Free Thinking

I Fear Nothing But Fear Itself

The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Friday, 8 July 2016

Mlevi hakuangusha futari mwaka huu

Japo wengi wamejivuvumua kwa kuangusha futari la kukata na kisu kama siyo shoka, mwenzenu mwaka huu sikujaliwa kuwafurisha walevi. Kwanza, mimi si mtu wa kufuata mkumbo kama wengine ninaowajua waliofanya hivyo. Pia nikiangalia gongo, bangi na njia nyingi haramu nyingi ninazotumia kupata njuluku, nilimuogopa bwana God hata kama siamini kama yupo au hayupo na kama ni ke au me au it.
            Japo walaji hawaulizi namna mfuturishaji au mtoa sadaka alivyochuma njuluku zake na kama analipa kodi au aliuza bwimbwi au kupiga toka kwenye fuko la umma au kuhonga mwili akapata cheo, nafsi yangu ilinisuta. Maana njuluku ya bangi na gongo wapi na wapi kununulia futari. Mimi siyo kama wale wagema pombe maarufu wa Msimbazi ambao eti nao wanafurisha. Kwa vile njuluku zangu ninazokopesha walevi wenzangu huwa natoza riba, naona kama njuluku yangu ni haramu kununulia futari ukiachia mbali bi mkubwa niliye naye kuwa kimada na si mke niliyempata kwa ndoa. Kama haitoshi, mimi huwa nafunga usiku wakati nikienda kulala. Hivyo, niliona kama nitakuwa nafanya unafiki kuandaa futari wakati sitimizi vigezo. Hivyo, wenzenu baada ya mwezi mtukufu kupita, nitalisha badala ya kufuturisha. Hata hayo mavazi ya kimanga mie sivai. Kwa sababu dini si mavazi kama tutaondoa kuingia mkenge hadi tukapwakia utamaduni watu–huku tukitukana wetu–na kuugeuza dini. Kwa mfano, mwenzenu sikuona sababu ya kulanguliwa ile kitu inayoagizwa umangani eti kufuturia utadhani uswahilini hatuna vyakula. Jamaa yangu aliniacha hoi aliposema eti ukila ile kitu unapata dhawabu kana kwamba ukila viazi hupati. Basi ingekuwa hivyo hata maji na vyakula vingine vingeagizwa huko japo havipo  zaidi ya hiyo kitu.
            Nimeamua kutoa maelezo ili wabaya wangu wasijesema sikufanya hivyo kwa sababu sikuwa na njuluku au ubahiri kama wa ndugu zangu akina thithi tunathema ukweli mtupu hata wakiongopa. Hasha. Nilikuwa nimepata fedha toka kwa baadhi ya mafisadi ambao wameomba nisitaje majina yao baada ya kuwatishia ningewachoma kwa Dk Kanywaji awatumbulie mbali.
Naona yule anatikisa kichwa. Vitu vyote duniani haramu lakini siyo njuluku. Uliwahi kuona kanisa au msikiti vikikataa kupokea njuluku au kuuliza wanaotoa sadaka walilpataje njuluku zao? Mara hii umesahau kanisa moja kule Kinondoni lililopewa minjuluku na fisadi wa EPA likasepa na kumbariki? Nilikuwa nangojea kusikia mafwisadi wa Escrow nao wafuturishe ili nimwage radhi kwa waroho ambao wangepwakia njuluku haramu kama hii japo bado wengi wamepwakia haramu nyingine na radhi yangu iwakumbe.
            Japo dini yangu ni ganja na ulabu, niliamua kujiuliza maswali kadhaaa. Kwani mimi ni wa kwanza kutumia njuluku-shaka kufuturishambo mbona juzi nilimuona yule kinara namba mbili mama wa Suluhu akiwa sambamba na fisadi wa UDa wakitoa misaada kwa ajili ya futari? Kwa hiyo basi, usishangae hata changu, muuza unga, mlevi, fisadi hata jambazi akafuturisha. Wote tunahitaji maghufira au vipi?
            Pili, sikutaka kuwakwaza wachovu wanaoweza kula chochote kiwe halali au haramu ilmradi cha dezo. Unaposikinisha walevi–hata kama utahakikishwa ulinzi–lazima ujue unatenda dhambi isiyo na msamaha ardhi na mbinguni ya kuwageuza wala chochote ka nchwa.  Wapo ambao wasingejali hata kama futari yangu ingeaandaliwa na nyumba ndogo au kafiri. Walevi wangetafunilia mbali ili baadaye wamalizane na huyo muumba wao. Kwa vile mlevi nimesoma falsafa ya kila kitu, najua kuwa uharamu wa vitu mara nyingi uko kwenye mila lakini si vitu anwai. Uliwahi kusikia kiazi, yai au nyanya za Kiswahili zikiitwa haramu? Walioleta hii kitu kweli waliwazidi waswahili ujanja. Walifanya mila zetu kuwa haramu na zao takatifu lakini si makulaji yetu. Ulitaka wafe njaa?  Hata huu mma tunaopiga waliukataza ili tusilewe tukawapuyia hadi tungoje tuingie kutamuni. Mwenzenu nakata kalaji hapa hapa huko sijui kama nitakuwa na umio wala tumbo ya kutunzia ulabu wenyewe.
            Siku moja jamaa mmoja asiyeamini Mungu aliniacha hoi. Alisema eti kama dini zingebatilisha vyakula kwa vile vimezalishwa na washenzi kwenye ardhi ya kishenzi isiyo takatifu, basi angeziheshimu.
            Hebu niulize kibangi bangi. Hivi hawa waliowasikinisha walevi kupitia ujambazi kila aina nao walikuwa wamefunga kweli? Ili iweje wakati wao walishafungwa ahera na duniani? Hata hivyo sishangai. Maana juzi nilivyowaona akina shehe John, Paulo na Lameck wakifuturu bila kufunga nilibakia kucheka kama wanavyonicheka. Mambo ya siku hizi bwana, wakati mwingine yanachekesha badala ya kuliza. Kila mtu anataka afuturishe hata maofisi ya umma. Sijui hiyo njuluku inatoka bajeti gani? Hivi, kama wale waumini wa kimila wakitaka nsaada au nchango kwenye madogori yao makampuni yatajihimu kuwachangia kama “yanavyofuturisha” hata kama ni kulisha tu?
            Naona yule anasonya. Kama nimekukwaza kaka samehe sabini mara sabini au vipi? Sisi tuliosoma falsafa ya utamaduni na ukombozi (Cultural emancipatory philosophy) uhoji kila kitu hata mama zetu walivyotubeba matumboni. Hatumuogopi , kumuonea wala kumpendelea mtu au jambo. Sijui kama umangani naweza kwenda na mibangi na gongo yangu na kufanya vitu hadharani kabla ya kunyotolewa roho. Mila ya babu zangu ni kwamba kitoto kikizaliwa lazima kipewa ulabu ili kutibu tumbo na kukikaribisha duniani. Lakini kwa wenzetu kitu hii ni ushenzi na haramuni! Ya kweli hayo? Hebu tuyaache. Wakati mwingine halali inaweza kuwa haramu na haramu ikawa halali kama hakikisho la wanene alilotoa Dk Kanywaji hivi karibuni. Sijui naye nimtumbue?
Chanzo: Nipashe Jumamosi.
Posted by Ndugu Nkwazi N Mhango at 20:29

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Cordially and unlimitedly welcome to this blog.


Writing and reading are two different processes but which share the same goal-to educate, communicate and entertain.
It is my pleasure to have you as the guest of this tablet.
I, thus, warmly and always, welcome you to share ideas.
Importantly and eminently, shall there be anything amiss or you think can advance this blog, please donate it.
Allow me to humbly and kindly welcome you once again.
Nkwazi N Mhango- A Man And a Half

When wisdom brings no profit, to be wise is to suffer. Not all thoughts are good and constructive. Others are even worse than bullets. The good thinkers are the ones that think constructively for the manumission of all bin-Adams regardless their diversity. Mwl. Nkwazi N Mhango,
Canada.


I Love My Country Tanzania

I Love My Country Tanzania

The Curse of Salvation

The Curse of Salvation

Gen Z and Internet Revolution

Gen Z and Internet Revolution

I Cry for Ambazonia and Darfur

I Cry for Ambazonia and Darfur

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do.

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

Yoo-hoo, Africa Is Yowling

The Story of Stories

The Story of Stories

The Chant of Savant

The Chant of Savant

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA’S CONTEMPORARY FOOD INSECURITY Self-inflicted Wounds through Modern Veni Vidi Vici and Land G

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

AFRICA MUST DEAL WITH BLATS FOR ITS TRUE DECOLONISATION

Epistle to Afrophobic South Africa

Epistle to Afrophobic South Africa

Magufulification

Magufulification

BORN NUDE

BORN NUDE

Total Pageviews

Heko Rais Magufuli

Heko Rais Magufuli

DECOLONISING EDUCATION

DECOLONISING EDUCATION

Kudos President Magufuli

Kudos President Magufuli

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

JOKEY HORSE-JOCKEY NORTH-SOUTH RAPPORT Diagnostic-cum-Prognostic-Academic Perspectives on Who Truly

The Family Friend of Animals

The Family Friend of Animals
Children's Book

Matembezi Mbuga ya Wanyama

Matembezi Mbuga ya Wanyama
Kitabu cha Watoto

Our Heritage

Our Heritage
Children's Book

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

How Africa Developed Europe:Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth...

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

Africa's Dependency Syndrome: Can Africa Turn Things around for the Better?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

'Is It Global War on Terror' or Global War on Terra Africana?

Perpetual Search

Perpetual Search

Africa's Best and Worst Presidents

Africa's Best and Worst Presidents

Psalm of the Oppressed

Psalm of the Oppressed
Psalm of the Oppressed

AFRICA REUNITE or PERISH

AFRICA REUNITE or PERISH
A new approach towards empowering Africa

BORN WITH VOICE

BORN WITH VOICE

Soul on Sale

Soul on Sale

Soul on Sale

Nyuma ya Pazia

Nyuma ya Pazia

We are one

We are one

SAA YA UKOMBOZI

SAA YA UKOMBOZI

Feel at home

You are always welcome to this epistle again and again time after time, ad infinitum.


Most read Posts

  • Sarkozy’s Take on African Fat Cats a Welcome Move
    At last the chicken are coming home to roost! French authorities made a groundbreaking decision by culling three most corrupt African presid...
  • Napanga kuanza kuuza mitumba na si maneno
    Ingawa mimi si mtumba, napanga kuuza mitumba. Nimechoshwa na jamii ya mitumba. Kila kitu mitumba. Mitumba, mitumba mitupu. Siasa za mitumba...
  • Better or Bitter Life for all?
    When I deeply muse on how an arrogant and brutal cabal of hoity toity (Coverted Con Men (CCM)) is tirelessly hoodwinking and dividing the ho...
  • Africa's Becoming more Despotic and Nepotistic
    "King of Kings" Gaddaffi The seven-day 40th anniversary of Libya strongman’s autocratic rule and charade elections in Gabon where...
  • Kuna siku tutataifisha haya mahekalu haki ya nani
    Taarifa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige alinunua nyumba kwa zaidi ya shilingi bilioni moja licha ya kuwastua wananchi na...
  • Nyangumi mdogo akutwa amekufa ufukweni BC
    Hii ni picha iliyotolewa ya Nyangumi aina ya Humpback ambaye alikumbwa na maji na kutupwa kwenye ufukwe wa bahari ya Pasifiki kwenye eneo l...
  • Kikwete, Charity Begins at Home!
    President Jakaya Kikwete Pea...
  • Kweli binadamu si chochote wala lolote, wamkumbuka huyu?
    Walioko madarakani mkiabudiwa kama miungu au sanamu kumbukeni vijana hawa hata baba zao  ambao maiti zao zinaoza jangwani. Ungewaambia...
  • Pinda kulia hakutoshi, awajibike
    INGAWA kilio cha Waziri Mkuu, Mizengo Peter Kayanza Pinda, kinaonekana kuyeyusha hasira za Watanzania kwa muda, kuna haja ya kudodosa zaidi....
  • Hawa si wachungaji bali ni fisi na mbwa mwitu
    KUMEZUKA mtindo mchafu na wa rejareja wa baadhi ya wachumia tumbo na matapeli kumtania hata kumtumia Mwenyezi Mungu kufanya utapeli na ujamb...

Followers

Blog Archive

  • ►  2025 (42)
    • ►  July (6)
    • ►  June (7)
    • ►  May (5)
    • ►  April (4)
    • ►  March (6)
    • ►  February (8)
    • ►  January (6)
  • ►  2024 (92)
    • ►  December (7)
    • ►  November (4)
    • ►  October (11)
    • ►  September (9)
    • ►  August (7)
    • ►  July (9)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (7)
    • ►  March (6)
    • ►  February (7)
    • ►  January (8)
  • ►  2023 (118)
    • ►  December (10)
    • ►  November (10)
    • ►  October (9)
    • ►  September (2)
    • ►  August (4)
    • ►  July (6)
    • ►  June (9)
    • ►  May (8)
    • ►  April (18)
    • ►  March (13)
    • ►  February (9)
    • ►  January (20)
  • ►  2022 (208)
    • ►  December (14)
    • ►  November (14)
    • ►  October (20)
    • ►  September (20)
    • ►  August (12)
    • ►  July (25)
    • ►  June (22)
    • ►  May (18)
    • ►  April (13)
    • ►  March (18)
    • ►  February (18)
    • ►  January (14)
  • ►  2021 (323)
    • ►  December (23)
    • ►  November (34)
    • ►  October (26)
    • ►  September (13)
    • ►  August (19)
    • ►  July (21)
    • ►  June (29)
    • ►  May (25)
    • ►  April (23)
    • ►  March (43)
    • ►  February (29)
    • ►  January (38)
  • ►  2020 (290)
    • ►  December (33)
    • ►  November (37)
    • ►  October (28)
    • ►  September (35)
    • ►  August (31)
    • ►  July (26)
    • ►  June (17)
    • ►  May (21)
    • ►  April (18)
    • ►  March (15)
    • ►  February (17)
    • ►  January (12)
  • ►  2019 (160)
    • ►  December (8)
    • ►  November (7)
    • ►  October (12)
    • ►  September (9)
    • ►  August (27)
    • ►  July (18)
    • ►  June (18)
    • ►  May (11)
    • ►  April (11)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (14)
  • ►  2018 (162)
    • ►  December (12)
    • ►  November (6)
    • ►  October (13)
    • ►  September (10)
    • ►  August (20)
    • ►  July (9)
    • ►  June (14)
    • ►  May (9)
    • ►  April (16)
    • ►  March (21)
    • ►  February (17)
    • ►  January (15)
  • ►  2017 (306)
    • ►  December (20)
    • ►  November (23)
    • ►  October (20)
    • ►  September (26)
    • ►  August (31)
    • ►  July (31)
    • ►  June (34)
    • ►  May (26)
    • ►  April (24)
    • ►  March (20)
    • ►  February (28)
    • ►  January (23)
  • ▼  2016 (269)
    • ►  December (22)
    • ►  November (21)
    • ►  October (22)
    • ►  September (15)
    • ►  August (12)
    • ▼  July (27)
      • Happy Birthday Nkwazi Mhango Jr.
      • Je uraia wa nchi mbili ni kwa wageni tu Tanzania?
      • Mlevi atamani kufanya biashara na NSSF
      • Kijiwe champongeza Dk Kanwyaji
      • Makonda upangaji Nyumba za Msajili ni jipu lako
      • Makufuli tumbua wachunaji
      • Kijiwe chastukia uraia pacha wa Kanji
      • Our Lives in History, Today 18 Years Ago
      • Twarana na nii (Nenda nami) -Jane Muthoni
      • Tulia Ackson anapaswa kutulia
      • Hotuba ya Mlevi kwa waziri mkubwa wa Hindi
      • Wiki hii niliwarusha makamanda wangu
      • Tusinunue ndege kwa 'madesa'
      • Tunamsihi rais aongee lugha ya taifa
      • Kijiwe: Makufuli tukumbuke kwa maburungutu
      • Dikteta anaposhuka kwenye gari kuchimba dawa
      • Kunashangaza kule hakuna mizigo
      • Fighting graft: Let’s fry all fish like China
      • Kumbe tukiamua kama taifa tunaweza!
      • Mlevi hakuangusha futari mwaka huu
      • Hapa Dokta Magufuli akubali ameteleza
      • Kumbe tukiamua kama taifa tunaweza!
      • Kwa wanandoa na watarajiwa burudika na wimbo huu w...
      • Milioni saba kwa dakika; kijiwe chanena
      • Tuwanyonge mafisadi na wahujumu uchumi kama China
      • Transparence: Let’s open every boozer’s closet
      • Mlevi kuomba appointment na rahis kupata maelezo
    • ►  June (24)
    • ►  May (23)
    • ►  April (29)
    • ►  March (26)
    • ►  February (27)
    • ►  January (21)
  • ►  2015 (399)
    • ►  December (34)
    • ►  November (24)
    • ►  October (22)
    • ►  September (34)
    • ►  August (29)
    • ►  July (37)
    • ►  June (22)
    • ►  May (32)
    • ►  April (35)
    • ►  March (46)
    • ►  February (47)
    • ►  January (37)
  • ►  2014 (502)
    • ►  December (47)
    • ►  November (49)
    • ►  October (47)
    • ►  September (37)
    • ►  August (40)
    • ►  July (42)
    • ►  June (30)
    • ►  May (35)
    • ►  April (47)
    • ►  March (44)
    • ►  February (39)
    • ►  January (45)
  • ►  2013 (399)
    • ►  December (37)
    • ►  November (27)
    • ►  October (31)
    • ►  September (26)
    • ►  August (33)
    • ►  July (39)
    • ►  June (28)
    • ►  May (40)
    • ►  April (44)
    • ►  March (39)
    • ►  February (26)
    • ►  January (29)
  • ►  2012 (597)
    • ►  December (27)
    • ►  November (26)
    • ►  October (27)
    • ►  September (30)
    • ►  August (47)
    • ►  July (94)
    • ►  June (86)
    • ►  May (119)
    • ►  April (83)
    • ►  March (23)
    • ►  February (17)
    • ►  January (18)
  • ►  2011 (261)
    • ►  December (20)
    • ►  November (19)
    • ►  October (20)
    • ►  September (21)
    • ►  August (27)
    • ►  July (12)
    • ►  June (15)
    • ►  May (20)
    • ►  April (27)
    • ►  March (32)
    • ►  February (24)
    • ►  January (24)
  • ►  2010 (205)
    • ►  December (25)
    • ►  November (23)
    • ►  October (23)
    • ►  September (23)
    • ►  August (17)
    • ►  July (13)
    • ►  June (12)
    • ►  May (10)
    • ►  April (18)
    • ►  March (9)
    • ►  February (16)
    • ►  January (16)
  • ►  2009 (163)
    • ►  December (19)
    • ►  November (14)
    • ►  October (11)
    • ►  September (6)
    • ►  August (12)
    • ►  July (9)
    • ►  June (11)
    • ►  May (20)
    • ►  April (22)
    • ►  March (14)
    • ►  February (12)
    • ►  January (13)
  • ►  2008 (191)
    • ►  December (12)
    • ►  November (11)
    • ►  October (14)
    • ►  September (15)
    • ►  August (16)
    • ►  July (23)
    • ►  June (10)
    • ►  May (19)
    • ►  April (16)
    • ►  March (19)
    • ►  February (17)
    • ►  January (19)
  • ►  2007 (33)
    • ►  December (13)
    • ►  November (20)

About Me

My photo
View my complete profile

Travel theme. Powered by Blogger.