidi kutukandamiza, kutudharau na kututesa kwa umasikini,ujinga na maradhi.
Post a Comment