How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Thursday, 6 November 2014

Nimeipenda hii kitu


Badala ya jeshi kulinda umma linalinda ufisadi siyo? Je hili jeshi ni la nani? Kuna haja ya kwenda Burkina kujifunza jinsi ya kukomesha uchafu huu haraka sana. Ajabu, wakati jeshi likilinda uoza,licha ya kusahaulika na kunyonywa sawa na wananchi,linalipwa kwa kodi zao ili kulinda wale wanaowahujumu. Hivi nani aliyewaroga wabongo ambao ICC imesema itawafunga watakaojaribu kuwaua na msichukue hatua? Hongera Masoud Kipanya kwa kutuchangamsha huku ukiwasuta.

2 comments:

Anonymous said...

Tungewezaa kupat vichwa kama hivi angalau 2000 tuu afrika ingebadilika kuwa na maendelea vitendo siyo hadithi na mitutu inayoendlea kushikiria wahalifu...kama anavyoelezea hapa Professor Patrick Loch Otieno Lumumba
https://www.youtube.com/watch?v=4cbEuwqKKqE

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon si kwamba vichwa havipo. Vipo vingi sema vimezimwa iwe ni kwa kuuawa au kwa kuhujumiwa visisogee mbele. Kuna watu wana vichwa vinavyochemka lakini hawana uchungu na nchi zao. Ni waroho na walafi wenye roho mbaya kuliko hata fisi. Wako tayari kuwauza hata mama na baba zao ilmradi lao litimie. Nadhani hiki ndicho chanzo cha msiba wetu kama waswahili.