How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Tuesday, 4 March 2014
Hatimaye Ridhiwan aonyesha uchu wake na utawala wa kifalme
Taarifa tulizo nazo ni kwamba mwana wa mfalme wa Danganyika, Ridhiwan Kikwete "alishinda" kura za maoni katika chama cha baba yake Mfalme. Matokeo ya mnyukano wa kugombea nafasi ya atakayepeperusha bendera ya Chama Cha Marithishano (CCM) yanasomeka kama ifuatavyo:
Prince Ridhiwan Kikwete kura 758
Shebby Iman Madega kura 335
Othman Ramadhani Maneno kura 206
Changwa Mohamed Mkwazu kura 12
Jumla ya kura halali ilikuwa ni 1363 na kura 5 ziliharibika.
Japo ni haki ya kila mtanzania kugombea cheo chochote, kuja kwa mwana wa mfalme ambaye ametajwa kwenye skandali nyingi za ulaji kuna mgongano wa kimaslahi.
Kama ilivyotokea Arumeru Mashariki, Kalenga, Bumbuli,Kwahani na kwingineko ambako vigogo wameweka watoto wao ili wawatawale watu wao, Chalinze pia imefanya hivyo hivyo. Kesho utasikia first lady akigombea kabla ya shemeji yake yaani kaka yake mfalme kugombea. Huu ni uroho wa aina yake na ni upuuzi kutumia demokrasia kwa vigogo kurithisha madaraka kwa watoto wao. Ukiachia jina Kikwete Ridhiwan ana nini cha mno kufaa kuliko magwiji kama Iman Madega? Ana tofauti gani na wana wafalme wenzake kama vile Hussein Mwinyi, Adam Malima, Januari Makamba, Emanuel Nchimbi, Vita na Zainab Kawawa,Violet Mzindakaya, Godfrey Mgimwa, Sioi Sumari na wengine waliofichwa kwenye sehemu nyingine za ulaji? Je Mwalimu Julius Nyerere angekuwa kipofu na mchoyo hivi akina Ali Hassan Mwinyi na Kikwete ambao wameonyesha upogo wa kuwarithisha watoto wao madaraka wangekanyaga hata ikulu? Mkapa pamoja na udhaifu wake angalau kwenye hili hayumo japo ana mchango katika kurutubisha ufalme huu uchwara. Ni aibu na machukizo hakuna mfano kushuhudia wanyonge wakizidi kuandaliwa viongozi watokanao na koo. Huu, hakina, nao, ni ufalme wa mlango wa nyuma. Je watanzania wataendelea kuubariki na kupigia mhuri ufalme huu wa kifisadi kwa kuupa kura ili ule au wataukataa na kuukatisha? Ni bahati mbaya sana. Tofauti na Kalenga, watu wa Chalinze hawana ubavu. Lazima mwana wa mfalme ashinde hata kama ikibidi kuchakachua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
10 comments:
Jamaa hawana aibu. Lakini unajua kuwa na aibu kunahitaji upeo fulani. Maana pamoja na mmoja wa washindani hapo kusema kuwa kuwe na "fair play" lakini mtoto wa mfalme lazima ashinde. Hizo hela walizoiba haziwatoshi?
Jaribu unauliza jibu siyo? Hawa ukitaka pesa iwatoshe unatumia ile rationale niliyowahi kukwambia rafiki yangu aliyesema kuwa unatembeza kisu au kitanzi. Natamani yualiyotokea Libya yatokee hata kesho tuone wateule wakiuawa kama vibaka au nguruwe. Kuna kipindi ukisikiliza baadhi ya watu unacheka kwa uchungu kama jamaa yangu aliyeniandikia email baada ya kutundika uzi huu kuwa anatamani enzi za mapinduzi zirudi angalau tutaheshimiana. Nilimkatalia kuwa hata hao wanaopindua huishia kuwa kama hawa waliopindua sanduku la kura ili wale. Iringa tuna Prince Godfrey na Chalinze Prince Ridhiwan. Kamani hivyo basi wangekuwa wanakufa wenye watoto ili warithi watoto wao badala ya wengine kama Bwanamdogo aliacha nafasi mwana mfalme arithi.
Nyongeza ya princess, Joseph Kabila, Bongo, Kenyata....nk
Tunaendelea kukusanya fedha chafu kwa ajili chaguzi mwakani......soma hii habari....http://www.freemedia.co.tz/daima/mauzo-ya-iptl-yamwibua-zitto/
Anon acha nikukosoe. Ni princes kwa vile hawa ni wanaume. Anon wa pili shukrani kwa kuwekea mkazo huu ujambazi ambao unafanywa huku waathirika wakinyamaza kana kwamba hauwahusu.
Ndiyo Mhango, jamaa hawa wameishiwa sera, yaani siku hizi hata hawangaiki kujaribu kuwarubuni watu, sasa ni nguvu tu ya kimafia kama, "Sasa mtatufanya nini?" Maana kama kwenye link ya Anon ya juu hapo na mambo haya ya IPTL ya "mikataba mibovu" ya kampuni kuja na dola 50 halafu kulipwa dola laki moja kwa siku; halafu kuja na viini macho vya "mahakama, escrow accounts" halafu na hiyo hela kuja kutoweka; unajua kuna mkono wa Jakaya na genge lake. Hawataridhika mpaka waache nchi taaban.
Tumpe nafasi lakini bwana mdogo kaanza zamani siasa tangu enzi za Kabwe na mdee manzese tumpe nafasi lakini ya Kalenga hata kipofu ataona
Anon go tell it the birds. Kaanza zamani ipi na kwanini sasa kama kaanza zamani? Hana sifa yoyote ya maana zaidi ya jina la baba yake. Hivyo, hafai. Na nadhani watanzania hawahitaji usultani ambao unaanza kurejeshwa kwa mlango wa nyuma.
Jaribu umenena vyema. Tanzania kwa sasa licha ya kuwa shamba la chizi ni Danganyika hasa yenye kumilkiwa na Bongolalalanders.Kesho utasikia mama yake wa kambo akigombea ubunge Lindi naye utasema alianza zamani siyo?
Naye wanamsuka awe mwanasiasa. Kulikuwa na mjinga mmoja aliuliza mbona Marekani wakina Kennedy wengi nao walikuwa wanagombea? To which I answered, "Kikwetes are no Kennedys." Upande mmoja mbumbumbus wenye kipaji cha wizi, upande mwingine watu wenye akili zao.
Huyo aliyetaka kuwalilnganisha akina Kennedy na Kikwetes ana matatizo. Pamoja na Marekani kuwa na ufamilia nepotism through George Bushes angalau kuna jithihada binafsi za mhusika. Wananikumbusha kitabu na In praise of Nepotism cha Adam Bellow.
Hata kama akina Bush ni mataahira kwa hasa George Bush Jr wana nafuu ukilinganisha na wetu hawa ambao hawana tofauti na mbuzi.
Post a Comment