The Chant of Savant

Friday 7 March 2014

Mjue nshomile mwizi anayeita dola milioni 75 pesa ya ugoro.



Kwa wasiojua ujambazi wa wa IPTL ambao Tanzania imefanyiwa tangu mwaka 1995, nyuma yake kuna nshomile mmoja aitwaye James Rugemalira mmilki wa Mabibo Breweries. Mwizi huyu alitoa mpya juzi alipokaririwa akisema, "Niliiambia Serikali kuwa nyie mmeibiwa na sisi tumeibiwa. Mimi nikawaambia kuwa ‘the end justify the means’ (jambo la muhimu ni matokeo, si njia ulikopitia), mwisho tulikubaliana kwamba kwa masilahi ya Taifa tumalize kesi hii, na mimi ndiyo nikalipwa hivyo vijipesa vya ugoro."
Ashuukuru Mungu nchi inatawaliwa na wezi vinginevyo ingekuwa wakati wa mwalimu Nyerere angeozea gerezani. Ni ajabu kwa nchi inayokopakopa kuwa na mtu mwenye kuita bilioni 120 pesa ya ugoro. Je huyu jamaa ana ukwasi kiasi gani?
Wakati akijitapa, vyombo vya habari vimegundua kuwa kumbe yeye na washirika zake toka Malaysia wamekuwa wakilipwa dola 100,000 kwa siku kitapeli kwa kudai walikuwa na mtaji wa dola 50,000,000 wakati ukweli ni kwamba walikuwa na mtaji wa dola tano. Hata hivyo, ana hofu gani iwapo aliyekuwa waziri wakati wizi huu unafanyika sasa ni rais? Hata ukiangalia jina la kampuni ya mwizi huyu la VIP Engineering unapata swali moja kuu: Je kuna VIP nyuma ya wizi huu wanaompa kiburi huyu mwizi hadi kukufuru?

4 comments:

Anonymous said...

Toba tumekwisha
Wazungu wa kweli hawawekezi Tanzania
Wanaiogopa Tanzania Kama ukoma
Hata wahindi na wachina wawekezaji Walikuwa kwenye viwanda na siyo kwenye rasilimali Kama madini na mbuga za wanyama . Toba Toba Watanzania

Anonymous said...

Hakuna mwekezaji makini atakuja wekeza sehemu ambayo haijtayarishwa kwa mazingira ya vitendo za nyenzo za biashara...Iwapo...Hakuna utaratibu timilifu katika utawala, hakuna maji ya uhakika na umeme, Hakuna nguvu kazi yenye maarifa, hakuna haki na usalama wa mali kutokana vyombo husika kuwa dhaifu inayosababishwa na mambo lukuki kuleta hisia maslahi binafsi na mfumo sugu kutowajali wanausalama hasa polisi...

Hakuna mwekezaji makini atawekeza mahali ambapo umeme unaweza kupandishwa bei hata kwa aslimia arobaini kila mwaka....

Kimsingi mwekezaji anweza kuwekeza hapo atakuwa anaendana sawai kimtazamo na watawala wetu kwamba njoo iba utakatosheka ondoka

Inauma lakini kwamba wenzangu pia inawauma ili jambo kama linavyoniuma mimi....Iwapo ingekuwa kweli inawauma ningetegemea hata mikutano ya ccm ingenguwa na mahudhurio hafifu sana...lakini ni kinyume chake....Hata huu mchezo wa kuigiza unaendelea hivi katika Bunge la Katiba naona watu wote walihusishwa ni wale wale na mawazo ya yale yale ya mwaka 1947...NN Mhango na wengineo wote wazalendo wenzangu naomba angalia hii video...http://www.youtube.com/watch?v=VxA5cxdQ2uA..na pia iwe kama ndiyo kifungua kinywa kwa wazalendo wote.

Maana mimi naitumia kila siku kuisikiliza kuniletea munkari zaidi na zaidi.......

Jaribu said...

Anonymous nimeangalia hiyo video na nimeipenda, kumbe Mchungaji Msigwa ni mtu wa point, kwa sababu amegusia themes zile zile ambazo nazipenda mwenyewe.

Hasa imenigusa point yake ya Waziri fulani juha kusema nchi iombewe. Serikali jukumu lake siyo kuhimiza watu waombe, bali kutatua matatizo yao. Wanatumia mbinu za "slave masters" za zama zile kuwahenyesha watumwa wiki nzima, halafu kuwaambia wakaombe Jumapili au Ijumaa for that matter. "Nyinyi subirini mpaka mkifa mwende peponi, lakini sisi pepo yetu itakuwa hapa hapa." Ndio maana Watanzania wengi wanajifariji kwa imani kuwa viongozi wa CCM wataishia jehanamu.

Labda inaweza kuwa kweli, lakini sisi wengine tunataka wapate hukumu yao hapa hapa duniani, wakati miili yetu bado ina three-dimension. Turidhike kuwa hawa wakora wamepata their comeuppance.

Mhango, huyu Rugetaahira labda nijifariji tu kuwa ana sura ya sokwe, kwa sababu ananipa donge na siwezi kufanya lolote zaidi ya kuandika donge langu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hata mimi nilifurahi sana kuwasikia akina Msigwa na kuchukizwa na yule mshenzi wa kirundi Peter Serukamba aka mr F*** you. The guy has been f**ed so much so that he thinks everybody is just like him.