The Chant of Savant

Thursday 6 March 2014

Saadi Gaddafi arejeshwa Libya

Facebook pictures of Saadi Gaddafi 6 March
Mtoto wa kiume wa imla wa zamani wa Libya, Saadi Gaddafi alirejeshwa juzi nchini kwao kupambana na mkondo wa sheria baada ya serikali ya kifamilia ya baba yake kuangushwa mwaka 2011. Gaddafi alikimbilia nchini Niger baada ya kuangushwa na kuuawa kwa baba yake, Muamar Gaddafi. Saadi ni mmojawapo wa ndugu wengi wa Gaddafi wanaowindwa na mamlaka nchini mwao warejeshwe ili wajibu mashtaka mbali mbali yatokanayo na matumizi mabaya ya madaraka.
                 Wakati Gaddfi mdogo aliyesifika kwa ufuska,  kupenda mpira na matanuzi kwa vile baba yake alikuwa rais akirejeshwa, nchni Tanzania ndiyo watoto wa marais wanaanza kujitokeza kufaidi madaraka ya wazazi wao. Kurejeshwa kwa Saadi kumekuja siku moja baada ya Ridhiwani Kikwete mtoto wa rais Jakaya Kikwete kupitishwa na chama chake kugombea ubunge ili arejeshe jimbo la baba yake kama alivyokaririwa hivi karibuni akisema sambamba na mtoto mwingine wa kigogo Godfrey Mgimwa anayegombea jimbo la Kalenga kurejesha jimbo la baba yake. Wakati haya yakitokea sijui kama watawala wetu waroho na wabinafsi wanajifunza chochote. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

2 comments:

Jaribu said...

Si ndio maana walitoka povu Ghaddafi alivyotimuliwa? Hawa wezi wote wanatakiwa wawe jela kama walivyomfanyia Babu Seya.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu usinikumbushe ugomvi wa mabibi kati ya hawa wakware wawili mmoja mwenye madaraka na mwingine midenguo. Sijui kwanini Ridhiwani hampigii chapuo baba yake wa kufikia.
Ya mwana wa Gaddafi imenifurahisha. Ila sitafutahi kama alivyokamata Seif al Islam aka Ridhiwani wa Libya.