Kuna wanandoa kwa kukosa kujiamini, ulimbukeni, ujinga, na uzembe ima wavuruga hata kuvunja ndoa zap au Kinyua furaha na raha. Hawa ni wale ambao hawafanyi au kuona kitu bila kuwakimbizia maradi au mashoga zao. Ndoa si chama, klabu, au taasisi ya urafiki. Ni ya siri baina ya wawili tu. Wapo watu ambao wengi huitwa mafriji yasiyofunga. Hawa, wasifanye au kuona jambo. Mbio, anampelekea rafiki yake. Unaaminije kuwa atakutunzia siri zako? Hata akizitunza, inakusaidia nini wewe au yeye zaidi ya kutengneza maisha hatarishi kwa ndoa yenu? Unapomwambia mtu siri zako, unajivua nguo wewe na mwenzako. Unampa udhaifu wako jambo ambalo ni hatarishi kwa ndoa nyingi.
Mfano, mkifarakana, kutofautiana, au kugombana. Unamwambia mtu ili iweje na kwanini? Mkilala njaa au kushiba, unamwambia mtu mwingine ili iweje na ili upate nini? Huu japo ni utoto, umezidi. Hata tukiuita ulimbukeni au umbea, haitoshi. Tunachoweza kusema ni kwamba tabia ya kutoa siri za ndoa nje ni balaa na hatari lipaswalo kuepukwa kwa gharama na namna zozote. Kama ni ugonjwa, basi ni kansa. Na wengi wanajua kuwa kansa ni gonjwa hatari lisilotibika japo laweza kuzuilika likiwahiwa. Wenye tabia hizo, huu ni wakati wenu na fursa kuuwahi ugonjwa kabla haujakuwa na kufikia kiwango cha kutotibika.
Kwa wanaotaka kudumisha na kufaidi ndoa zao, hakuna kutoa siri zenu au kuhusisha wengine kwenye mambo yenu binafsi. Hata wakikuamini na kukumwagia mambo na siri zao, usijaribu kuwaambia au kutoa siri zako. Kwani, hiyo ni kasoro au uzembe wao. Ni hatari na mwiko. Miiko na siri vya ndoa vinapaswa kubaki hivyo hivyo.
Kuna wanandoa wawili marafiki sana. Mmoja huwa anamwambia kila kitu cha ndoa yao. Mwenzie huwa hamwambii yake. Na badala yake, alitumia fursa hii kumtaka na kumpata mke wa rafiki yake. Kila wagombanapo, jamaa hukimbizia umbea kwa mwenzake asijue kwake ni fursa ya kumsaliti na kula vyake. Kila wakigombana, humfukuza mkewe kwenda kwao. Naye mke kwa vile walishalianzisha, huenda kwarafiki wa mumewe ambaye ni msela na kula maisha hadi wakichoka. Hapo, ndipo rafiki wa mume mtu humtafuta mumewe na kumshawishi amrejeshe mkewe.
Tokana na rafiki wa mume huyu mbea kujua karibu kila siri za ndoa ya rafiki yake, kila amtakapo mkewe, hupanga na mkewe kumkoroga mumewe ili amrudishe kwao wakaendelee na yao. Kwa vile jamaa ni fala anayemuamini rafiki asiyeaminika na kumsikiliza amchotaye akili na kuzitumia dhidi yake,akishagombana na mkewe, huenda kuomba ushauri kwa mgoni wake ambaye humwambia kuwa mke ni mgumu wa kujifunza. Hivyo, amrejeshe kwao akajifunze zaidi asijue anakwenda kwenye yake.

Kibaya zaidi, katika ugoni huu ulioanzishwa na umbea wa mume, mke alinogewa hadi akamzaliwa mtoto wawili hawara yake huyo kama kumbukumbu ya uhusiano wao. Ni kichaa au mpumbavu angesikiliza hili achia bali kulitimiza. Wangapi wanachezewa hivi na wakajiona wanjanja wakati wanaandaa ima majuto au mauti yao? Je, wapo wangapi wanafanya haya? Tugemee nini dhambi, kama dhuluma, au siri hii ikifichuka? Hatujui kama wanaotenda ukatilili, uovu, na usaliti huu wanajua kinachoweza kuwakuta au namna wanavyowaumiza wenzao ufilauni wao unapofichuka. Tatizo la wanaotenda haya, wakati wakiyatenda, huwa hawajiulizi ni kitatokea siri ikifichuka au wangekuwa wao wangetaka watenzwe vipi.
Unaona hatari hii? Ungekuwa wewe, ungefanyaje? Je, kitendo cha mama naye kujiachia ni haki au kisasi? Je, hapa nani wa kulaumiwa japo wote watatu wana makosa? Nani mwenye makosa zaidi na mwanzilishi wa tatizo kama siyo mume?
Japo wanandoa wanaofanya haya wanapaswa kujilaumu, kubadilika, na kujirekebisha, wanachofanya, licha ya kutokuwa sahihi, ni hatari kwa pande zote. Hivi, huyu bwege mbwaga siri akigundua, unadhani anaweza kufanya nini? Binadamu ni viumbe wanaojipendelea sana. Akigundua, usishangae kusikia kaua kwa vile alipokuwa akitoa siri zake nje, hakuona kama ni kosa bali jambo la kawaida wakati siyo.
Mwisho, tusisitize na kushauri. Wanandoa achene kutoa siri zenu nje na pia kukomoana, kulipiza visasi, au kusalitiana. Kwani, mwisho wa siku, wanaoumia ni nyinyi na watoto wenu. Hayo ndiyo madhara ya kutotunza siri za ndoa hadi mnazibomoa wenyewe msiwe na wa kumlaumu balil nyinyi weneye. Kama umesoma kwa makini na kuelewa, tungeomba utoe maoni au uzoefu wako. Vaa viatu vya wahusika ndipo utoa mchango wake vizuri.
Chanzo: Mwananchi J'pili leo.

No comments:
Post a Comment