How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Tuesday, 9 December 2014

Unapotimiza miaka 53 ukiwa katika hali hii tafakari!


Je hiki kibonzo ni utani au ukweli? Ni mtanzania gani anaweza kusema hayuko hivi? Kama hauko hivi basi ndugu, majirani hata ndugu wa ndugu wa ndugu zako hata marafiki wa marafiki wa marafiki zako wako katika hali hii. Nawaona Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wakiwa wamevuaa manyang'unyang'u huku wakikalia mwamba wa almas. Je hapa tatizo ni akili au utashi?  Je tatizo ni utaahira au upumbavu? Tatizo ni upofu au ugonjwa? Sijui tatizo ni nini kati ya uroho na roho mbaya. Je kwa watanzania walio wengi ambao ni maskini tunasherehekea Uhuru au Udhuru? Tafakarini?

2 comments:

Anonymous said...

Mafanikio yetu kama ifuatavyo...Kuuzwa NBC kitapeli wahusika wanapeta tuu, Waliosaini IPTL mpaka leo wanakula mafao yao(Escrow Money), Meremeta, Kagoda,Richmond-Dowans na Sasa Symbion, EPA, Rada na wahusika kuendelea kupeta, Ndege ya Rais,Wagonjwa hosptalini kulazwa sakafuni, Viongozi wa juu serikalini wanaumwa kutibiwa ughaibuni, Mahuaji Bulyanhulu Mines, Ulimboka na Kibanda kuteswa....nk

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon umeua. Sina cha kuongeza zaidi ya kukupongeza na kukukaribisha tena na tena uje na kuweka vitu kama hivi vilivyokwenda shule.