How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday 27 December 2017

Picha ya kufungia mwaka kwa furaha

Watuhumiwa wakuu wa wizi wa Escrow James Rugemalira na Harbinder Sing wakiwa mahakamani
                           Kwa wanaojua namna Tanzania ilivyochezewa kiasi cha kugeuka shamba la bibi, au tuseme shamba la chizi, chini ya utawala Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa akitawaliwa na mkewe Anna Tamaa Mkapa na Jakaya Kikwete, wanapoona picha za mafisadi nyangumi kama hawa lau wanafarijika. Hata hivyo, juzi fisadi James Rugemalira aliamua kuanza kumwaga mtama akitaka akutane na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) ampe ushahidi juu ya nani mwizi wa fedha zinazohusika kwenye kesi inayomkabili. Kwa wanaojua sakata la IPTL, hawatasita kujikumbusha kuwa walioiasisi na kufaidi na Mkapa na Kikwete. Hawa wengine ni vidagaa tu wanaotolewa kafala kuwanusuru wakubwa. Je serikali iko tayari kupokea ushahidi wa Rugemalira na kuufanyia kazi au kujifanya haisikii? 
                           Ukitaka kujua kuwa Rugemalira anawajua wenzake hasa wale mabwana zake waliomtumia, jiulize, wale aliowakatia mshiko ambao unajulikana ni wa wizi kama vile Andrew Chenge, Anna Tibaijuka, William Ngeleja, jaji Aloysius Mjulizi, askofu Methodius Kilaini, askofu Eusebius Nzigilwa na wengine wengi wamechukuliwa hatua gani? Je sheria yetu inatumika kibaguzi au mkono mrefu wa serikali utawakamata na kuwasweka ndani hadi watakapoachiwa na mahakama kama hawa washirki wenzao? Je kesi ya Escrow itauawa kimya kimya kama vile ya EPA ambapo wezi waliambiwa warejeshe fedha yakaisha ili kuepuka kumfichua mtuhumiwa mkuu ambaye ni Kikwete na Mkapa? Je mwanzo wa mwisho wa Rugemalira ndiyo unaanza? Je ataachiwa amwage mtama au kuKolimbwa? Ngoja tuone mwaka unaoanza serikali itakuja na sinema ipi au kuchukua hatua zipi mujarabu. Nawatakie mwaka mpya 2018 wenye amani na mafanikio.

No comments: