How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do
Wednesday, 5 August 2020
MEMBE KAMA LOWASSA UKIACHIA MBALI TUNDU LISSU
Aliponyimwa nafasi ya kugombea urais, waziri mkuu wa zamani aliyeachia ngazi baada ya kukumbwa na kashfa ya ubadhilifu, Edward Lowassa, aliamua kujitoa kwenye chama kilichomzaa na kumlea, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia upinzani ambako alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichomteua kugombea urais akaangukia pua. Baada ya hapo, kilichotokea kinafahamika. Hata hivyo, si vibaya kugusia ni kwanini Lowassa alihamia upinzani na kugombea urais. Hakuwa na la kupoteza bali lau ima kuukwaa urais au kuonyesha hasira zake. Kadhalika, hasidi wa Lowassa, Bernard Membe, amerudufu kile alichokifanya hasidi wake. Baada ya kunyimwa kugombea urais, japo hakwenda moja kwa moja kujiunga na upinzani, alidhani anaweza kulipiza kisasi na kufikia malengo yake akiwa ndani humo humo. Yake ilikuwa: Tutabanana humu humu." Kwa kiasi kikubwa, Lowassa alifanikiwa kuiadhibu CCM kwa kupata kura nyingi. Tofauti na kipindi hiki, Membe na mwenzake Tundu Lissu wanaotaka kulipiza kisasi, hawataweza kuiadhibu wala kuiumbua CCM kwa sababu, Lowassa alipata fursa tokana na upya wa rais John Magufuli na uchakavu wa CCM ambayo kwa sasa imefufuliwa tokana na utendaji wa hali ya juu wa Magufuli. Hivyo, wawili hawa wataangukia pua. CCM itapata ushindi wa kishindo tokana na mafanikio ya Magufuli. Hivyo basi, wanachofanya wawili hawa, japo ni haki yao ya kidemokrasia, mipango yao, itachacha na kuwaumbua. Sitaki niwahukumu japo wanahukumika kirahisi, wataangukia pua na wameingia choo ya kike kama wasemavyo Dar. Kwa upande wa Zanzibar, hali itakuwa hivyo hivyo kwa maalimu Seif Sharif Hamad. Kwanini wasikengeuke kujiuliza ni kwanini Zitto Kabwe au Freeman Mbowe wametema nafasi hii yenye ujiko na marupurupu kibao? Kwa kujua kuwa kushinda ni ndoto ya mchana, wenye vyama wameamua kugombea ubunge badala ya urais. Isitoshe wanajua kuwa wagombea wao wakishindwa hawatakuwa na uwezo wa kutishia madaraka yao kichama kwa vile hawatakuwa na jipya la kuonyesha zaidi ya kushindwa. Kwa mfano, kwa kujua kuwa ACT-Wazalendo hakina bao visiwani, Zitto ameamua kumwachia Seif, ambaye umri umemuacha, agombee na kujifurahisha lau kutafuta sababu ya kuwa na mantiki kisiasa kwa kuanzisha malalamiko baada ya kubwagwa ili lau aendelee kuwa na ushawishi, kwa maslahi binafsi, visiwani. Ukisilikiza kwa makini hotuba ya Membe ya kushukuru kuteuliwa na anavyosema lazima Zitto awe bungeni na siyo kwenye serikali, basi unapata jibu haraka. Hata ukisikliza maneno ya Lissu kuhusiana na Zanzibar, unaona wazi jinsi wasivyotegemea kushinda. Anajua fika kuwa Hamad anagombea kwa mara ya sita. Nini anacho au atafanya mara hii ambacho kilimshinda mara tano zilizopita? Ukiaongezea na ukweli kuwa king'ang'anizi mwingine Prof Ibrahim Lipumba atakuwa kwenye debe, hali inakuwa wazi kabisa.Sambamba na Hamad, ni Lipumba. Naye hana jipya la kuwaambia wapiga kura.Lowassa aliweza kupata wingi wa kura alizopata tokana na upinzani kuungana. Je hali itakuwaje baada ya upinzani kusambaratika na kila chama kuweka mtu wake tena asiye na sera wala mvuto zaidi ya kutaka kulipiza visasi na ung'ang'anizi? Habari ndiyo hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment