The Chant of Savant

Friday 28 August 2020

KWA MTAJI HUU HAKUNA AWEZAYE KUMSHINDA MAGUFULI KATIKA UCHAGUZI UJAO

Mimi na Cde Pius Msekwa tulipoandika kitabu cha Magufulification: New Concept that Will Define Africa's future and the Man who Makes Things Happen, tuliyazingatia haya ambayo ofisi yake sasa imeamua kuyaweka bayana, yaani utendaji wake wa kipekee katika kuiinua Tanzania na kuhakikisha inatumia na kufaidika na raslimali zake ilizojaliwa na Mwenye Mungu. Ukisikiliza maelezo na ushahidi wa utendaji wa rais John Pombe Joseph Magufuli, utakubaliana nasi kuwa hiki ndicho tunachokiita Magufulification of Tanzania and Africa. Tazama kipindi hicho juu, utakubaliana na uchambuzi wetu. Kwa kuzingatia utendaji wa Magufuli au Magufulification kwa lugha ya kitaalamu, Magufuli amenaweza kushinda uchaguzi hata bila kuhangaika na kupiga kampeni. Kwani kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza. Wahenga walinena. Mwenye mato haambiwi tazama; na mwenye masikio na asikie.

 

No comments: