The Chant of Savant

Sunday 18 August 2019

LALA MAHALI PEMA PEPONI JOHN NG'AMG'A Hurúka thayú ithe wa Cikú

John DeMathew.

Gari aliyokuwa akiendesha marehemu inavyoonekana baada ya ajali
               Kwa wakenya, ukiondoa watoto wachanga na wenye maradhi ya akili, sina shaka kama kuna asiyemfahamu John Demathew gwiji la muziki wa kikuyu aliyetingisha bila mfano wala mpinzani. Kwa watu wa kabila lake la Kikuyu, wanaojua lugha ya kikikuyu na hata wasiojua lakini wapenzi wa muziki wa Kenya, John Demathew ni mgeni katika kila nyumba kuhusiana na muziki.              Habari zilizotufikia ni kwamba John Demathew hatunaye tena. Amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga Lori na kufia hospitali. Kwangu mimi, ukiwaacha Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, David Masondo, Paul Nkabinde Mahlathini, Spokes Mashiyane, Ndux Sr, Oliver Mutukudzi, Cephas Mashakada na Lapiro de Mbanga, (wote marehemu), Nana Moskouri, Ndux Jr, Mahotela Queens, hakuna mwanamuziki aliye hai alinivutia kama Demathew. Ameacha urathi wa album zaidi ya 50. Mungu iweke mahali pema peponi roho ya John Demathew, nani atasema eni kwenye tenzi zake. 
Thia wega muini munene wa nyimbo njega
Thia wega kikuo ni magegania murata wakwa
John Demathew jamba nene. 
Ngai ni mwega akurathime
Thia na wini waku mwega
Amina.

No comments: