Kumbe Seif na Kabwe walipohubiri kula bata wengi hawakuwaelewa wasijue nani watakula bata na nani wataambulia kutoa mimacho huku wenyewe wakijichana hata bila kuwakumbuka waliowawezesha kula mibata! Ama kweli, wajinga ndio waliwao! Mwalimu wangu usinibaini. Nikipata kumi tano yako! Yametimia.
Kitendo cha rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi kuwateua wapinzani kujiunga na serikali yake ni cha kuigwa na kupigiwa mfano. Pamoja na kushinda vibaya, Mwinyi ameamua kufunika kombe il mwanaharamu apite. Kwa waliomsikia makamu wa kwanza wa rais Maalimu Seif Sharif Hamad akiapa watakuwa wamegundua alivyokuwa ni sizitaki mbichi hizi hasa baada ya kutembezewa kichapo ambapo CCM imezoa karibu kila kitu ikiwaacha wapinzani uchi. Niliwahi kuuliza nani anamtumia nani kati ya Zitto Kabwe na Seif. Sasa jawabu limejitokeza. Hii ni kutokana na Seif kujua kuwa katiba ya Zanzibar ilikuwa na upenyo wa kumbeba. Hata hivyo, licha ya kumpongeza Mwinyi nafurahi kuwa mbio za Seif za kuusaka urais zimeishia hapa hasa ikizingatiwa kuwa umri ushamtupa mkono. Ama kweli imethibitika kuwa mtoto wa nyoka ni nyoka na mtoto wa njiwa ni njiwa. Busara za Dk Mwinyi zimeivusha Zanzibar kwa mara nyingine. Maana yale madai kuwa kuna watu waliuawa yalikufa siku Seif alipopata alichokuwa akikitafuta. Ama kweli ukijua huu wenzio wanajua ule1 Hongera Dk Mwinyi kwa kuepuka mtego uliolenga kukuonyesha kama kiongozi mbaya wakati ni lulu.
No comments:
Post a Comment