Juzi baada ya wakenya kumwagana damu wakiwagombea mafisadi wao, nilidhani nisingerejea Nairobi kutia stori na washikaji zangu kwenye kijiwe chetu maarufu mitaa ya Kimathi, Ghana, Rivaroli (River road) Ngala na mingineyo.
Nilikwenda kusuluhisha vijiwe vya huko baada ya kuchenjiana.Baada ya hali kutulia, nilijimwaga zangu Moa nikaingia Mombasa raha nikijifanya Mduruma. Nilichukua jina la Nyae Mduruma. Huyo zangu Mombasa sehemu za Miritini na Chuda!
Nimelazimika kuingia kwa njia hii ya mazabe kuogopa kuchukua pasi ya Tanzania. Maana tangu jeshi letu lilipowanyonga majambazi wa Kenya askari wa kule waliamua kutulipishia sisi kisasi utadhani sisi ndiyo tuliowatuma au kuwanyonga! Isitoshe pasi za bongo si mali kitu baada ya wasomali, waethiopia, wanyarwanda na warundi kuzichangamkia kuzamia zao majuu.
Pale Mombasa nilitia stori kidogo nikasikia malalamiko ya wapwani dhidi ya wabara na vita kwenye pori la Murungunipa huyo sikufurahishwa nikaamua kuingia zangu Nairobi au Nyairofi kama wenyewe wanavyopaita.
Zamu hii nilikuwa na washirika zangu akina Mureithi, Ndamu, Kinyanjui, Njema, Jadwong, Mukami, Boit na Vaite Kiraitu.Nikiwa natafuna miraa (mirungi). Huku ni halali.
Mara namuona Muthamaki Njema anatia guu. Ananiamukua. "Mu-TZ umekunjanga lini Kenya hii? Huongopi kuona tunanyongana!"
Akiwa anashangaa Mureithi anaingilia. "Wewe hjuangi wa-TZ. Hii iko akili mingi. Don’t you remember wamezoea vita ya kutengeneza marais ya nchi nyingine Afrika?"
Jadwong naona hakupendezwa na maongezi juu ya hili. Anaingilia. "Omera I like prezo (Rais) yenu. Amesaidia Kenya to reach to the agreement na Kibaki."
Kabla Jadwong hajaendelea, Ndamu anaingilia. "Wewe napenda prezzo ya TZ juu ya nini? Kama najua kutongorya (Kuongoza) bona ile conflict ya Zanzibar nashinda yeye? Aache mabo ya Kenya kwa Kenyans."
Kabla Ndamu hajamaliza,Mutiso anaingilia. "Mwana wa Kaneza nasikia kibeti (mke) ya Prezzo yenu najua biasara. Eti nauda NGO inamtengezea chapaa sana."
Mambo yamekuwa mambo. Boit anaingilia. "Your prezzo ni hypocrite. Mbona hakamati ile mafisadi tena wengi Indians? Bona kuna MTZ alini-tell kuwa iko sirika na ile wevi yote naibia TZ?. Nasema ile gavana ya central banki naiba na kwenda America. Sisi yetu najaribu nafuta yeye na kupeleka yeye kortini."Njuguna anaingilia. "
Boit sidaganye MTZ. Bona ile Kalenjin Kotut naiba na Moi naache yeye. Kitu moja nasapoti wewe. Prezzo yote wevi kama Moi."
Mukami anaingilia na kumuunga mkono Boit. "Hapa watu nataka kukwepa issues. Mimi haikoona tofauti ya prezzo ya TZ na Moi au Kenyatta. Moi alizoea kwenda Church na kupozi kama born again lakini wajua ni machafu gapi Moi nafanyia Kenya? Prezzo ya TZ ni politician. Yeye kama twilight girls wa Koinange street. Naweza tembea na bwana yoyote mradi chapaa."
Anageuka na kuniangalia na kuendelea. Washenzi wamezibuka hawana akili nzuri!"
Nasikia nyinyi iko nayo street naitwa Ohio. Yes. Politicians ni kama hao girls. Leo wale nakuwa napinga Kibaki kuogea na Raila iko bele kusema nataka reconcialiation!"
Mvaite Kiraitu anaingilia. "Hii kitu kawaida. Huoni Moi nakuwa rafiki na Kibaki. Hata nasikie prezzo ya TZ imefuta kesi yote ya former prezzo iliyoiba pesa mingi na bibi yake na watoto yake."
Kuona wamezidi kunishindilia naamua kuingilia kidogo. "Naona waheshimiwa mmepatia. Kwanza nakubaliana nanyi ni unafiki kusuluhisha mgogo wa nchi kubwa kama yenu tukashindwa wa visiwa vidogo tena karibu na nchi moja."
Kabla ya kuendelea naona Wakashohi anamnong’oneza Njoroge. Anasema. "Unasikia Swahili yake ilivyo poa?"Wakashohi anasema. "Swahili poa lakini English bovu."
"Goof not my friends. What is unique with English in the first place? Do you want puritans in English as if we are British. Even Britons sometimes, make mistake. That’s why they came up with common mistakes?"
niliamua kujibu mapigo kiasi cha kuwaacha hoi wasijue wamechokoza mtu anayeongea ung’eng’e wa malkia tena wa London.
Mureithi kaona tunavuka mipaka. Anaamua kuokoa jahazi. "Wajameni. Sisi iko dugu. Kwanza wote nateswa na politicians. Tanzania haiko na chapaa na Kenyans haikuo na land. Tanzania juzi nafukuza premier Kenyans na-contain Kibaki."
Kabla ya kuendelea na busara yake mara Kinyanjui anaingilia. "Eti capital city yenu haiko na jumba kubwa kama yetu Kenya? Nasikia Nyerere alikuwa kisema kwanini kweda London while Nairobi iko!""Pia nasikia Indians naiba pesa mingi TZ? Sisi Kenya politicians ndiyo naiba pesa mingi. Naona ile jumba refu ghorofa thalathini along Kenyatta avenue? Ile ni mali ya Githunguri. Ile mingine ni ya Kanyottu na mingine kule ni ya Waithaka Waititu."
Anageuka na kuniangalia. "Eti nyinyi politicians yenu naficha pesa yote ije? Kwanini nakuwa na tabia kama panya?" Alijigamba Njuguna.
Jadwong kasikia jina la Mwalimu. Naona anatabasamu. "Mimi napenda sana Nyerere. Ilikuwa friend ya Jadwong Oginga Odinga. Leo naongelea politicians fisi na fisadi. Nyerere na Oginga haikuiba mali ya wanaichi. Hata hakuacha na bibi yake wala watoto na mali mingi kama yetu hapa inaacha land sawa na province yote."" Zamani TZ likuwa naita sisi nyang’au. Leo iko na nyang’au mingi kuliko yetu hata kama nasuluhisha sisi.
Kijiwe hakina mbavu jinsi wanavyowachambua wanasiasa. Mei kiroho kinaniuma kuona mifano inatolewa kwa mtu wetu lakini nani anajali? Siku hizi hakuna cha kujuana bali kutimiza malengo kwa umma bwana.
Mukami anaamua kubadili mada baada ya kuona tunaanza kunyambuana ilhali wote ni walalahoi. Anasema. "Sisi Africans tuko na problems. Naangalia watu ya siasa nasahau watu ya dini. Bona haisemi Revered Muiru iliyogombania uprezzo na kuchaganya mafuta na maji? Bona naogopa kushakiza (kutoa changamoto) kwa raiaa iliyokubali kuuana kulida watu ya siasa chafu? Sisi Kenya na TZ napaswa raiaa kuugana na kutosha watu chafu yote."
Jaduong anaamuunga mkono. "Sisi raiaa iko na makosa kubwa. Leo nasherehekea coalition yetu kati ya ODM na PNU. Lakini hapana jali ile ya Ugunja!"
Nami namkusoa na kusema Unguja siyo Ugunja ya Mombasa.Anaendelea. "Mimi sisifu prezzo ya TZ. Kwanini nakuja okoa Kenya naacha nchi yake kwa moto?"
Mureithi kapata upenyo. Analonga. "Hii coalition siyo muzuri. Inaangalia personalities badala ya issues na nchi. Kama yenyewe naugana wapi naweka vyama nyingine ya opposition? Nao inyongane diyo ipewe powers?"
Kijiwe kikiwa ndiyo kinaanza kunoga mara karau (polisi) walitutokea wakitaka chapaa. Mie sikujivunga nilianza kuangusha ung’eng’e wakadhani ni Mjamaica hivyo hawakunitoa chapaa.
Baada ya mandata kuishia mara lilikuja gari la mpambe wa Raila likiwa linatoa matangazo juu ya mkutano wa usuluhishi pale Kamkunji stadium. Hivyo Kijiwe nacho kwa nyonde nyonde kilihamia baa kucheza mwomboko na mwihiguro kusherehekea ushindi wa Jadwong Raila Ajuma Oginga Odinga dhidi ya Muthamaki Mutongorya Stanley Emilio Githinji wa Moi mwana wa Othaya.
Mara wimbo ulianza kutumbuiza. Jambo? Jambo Bwana Kenya yetu hakuna matata. Wageni mwakaribishwa Kenya yetu hakuna matata.Nilikumbuka jinsi tulivyokaribisha wageni wa kihindi wakatutia kwenye matata ingawa leo tunasifiwa kusuluhisha ya wenzetu Kenya wakati Pemba imegeuka kuwa fupa lililomshinda chifu Emeka Anyauko na Commonwealth ya Malkia Elizabert mke wa Philip Mountabaten!
Ama kweli hakuna unafiki kama kuhami kwa mwenzio ilhali kwako kunateketea. Kama ni mapenzi basi ni ya mshumaa.Tukutane kijiwe kijacho. Mpayukaji toka Nairobi Kenya kulikoungua shoka ukabakia mpini alioudandia Kikwekwe.
Source: Tanzania Daima Machi 12, 2008.
No comments:
Post a Comment