How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 19 March 2014

Zuma apatikana na hatia ya kutumia pesa ya umma kwa matumizi binafsi


 Taarifa ya Mlinzi wa Umma (Public Protector)  Thuli Madonsela imebainisha kuwa rais Jacob Zuma alitumia jumla dola 23,000,000 kwenye makazi yake binafsi huko kwao Nkandla. Wakati kashfa hii ikifumka, Zuma anakabiliwa na mashitaka mengine ya kulidanganya bunge na taifa pale aliposema kuwa hakuna pesa ya umma iliyotumika kwenye ujenzi wa makazi yake ya kifahari. Alidanganya kuwa makazi yake yamejengwa kwa pesa yake wakati si kweli. Hata hivyo, chama chake cha ANC kinaonekana kuendelea kumtetea kwa vile kinatawaliwa na mafisadi karibu katika kila ngazi.  Zuma anazidi kuwa mzigo kwa ANC hasa ikizingatiwa kuwa hii si kashfa ya kwanza. Amekuwa akipangua kashfa moja baada ya nyingine kuanzia ubakaji, ufisadi,uongo, matumizi mabaya ya fedha za umma na nyingine nyingi. Hao ndiyo viongozi wetu. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

3 comments:

Anonymous said...

Kuna msemo mmoja unasema "alikwisha zoeha kuchinja, hawezi vya kunyonga na vice-versa...Sasa watanzania kuna mgombea mmoja mtarajiwa wa kiti cha Urais kutoka chama kikubwa kabisa hapa Tanzania ambaye naye anazo sifa zote kama kama hizi Bwana Zuma anatumia jitihada zake zote kuwalaghai watanzania, ili afanye kama huyu mwenzake alivyofanya huko Afrika ya Kusini

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon,
Tutajie huyo mtu tumjue lau tuepuke maafa wanayokumbana nayo Afrika Kusini.

Jaribu said...

Si anayegombea tu, hata huyu anayetawala sasa naye ni hivyo hivyo, ndio maana yeye na Zuma ni kama pwagu na pwaguzi, au dumb and dumber.