How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 2 June 2014

Angalia wanigeria wanavyomsanifu first lady wao asiyejua kiingereza

Wanigeria haana masihara na viongozi wao. Baada ya kugundua kuwa mke wa rais wao kiingereza hakipandi huwa hawaachi kumzodoa ili lau apate somo kama si wengine. Natamani kupata kitu kama hicho hapo juu kuhusiana na first lady wetu Salma Kikwete (wanafanana hata kwa sura) ambaye naye kama Patience Jonathan hakipandi na akijaribu kukiongea huloa jasho kama mtu anayekaribia kufa kwa shinikizo la moyo.
Kusikia Salma anavyobukanya kimombo huku akikaribia kupasupa, BONYEZA HAPA https://www.youtube.com/watch?v=aHKzLS9yG2Q


5 comments:

Anonymous said...

Kwa hili napingana nao kiingereza ni lugha Kama Kiswahili. Au kimakonde
Kujua kiingereza hakumanishi wewe mwelevu kuliko wasiojua kiingereza
Kwani. UK, USA hakuna wajinga

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hujakosea. Nami sisemi kuwa kujua kiingereza ndiyo kujua kuliko wengine.Kinachogomba ni watu kuacha kuongea lugha zao wakadandia za wenzao waonekane wanajua au wamesoma. Angeongea kikwao nani angehangaishwa na hilo?

Anonymous said...

Umenena
Nashangaa viongozi wa Tanzania kuongea kiingereza wakati Watu wa Tanzania au walipa kodi asilimia 70 hawajui kiingereza
Inashangaza hata hotuba au dhifa ya taifa viongozi wanaongea kiingereza hata UN
Halafu hao hao wanataka Kiswahili ki we lugha ya kimataifa

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Kwa taarifa yako wanaikonea aibu Kiswahili kiasi cha kujilazimisha kuongea Kiingereza huku wengi wakionyesha wazi hawakijui. Japo siwasemei, kwao kusoma ima ni kuongea Kiingereza au kughushi na kuitwa daktari kama wengi wa mawaziri wao walivyo kwa sasa. Huoni wakenya wanavyotutapeli wakitujazia walimu feki kwenye shule zetu za kimataifa ukiachia mbali kuhangaisha watoto wetu kwenda kusoma Uganda na Kenya.

Anonymous said...

Na hata huku ulaya walimu wengi wa Kiswahili toka Kenya hadi Ghana
Tumekwisha