The Chant of Savant

Friday 7 March 2014

Mkipitisha mafisadi najinyonga

Niliposikia majina ya wanaotaka kugombea urahisi kupitia genge fulani nilishikwa na tumbo la kuendesha. Si kwa woga bali hasira. Hebu fikiria, mfano, unakurupuka usingizini na kuambiwa kuwa genge, sorry, chama fulani eti kimempitisha mtuhumiwa wa ufisadi kama Eddie Ngoya-yai, au Bill Ngeleja au Stivi wahassira kugombea urais. Kwa akina sie wanaopenda kaya kuliko maisha yetu ujue hapa ndipo mwanzo wa kujinyotoa roho.
Hivyo, wale wanaotaka kunusuru uhai wangu, nasema wazi. Tafadhali kwenye meza ya kupendekeza majina ya ugombea urais sitaki kusikia majina kama Freddie Summayye au Ben Maembe au Sam Sixx. Pia msituletee watoto wa vigogo kama Jan Maka-mba, Emmy Nchim-bii na Hossein Ali Mwinyie. Kwani kaya yetu haina watu wengine wenye udhu na mawazo mapya hadi tuletewe wale wale waliopewa nafasi wakazichezea? Hivi mtu kama Lowa-sir ambaye aliingiza kaya kwenye hasara ya Richmonduli ambayo licha ya kumeza njuluku zetu ilituacha kwenye mabalaa ya migao na kulanguliwa umeme ana lipi jipya kama si kutafuta kutututumia zaidi kwa kuingiza Ma-Richmonduli mengine? Sijui mtu kama Summayye ambaye alikuwa kiranja msaidizi wa mkuu Ben Mkapppa aliuza na kugawa viwanda vyetu kabla ya kujitwalia yeye na mkewe, wakwe, vivyele na marafiki zake kama ana jipya la kutufanyia. Watu kama hawa walipaswa kubanwa na kuelezea tuhuma zinazowakabili kabla ya kuongozwa lupango wakajifunze. Huwezi, mfano, kutuibia halafu ukatumia njuluku hiyo hiyo kuwahonga wachovu wetu ili wakupe kura ya kula. Haiwezekani na haikubaliki hata kidogo.
Mtu kama Sam Sixx pamoja na kutusaidia kumfurusha fisadi Lowassssa, naye alichemsha pale alipopewa kacheo ka uwaziri akatelekeza yale aliyokuwa akisimamia hasa ile kugundua kuwa kumbe yeye na Mwakiwembe na Ma-tormatoes aka Manyanyanyanya walikatiwa kitu kidogo na maulaji wakatua solemba walevi tuliowaamini. Hawafai hawa hata wakisema wametubu na kuzaliwa upya kisiasa na kimkakati. Mtu kama Ben Maembe anajulikana asivyo na sera wala sura.
Walevi tunasema wazi: We don’t want corrupt bigwigs who in essence are looking for presidency so that they can rob us even more. Get it guys? Okey dokey, Well it is honky tonky! Woooi! Naona mibangi na gongo leo vimependa ukamaruni. Hata hivyo mie sikughushi acha nijisifu japo kidogo au vipi?
Kusema walevi wanasema wazi: hawaoni rais humu. Wana sababu kuntu. Kwanza, wanasema wahusika wana papara. Kwanini wasingoje wakati wa kuchuana waanze wao? Hii ni kuvunja sheria. Ina maana wakiwa kwenye ulaji wakawa juu ya sheria si watazivunja zote kwa uroho na maslahi yao?
Wengi wao wanatembeza fweza ambazo hawaelezei walikozipata ukiachia mbali kutoelezea hicho wanachotaka kununua. Je hii pesa imelipiwa kodi? Je wananunua nini ili kupata nini? Kama wanatoa fweza kutokana na mapenzi ya ghafla bin vu, kwanini sasa ni zamani?
Walevi wamenituma niseme wazi tena kwa kinywa wazi na kipana kuwa hata mafisadi na wabangaizaji wapigana vikumbo vipi hawawapi kura za kula. Wanawaona wanavyomwaga njuluku ambazo hawazitolei maelezo jinsi walivyozipata. Ajabu, hata wale waliokataliwa na mzee Mchonga akitaka watoe maelezo ya ukwasi wao eti nao wamo! Je wanadhani tumesahau kirahisi hivi? Tuliingizwa mkenge na mwenzao mara moja baada ya Mchonga kurejesha namba. Kwa aliyotufanya, si rahisi turuhusu fisadi na msanii mwingine hata angetupa ahadi ya kutupeleka peponi achia mbali Kanani. Mijitu inakuja na kutupa ahadi tamu lakini inaishia kututenza kwa uchungu. Nani anapenda rais atokanaye na ahadi nyingi lakini hewa na uongo mtupu kama ilivyotokea kwa maisha supa kwa wote? Nani anataka rais mzururaji asiyekaa ofisini badala yake akawa kiguu na njia kufukuzia matanuzi na per diem? Kwani hatuwaoni jamani hata kama sisi ni walevi? Kuna nini pale kwenye mjengo mweupe zaidi ya kuwa sehemu ya kusukia misheni kwa walaji wachache? Nani mpuuzi na juha arudie upuuzi huu kwa maangamizi yake?
Walevi tunasema wazo kuwa tumeishaistukia janja yao uchwara ya kutaka kutubamiza mkenge mwingine. Wale wanaotudanganya kuwa wanaweza kuwadhibiti licha ya kuwagwaya na kushirikiana nao waliingia hivyo hivyo. Hivi mnategemea nyani amzuie ngedere kula mahindi wakati wote ni nyani wale wale kwenye msitu ule ule? Tunawatahadharisha wale wote wanaotaka kujitwisha mkenge kwa kuamini kuwa wenzao wanaweza kuwakaripia na kukwazuia kutuibia tena. Msikubali maneno au makaripio yao. Lao ni moja kama alivyowahi kusema Lowassssa kuwa usuhuba na ushoga wao si wa kukutana barabarani. Wao ni damu damu dumu lije jua au mvua.
Hakuna kitu kimewaacha hoi walevi kama watoto wa mafisi na mafisadi eti nao kutaka kuwania urais wale kama walivyokula baba zao bila kunawa wala kuomba. Shame on you! Hivi vitegemezi vya wazito vina jipya gani zaidi ya kuendekeza business as usual ya kuwageuza walevi mataahiri na vihongwe wa kuwabeba wao, mizigo yao hata mashoga zao? Who wants such goon in the holy of the holy in the first place? Washikaji leo tusameheane. Baada ya kutoka kwenye mkutano wa kupamba ujangili kule Ulondon nimejikuta nikiwa na allergy na umombo.
Japo hii ilikuwa top secret ya confidential ya usalama wa taifa, leo nimeamua kuiweka wazi kuwa mkituletea wezi mafisadi na vitegemezi vya vigogo kurithi maulaji ya wazazi wao basi mwenzenu nitahama kaya. Pamoja na kwenda kwenye conference ya kuwazuga watasha kuwa nitapambana na ujangili kama nitaula, moja ya mipango yangu iliuwa ni kuandaa makazi mapya kwa maza iwapo mtaleta wagombea wezi watakaonunua walevi na kupewa kura zangu. Na hakika sitanii. Nitahama kaya na kwenda kujipanga upya ili nitakaporejea nije niwanyotoe roho kwa kujilipua na mibomu kama wale wahuni waitwao magaidi. Sikubali kaya yangu itokewe na kile ambacho kwa maza huita to go to dogs. Who wants his hunk to go to dogs? My foot! Si mfalme wa walevi hata kidogo.
Chanzo: Nipashe Jumamosi Machi 8, 2014.

2 comments:

Anonymous said...

Wagombea sahihi kwa mazingira ya sasa wanatakiwa watoke kwwa watu kama hao vitegemezi vyako na vitemgemezi wengine wowowte wailopo popote dunaini. maana huku nyumbani tulikuwa karibuni ndiyo hao hao na akili zetu zilivyodumaa ni wepesi wa kusahau, pia wepesi kujutia wakti maji yameishamwagika

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon usemayo ni kweli japo tunapaswa kubadilika maana hii ni sifa ya binadamu zaidi ya wanyama. Ila sikubaliani nawe unaposema wagombea lazima watoke kwenye hili genge la mafisadi papa wanaotaka kuleta usultani kwa mlango wa nyuma.