Kwa wachambuzi na wataalamu wa siasa, kitendo cha mbunge wa Ubungo aliyemaliza muda wake Said Kubenea kutimkia Chama cha ACT-Wazelendo ni pigo kubwa kwake na chama chake kipya. Kubenea ambaye alipata umaarufu baada ya kumwagiwa tindikali, hana sifa yoyote ya siasa ukiachia mbali kuwa hana taaluma wala elimu yoyote japo ya msingi, anachofanya ni kujikaanga kwa mafuta yake kama samaki. Kwa tunaomjua na tuliofanya kazi naye, Kubenea si mwanasiasa bali msaka tonge sawa na wasaka tonge wengine. Ni mbabaishaji ambaye hana ithibati kimaadili wala kisiasa. Kwa wale watakaokumbuka andiko hili, watakuja sema kuwa nilisema kuwa alichofanya Kubenea si chochote wala lolote bali kuanzisha mwanzo wa mwisho wake kisiasa. Ama kweli, la kufa halisikii dawa. Na isitoshe, ujanja ujanja una sifa ya kujenga mbegu na chembe za maangamizi ndanimwe. Kubenea si mpinzani bali msaka tonge ambaye yuko tayari kuuza utu wake kwa lolote. Kama anadai ana makazi Kinondoni na ana ofisi Kinondoni, kwanini aligombea ubunge Ubungo? Si aseme amemkimbia profesa Benephace Jocob ukiachia mbali kutapatapa? Sioni tofauti ya Kubenea na akina Gwajima na wasasi wengine wa tonge na ngawira. Ukiachia mbali kutapatapata, Kubenea unasumbuliwa na ukafu ambao umemfanya amfuate maalim Seif Sharif Hamad. Kwanini Kubenea ameshindwa kung'amua kuwa Zitto Kabwe mwenye ACT-Wazalendo atawatumia yeye Seif na Bernard Membe kama ambayo CHADEMA waliwatumia akina Edward Lowassa na Fredrick Sumaye na kuwatema kama ganda la muwa? Ugwiji wake wa kufanya utafiti uko wapi hapa wakati anaingia mkenge mchana kweupe? Kubenea amesahau kuwa watanzania sasa wanajua kuwa umaarufu wake haukutokana na sifa wala umahiri bali kumwagiwa tindikali. Hivyo, alipata kura za kuonewa huruma ambazo kwa sasa hazitakuwapo. Je huu ni mwanzo wa mwisho wa Said Kubenea msaka tonge aliyepata umaarufu baada ya kumwagiwa tindikali?
No comments:
Post a Comment