How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 13 March 2014

Mabilioni ya Uswisi: Vigogo wazidi kupeta huku tukipigwa changa la macho


Angalia wezi wetu wanavyotanua huku tukiangamia

Taaarifa kuwa majambazi wa Kitanzania walioficha pesa nchini Uswizi wamefanikiwa kuanza kuhamisha chumo lao ni pigo kwa watanzania tena maskini. Vyanzo vya habari ndani ya mamlaka za Uswisi vinaonyesha kuwa pesa iliyokuwa imefichwa nchini mle imepungua. Hii maana yake ni kwamba inahamishwa. Wakati hili likifanyika serikali ya Tanzania imeshikwa na kigugumizi. Wengi wanaokumbuka vitisho vya Mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredrick Werema kwa balozi wa Uswisi  Olivier Chave aliposema kuwa serikali ya Tanzania imegoma kushirikiana na ya Uswisi kurejesha pesa husika unajua kinachoendelea. Ni ajabu rais Jakaya Kikwete na genge lake anaendelea kuchekelea huku mali yetu ikizidi kufujwa na kufichwa? Je Watanzania wataamka lini na kuiandama serikali iache kulala kitanda kimoja na wezi? Je wewe kama Mtanzania unatoa ushauri gani kwa wenzako juu ya ni nini kifanyike? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

2 comments:

Anonymous said...

Wanahamishia Dubai

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kumbe wanahamishia Dubai! Hapa wametupata maana hichi kijiinchi ni cha kijambazi God knows. Tunapaswa kuwazuia kwa kuwanyima fursa ya kuendelea kututawala na kutula kama ujaka au vipi?