The Chant of Savant

Monday 3 March 2014

Mlevi azimia Kawa-dog’s Failure Formulae

    ASILIMIA 60 WALIOPATA SIFURI WAZIDI KUMLIZA MBATIA, ASISITIZA MITAALA ...
 
Nivwa izwyi lako lino likunjita
Kuti nkasambe mu umwanzi wakwe Mfumu
Ndikwiza mpfumu
Niza                         
Nkwiza kwe wewe
Nkwiza nswevya umwazi uno wanswizile x2
Nasikia sauti yako ikiniita
Nije nikatakasike kwenye
Damu yako Bwana
Nakuja mponya
Nakuja kwako
Nije nitakasike
 Kwenye damu iliyonikomboa
Guys, I’m serious today. Tuache mambo ya kuimba. Naanza na kimombo ili mjue nimebukua pamoja na kuwa mlevi. Isitoshe, wanasayansi wamegundua kuwa ukipiga ulabu kimombo kinapanda. Pia, waligundua.  Ukipiga bwimbwi kujihadaa kuwa uko mitaa ya majuu nako kunapanda. Pia, ukichaguliwa bunge la katiba, kujihisi uheshimiwa na kutaka mshiko mkubwa navyo hupanda. Hayo tuyaache. Humu si mwake.
 Baada ya kuyashuhudia madudu yaitwayo matokeo ya mtihani wa kidato cha Form Four Failure yaliyotangazwa hivi karibuni, nimegundua kitu kimoja. Ukitumia Kawadog’s formula of abracadabra and hanky panky, unaweza kutoka na ushindi mahali ambapo umeshindwa.  Sina shaka. Fomula hii itanisaidia sana kwenye harakati zangu za kutaka kugombea urais wa kaya ili niweze kuwa tajiri haraka mimi ukoo wangu na washikaji zangu.
Kwanza, nitoe tahadhari. Wale ambao vitegemezi vyao vimefeli wala wasikonde. wasijihangaishe wala kuhuzunika kutokana ukweli wa kisayansi kuwa elimu siku hizi si ufunguo na kama ni ufunguo basi ni wa kufungulia bia na si maisha kama ilivyokuwa zamani. Chini ya dhana na kanuni ya mwanasayansi aitwaye Ben Mkapae Tunituni ni kwamba vitegemezi vyenu vinaweza kufanya maajabu vikatajirika hata bila kuwa na elimu. Mtaalamu huyu aligundua kuwa kumbe ili kupata maisha bora uhitaji kuwa na elimu kubwa. Kwani mtaji wa maskini ni mtaji wake na si elimu yake. Simpo. Inawezekana huyu jamaa ndiye aliyeandika shairi la Karudi Baba Mmoja au Kama Mnataka Mali. Wale waliosoma miaka ya 47 nadhani wanakumbuka kitu hii kwenye fomu four au vipi?
          Nimefanya uchambuzi analysis, synthesis, synopsis, thesis na emphasis nikaibuka na kitu kimoja. Chini ya kanuni hii ya Kawadog chakachuazation and politicization of everything, ukiona watahaniwa wamefeli, unaamua kubadili mfumo kwa kuwazawadia waliofeli na walioshinda ili kuondoa malalamiko. Kwa vile nikiwa rais vitegemezi vyangu ima vitakuwa vikisoma ughaibuni au kuwa vimeishaanza maisha kiasi cha kuchangamkia dili chini ya uongozi wa baba yao, nitakuwa na hasara gani nikitumia Kawadog’s formular of making impossible possible?
          Chini ya Kawadog formula, ukitaka elimu au hata uchumi kupanda, uhitaji kujihangaisha na kufanya kazi kwa bidii. Uhitaji mikakati toka kwa wasomi kama vile wachumi au wataalamu wa elimu. Unachohitaji ni kuwa na wataalamu wa takwimu au statistics kwa kimakonde.  Ukishawapata watalaamu wa stats unawaamrisha wafanye vitu kuonyesha kuwa kiwango ima cha uchumi au ushindi kimeongezeka kwa kupunguza sufuri kwa kuzigeuza kuwa divisheni four. Simple, you easily get away with it au siyo?
          Kitu kingine ambacho nimejifunza toka kwenye kanuni hii ya Kawadog ni kwamba ukiona watu hasa genge lako limekustukia kiasi cha kukuita ujieleze baada ya fyatu fulani gengeni kukuita mzigo, unakwenda kwa rafiki yako jioni mnazoza na kukubaliana awazodoe kwa kujifanya hamnazo au hasikii kelele zao.  Ukitoka hapo unaitisha mkutano wa waandishi wa umbea na kutoa karipio na vitisho ukiwaambia viherehere kuwa huna muda wa kulumbana nao bali kungoja kukutana nao huko wanakotaka ili uwaonyeshe kilichomnyima nguwe urembo. Hapa unatumia kanuni nyingine moja itwayo Jake MriKiquette’s formular of killing noises. Chini ya kanuni hii ni kwamba ukisikia mafyatu wanaendelea kupiga kelele unajifanya husikii hata kama unasikia kila kitu. Ukiona umechoka na kelele zao unatumia kanuni iitwayo zodoazition ambapo unatoa lugha za vitisho na kejeli mfano kelele za mpangaji hazimnyimi usingizi mwenye ubavu wa mbwa. Simple, you get away with it.
          Ukiona washenzi na fyatu wanajifanya hamnazo kama wewe kwa kuendelea kuzoza na kupiga kelele unabadili fumula. Unatumia ile iitwayo enough is enough now ambayo pia iligunduliwa na gwiji Jake Mirish Kiquette. Chini ya dhana hii, unatumia lugha za vitisho kama vile “unyonge basi” na madude mengine kuwatisha wapinzani wako. Ila unapotumia kanuni hii unapaswa kuwa makini. Wakati mwingine hufanya kile kitu ambacho watalaamu huita ricochet resulting from blowback effects kwa lugha ya kimakonde. Inaweza kukuachia madhara ambayo kwa kimakonde huitwa the effects of aftermath ambapo walengwa wanaweza kutumia kanuni yako kukugeuzia kibao ukaishia kunywea kama mbwa aliyeiba mafuta.
Turejee Kawadog’s formula. Chini ya kanuni hii, ukishawatumia wataalamu wa takwimu kupika matokeo, unahakikisha unayatangaza kwa ufundi. Hapa kitu muhimu ni timing. Yaani kuwataimu walengwa na kuwastukiza ili ukiwaambia vitu visivyoingia akilini wasiwe na muda wa kukusulubu na maswali. Hivyo, unachofanya ni kungojea kuwapo tukio linalovuta walio wengi. Mara nyingi inashauriwa uvizie tukio la kisiasa lenye kuhusiana na mambo ya mshiko mshiko, sheria hata katiba ndipo ulipue bomu lako.
Ukishatangaza bomu lako unahakikisha unajipiga kifua kuwa umefanikiwa pale ambapo wengi hawakutegemea. Ikiwezekana unatafuta magazeti ya umbea ambayo yako tayari kutumika kama nepi na kuyaamuru yaandike uzuri wa kanuni yako kwa maendeleo ya kaya kielimu. Ikitokea wakajitokeza watu kukupinga kwa kutaka utoe takwimu za kisayansi, unazidi kujifanya hamnazo kwa kusema kuwa huna muda wa kujibizana na watu wasiojua wanachosema hata kama moyoni unajua fika kuwa wewe ndiye usiyejua unachosema. Wakati mwingine mambo ya usanii yanataka ujifanye hamnazo kweli kweli ili kuweza kusema vitu ambavyo hata massaburi hayawezi kusema ili mkono uende kinywani.
Kwa vile nimo mbioni kutangaza kugombea urais, nitatumia hizo kanuni hapo juu kuhakikisha naukwaa na pia kuwawezesha vitegemezi wangu kutawala baada yangu. Maana nitawahimiza wachovu kukubali kila nitakachosema kuhusiana na matokeo ya vitegemezi vyao ambavyo lazima viongezewe ujinga ili vitegemezi vyetu vivitawale na kuwala kama nitakavyokuwa nafanya mimi.
Kwa vile mimi na bi mkubwa na mwanetu ni wajumbe wa Bunge la Katiba, naachia hapa ili niwahi kutoa ushahidi na hoja ni kwanini tuongezewe mshiko. Chao!
Chanzo: Nipashe Machi 1, 2014.

7 comments:

Jaribu said...

Shukuru ana Phd lakini hana tofauti na bosi wake mwenye Phd hewa nyingi.

Anonymous said...

PHD yake ni katika field gani, maana ameingia katika utawala wakati hana hizo vitu muhimu katika nyajna hiyo hivyo ni vizuri kujitambua ingawa ukweli pengine anaogopa maisha uraiani ndiyo sababu waliowengi wanaendelea kuwapo ktk madaraka hata wanavurunda, na pia kumbuka kuna suala kulindana kwa lolote lile linafanyika halali au kwa kuvunja sheria na maadili

Jaribu said...

Engineering, nafikiri Civil. Haimanishi ukiwa na Phd utaweza kuwa waziri.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu na Anon wawili hapo juu ni kwamba kuwa na PhD ni jambo moja. Kuitumia vizuri hiyo PhD ni jambo jingine. Tunao watu wengi wenye PhD lakini ukiwasikiliza unashangaa walifikaje pale. Walichofanya ni kukariri na kuvuka mtihani bila kuelimika. Hebu chukulia mfano Abeid Karume aliyeweza kujenga maghorofa ya Michenzani yakamshinda Dk Salimin Amour hata kuyapaka rangi. Hivyo usishangae kuona haya madudu ya huyu jamaa ambaye ametumia urafiki wake na Jakaya kubaka elimu yetu. Hata hivyo wana hasara gani iwapo wanaiba kodi za wanyonge na kusomesha watoto wao nje. Hamkuona huko Kalenga jinsi hawa mafisi na mafisadi walivyoteua mtoto wa kigogo mwenzao kugombea ubunge bila hata sifa zaidi ya jina kubwa?

Anonymous said...

Oops na huyo naibu waziri wake kuvaa manywele ya bandia naibu waziri wa elimu watoto watapona hivi Tanzania hakuna Watu wanaowapa ushauri watu
Nampenda waziri wa utamaduni napenda sana style yake nywele

Jaribu said...

Ni kweli Mhango. Nilikuwa naangalia video ya Professor mmoja wa Tanzania akiongea, huku wanafunzi wake wakiinamisha kichwa kwa aibu. Aliyekuwa rais wa Brazil, Lula da Silva hakufika hata darasa la nne lakini aliukuza uchumi wa Brazil mpaka ukapita wa Uingereza.

Elimu ya Shukuru ya kukariri ndio inmetufikisha hapo, ndio maana inabidi walindane kwa kurithishana ubunge. Na waziri mzigo anaweza kutimuliwa, lakini rais mzigo ndio atafanywa nini?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu mie sishangai. Sie tulioanza ualimu kwa ngazi ya sekondari nakumbuka sana watoto walivyokuwa wakichukia kipindi cha kiingereza. Umenikumbusha mwalimu mmoja mwenzetu ambaye alikuwa akiongea kiingereza tunainamisha vichwa. Huwezi kuamini kuwa baadaye aliweza kumilki shule yake. Si hilo tu, tuna maprofesa wengi ambapo ukweli ni kwamba bado wako shallow sema mfumo wenyewe tu unawabeba. Hata huyu mkuu wa chuo cha Manzese nina wasi wasi ni mwanasiasa tena mwenye kujikomba zaidi ya profesa. Kimsingi, sasa Tanzania ni upuuzi na utapeli mtupu. Je umeinyaka ya mwana wa mfalme RizOne kuteuliwa mgombea ubunge wa Chama Cha Marithishano?