The Chant of Savant

Wednesday 12 November 2014

Nani atanusurika kati ya bunge na IPTL

7 comments:

Anonymous said...

Bila shaka, IPTL($,TZS) itanusurika kwa sababu ni kubwa na ina nguvu kuliko bunge.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umesema vyema kwa vile IPTL ni zaidi ya Rugemalira na Ponjoro Singh. Ni serikali ndani ya serikali au vipi?

Anonymous said...

Kumenuka bunge la South Africa wabunge hawamtaki Zuma kwa ufisadi CNN wametoa leo
Bado Tanzania kiama cha CCM ama kweli mungu analipa
UKAWA chukueni matokeo yote haya duniani kuwaonyesha Watanzania kwamba they need change, Na mabadiliko na maendeleo yataletwa na nyinyi UKAWA

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umesema vyema. Tanzania haiwezi kuwa kisiwa vinginevyo iwe imekaliwa na mataahira na wendawazimu. Sitaki niamini hivyo. Nadhani kiama cha CCM kinapaswa kufikishwa haraka hasa wakati huu ambapo ICC inatisha kwa wale wanaotaka kutumia polisi kushambulia waandamanaji. Nadhani kama ulivyoonyesha, ni kama upinzani unalaza damu. Walipaswa kuwahamasisha watanzania kufanya walichofanya wenzetu wa Burkina Faso hivi karibuni.

Anonymous said...

Nina mashaka sana na kuhamasisha kwako NN Mhango. Nidhamu ya uoga na amani( tuite "utulivu"). Imejengwa na misingi ya huoga na hofu kujitokeza hadharani mfano halisi hapa ungani, bado tunajificha wakati wa kutoa maoni.

Pia inawezekana pengine waandikaji maoni haya hapa wengi wao wanaishi au makazi yao ni ughaibuni wangali wanajificha sembuse sisi tuliyohapa Tanzania mnataka tukaandame kwa lipi hasa.

Iwapo ninyi waandika maoni mtakapo anaza kujitokeza inaweza kuleta hamasa kwetu kwamba tupo pamoja katika kupambana na changamoto hizi.

Anonymous said...

Tunajificha kwa sababu CCM ni chama dikiteta unataka watuulikomba
Kama si sisi familiya zetu bongo
Lakini tusemayo yana ukweli Na nyinyi muishiyo bongo ndo wenye kuathirika na utawala wa CCM , lakini hamfungui macho yenu, kanga, vitenge, fulana, mnauza kura zenu.wenzenu wanatanua tunao Kila leo ughaibuni na wengine wananunua majumba ughaibuni kwa kodi zenu. Sisi ni kama changamoto kwenu

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon wa kwanza hapo juu si kweli kuwa tunajificha ughaibuni kwa woga. Nadhani uwepo wetu huku umetuwezesha kupata fursa kisomi na kiuchumi kupambana na mfumo huu kwa kuuchambua. Mimi nimeandika vitabu ambavyo kama ningekuwa huko huenda nisingefanya hivyo. Hivyo, mapambano si lazima wote tuwe dani.
Anon wa pili nakubaliana na hoja zako kuwa walioathirika sana wamo nchini. Sisi tungekuwa wachoyo basi tungenyamaza na kuendelea na "anasa" zetu kama alivyosema anon wa kwanza lakini hatufanyi hivyo kwa vile tunaipenda nchi yetu na watu wetu.