How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Saturday, 16 July 2016
Hotuba ya Mlevi kwa waziri mkubwa wa Hindi
Baada ya kushuhudia ugeni wa mashaka toka Ugabacholini ulioongozwa na Nyabenda Moody waziri mkubwa ukija Bongo na kuondoka bila kujihangaisha kukutana na uongozi wa walevi, nimeshauriwa kutuma hotuba hii kwenye ubalozi wao ili kuwawasilishia yale ambayo rahis hakuyagusia kwenye kuwakaribisha hawa wageni wake tokana na sababu anazojua mwenyewe. Kwa wasiomjua huyu Moody, ni mnyasa wa Mbamba Bay aliyepotelea ugabacholini pamoja na jamaa waitwao Jarawa wanaobaguliwa kama wanyama kule.
Kuna mambo mengi tulitegemea rahis ayataje tena bila kumung’unya badala ya kumwaga ujiko kwa jamaa hawa wanaosifika kwa kubagua waswahili wakiwaita absii, bander, kalu au manyani na majina mengine mabaya tu wakati sisi tukiwaendekeza hapa kaya kiasi cha kuendelea kutubagua bila hata aibu na adabu.
Japo rahis aliipa ujiko sana Ugabacholini kwa kuwekeza kayani, tunachojua ni kwamba imekuwa ikichukua na si kuwekeza hasa ikizingatiwa kuwa kwa sasa ugabacholini inaongoza kwa kuuza tanzanite na si hindinite jambo ambalo rahis alikiri. Hii maana yake ni kwamba wanatuibia madini yetu jambo ambalo ni jinai ambayo rahis alipaswa ailalamikie badala ya kuisifu. Sijui yeye ananufaika vipi na jinai hii?
Ugabacholini imefanikiwa kutujazia wachovu wake wasio na ajira kuja kuajiriwa hapa kibaguzi kwa kujali rangi na asili badala ya maslahi ya pande zote mbili. Anayebisha aende kwenye viwanda vingi vya magabacholi na mahoteli aone waganga njaa waliojazana kule kutoka ugabacholini wakifanya kazi ambayo wachovu wanaweza kufanya. Aende kwenye makazi yao aone wanavyoishi kwa kujitenga.
Wachovu tunaojazia hawaishii kuchukua kazi tu bali wajihusisha na kuvusha mali zetu kama tanzanite japo rahis alisema eti kuna maslahi ya pamoja wakati ni ya upande mmoja.
Hakuna sehemu rahis aliwaacha hoi walevi kama kuridhia ubaguzi katika kutoa uraia wa kaya mbili au zaidi kwa mlango wa nyuma. Rahis alisikika akisema kuwa baadhi ya magabacholi waliokwenda pale kumpokea mgeni wake ni wabongo waliompigia kura Moody huko ugabacholini. Hii maana yake ni kwamba wana uraia wa kaya mbili jambo ambalo ni jinai kwa sheria za kaya. Watakuwaje na uraia wa ugabacholini wakati wao ni Wadaganyika wanaopaswa kuwa na uraia wa kaya moja au uraia wa kaya nyingi unawafaa wageni kuliko wazawa?
Rahis alisema kuwa Hindi inasaidia kaya za Kiswahili wakati inazijazia bidhaa feki na wasasi ngawira na kazi bila kusahau kuzijazia bidhaa feki na vya chini ya kiwango (substandard goods).
Rahis alishindwa kugusia namna magabacholi walivyogeuza wanyama ndugu zetu waitwao Jarawa kwenye visiwa vya Andaman tokana na Hindi kujengwa kwenye apartheid iitwayo caste system ambayo inafanyika hata kwenye kaya zetu ikitendwa na wale walioletwa na wakoloni kutuibia na kutunyonya ukiachia mbali kuendelea kutumiwa na wezi wazawa wenye mamlaka.
Inashangaza kusikia kuwa tuna magabacholi kumi mjengoni wakati mamia ya waswahili waishio kwenye visiwa tajwa waligeuzwa vivutio vya utalii bila huduma yoyote ya afya kiasi cha tofauti yao na wanyama kuwa sura zao tu. Kwa wanaotaka kujua zaidi ubaguzi huu http://www.aljazeera.com/indepth/features/2014/01/time-ticking-india-jarawa-tribes-20141314281424904.html.Inasikitisha sana kuona wale walioletwa na wakoloni wakila kuzaliana, kunenepeana wakatajirika na kuita wengine wakati ndugu zetu wakiteseka kwa sababu ya rangi ya ngozi yao.
Hapa tunaongelea ubaguzi ambao rahis aliogopa kuugusia. Hatujagusia jinsi magabacholi wanavyoingiza wenzao kayani kufanya kazi ambazo wachovu wanaweza kuzifanya. Ajira zao nyingi ni za kibaguzi. Rejea kukamatwa kwa magabacholi wengi waliokuwa wakiishi kwenye kaya bila vibali. Hapa hatujagusia ubaguzi wa wazi wazi hata kwenye makazi ambapo magabacholi wengi wenye mahekalu, hata viwanda kuendelea kuishi kwenye kaya za bei mchekea za Asajile Mwaijumba katikati ya jiji huku wazawa wakitimkia Pugu Kajiungeni na Kimanzichana. Ukiingia downtown Bongo usiku unaweza kudhani uko Bombay. Sijui huyu Bwana Mdogo Po Makondakonda anashindwa nini kupitisha amri kuwa kila wenye uwezo wa kujenga mahekalu shurti waishi kwenye mahekalu yao badala ya kuwabana walevi kwenye nyumba za Asijile za bei poa.
Mlevi amewahi kuishi ugabacholini kwa miezi michache akifanya utafiti juu ya ubaguzi ambao umekuwa ukitokea ugabacholini ukiachia ule wa kwenye kaya ambao tawala zote zilijifanya kutouona. Hebu nionyesha lau binti mmoja wa kigabacholi aliyeolewa na mswahili nitajinyotoa roho kwa aibu ya kusema uzushi.
Kipindi fulani waziri mmoja aitwaye Idd Lion aliwahi kudai kuwa magabacholi kumi tu walikukwa wakimilki uchumi wote wa kaya ya Danganyika. Hata sasa, ukimuondoa mzee Bhakresa, matajiri wakubwa ni magabacholi; kwanini wakati hakuna waswahili matajiri ugabacholini ambako hata kwenda kusoma ni ubaguzi wa kuua mtu hadi waswahili kuitwa absii, bander na kalu yaani manyani.
Walevi wameshangazwa sana kitendo cha rahis kushindwa kumtaka waziri mkubwa wa ugabacholi kuomba msamaha kwa binti wa kitanzania (jina kapuni) akiwa na mwenzake aliyedhalilishwa na kupigwa hadharani baada ya msudani ambao hupenda kujiita wamanga wakati wamanga wanawaona kama watumwa kumgonga maza mmoja wa kigabacholi.
Tumalizie kwa kusema kuwa walevi hatukuridhishwa na namna masuala yenye siha yalivyotalekezwa zikamwagwa sifa kwa jamaa ambalo halikufaa kumwaiwa ujiko wote huku wakati linaongoza kaya inayosifika kwa ubaguzi na unyonyaji wa waswahili. Lazima usuhuba huu mpya baina ya Bongo na ugabacholini upigwe darubini tusiendelee kulizwa.
No comments:
Post a Comment