How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Saturday, 2 May 2015

Sikanyagi tena Dar yenu!.

  • An aerial view of the Dar es Salaam city.
          Baada ya kugundua kuwa usanii, ufisi, ufisadi, ubabaishaji,na ukiukwaji wa kanuni hata za kitaalamu na za kimaumbile vimegeuka sera, nimeamua kuchukua hatua mujarabu kabla mauti ya kutengenezwa na ushenzi huu hayajanichukua kabla ya wakati wangu. You know what. Kunazia unaposoma waraka huu toka kwa mtakatifu Mlevi mwana wa Fyatu wa Wafyatue hutaniona tena katikati ya jiji la Dar si Salama. Tokana na ujenzi wa hovyo na wa kifisadi, nachelea kupoteza uhai kana kwamba sina akili.
Pili, nikizingatia kilichotokea mjini Kathmandu Nepal nilikokuwa kikazi hivi karibuni lilipotokea tetemeko la ardhi, sina hamu ya kuishi kwenye miji iliyojengwa kifisadi na kishenzi kama jiji la Bongo na majiji mengine uchwara yaliyotamalaki kayani.  Naona yule anatikisha kichwa akidhani najipa ujiko kusema nilikuwa Kathmandu. Unadhani kuna jipya huko zaidi ya ukata na ukapa na ukwete? Si kama wanaozobokea Bombei wakati tofauti na Bongo ni njaa na uchafu uliojazana huko. Hamuoni magacholi wanavyoukimbia kuja Bongo nini? Hayo tuyaache.
Washikaji zangu wa Dar nawaageni. Uwanja wa Fisi mtanimiss sana bila kusahau jamaa zangu wa escrow, IPTL VIP EPA Ikulu na wengine wengi niliowapa changamoto japo sitaacha kuwatupia vimondo. Guess what. Juzi nilisoma sehemu kuwa mafisadi wa escrow na wametoa mchango wa vyandarua 700 kupambana na malaria! Unaiba mabilioni na kuwahonga wachovu vijisenti uonekane unaijali jamii wakati wewe ndiye muuaji wake mkubwa kuliko hata hiyo malaria.
Kwa wale ambao hawajaipata vizuri ni kwamba sitakanyaga katikati ya jiji la Bongo kwa vile naogopa kudondokewa na kunyotolewa roho na mighorofa yaliyojengwa hovyo na kifisadi. Nilidhani ile ya Kisutu iliyomshinda Profedheha Anna Kajuamlo Tiba-Ijuka ilitosha kumbe najidanganya! Mghorofa wenyewe bado unapeta pamoja na kuamriwa uvunjwe. Unacheza na rushwa nini? Ukiona mighorofa itokanayo na njuluku haramu ya ufisadi, ukwepaji kodi, miunga na ujambazi mwingine inavyoota utadhani maendeleo kumbe maangamio.
Kitu kingine ambacho utaalamu wangu unaniambia kuwa ni chanzo kizuri cha kuongezeka kwa magonjwa ya akili na moyo ni msongamano wa mikangafu inayotoa moshi utadhani majiko ya mkaa au gari moshi la wakati wa mkoloni. Moshi nao si mzuri kiafya. Ni chanzo kizuri cha magonjwa ya moyo pia ukiachia mbali upofu na uharibifu mwingine wa mazingira.
 Mnajaza mikangafu na mighorofa uaji mnajisifu ujinga msijue siku moja mtalia kama vichanga. Majiji yenye akili wanapunguza matumizi ya mikangafu nyinyi mnaibiana na kuijaza na kujisifu mmekuza uchumi kama alivyowahi kusema mjingamjinga mmoja mjivuni kuwa ukiona misongamano ya mikangafu inaongezeka jua uchumi umekua wakati si kweli. Sijui kilaza huyu alipataje shahada ya uchumi!
Kwa vile siku hizi nazinyaka si haba, sipendi kwenda downtown kwa kuogopa vibaka hasa maeneo ya Migomigo na Feri. Pia mibaka inayobaka uchumi wetu inanifanya nichukie kwenda downtown. Maana ukienda kule unakutana na mishangingi yao wakipiga dili kwenye mawizara na ofisi za umma. Kwa vile nina hasira kama morani, naweza kuzaba mtu vibao nikaishia kupoteza muda wangu kwenda kwa ndata kutoa maelezo.
Kingine kitakachofanya kuacha kwenda katikati ya jiji ni wazee wa mabao ambao hukwambia upaki pembeni na kuanza kujifanya wanakagua mkangafu wako kugundua makosa wakati ukweli ni janja ya kukutoa uchache. Sina haja ya kuweka mbanta ndata bure nikaishia kuambiwa nimedharau crown japo wao wanaidhalilisha na kujifanya wanailinda. Huwezi kula rushwa ukawa unaiheshimisha crown zaidi ya kuidhalilisha tena vibaya.  Hapa sijasema tishio la miwaya hasa kutokana na jijini kujaa midada poa inayouza miili yao utadhani majani au nyanya. Mtaisha kwa miwaya. Kwani lazima kuuza miili kana kwamba hamna akili?  Hapa hujaongelea usumbufu wa machinga ambao ukiwa unapata kanywaji huja na kukubughudhi na bidhaa uchwara. Badala ya kwenda kuwaghasi waliowafanya maskini kwa kuruhusu machinga wa kigeni hasa toka China na India kuongeza umaskini wanatughasi tunaopata kanywaji kwa raha zetu.
Kitu kingine kinachonifukuza jijini ni joto. Baada ya mijengo mingi kushushwa katikati ya jiji, joto limeongezeka kiasi cha jiji kugeuka kama tanuri ambalo usipoangalia linakuuguza taratibu. Licha ya kusababisha usumbufu, uchovu na magonjwa ya ngozi, joto husababisha kukosa hamu ya kula na kukosa usingizi wakati wa usiku.
Hakuna kitu kilichonifanya kuogopa katikati ya jiji kama ukoma kama mafuriko ya vinyesi wakati wa masika. Mijengo yote hii iliyooteshwa bila mpango wala kufuata sheria za ujenzi itakujazama kwenye bahari ya vinyesi inayozalisha hasa utapishaji vyoo wakati wa masika. Jamani hata kuzagaa mavi mitaani nayo ni maendeleo au kielelezo kuwa kaya hii sasa ni ya wapumbavu hata wasioona kinyaa kuogelea kwenye vinyesi? Sijui wale wanaopenda kujifisia kuwa wamekuza uchumi kupitia upuuzi watasemaje kuhusu mafuriko ya vinyesi. Usishangae kusikia mjivuni kiherehere akisema kuwa ukiona mafuriko ya vinyesi jua watu wanashiba. Go tell it the birds. Huu ni ushahidi kuwa wanaotawala miji inayofurika vinyesi ni hamnazo na hawana tofauti na inzi mpenda mavi na mizoga. Vinginevyo wangekuwa na akili timamu wakengeona aibu na kuchukia uchafu. Mnalishana mavi halafu mnajisifu? Akili au matope?
Yote tisa, kumi ni kelele za wauza kanda waadhini misiki…. na magari. Nani anataka kufa kwa ugonjwa wa moyo utokanao na makelele hivi? Kama hamjainyaka basi inyakeni kuwa makelele huchangia sana uchafuzi wa mazingira na kusababisha magonjwa ya moyo na ya akili.
Leo naaga kwa kuwataka manesi na wakunga wanaopiga wajawazito hadi wakanyotoka roho au vichanga vyao waache kabla sijahamasisha wachovu wawachome moto kama vibaka.
Kwaheri Bongolala!
Chanzo: Nipashe Mei 2, 2015.

No comments: