Wakati tunakuwa, kunyonyesha lilikuwa jambo la kujivunia tena la kawaida kwa kila mama mwenye mtoto. Hakuna aliyeona kinyaa kwa mama kumnyonyesha mwanae. Wengine, hadi sasa, tunachukulia kuwa kunyonya na kunyonyesha ni haki ya binadamu ya kila mtu. Ajabu ya maajbu, kadiri siku zinavyokwenda, kunyonyesha kunaanza kuonekana kama kosa la jinai hata aibu. Kwa upofu, tumepwakia mila za ajabu za kimagharibi kiasi cha kuanza kujivua nguo wenyewe. Hapo juu, mama wa kiafrika ambaye ni mbunge huko Kenya, anatimuliwa bungeni na baba wa kiafrika ambaye ni spika wa bunge la nchi hiyo. Hii ni ajabu kidogo.
No comments:
Post a Comment