Mwanaidi Majaar mama aliyetuhumiwa kusaidia wizi wa EPA aliteuliwa balozi na hatimaye ulaji mwingine kama kulipwa fadhila. Je Kikwete ana nni na wanawake hawa? Mbona wamepanda haraka haraka wakati hawana sifa hata robo kwa walio wengi. Na hawa ni tone la maji kwenye bahari ya nyangumi Kikwete
Kwa wanaofuatilia uteuzi wa Kikwete wa watu wa kushika nafasi mbali mbali, watakubaliana nasi kuwa kuna udini, kujuana, ushikaji hata uhawala kwenye uteuzi wake. Ukiangalia wakuu wa mikoa, wilaya, mawaziri, wabunge wa kuteliwa, majaji na walaji wengine utagundua hili. Ni balaa. Utumishi wa umma umegeuzwa biashara ya kuhongana ulaji na kulipana fadhila. |
No comments:
Post a Comment