How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Wednesday, 12 November 2014
ijiwe chalaani uhuni dhidi ya Warioba
JAPO nguli Jose Shinda Warioba si mwanakijiwe wetu, huwa tunamzimii hasa kwa utaua na usafi wake ukiachia mbali ujasiri wake wa kupambana na ufisadi na ushenzi hasa uchakachuaji wa Katiba.
Hivyo, leo maprofesa wanakijiwe wanajadili kadhia iliyomfika nguli huyu aliyesalia pekee baada ya kuondoka kidume Mzee Mchonga (May Peace be Granted to Him).
Leo linaanzishwa na Mgosi Machungi anayeonyesha wazi kukereka. Akiwa amekunja ndita na kusonya hovyo hovyo akitishia kumpiga mtu zongo anasema, “Waheshimiwa Mapoofesa, mmeonaje uhuni wa kinyangaika anayeitwa Makondaa kutaka kumshambulia mzee Jose Waioba”
Hangoji tujibu. Anakatua mic tena, “Leo natoa onyo kwa maa ya kwanza na mwisho, huyu Makondaa asipoomba msamaha toka kwa mzee Waioba mie nitamtokea personally na kumfanyia kitu mbaya haafu nampiga zongo.”
Kapende aliyekuwa akimsikiliza Mgosi kwa makini anakula mic, “Profesa Mgosi umefanya vizuri kuleta hoja hii. Nyie hammjui huyu bazazi Makondaa. Namfahamu tangu anazaliwa hadi hapo alipo akijitoa mhanga kutumika kana nepi ya kusafisha uchafu wa mafisadi. Huyu anasumbuliwa na njaa na ile hali ya kutopata malezi bora.”
Mijjinga hangoji Kapende aendelee. Anakula mic, “Profesa Kapende nakuunga mkono. Huyu kichaa licha ya kubangaiza kwa kujikomba na kujidhalilisha, bila shaka anatumiwa na wale tuliowasikia kwa masikio yetu wakishangilia yaliyomsibu mzee Waryuba. Hamkumsikia Njaa Kaya akimpiga kijembe akisema asingetamani yamkute haya wakati akijua wazi yuko nyuma yakeYamkuta mara ngapi wakati akishakitoa tutamweka lupango kwa madhambi yake”
“Mie wazee nasema wazi wallahi. Heri yaliyompata Warioba yamemuongezea hishima kuliko hawa manyang’au wasiojua yaweza kuwakuta yaliyonkuta Blaise Compaore aka Ebola. Heri Warioba yalomkuta yanaonyesha usafi na uzalendo wake kuliko hawa waathirika wanioanguka hovyo hovyo.” Anakandia Mpemba huku akibwia kahawa yake.
Msomi Mkatatamaa hangoji. Anabutua mic, “To be honest with you, sioni aibu yoyote kwa Warioba bali aibu kwa wale waliowalipa wahuni kwenda kumfanyia fujo. Huu ni utovu wa nidhamu. Kwani ukimfundisha mwanao kutukana wakubwa hatimaye atakutukana wewe. Hili si jambo la kushangilia wala kurusha vimondo.”
Anakohoa kidogo na kuendelea, “Hawa wanaoshangilia masahibu ya Warioba hawana akili sawa sawa hata kama ni wakubwa. Ni wakubwa kwa umri na nyadhifa lakini vichwani ni makinda tu.”
Mipawa hangoji, “Tulipowaambia kuwa kaya yetu ina ugumba wa uongozi tulimaanisha haya wanayofanya hawa mwatwahuti ambao hawana tofauti na Boko Haram kisiasa. Hata hivyo, sishangai. Kama wameshindwa kushupalia mambo ya muhimu kama kushughulikia wezi wa njuluku zetu watashindwaje kushupalia uovuAsiyejua maana haambiwi maana.”
Sofia Lion aka Kanungaemba hangoji. Anaphora mic na kupayuka, “Sioni sababu ya kuwahusisha watu wasiohusika na vurugu za Makondaa. Nadhani Makonda alifanya hivyo kutokana na hasira na sababu zake. Hivyo, tuwe makini tunapowaingiza watu wasiohusika.”
“Go tell it to the birds Sofi. Hivi unadhani inahitaji digrii ya upelelezi kujua nani walimtuma MakondaaLaiti ndata wetu wasingekuwa wanachama wa Chama Cha Mafisi na Mafisadi (CCMM) wakatumia sheria kibaguzi, wangembana huyu zuzu akawataja mabwana zake waliomlipa na kumtuma azushe fujo.” Anarejea Msomi.
Mheshimiwa Bwege aliyekuwa akisoma gazeti anakula mic, “Nyie hamjui. Hizi ndizo sera za watu walioishiwa kulhali. Mnashangaa kufanyiwa fujo mzee WariobaNani mara hii kasahau fujo wanazofanyiwa walevi kuanzia kuwapiga hadi kuwanyotoa roho kama ilivyotokea Arusha ambapo walevi waliuawaMmesahau sakata la hivi karibuni kule Kyera ambapo mkuu wa ndata alikwenda usiku wa manane kwa kiongozi wa upinzani eti kuzuia mkutano uliokuwa uhutubiwe na iron lady Halima Mndee”
Kanji hataki kupitwa. Anakwanyua mic, “Mimi ona baya sana ile toto vamia zee Wariboa. Kama sema Sofi, hapana ingiza vatu yote kwa fujo nafanya hii toto chafu Konda tovu ya nidhamu.”
Kabla ya Kanji kuendelea Mbwamwitu anampora mic na kuzoza, “Kanji na mshikaji wako Sofi mnapaswa kuelewa kuwa hakuna anayewaburuza watu kwenye aibu hii bali wao wenyewe. Kama hawataki kuhusishwa wana-comment nini”
“Mmwagie huyo na hata Kanji na Da Sofi hadi wazimie. Maana profesa Mbwamwitu ametoa pwenti si mchezo,” Kapende anamwambia muuza kahawa ampe kahawa Mbwamwitu. Kanji hakubali, “Veve Pende acha tuna sisi. Veve weza mwagia mimiHapana ona gahawa iko moto”
Kapende anacheka na kusema, “Mimi simwagi matusi na vujo kama nyinyi na Makondaa yenu. Namwaga raha tu au vipi” Msomi kuona utani unataka kuharibu mada, anakwanyua mic, “Mimi naona tupange jinsi ya kumtia adabu huyu kidhabi ili liwe somo kwa wengine. Mnaonaje tukamfuata kwake na kumfanyia kitu mbaya yeye na mkewe ili liwe onyo kwa wanamtuma kuwa wajiandae kuliwa”
Mijjinga hangoji. Anakula mic, “Mie nitakuwa wa kwanza kumuingia. Maana hatuwezi wote kuonekana woga.”
“Yakhe hata kama mie sitaki shari, hili sintovumilia wallahi. Heri tunsake huyu Makondaa tuntie adabu wallahi.”
Kijiwe kikiwa ndiyo kinanoga si akatokea Makondaa. Wacha tumshike na kumvutia uchochoroni tayari kumshughulikia ili liwe onyo kwa mabwana zake na wahuni wenzake.
Chanzo: Tanzania Daima leo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Warioba kwanini huhami au kuicha CCM.Nyerere alisema CCM si mama yake.
CCM wamekufanyia hao, mawaziri, wabunge wa CCM wamekukashifu sana kwenye vyombo vya habari,sishangai kufanyiwa fujo ni CCM hao, tangu ulipo fanyiwa vurugu leo ya ngapi na video inaonyesha wote wahusika ,mbona hawajakamatwa mpaka sasa.au uchunguzi unaendelea ili tusahau kama kawaida Yao.
Watalipa hii 2015
Post a Comment