Napendekeza tuvunje muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutokana na sababu zifuatazo:
Tukifanya hivyo tutatenda
haki kwa CCM na wale wanaotaka serikali tatu.
Tutatofa fursa kwa nchi
mbili kutafakari kuungana upya kwa masharti mapya au la.
Tutatoa fursa kwa pande
zote mbili kuishi bila kuungana na kuona madhara au faida zake.
Tutaokoa muda wa malumbano
na upotevu wa pesa za umma.
Wananchi wa pande zote mbili kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 1964 watapata fursa ya kufaidi nchi zao asilia.
Wananchi watapata fursa ya
kutumia uraia wao bila utata wala kuutelekeza mwingine.
Tutaepusha muungano wa
migongano na mashaka ambao umekuwa ukimomonyolewa taratibu kama alivyobainisha
jaji Warioba hivi karibuni aliposema, “Waasisi walituachia mambo 21 (ukiacha
usajili wa vyama) kwenye orodha ya Muungano. Katika kipindi cha miaka ishirini
iliyopita yamepunguzwa. Mambo yote yaliwekwa kwa utaratibu uliowekwa na Katiba
lakini yameondolewa kinyume na Katiba.”
Tutaondoa malalamiko ya
pande mbili ya kunyonywa
Pande mbili zitafaidi uhuru
wa kuwa mbali na mwingine.
Ukidhani ujuzi ni aghali
basi jaribu ujinga. Vivyo hivyo ukidhani ndoa ni kero jaribu talaka.
8 comments:
When poverty comes in at the door, love flies out of the window...this is all about this symbiotic union....
Let us walk out alone then we see and lives the door open for Zanzibar to come back under new rules and conditions as Tanganyika will be on driving seat on negotiation without humbling.
Anon,
You've made good points. The thing is if Zenj goes solo CUF will devour it and the results will look exactly the same as the ones in Commoro.
Ukraine. Ukraine
We should do that in Tanzania as well
Sipendi muungano usio na tija
Tujaribu Kama ujerumani. Shirikisho
Chadema wana sera nzuri ya majimbo
Nafikikiri hiyo ni nzuri sana
Tuwe na serikali moja tu
Nimesoma kwa michuzi
Eti waturuki wanakuja kuwekeza kwenye fani ya ukandarasi eti sababu wameridhishwa na utendaji wa Tanzania
Jamani mturuki naye muwekazaji
Mbona mpaka Leo wazungu wenzake hawajamkubali Kuwa member wa EU
Wanajua matatatizo ya uturuki
Chonde Chonde Watanzania mturuki si mtu mtu pesa
Sera ya uwekezaji kwa nchi Tanzania na tabia iliyojengeka kwenye vichwa vyetu katika jamii nzima ya watanzania. Mwekezaji anachagualiwa kutokana na vitu viwili tuu kama vigezo visivyotajwa kwa uwazi ambavyo ni Rushwa na haiba(ukiwa unatoka njea ya Tanzania basi inatosha kuitwa mwekezaji
Anon hapo juu usiyependa muungano una hoja kuwa tujaribu shirikisho lau kila mtu ajue mipaka ya ukuu wake. Anon wa pili umenena. Hawa waturuki huenda kuna mhindi amewalete kuchota kama walivyofanya RITES. Maana nchi yetu inatawaliwa na mabwege na wanafiki. Hukumsikia eti Sumaye analalamikia mikataba ya uwekezaji wakati yeye na Mkapa ndiyo walioanzisha ujambazi huu kwa kuruhusu wake na shemeji zao watumie ofisi zao kupiga deals.
Tena niliposoma hii habari ya Sumaye na maneno yake yakanithibitishia kweli sisi walafi tunakosa maarifa...tupo tayari kusema lolote lile bila aibu kujaribu kuwadanya watu wasiojua kujisomea na kufanya tafiti....Ingekuwa mimi mmmoja wa washirikia alipokuwa anaongea hayo ningemkumbushia historia tuliwaona mababu zetu kuwa majuha walipo sainishwa mikataba na wakoloni wakati huo wao hata kusoma na kuandika walikuwa hawajui...Tena huyu Sumaye amefanya Harvard University Masters Degree....NN Mhango tusaidia kwenye tafiti...Maana walakini unaanza kujitokeza....Wee weee Sumaye acha kabisa kutudanganya sisi tuliokosa fursa ya kupata maarifa .....Acha kabisa husirudie tena tena na kukemea weee Sumaye
Anon,
Nadhani Sumaye amepata ujumbe wake. Kesho utasikia hata Mkapa akindandia huu ujambazi ulioanzia kwake. Kesho kutwa utamsikia Njaa Kaya Kikwete naye akikandia wakati ataacha balaa sawa na lile aliloacha Mwinyi.
Post a Comment