The Chant of Savant

Friday 16 August 2019

UJUMBE HUU NI MAALUMU KWA RAIS MAGUFULI NA WASHAURI WAKE

     The prime minister, Ahmed Abiy, plants a tree in Addis Ababa, Ethiopia. 
John Magufuli: Tanzania president sweeps the streets outside state palace
Mheshimiwa rais John Pombe Magufuli, PhD,
Sina mazoea ya kutumia vyombo vya habari kuwasiliana na viongozi zaidi ya kuandika kwa ajili ya wote wanaosoma maandiko yangu. Leo navunja mwiko. Naandika andiko hili fupi mahsusi wewe usome, kama si wewe washauri wako au watu wako wa karibu.
        Hivi karibuni jarida maarufu la the Guardian liliandika habari njema toka Afrika pamoja na ukweli kuwa vyombo vingi vya habari vya Magharibi huwa havioni mazuri yanayofanyika barani Afrika. Jarida lilioandika kwa mstuko na upekee kupandwa jumla ya miti milioni zaidi ya 350 nchini Ethiopia kwa muda wa masaa 12 huku ikipandwa jumla ya miti zaidi ya bilioni mbili ndani ya miezi michache iliyopita. Haya ni matokeo na fikra za kiongozi mpya wa Ethiopia Ahmed Abiy, kijana anayeonekana kuleta chachu ya maendeleo na mageuzi ya kiutawala barani Afrika kama ambavyo nawe umekuwa ukifanya.
      Kwa vile janga na mabadiliko ya tabia nchi ni matishio kwa maisha ya wanadamu wote wakiwamo watanzania, nashauri uige mfano wa kiongozi huyu na kuhimiza watanzania si kupanda miti tu bali kupanda kwa wingi hata ikiwezekana wavunje rekodi ya Ethiopia. Pia lile zoezi lako la kusafisha makazi wa wananchi kila wiki lirejerewe na kupewa mwamko mpya. Maana siku hizi halisikiki tena.

No comments: