How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Saturday, 9 December 2017
Waafrika na utumwa wa kujitakia!
Hivi karibuni kulivuma habari ya waafrika kuuzwa utumwani nchini Libya. Ni ajabu kuwa waathirika, yaani waafrika, wameendelea kukaa kimya huku wakipaza sauti kupinga mambo yasiyowahusu badala ya kuwaachia wenyewe. Nchini Tanzania, baadhi ya magazeti yenye mwelekeo wa Kiislam yalishutumu utawala wa Myanmar kwa kuwafukuza waislam wa kibengali toka nchini mwake ukisema warejee kwao Bangladesh. Hivyo, waislam wenzao wa Tanzania na nchi nyingine za kiafrika waliona kama hiyo si haki.
Hata hivyo, waislam hawa hawa ambao wenzao toka baadhi ya nchi za Afrika Magharibi wanauzwa nchini Libya, hawakujishughulisha na kadhia ya wenzao. Kama haitoshi, hivi karibuni rais mbaguzi wa Marekani Donald Trump aliutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa taifa la Israel. Hatua hii ilizua laana, maandamano, mitafaruko na purukushani duniani hasa Mashariki ya Kati. Umoja wa waislam wa Bonde la Ufa nchini Kenya ulitoa tamko kali sana dhidi ya hatua hii ya kisiasa lakini ukakaa kimya kuhusiana na kadhia ya utumwa nchini Libya. Je huu si ulimbukeni na utumwa wa kujitakia wa waswahili kushupalia ya wenzao wakati yao yakiwashinda? Hiyo picha hapo juu inamuonyesha bwana wa kiarabu na mtumwa wake wa Kiswahili jambo ambalo ni ruksa katika uislam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment